UCHAMBUZI WA KATIBA INAYOPENDEZWA

UCHAMBUZI WA KATIBA INAYOPENDEKEZWA
Utangulizi
Bunge la Katiba lilitoa Rasmi Rasimu ya Katiba inayopendekezwa na kuikabidhi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete siku ya tarehe 08/10/2014 mjini Dodoma.
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, japo hakikuridhishwa kabisa na mchakato tokea Sheria ya Mabadiliko ya Katiba hususan Bunge la Katiba lilipoundwa na kuweka wanasiasa wengi kuliko wawakilishi wa wananchi, hata hivyo kimeichambua Katiba inayopendekezwa kama ifuatavyo hapa chini kwa lengo la kuwaelimisha wananchi kilichomo katika Katiba hiyo inayopendekezwa.
Kwa ufupi Katiba inayopendekezwa ni kinyume kabisa na maoni ya wananchi kwa mujibu wa Rasimu ya Pili ya Katiba. Masuala mengi yaliyoainishwa na wananchi kupitia Rasimu ya Pili hususani katika uongozi wa nchi na Uwajibikaji yameondolewa kabisa.
Uchambuzi huu umejikita katika Dhima tatu yaani masuala ya Utawala Bora, Haki za Binadamu na Muungano.
I. HAKI ZA BINADAMU
Haki za Binadamu zimeorodheshwa katika Sura ya Tano ya Katiba Inayopendekezwa zikiwa na sehemu kuu mbili yaani (a) haki za binadamu (Ibara ya 32 had 59) na (b) wajibu wa raia, Jamii na mamlaka ya Nchi na mipaka ya haki za binadamu (Ibara ya 60 hadi 67). Awali sura hii ilikuwa ni ya nne katika Rasimu ya Pili ya Katiba ikiitwa; Haki za Binadamu, Wajibu wa Raia na Mamlaka za Nchi ikiwa na jumla ya ibara 26 badala ya 28 zilizomo kwenye Katiba Inayopendekezwa kwa sasa.

Haki za binadamu zilizoanishwa nyingi ni haki ambazo ziliorodheshwa katika Rasimu ya Pili ya katiba na hata Katiba ya mwaka 1977 inayotumika sasa. Hata hivyo kuna haki ambazo hazikuwepo kabisa katika katiba ya sasa ambazo zimeongezewa baada ya mapendekezo ya wananchi.
Haki hizo ni pamoja na haki za makundi na haki za Jumla ambazo zimeongezwa katika Katiba Inayopendekezwa ni Ibara ya 46, 51 na 59. Haki hizo ni kuhusu haki za wakulima wafugaji, wavuvi na wachimbaji wadogo , haki ya afya na maji safi na salama, na haki za Uhuru wa taaluma,ubunifu, ugunduzi na usani.
Pamoja na kuongezwa kwa ibara zinazotamka haki hizi lakini kuna baadhi ya haki zimeondolewa ambazo zilitamkwa kwenye Rasimu ya Pili ya Katiba ikiwamo haki ya uraia iliyokua katika ibara ya 48. Pia baadhi ya ibara zimebadilishwa kwa kuongezea baadhi ya maneno au kuondolewa baadhi ya maneno ikiwamo kuondolewa kwa ibara zote zilizotamka juu ya utekelezaji wa Haki zilitoainishwa, Ibara hizi za utekelezaji awali zilikuwa zimeorodheshwa kwenye Rasimu ya Katiba zikitoa masharti juu ya namna haki hizo zitakavyotekelezwa, kinyume chake Katiba Inayopendekezwa imeweka masharti ya kutungwa kwa sheria juu ya utekelezaji wa haki zilizoanishwa. Hivyo kupunguza ubora wa nia ya maoni ya wananchi katika haki husika.
Angalizo; Sehemu zote za ibara hizi ambazo zimeitamka juu ya utekelezaji wa Haki zilitoainishwa zimeondolewa, ambapo awali zilikua zimeorodheshwa kwenye Rasimu ya Pili ya Katiba zikitoa masharti juu ya namna haki hizo zitakavyotekelezwa, kinyume chake Katiba Inayopendekezwa imeweka maasharti ya kutungwa kwa sheria juu ya utekelezaji wa haki zilizoanishwa ama kutokuweka kabisa hivyo kupunguza ubora wa nia ya maoni ya wananchi katika haki husika
Haki za Makundi
Haki za makundi mbalimbali katika jamii zimeorodheshwa katika ibara ya 45 na 46, pia kuanzia ibara ya 53 hadi ibara ya 58 za Katiba Inayopendekezwa. Haki hizo zimedadavuliwa kama ifuatavyo;
Haki za wakulima, wafugaji, wavuvi na wachimbaji madini- ibara ya 46 ambayo ni mpya kutokana na awali kutokuwemo kwenye Rasimu ya Pili ya katiba. Ibara hii inaorodhesha haki za makundi tajwa kuwa ni; haki ya kumiliki, kutumia na kuendeleza ardhi kwa ajili ya shughuli zao, kupata taarifa na maarifa kwa lengo la kuboreshashughuli zao, kumiliki na kunufaika na rasilimali za kijenetiki zao, pamoja na kushirikishwa katika utungaji wa sera, sheria na mipango mbalimbali inayohusu shughuli zao. Mapungufu ya ibara hii ni kutotamka namna utekelezaji wake utakavyokua. Pia ibara hii haifafanui maana ya ‘wachimbaji’ madini kuwa ni wapi, kwani kuna wachimbaji wa dogo na wachimbaji wakubwa, watanzania wengi ni wachimbaji wadogo, je haki hii ni kwao au ni kwa wachimbaji wote. Haki hii imetamkwa kisiasa zaidi kwa lengo la kuteka hisia za makundi ya watu mbalimbali. Pia ibara ndogo ya 1(a) haiko wazi kwani mvuvi hamiliki ardhi kwenye shughuli zake za uvuvi. Pia ibara hii imerundika haki za makundi matatu tofauti ambayo hayaendani; kwa mfano mvuvi na mchimbaji mdogo!
Haki za Mtoto – Ibara ya 53 ambayo ilikuwa ibara ya 43 katika rasimu ya rasimu ya katiba, haki za mtoto zimeboreshwa zaidi kwa kuongezwa kifungu kidogo cha 3 kinachotoa tafsiri ya umri wa “mtoto” kuwa maana yake ni mtu mwenye umri wa chini ya miaka kumi na nane.
Haki na Wajibu wa Vijana –ibara ya 44 awali ibara hii ilikuwa ni ya 54 katika rasimu ya katiba. Ibara hii imeboreshwa kwa kuongeza ibara ndogo ambayo inatoa masharti kwa Bunge kutunga sheria itakayosimamia pamoja na mambo mengine, uanzishwaji, muundo, majukumu na uendeshaji wa Baraza la Vijana la Taifa.
Haki za watu wenye Ulemavu – ibara ya 55 ambayo awali ilikuwa ni ibara ya 45 katika rasimu ya katiba. Baadhi ya mabadiliko hasi yaliyofanyika ni pamoja na kuondolewa kwa haki zilizotamkwa kwenye ibara ya 45 ya rasimu ambazo ni pamoja na haki ya kusoma,kujifunza na kuchanganyika na watu wengine; na kupunguzwa kwa haki ya kugombea nafasi za uongozi katika nyadhifa mbalimbali kwa usawa.

Haki za Wanawake – Ibara ya 57 ambayo awali ilikuwa Ibara ya 47 katika rasimu ya katiba, Haki za wanawake zimeendelea kuwepo. Haki hizo zimeboreshwa zaidi kwa kuongeza maneno; kuthaminiwa na kutambuliwa, kulindwa dhidi ya ubaguzi, udhalilishaji, dhuluma, unyanyasaji,ukatili wa kijinsia na mila potofu. Pia kupata huduma bora ya afya ikiwemo afya ya uzazi salama; na kumiliki mali. Pamoja na mazuri ya ibara hii, bado haijatamka juu ya utekelezaji masharti yaliyoainishwa. Kifungu cha Utekelezaji kimeondolewa. Pia kifungu cha usawa wa 50 kwa 50 kimeondolewa kabisa katika Katiba Inayopendekezwa.
Haki za Wazee- ibara ya 58 ambayo awali ilikuwa ni ibara ya 48 katika rasimu ya katiba, ambapo yameongeza maneno katika ibara husika yakiwemo; kujiendeleza kulingana na uwezo wake ikiwa ni pamoja na kufanya kazi, pia ibara hii imeongeza uzito kwa haki kuweka masharti ya ulinzi kwa wazee dhidi ya unyonyaji, ukatili na mateso pi akuweka miundo mbinu waweze kwenda watakapo kwa usafiri wa umma kwa bei nafuu.

Angalizo: Katika Haki zote za makundi zilizotajwa, hakuna tafsiri za makundi hayo isipokuwa haki za makundi madogo na Haki za Mtoto.

Uhuru wa taaluma, ubunifu, ugunduzi na usanii – ibara ya 59 ambayo ni mpya na haikuwepo katika rasimu ya katiba inaainisha haki za taaluma, ugunduzi na usanii. Ibara hii pamoja na mambo mengine inatamka uwepo wa uhuru wa kushiriki kwenye mambo yanayoendeleza na kukuza sanaa, taaluma, ubunifu na ugunduzi. Pia uhuru wa kujifunza, kufundisha, kutafiti na kueneza matumizi ya matokeo ya utafiti kulingana na kanuni za kitaaluma na za kiutafiti. Pia ibara inatamka kwamba Bunge litatunga sheria ambazo zitalinda hakimiliki na hataza na haki za wabunifu, watafiti na zitalinda hakimiliki na hataza na haki za wabunifu, watafiti na wasanii, kuwezesha taasisi za elimu na za utafiti kutumia ugunduzi wao kwa manufaa ya taifa; zitasimamia uhamishaji wa sayansi na teknolojia, zitawezesha kukuza rasilimali watu kwenye nyanja za kitaaluma, sayansi, teknolojia na ubunifu na zitalinda na kusimamia ubora wa taaluma, utafiti na matumizi ya ugunduzi na ubunifu.

Haki ya elimu – ibara ya 52 ambayo awali ilikua ibara ya 42. Katiba Inayopendekezwa imeondoa baaadhi ya mambo ambayo yalikuwemo kwenye rasimu ya katiba ambayo ni ya msingi, baadhi ya masuala hayo ni pamoja na kuondoa neno ‘kujifunza’ na kuondoa ibara ndogo inayotoa haki ya kupata fursa ya kupata elimu bora bila vikwazo. Pia Katiba Inayopendekezwa imeondoa ibara inayotoa haki ya kupata elimu bora inayotolewa nje ya utaratibu wa umma kwa gharama nafuu, suala hili ni nyeti kwa sababu watanzania wengi ni masikini na wanashindwa kumudu gharama za elimu nje ya mfumo wa umma Hivyo kushindwa kupata elimu.

Hifadhi ya haki za binadamu – Ibara ya 64 ambayo awali ilikua ni ibara ya 53 ya Rasimu ya Pili ya Katiba. Ibara hii imeondoa/ imefuta ibara ndogo muhimu ambayo ilikua kwenye rasimu ya katiba yaani ibara ya 53(3) ambayo inaweka wajibu wa Mamlaka za nchi bayana kuwa Mikataba ya kikanda na ile ya kimataifa kuhusu haki za binadamu ambayo Jamhuri ya Muungano imeridhia, [isipokuwa masharti ambayo Jamhuri ya Muungano imeeleza kutojifunga nayo], zitakuwa sehemu ya haki za binadamu zilizoainishwa katika sura ya 4 ya rasimu hii ya pili.
Usimamizi wa Haki za binadamu umeainishwa katika ibara ya 65 ya Katiba Inayopendekezwa, ambapo awali ilikua ni ibara ya 54 ya Rasimu ya Pili ya Katiba. Mahakama imeongezewa nguvu ya kusimamia ulinzi wa haki za Binadamu za mtu mmoja mmoja au makundi kwa kuipa mamlaka ya kubatilisha sheria au kushauri mamlaka za kiserikali au mamlaka za kutunga sheria kufuta sheria au vifungu vya sheria ambavyo inakinzana na haki, uhuru na wajibu kama ilivyotamkwa kwenye ibara za 32 hadi 59 za Katiba inayopendekezwa. Pamoja na ulinzi huu kupitia mahakama, kuna kasoro kubwa ambayo inatokana na kuondolewa kwa ibara ya 119 (a) ya Rasimu ya Pili ya Katiba iliyokuwa inaweka ulinzi juu mabadiliko ya Hati ya Haki za Binadamu kwa kuweka masharti kwamba ili kuwezesha masharti ya sehemu hii kubadilishwa ni lazima kuungwa mkono kwa zaidi ya theluthi mbili ya wananchi wa Jamhuri ya Muungano kutoka kila upande wa Jamhuri ya Muungano kwa Kura ya Maoni itakayoendeshwa na kusimamiwa na Tume Huru ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa sheria za nchi. Mabadiliko haya yanayopoka haki za msingi za wananchi ikiwemo kubadili masharti ya katiba yao.

UTAWALA BORA
Masuala yanayohusu utawala bora karibu yote yamechezewa na pengine kuondolewa kabisa na Katiba Inayopendekezwa. Kwa mfano; Kuondoa vifungu vya Uwajibikaji kwa mfano wananchi kumwajibisha Mbunge wao; Kuweka masharti magumu kwa mgombea huru na kumzuia kujiunga na chama chochote akiwa mbunge; Haki ya kuishi bado iko kwa mujibu wa sheria; Kuchanganya Tume ya haki za Binadamu na Utawala Bora,; Kuongeza makamu wa rais kufikia watatu katika mfumo wa serikali 2. Gharama walizokuwa wakisema kuhusu serikali 3 bado zitakuwa palepale.
Masuala mengine ni kuondoa tunu za taifa za Uwazi, Uadilifu na Uwajibikaji; Kuulinda Muungano kupita kiasi. Kwa mfano Nyongeza ya Pili na Tatu zote zinalenga kulinda mfumo na uwepo wa Muungano; Ukomo wa Mbunge umeondolewa; Spika wa Bunge anaweza kuwa Mbunge au asiwe Mbunge; Naibu Spika ni Lazima awe Mbunge; Idadi ya wabunge kufikia Mia tatu na tisini; Sifa ya Mbunge kielimu ni kujua kusoma na kuandika tu. na Waziri anaweza bado kuwa mbunge

MUUNGANO
Muundo wa muungano unapatikana katika sura ya saba na serikali ya jamhuri ya muungano imefafanuliwakatika sura ya nane ya Katiba Inayopendekezwa.

Muundo wa Muungano katika Rasimu ya pili ya Katiba ibara ya 60 uliainisha muundo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa ni shirikisho lenye serikali tatu ambazo ni: Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Tanganyika. Hata hivyo Katiba Inayopendekezwaibara ya 73 imebadilisha muundo huo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa muundo wa Serikali mbili ambazo ni: Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Kuondolewa kwa muundo wa muungano wa serikali tatu na kuwa mbili ni kutozingatia maoni ya wananchi kama yalivyokuwa kwenye rasimu ya pili ya Katiba. Kilio cha watanzania ni kutatua kero za muungano, hivyo kurudisha serikali 2 badala ya 3 bila kusema ni kwa jinsi gani kero hizo zitatatuliwa ni kuwarudisha watanzania nyuma.

Pia Katiba Inayopendekezwaibara ya 75 imeongeza ukuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano kuwa na mamlaka ya utekelezaji katika Jamhuri ya Muungano kwa Mambo ya Muungano na kwa mambo yote yasiyo ya Muungano yanayohusu Tanzania Bara. Na ibara ya 76 imetamka kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itakuwa na mamlaka na haki juu ya mambo yasiyo ya Muungano yanayohusu Zanzibar.

Jambo hili ni kinyume na rasimu ya pili ya Katiba ibara ya 62 amabayo imezungumzia mamlaka ya Serikali ya jamhuri kuwa na utekelezaji kwa mambo yote yaliyoorodheshwa kuwa mambo ya muungano kwa kuzingatia mamlaka itakayopewa chini ya katiba hii. Hivyo basi ni wazi kuwa serikali ya muungano imepewa madaraka makubwa ya utekelezaji wa mambo ya Tanzania bara pekee wakati Zanzibar imepewa mamlaka kamili kuhusu mambo yake.

Vilevile Katiba Inayopendekezwaibara ya 78 imeongeza idadi ya viongozi wakuu wenye wajibu wa kulinda muungano Hata hivyo Katiba hiyo imefuta nafasi ya Rais wa Tanganyika na kuongezwa kwa waziri mkuu wa jamhuri ya muungano na makamu wa rais wa Zanzibar. Hali hii inaifanya Tanzania kuwa shirikisho la nchi mbili Tanganyika na Zanzibar, japo Tanganyika inazidi kuwa mafichoni.

Jambo lingine ambalo Katiba Inayopendekezwaimeondoa ni madaraka ya Rais yaliyokuwa yameainishwa katika rasimu ya pili ibara ya 75 na badala yake ikasema Rais atakuwa na madaraka na majukumu kama yatakavyoainishwa kwenye sheria zitakazotungwa na Bunge. Pia majukumu ambayo hayakuainishwa katika Katiba hii na ambayo hayakiuki Katiba hii na sheria zitakazotungwa na Bunge. Hii ni kwa mujibu wa ibara ya 81 ya Katiba pendekezi.
Hali hii ya kutokuweka bayana madaraka ya Rais kunazidi kutengeneza mwanya wa Rais kuamua atakavyo na si kwa kuongozwa na misingi ya sheria.
Pamoja na hayo bado Katiba Inayopendekezwa ibara ya 88 imeondoa kipengele kinachotaka sifa za Rais ni pamoja na kuwa mwadilifu, anayeheshimu haki za binadamu na ambaye sera za chama chake sio za mrengo wa kuligawa Taifa.

Utekelezaji wa madaraka ya Rais kwa mujibu wa rasimu ya pili ya Katiba ibara ya 73 ni pamoja na kuanzisha au kufuta nafasi za madaraka katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano. Kwa kuzingatia masharti kuhusu uthibitisho wa Bunge, mamlaka za serikali au mahakama zilizopewa madaraka ya kumshauri.
Hata hivyo kipengele hiko kimeondolewa cha Rais kuzingatia masharti kuhusu uthibitisho wa Bunge katika nafasi za madaraka na vile vile ushauri wa mamlaka za Serikali, Bunge au Mahakama zilizopewa madaraka ya kumshauri katika kufanya uteuzi, kuanzisha au kufuta nafasi za madaraka katika utumishi wa Serikali kwa mujibu wa ibara ya 82. Hali hii inazidi kumfanya Rais awe mtawala badala ya kuwa kiongozi.

Pia Katiba Inayopendekezwaimeongeza uhuru uliozidi mipaka kwa Rais katika utendaji wa kazi na shughuli zake kwamba hatalazimika kufuata au kuzingatia ushauri atakaopewa na mtu yeyote au mamlaka yoyote isipokuwa pale tu anapotakiwa na Katiba hii au sheria nyingine yoyote kufanya jambo lolote kulingana na ushauri anaopewa na mtu au mamlaka yoyote.
Hii ni kutozingatia maoni ya wananchi kama yalivyoainishwa katika rasimu ya pili ya Katiba ibara ya 74 kuwa Rais atakuwa na wajibu wa kufuata na kuzingatia ushauri atakaopewa na mamlaka za nchi, na endapo hakubaliani na ushauri aliopewa, sharti atoe sababu katika Baraza la Mawaziri kuhusu sababu ya kutokubaliana na ushauri aliopewa.
Pia Katiba Inayopendekezwaimebadilisha ibara zote zinazozungumzia kila uteuzi lazima uthibitishwe na bunge kwa kura zaidi ya asilimia hamsini ya Wabunge wote bali uteuzi utathibitishwa na Bunge kwa wingi wa kura za Wabunge wote. Mabadiliko haya yanapatikana ibara ya 85 na 105 za Katiba pendekezi.

Pia Katiba Inayopendekezwaibara ya 86 imerudisha cheo cha waziri mkuu badala ya waziri mwandamizi kwamba ndiye atakayetekeleza madaraka ya Rais endapo nafasi yake itakuwa wazi kutokana na kutokuwepo katika Jamhuri ya Muungano. Cheo cha waziri mkuu kilifutwa katika Rasimu ya pili ya Katiba.

Jambo chanya katika Katiba Inayopendekezwa(ibara ya 90 (2)) ni kuhusu malalamiko ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Rais kuwa yatawasilishwa Mahakama ya Juu ndani ya muda wa siku saba baada ya siku ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa Rais. Pia Mahakama ya Juu itasikiliza na kutoa uamuzi wa shauri la kupinga matokeo ya uchaguzi wa Rais ndani ya siku kumi na nne tangu kupokea malalamiko yaliyowasilishwa kwa mujibu wa ibara ndogo ya (2) na uamuzi huo utakuwa wa mwisho.

Hata hivyo bado Katiba hii pendekezi inajikanganya katika ibara ya 82 inaposema Rais Mteule ataapishwa na Jaji Mkuu au Naibu Jaji Mkuu endapo Jaji Mkuu hayupo na atashika nafasi ya madaraka ya Rais siku saba baada ya kutangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi au mara baada ya kuthibitishwa na Mahakama ya Juu. Kuapishwa kwa Rais kumeharakishwa mno bila kuzingatia muda uliowekwa wa kupeleka shauri mahakamani kupinga matokeo.

Vilevile Katiba Inayopendekezwaibara ya 98 imesema Rais atalipwa mshahara na malipo mengine, na atakapostaafu atapokea malipo ya uzeeni, kiinua mgongo au posho kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina na Bunge litatunga sheria kwa ajili ya utekelezaji wa masharti ya Ibara hii. Ibara hii inapingana na maoni ya wananchi kwenye rasimu ya pili ibara ya 89 kuwa Rais atalipwa mshahara na malipo mengineyo kama yatakavyoainishwa na Tume ya Utumishi wa Umma na atakapostaafu atapokea malipo ya uzeeni na stahili nyingine kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina.
Rais ni mtumishi wa umma hivyo kitendo cha kuondoa malipo yake kutoka Tume ya Utumishi wa Umma siyo jambo jema. Mshahara wa Rais ni vizuri ukaratibiwa na Tume ya Utumishi wa umma ili kukuza uwazi na uwajibikaji.

Pamoja na hayo bado Katiba Inayopendekezwaibara ya 99 imeongeza makamu wa rais kufikia watatu kutoka mmoja aliyeainishwa kwenye rasimu ya pili ya Katiba ibara ya 90. Makamu hao wa rais ni Makamu wa Kwanza wa Rais, Rais wa Zanzibar ambaye atakuwa Makamu wa Pili wa Rais; na Waziri Mkuu ambaye atakuwa Makamu wa Tatu wa Rais. Kuweka makamu wa Rais watatu ni kuongeza gharama za uendeshaji kwa serikali jambo ambalo linapingana na madai ya awali kuwa serikali 3 ni mzigo.

Kuongezwa kwa wajumbe wa baraza la mawaziri katika Katiba Inayopendekezwa kutalifanya baraza la mawaziri kuwa na sura ya serikali zaidi. Pia Tume ilipendekeza kuwa Baraza la Mawaziri liwe ndio chombo mhimu cha kumshauri Rais. Katiba Inayopendekezwaimeondoa na hivyo kuwafanya wawe ni sehemu moja na Rais hivyo kukosa ufanisi katika utendaji kazi za serikali.

Pia mamlaka ya Rais kuteua mawaziri na naibu mawaziri yameongezwa. Ukubwa wa baraza la mawaziri kuwa arobaini ni mzigo. Uteuzi wa naibu mawaziri bila kuzingatia uwakilishi wa nchi washirika unaweza kusababisha upendeleo. Hii ni kwa mujibu wa ibara ya 115 ya Katiba pendekezi.

Jambo lingine hasi ni kutozingatiwa kwa maoni ya wananchi kwenye rasimu ya pili ya Katiba kuwa waziri na naibu waziri kutokuwa wanasiasa hayajazingatiwa. Hii itazidi kuleta mkanganyiko hasa katika utendaji kazi wao. Katiba Inayopendekezwaibara ya 116 imerudisha kigezo kimojawapo cha mtu kuteuliwa kuwa waziri au naibu waziri ni lazima awe mbunge. Pia suala la Waziri kuwajibika binafsi na kwa pamoja kwa Rais katika utekelezaji wa majukumu na katika kutumia nafasi ya madaraka ya waziri limeondolewa katika Katiba Inayopendekezwaibara ya 117.
Maoni ya ujumla kuhusu Muungano
Kwa ujumla Katiba Inayopendekezwa katika muundo wa muungano na Serikali ya Jamhuri ya muungano haijazingatia kabisa maoni yote yaliyotolewa katika rasimu ya pili ya Katiba ambayo ni maoni yaliyotolewa na wananchi. Kwa mujibu wa randama ya rasimu ya Katiba wananchi walio wengi walitoa maoni yao ya kutaka kuondoa kero za muungano ambazo kwa kiasi kikubwa zimetokana na muundo wa serikali mbili kwa kukosekana kwa mipaka iliyo wazi baina ya mambo ya muungano na mambo yasiyo ya muungano. Hivyo ni dhahiri kuwa wajumbe wa bunge la Katiba kwa makusudi waliamua kupuuzia maoni hayo na kutanguliza mbele maslahi yao binafsi au ya vyama walivyoviwakilisha.

UCHAMBUZI WA SURA YA 1 KATIKA RASIMU YA PILI NA KATIBA INAYOPENDEKEZWA
KIFUNGU KWA KIFUNGU

Ibara RASIMU YA PILI YA KATIBA KATIBA INAYOPENDEKEZWA
TOFAUTI MAONI
Utangulizi KWA KUWA, sisi wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumeamua rasmi na
kwa dhati kujenga katika nchi yetu jamii inayoheshimu na kuzingatia misingi ya utu, uhuru,
haki, usawa, udugu, amani, umoja na mshikamano katika nyanja zote za maisha yetu;
NA KWA KUWA, tunaamini kuwa misingi hiyo inaweza tu kutekelezwa katika jamii yenye
mfumo wa demokrasia na utawala bora ambayo Serikali yake inasimamiwa na Bunge lenye
Wabunge waliochaguliwa na wanaowakilisha wananchi, na Mahakama huru
zinazotekeleza wajibu wa kutoa haki bila woga wala upendeleo wowote, na kuhakikisha
kuwa haki za binadamu zinalindwa na kudumishwa na kwamba wajibu wa kila mtu
unatekelezwa kwa uaminifu;
NA KWA KUWA, tunatambua umuhimu wa kutunza mali ya Mamlaka za Nchi na ya
pamoja, kupiga vita aina zote za uharibifu, ubadhirifu na kuhimiza matumizi bora na
endelevu ya rasilimali na maliasili zetu pamoja na kulinda na kuhifadhi mazingira yetu kwa
mustakabali wa maisha ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo;
NA KWA KUWA, tunatambua umuhimu na faida za kujenga, kukuza na kuendeleza amani,
umoja, urafiki na ushirikiano miongoni mwa Watanzania, mataifa mbalimbali ya Afrika na
dunia kwa ujumla;
NA KWA KUWA, azma ya kujenga Umoja wa Bara la Afrika inadhihirishwa na
Muungano wa iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar;
NA KWA KUENDELEZA DHAMIRA YETU HIYO, ni muhimu:
(a) kulinda, kuimarisha na kuudumisha Muungano wa nchi za Jamhuri ya Tanganyika na
Jamhuri ya Watu wa Zanzibar;
(b) kujenga Taifa huru na linalojitegemea;
(c) kuimarisha na kuendeleza utawala wa sheria;
(d) kukuza na kuendeleza maadili, uwajibikaji na uwazi;
(e) kujenga umoja na mshikamano utakaowezesha kutimiza malengo ya kisiasa,
kiuchumi, kijamii, kimazingira na kulinda urithi kwa ujumla;
(f) kujenga na kuendeleza ukuu wa mamlaka ya watu;
(g) kujenga na kuendeleza utii wa mamlaka ya Katiba; na
(h) kuimarisha na kudumisha uzalendo kwa Taifa miongoni mwa Watanzania;
NA KWA KUZINGATIA, urithi tulioachiwa na Waasisi wa Taifa letu wa kujenga nchi
yenye umoja wa watu wake ambao hawabaguani kwa misingi ya ukabila, dini, rangi, jinsi au
xvii
ubaguzi wa aina nyingine yoyote;
NA KWA KUZINGATIA, uzoefu wa zaidi ya Miaka Hamsini ya Uhuru wa Tanganyika,
Miaka Hamsini ya Mapinduzi ya Zanzibar na Miaka Hamsini ya Muungano wa Jamhuri ya
Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, na umuhimu wa ushiriki mpana na bayana wa
wananchi katika utungaji wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
HIVYO BASI, KATIBA HII YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
ILIYOPENDEKEZWA NA BUNGE MAALUM LA KATIBA imetungwa na SISI
WANANCHI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA kupitia KURA YA
MAONI kwa madhumuni ya kujenga jamii kama hiyo, na kuhakikisha kuwa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania inaongozwa na Serikali yenye kufuata misingi ya demokrasia na
utawala wa sheria, kujitegemea na isiyofungamana na dini. KWA KUWA, sisi wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumeamua rasmi na
kwa dhati kujenga katika nchi yetu jamii inayoheshimu na kuzingatia misingi ya utu, uhuru,
haki, usawa, udugu, amani, umoja na mshikamano katika nyanja zote za maisha yetu;

NA KWA KUWA, tunaamini kuwa misingi hiyo inaweza tu kutekelezwa katika jamii yenye
mfumo wa demokrasia na utawala bora ambayo Serikali yake inasimamiwa na Bunge lenye
Wabunge waliochaguliwa na wanaowakilisha wananchi, na Mahakama huru
zinazotekeleza wajibu wa kutoa haki bila woga wala upendeleo wowote, na kuhakikisha
kuwa haki za binadamu zinalindwa na kudumishwa na kwamba wajibu wa kila mtu
unatekelezwa kwa uaminifu;
NA KWA KUWA, tunatambua umuhimu wa kutunza mali ya Mamlaka za Nchi na ya
pamoja, kupiga vita aina zote za uharibifu, ubadhirifu na kuhimiza matumizi bora na
endelevu ya rasilimali na maliasili zetu pamoja na kulinda na kuhifadhi mazingira yetu kwa
mustakabali wa maisha ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo;
NA KWA KUWA, tunatambua umuhimu na faida za kujenga, kukuza na kuendeleza amani,
umoja, urafiki na ushirikiano miongoni mwa Watanzania, mataifa mbalimbali ya Afrika na
dunia kwa ujumla;
NA KWA KUWA, azma ya kujenga Umoja wa Bara la Afrika inadhihirishwa na
Muungano wa iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar;
NA KWA KUENDELEZA DHAMIRA YETU HIYO, ni muhimu:
(a) kulinda, kuimarisha na kuudumisha Muungano wa nchi za Jamhuri ya Tanganyika na
Jamhuri ya Watu wa Zanzibar;
(b) kujenga Taifa huru na linalojitegemea;
(c) kuimarisha na kuendeleza utawala wa sheria;
(d) kukuza na kuendeleza maadili, uwajibikaji na uwazi;
(e) kujenga umoja na mshikamano utakaowezesha kutimiza malengo ya kisiasa,
kiuchumi, kijamii, kimazingira na kulinda urithi kwa ujumla;
(f) kujenga na kuendeleza ukuu wa mamlaka ya watu;
(g) kujenga na kuendeleza utii wa mamlaka ya Katiba; na
(h) kuimarisha na kudumisha uzalendo kwa Taifa miongoni mwa Watanzania;
NA KWA KUZINGATIA, urithi tulioachiwa na Waasisi wa Taifa letu wa kujenga nchi
yenye umoja wa watu wake ambao hawabaguani kwa misingi ya ukabila, dini, rangi, jinsi au
xvii
ubaguzi wa aina nyingine yoyote;
NA KWA KUZINGATIA, uzoefu wa zaidi ya Miaka Hamsini ya Uhuru wa Tanganyika,
Miaka Hamsini ya Mapinduzi ya Zanzibar na Miaka Hamsini ya Muungano wa Jamhuri ya
Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, na umuhimu wa ushiriki mpana na bayana wa
wananchi katika utungaji wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
HIVYO BASI, KATIBA HII YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
ILIYOPENDEKEZWA NA BUNGE MAALUM LA KATIBA imetungwa na SISI
WANANCHI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA kupitia KURA YA
MAONI kwa madhumuni ya kujenga jamii kama hiyo, na kuhakikisha kuwa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania inaongozwa na Serikali yenye kufuata misingi ya demokrasia na utawala wa sheria, kujitegemea na isiyofungamana na dini. Katiba Inayopendekezwa, imeweka vifungu vipya vya utangulizi kama ifuatavyo;

NA KWA KUWA, ni muhimu kulinda, kuimarisha na kuudumisha Muungano, kujenga Taifa huru na linalojitegemea, kuimarisha na kuendeleza misingi ya utawala bora na maadili ya viongozi, kujenga umoja na mshikamano utakaowezesha kutimiza malengo ya Taifa, kujenga na kuendeleza ukuu wa mamlaka ya wananchi, utii wa mamlaka ya Katiba na kuimarisha na kudumisha uzalendo kwa Taifa miongoni mwa

‘NA KWA KUZINGATIA, uzoefu wa zaidi ya Miaka Hamsini ya Muungano, na umuhimu wa ushiriki wa wananchi katika utungaji wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;

Hakuna tofauti.

Vifungu hivi vipya havina uzito wowote kimaudhui ya Katiba. Vimewekwa ili kuulinda zaidi muungano wa serikali 2 kwa mfano pale inapoeleza kuwa;

NA KWA KUWA, ni muhimu kulinda, kuimarisha na kuudumisha Muungano,….
Na
NA KWA KUZINGATIA, uzoefu wa zaidi ya Miaka Hamsini ya Muungano, ….

SURA YA KWANZA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
SEHEMU YA KWANZA
JINA, MIPAKA, ALAMA, LUGHA NA TUNU ZA TAIFA
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
1. 1.-(1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nchi na Shirikisho
lenye mamlaka kamili ambalo limetokana na Muungano wa nchi mbili
za Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, ambazo
kabla ya Hati ya Makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964, zilikuwa
nchi huru.
(2) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Shirikisho la
kidemokrasia linalofuata mfumo wa vyama vingi vya siasa, usawa wa
binadamu, kujitegemea, utawala wa sheria, kuheshimu haki za
binadamu na lisilofungamana na dini.
(3) Hati ya Makubaliano ya Muungano iliyorejewa katika ibara
ndogo ya (1), ndio msingi mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
na Katiba hii, kwa kadri itakavyorekebishwa, itakuwa ni mwendelezo
wa Makubaliano hayo.
1.-(1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi yenye mamlaka kamili
ambayo imetokana na Muungano wa nchi mbili za Jamhuri ya Tanganyika na
Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambazo kabla ya Hati ya Makubaliano ya
Muungano ya tarehe 22 Aprili, 1964 zilikuwa nchi huru. • Neno shirikisho limeondolewa kutoka kwenye Katiba inayopendekezwa

• Rasimu ya Tume imetaja tu Mwaka bila tarehe; ila Katiba inayopendekezwa imetaja tarehe ya Makubaliano ya Muungano

• Usawa wa Binadamu na Utawala wa Sheria vimeondolewa. Kwa kuondolewa neon shirikisho kutoka kwenye Katiba inayopendekezwa imeondoa dhana ya kuwepo kwa nchi mbili washirika kwenye Muungano kama nchi huru. Hii inaleta dhana ya kwamba nchi zote mbili zimepoteza utambulisho wake kwa kuingia kwenye Muungano.
Hii inaweka mfumo wa Serikali Mbili (Jamhuri na Zanzibar)
(2) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi ya kidemokrasia
inayofuata mfumo wa vyama vingi vya siasa, utawala wa sheria, inayoheshimu
misingi ya haki za binadamu, isiyofungamana na dini yoyote na inayojitegemea. Maneno – Shirikisho na usawa wa binadamu yameondolewa kutoka kwenye Katiba inayopendekezwa Hii ni Tunu ya muhimu sana kuwepo kwenye utambulisho wa Taifa.
(3) Hati ya Makubaliano iliyorejewa katika ibara ndogo ya (1) ndiyo
msingi mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Katiba hii, kwa kadri
Itakavyorekebishwa, itakuwa ni mwendelezo wa Makubaliano hayo. Imeondoa neno ya Muungano

Eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Eneo la Jmhuri ya Muungano. 2.- Eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni eneo lote la
Tanganyika likijumuisha sehemu yake ya bahari na eneo lote la
Zanzibar likijumuisha sehemu yake ya bahari.
2.-(1) Eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni:
(a) eneo lote la Tanzania Bara, ikiwa ni pamoja na eneo lake la bahari
ambalo kabla ya Muungano lilikuwa likiitwa Jamhuri ya Tanganyika
pamoja na maeneo mengine yatakayoongezeka; na
(b) eneo lote la Zanzibar, ikiwa ni pamoja na eneo lake la bahari ambalo
kabla ya Muungano lilikuwa likiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar
pamoja na maeneo mengine yatakayoongezeka. Rasimu ya Pili ya Katiba imeelekeza mipaka ya nchi washirika kwenye Jamhuri ya Muungano, yaani Tanganyika na Zanzibar.
Katiba inayopendekezwa imeelekeza mipaka ya Tanzania bara na Zanzibar na kutoa ufafanuzi kuhusu iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar
Katiba inayopendekezwa pia imeongeza fasili ya pili na ya tatu.
Fasili ya pili inaelezea mamlaka ya Raisi kugawa maeneo ya mikoa na maeneo mengine kwa bara, kwa upande wa Zanzibar Katiba inayopendekezwa imeelekeza kwamba Rais anaweza kukasimu mamalaka hayo kwa Rais wa Zanzibar.
Fasili ya tatu imetoa madaraka kwa Bunge la Jamhuri nya Muungano kutunga sheria inayoainisha mipaka ya Jamhuri ya Muungano.
(2) Rais wa Jamhuri ya Muungano atakuwa na mamlaka ya kuigawa Jamhuri ya Muungano atakuwa na Mamlaka ktk mikoa, wilaya na na maeneo mengineyo

(2) Rais wa Jamhuri ya Muungano atakuwa na mamlaka ya kuigawa Jamhuri ya Muungano katika mikoa, wilaya na maeneo mengine:
Isipokuwa kwa upande wa Tanzania Zanzibar, Rais atashauriana na Rais wa Zanzibar kabla ya kuigawa Tanzania Zanzibar katika mikoa, wilaya au maeneo mengine.
(3) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (1), Bunge litatunga sheria itakayoainisha na kufafanua mipaka ya eneo la Jamhuri ya Muungano.
mpya
Alama za Taifa zitakuwa ni:
3.-(1) Alama za Taifa zitakuwa ni:
(a) Bendera ya Taifa;
(b) Wimbo wa Taifa; na
(c) Nembo ya Taifa,
kama zitakavyoainishwa katika sheria za nchi.
(2) Sikukuu za Kitaifa zitakuwa ni:
(a) Siku ya Uhuru wa Tanganyika, itakayoadhimishwa tarehe 9
Disemba;
(b) Siku ya Mapinduzi ya Zanzibar, itakayoadhimishwa tarehe
12 Januari;
(c) Siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar,
itakayoadhimishwa tarehe 26 Aprili; na
(d) Sikukuu nyingine zitakazoainishwa na sheria za nchi.
(3) Kila Sikukuu ya Kitaifa itakuwa ni siku ya mapumziko 3.-(1) Alama za Taifa zitakuwa ni:
(a) Bendera ya Taifa;
(b) Wimbo wa Taifa; na
(c) Nembo ya Taifa,
kama zitakavyoainishwa katika sheria za nchi.
(2) Sikukuu za kitaifa zitakuwa:
(a) Siku ya Uhuru wa Tanganyika, itakayoadhimishwa tarehe
9 Disemba;
(b) Siku ya Mapinduzi ya Zanzibar, itakayoadhimishwa tarehe
12 Januari;
(c) Siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, itakayoadhimishwa
tarehe 26 Aprili; na
(d) sikukuu nyingine zitakazoainishwa na sheria za nchi.
(3) Kila sikukuu ya kitaifa itakuwa ni siku ya mapumziko. Hakuna mabadiliko kwenye Ibara ya tatu.

Lugha ya Taifa na Lugha za Alama

4. 4.-(1) Lugha ya Taifa ya Jamhuri ya Muungano ni Kiswahili na
itatumika katika mawasiliano rasmi ya kitaifa na kiserikali.
(2) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (1), lugha ya
Kiingereza au lugha nyingine yoyote inaweza kutumika kuwa lugha
rasmi ya mawasiliano ya kiserikali pale itakapohitajika.
(3) Serikali itaweka mazingira yatakayowezesha kuwepo kwa
mawasiliano mbadala zikiwemo lugha za alama, maandishi
yaliyokuzwa na nukta nundu kwenye sehemu muhimu za umma na
katika vyombo vya habari vinavyotangaza habari zake kitaifa kwa ajili
ya watu wenye mahitaji maalum.
Eneo la Jamhuri
ya Muungano
wa Tanzania.
Alama na
Sikukuu za
Taifa.
Lugha ya Taifa
4.-(1) Lugha ya Taifa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni
Kiswahili na itatumika katika mawasiliano rasmi ya kitaifa na kiserikali.
(2) Bila kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (1), lugha ya Kiingereza au
lugha nyingine yoyote ya kimataifa inaweza kutumika kama lugha rasmi ya
mawasiliano ya kiserikali, pale itakapohitajika.
(3) Kwa mujibu wa Ibara hii, lugha ya alama kwa viziwi na lugha ya
alama mguso kwa viziwi wasioona, zitakuwa lugha rasmi za mawasiliano.
(4) Serikali itaweka mazingira yatakayowezesha kuwepo kwa
mawasiliano mbadala zikiwemo lugha ya alama, lugha ya alama mguso,
maandishi yaliyokuzwa na nukta nundu kwenye sehemu muhimu za umma na
katika vyombo vya habari vinavyotangaza habari zake kitaifa kwa ajili ya watu
wenye ulemavu. i. Kwenye fasili ya pili kwenye Katiba inayopendekezwa neno kimataifa likimaanisha lugha ya kimataifa limeongezwa.
Fasili ya tatu ni mpya kwenye Katiba inayopendekezwa kuhusiana na lugha ya alama kwa viziwi na lugha ya
alama mguso kwa viziwi wasioona, kwamba zitakuwa lugha rasmi za mawasiliano.
ii. I. Hili ni ingizo zuri na la kufurahia kwamba sasa lugha hizo zitakuwa ni rasmi.
Tunu za Taifa
5. 5. Jamhuri ya Muungano itaenzi na kuzingatia Tunu za Taifa
zifuatazo:
(a) utu;
(b) uzalendo;
(c) uadilifu;
(d) umoja;
(e) uwazi;
(f) uwajibikaji; na
(g) lugha ya Taifa.
5. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaenzi na kuzingatia Tunu za
Taifa zifuatazo:
(a) lugha ya Kiswahili;
(b) Muungano;
(c) utu na udugu; na
(d) amani na utulivu. Kwenye Katiba inayopendekezwa nyingi ya Tunu zilizopendekezwa zimeachwa, kama vile uzalendo, uadilifu, umoja, uwazi na uwajibikaji.
Tunu tatu uadilifu, uwazi na uzalendo zimehamishiwa ibara ya 6 inayohusu misingi ya utawala bora
Tunu mpya zimeongezwa kama Muungano, undugu, amani na utulivu.

Muungano siyo tunu – maelezo yaliyotolewa na Chenge hayajitoshelezi –
Utulivu ni matokeo ya kuenzi hizo tunu
Tunu za Taifa ni mambo muhimu kulinganisha na hali ya Taifa letu kwa sasa. Tunu hizi ni muhimu sana kwa upande wa wananchi ambayo ina taathira yake kwenye mihimili mitatu ya dola kwa vile wanaofanya nkazi huko wanatokana na wananchi. Kwa kuziondoa tunu hizo kuna ombwe lililobaki kwenye Katiba iliyopendekezwa.
Kwa kuhamishiwa kwenye ibara ya 6 kwa uadilifu, uwazi na uzalendo, maana yake ni kwamba tunu hizo ni kwa wafanyakazi wa umma na siyo kwa wananchi kama ilivyopendekezwa kwenye Rasimu ya pili ya Katiba.

Misingi ya Utawala Bora
6.Mamlaka ya Wananchi 6. Jamhuri ya Muungano ni nchi inayofuata misingi ya
demokrasia inayozingatia haki ya kijamii, na kwa hiyo:
(a) wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata
madaraka na mamlaka yake kutoka kwa wananchi ambao
kwa umoja na ujumla wao wanaimiliki na kuipatia Katiba
hii uhalali;
(b) lengo kuu la Serikali litakuwa ni maendeleo na ustawi wa
wananchi;
(c) Serikali itawajibika kwa wananchi; na
(d) wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali kwa
mujibu wa masharti ya Katiba hii.
6. (1) Katika utekelezaji wa mamlaka au shughuli zozote kwa mujibu
wa Katiba hii au sheria za nchi, misingi ya utawala bora katika Ibara hii ni
lazima izingatiwe na kufuatwa na taasisi ya Serikali, ofisa wa Serikali au mtu
yeyote aliyepewa dhamana ya:
(a) kutumia au kutafsiri Katiba hii;
(b) kutunga, kutumia au kutafsiri sheria yoyote; na
(c) kufanya au kutekeleza maamuzi ya sera za kitaifa.
(2) Misingi ya utawala bora katika Jamhuri ya Muungano itajumuisha:
(a) uadilifu;
(b) demokrasia;
(c) uwajibikaji;
(d) utawala wa sheria;
(e) ushirikishwaji wa wananchi;
(f) haki za binadamu;
(g) usawa wa jinsia;
(h) umoja wa kitaifa;
(i) uwazi; na
(j) uzalendo. Hii ni ibara mpya kwenye Katiba inayopendekezwa

Uzalendo na umoja wa kitaifa siyo misingi ya utawala bora

Haya yote yaliyoorodheshwa siyo misingi ya utawala bora, bali mengine ni Tunu za Taifa.
SEHEMU YA PILI
MAMLAKA YA WANAN CHI, UTII NA UHIFADHI WA KATIBA
Mamlaka ya Wananchi

.
7.-(1) Wananchi ndiyo msingi wa mamlaka yote, na kwa hiyo:
(a) Serikali itapata madaraka na mamlaka yake kutoka kwa wananchi
3
ambao kwa umoja na ujumla wao wanaimiliki na kuipatia Katiba hii
uhalali;
(b) lengo kuu la Serikali litakuwa ni maendeleo na ustawi wa wananchi;
(c) Serikali itawajibika kwa wananchi; na
(d) wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali kwa mujibu wa
masharti ya Katiba hii.
(2) Kwa mujibu wa Ibara hii, Serikali ya Jamhuri ya Muungano na
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zitapata madaraka na mamlaka yake kutoka
kwa wananchi kupitia uchaguzi wa kidemokrasia utakaoendeshwa na
kusimamiwa na vyombo vitakavyopewa mamlaka na Katiba hii na Katiba ya
Zanzibar, kwa kadri itakavyokuwa. Mabadiliko ya kiuandishi yamefanywa. Neno “wananchi ndiyo msingi wa mamlaka yote” limewekwa kuwa ndiyo mada kuu kwenye Katiba inayopendekezwa.
Imeongezwa fasili ya pili kwenye ibara hii inayosema kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano na ile ya Zanzibar zitapata mamlaka yake kupitia kwa wananchi.
Imeondoa haki yua kijamii na demokrasia –

Hakuna tofauti kubwa kutokana na marekebisho yaliyo fanyika.

– Hii imelenga kupunguza nguvu na mamlaka ya Wananchi.
Watu na Serikali
7.-(1) Muundo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo
vyake, katika uendeshaji na utekelezaji wa shughuli zake, utazingatia
azma ya kukuza umoja wa kitaifa na kudumisha heshima ya Taifa.
(2) Kwa madhumuni ya masharti ya ibara ndogo (1), mamlaka
ya nchi na vyombo vyake vinawajibika kuelekeza sera, sheria na
shughuli zake zote kwa lengo la kuhakikisha kwamba:
(a) utu, heshima na haki nyingine za binadamu zinalindwa,
zinathaminiwa, zinahifadhiwa na kudumishwa kwa
kuzingatia mila na desturi za Watanzania na mikataba
mbalimbali iliyoridhiwa na Jamhuri ya Muungano;
(b) sheria za nchi zinasimamiwa na kutekelezwa;
(c) shughuli zinazofanywa zinatekelezwa kwa njia ambazo
zitahakikisha kwamba utajiri wa Taifa unaendelezwa,
unahifadhiwa na kutumiwa kwa manufaa ya wananchi
wote kwa jumla na pia kuzuia mtu kumnyonya mtu
mwingine;
(d) ardhi ikiwa rasilimali kuu na msingi wa Taifa inalindwa,
inatunzwa na kutumiwa na wananchi wa Tanzania kwa
manufaa, maslahi na ustawi wa kizazi cha sasa na vizazi
vijavyo;
(e) maendeleo ya uchumi wa Taifa yanapangwa na kukuzwa
kwa ulinganifu na kwa pamoja na kwa namna ambayo
inawanufaisha wananchi wote;
(f) kila mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi anafanya kazi, na
kazi maana yake ni shughuli yoyote ya halali inayompatia
mtu kipato chake;
8(1) Serikali na vyombo vyake, katika uendeshaji na utekelezaji wa
shughuli zake, itazingatia azma ya kukuza umoja wa kitaifa na kudumisha
heshima ya Taifa.
(2) Kwa madhumuni ya masharti ya ibara ndogo ya (1), Serikali na
vyombo vyake vinawajibika kuelekeza sera, sheria na shughuli zake zote kwa
lengo la kuhakikisha kwamba:
(a) utu, heshima na haki za binadamu zinalindwa, zinathaminiwa,
zinahifadhiwa na kudumishwa kwa kuzingatia mila na desturi za
Watanzania na mikataba ya kimataifa iliyoridhiwa na Jamhuri ya
Muungano;
(b) sheria za nchi zinasimamiwa na kutekelezwa;
(c) utajiri wa Taifa unaendelezwa, unahifadhiwa na kutumika kwa
manufaa ya wananchi wote na kuzuia unyonyaji wa aina yoyote;
(d) ardhi ikiwa ni rasilimali kuu na msingi wa Taifa, inalindwa,
inatunzwa na kutumiwa kwa manufaa, maslahi na ustawi wa kizazi
cha sasa na vizazi vijavyo;
(e) maendeleo ya uchumi wa Taifa yanapangwa na kukuzwa kwa
ulinganifu na kwa namna ambayo inawanufaisha wananchi wote;
(f) kila mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi anafanya kazi, na kazi
maana yake ni shughuli yoyote halali inayompatia mtu kipato chake;
(g) kunakuwepo fursa na haki zilizo sawa kwa wananchi wote,
wanawake na wanaume, bila ya kujali rangi, kabila, nasaba,
ulemavu, itikadi, dini au hali ya mtu;
(h) aina zote za dhuluma, vitisho, ubaguzi, ukatili, udhalilishaji,
unyanyasaji, rushwa, uonevu au upendeleo zinaondolewa nchini;
(i) utajiri wa rasilimali na maliasili za Taifa unaelekezwa katika kuleta
maendeleo, kuondoa umaskini, ujinga na maradhi; na
(j) nchi inaongozwa kwa kufuata misingi ya demokrasia, utawala wa
sheria na kujitegemea Mabadiliko kidogo ya kiuandishi yamefanywa kwa kuondoa maneno “muundo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake” na badala yake Katiba inayopendekezwa imetumia maneno ya “Serikali na vyombo vyake” Mabadiliko kidogo ya kiuandishi kwenye rasimu inayopendekezwa hayakubadili maudhui yaliyomo kwenye ibara hii.
Ukuu na Utii wa Katiba
8.-(1) Katiba hii ni sheria kuu katika Jamhuri ya Muungano kwa
kuzingatia masharti ya Katiba hii.
(2) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (1), endapo masharti ya
sheria yoyote yatatofautiana na masharti ya Katiba hii, masharti ya
sheria hiyo yatakuwa batili na yatatenguka kwa kiwango kile
kinachotofautiana na masharti ya Katiba hii.
(3) Mtu yeyote, chombo, taasisi, jumuiya na wakala wowote wa
mamlaka ya nchi na mamlaka binafsi zinao wajibu wa kuzingatia
masharti ya Katiba hii na sheria za nchi na kuzitii.
(4) Sheria yoyote, mila, desturi au uamuzi wowote wa chombo
cha dola, ofisa wa Serikali au mtu binafsi ni sharti ufuate na kuendana
na masharti yaliyomo kwenye Katiba hii na kwamba sheria, mila,
desturi au uamuzi wowote ambao hautawiana au kwenda sambamba na
masharti ya Katiba hii utakuwa batili.
(5) Serikali itaweka utaratibu wa kuwawezesha wananchi
kuifahamu, kuilinda na kuitii Katiba.
9.-(1) Katiba hii ni sheria kuu katika Jamhuri ya Muungano kwa mujibu
wa masharti yaliyowekwa na Katiba hii.
(2) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (1), endapo masharti ya sheria
yoyote itakayotungwa na vyombo vyenye mamlaka ya kutunga sheria
4
yatatofautiana na masharti ya Katiba hii, masharti ya sheria hiyo yatakuwa batili
na yatatenguka kwa kiwango kile kinachotofautiana na masharti ya Katiba hii.
(3) Mtu yeyote, chombo au taasisi ya Serikali, jumuiya, wakala yeyote
na mamlaka binafsi zitakuwa na wajibu wa kuzingatia na kutii masharti ya
Katiba hii na sheria za nchi.
(4) Sheria yoyote, mila, desturi au uamuzi wowote wa chombo cha dola
au ofisa wa Serikali ni sharti ufuate na kuzingatia masharti yaliyomo kwenye
Katiba hii na kwamba sheria, mila, desturi au uamuzi wowote ambao
hautawiana au kwenda sambamba na masharti ya Katiba hii utakuwa batili.
(5) Serikali itaweka utaratibu wa kuwawezesha wananchi kuifahamu,
kuilinda na kuitii Katiba hii.
Ibara ndogo ya 1) – neno kwa kuzingatia limefutwa – badala yake – imeandikwa [kwa mujibu]
Mabadiliko makubwa kiuandishi yamefanywa kwenye fasili ya tatu – kwa kufuta sentensi Hakuna tofauti kwenye maudhui ya ibara .

U hifadhi ya Utawala wa Katiba
Hifadhi ya Utawala wa katiba 9.-(1) Mtu au kikundi cha watu hakitachukua au kushikilia
mamlaka ya nchi isipokuwa kwa mujibu wa Katiba hii.
(2) Kitendo chochote kinachokiuka masharti ya ibara ndogo ya
(1) ni batili na ni kitendo cha uhaini kama itakavyoelezwa katika sheria
za nchi.
10-(1) Mtu au kikundi cha watu hakitachukua au kushikilia mamlaka ya
nchi isipokuwa kwa mujibu wa Katiba hii.
(2) Kitendo chochote kinachokiuka masharti ya ibara ndogo ya (1) ni
batili na ni kitendo cha uhaini kama itakavyoelezwa katika sheria za nchi. Hakuna mabadiliko yoyote kwente ibara hii.

SURA YA PILI
MALENGO MUHIMU, MISINGI YA MWELEKEO WA
SHUGHULI ZA SERIKALI NA SERA ZA KITAIFA

SEHEMU YA KWANZA
MALENGO MAKUU
RASIMU YA PILI YA KATIBA Katiba inayopendekezwa Mapungufu Maoni
Malengo Makuu.
10.-(1) Lengo Kuu la Katiba hii ni kulinda, kuimarisha na
kudumisha haki, udugu, amani, umoja na utengamano wa wananchi wa Jamhuri ya Muungano kwa kuzingatia ustawi wa wananchi na kujenga
Taifa huru lenye demokrasia, utawala bora, maendeleo endelevu na kujitegemea. 11(1)Lengo la Katiba hii ni kulinda, kuimarisha na kudumisha haki, usawa, udugu, amani, umoja na utangamano wa wananchi wa Jamhuri ya Muungano kwa kuzingatia ustawi wa wananchi na kujenga Taifa huru lenye demokrasia, utawala bora, maendeleo endelevu na kujitegemea. Kuna tofauti na rasimu ya Tume- ibara hii ni ya 11 badala ya ibara ya 10, na pia kuna mabadiliko ya kiuandishi ambapo Inatamkwa tu ‘lengo la Katiba’ bila kuonesha umuhimu wake
Pia imeongeza neno – usawa. Ibara hii yapaswa isomeke… Lengo KUU la Katiba ni …
Kwani kwa kutokuweka wazi lengo neno lengo kuu ni kuwanyima fursa za wananchi kutambua mambo ya msingi ya Taifa lao kupitia Katiba.
10 (2) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (1), lengo hilo
kuu litaendelezwa na kuimarishwa katika nyanja zote kuu,
ikijumuisha nyanja za kisiasa, kiuchumi, kijamii, kiutamaduni na
kimazingira. (2) Bila kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (1), lengo hilo kuu litaendelezwa na kuimarishwa katika nyanja zote kuu, ikijumuisha nyanja za kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.
KIP imeondoa mazingira katika malengo makuu ya Taifa
Pia ila kama ilivyo kwenye rasimu ya tume – Neno Nyanja kuu halijafafanuliwa Mazingira lirudishwe katika mojawapo ya malengo makuu
Maneno Nyanja zote kuu inabidi zifafanuliwe –
10(3) Katika kutekeleza malengo ya Taifa ya:
……….. Ibara ya 10(3) imebadilishwa na kusogezwa mbele
(3) Bunge litatunga sheria itakayofafanua juu ya utekelezaji wa malengo muhimu kwa mujibu wa Katiba hii. Kuna mabadiliko ambapo kwa mujibu wa Rasimu ya bunge Maalum – sasa kuna sharti kuwa Bunge kuachiwa kutunga sheria bila kuwekewa mipaka kunaweza kuhatarisha masharti ya ibara hii Sentensi ianze na maneneo ‘bila kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (1) nay a (2) …..
SEHEMU YA PILI
MALENGO YA KISIASA

12.-(1) Lengo la Katiba hii kisiasa ni kudumisha demokrasia na kuondoa ubaguzi wa aina zote. Lengo la kisiasa la taifa makini siyo tu kudumisha demokrasia na kuondoa ubaguzi kuna zaidi ya hapo– mfano uwajibikaji; uwazi; uzalendo nk. Ibara hii inatoa maelezo finyu kuhusu malengo ya taifa letu kisiasa. Ibara hii ibaki kama ilivyoko katika mapendekezo ya Tume.
Japo kuwa malengo ya kisiasa yamepewa uzito mkubwa. Hii siyo nzuri sana kwa sababu yamelenga kuwanufaisha wachache.
10 (3) Katika kutekeleza malengo ya Taifa ya: (a) kisiasa, Serikali itachukua hatua zinazofaa ili – (2) Katika kuhakikisha utekelezaji wa lengo hilo, Serikali itachukua hatua zifuatazo:
(i) kuhakikisha kuwa inazuia, inapinga na kuondoa dhuluma, vitisho, ubaguzi, unyanyasaji, rushwa, uonevu na upendeleo miongoni mwa wananchi kwa misingi ya itikadi, asili ya mtu, sehemu anayotoka, nasaba, kabila, jinsi, dini au imani yake; (a) kuhakikisha kuwa inazuia …….na kuondoa dhuluma, vitisho, ubaguzi, unyanyasaji, rushwa, uonevu na upendeleo miongoni mwa wananchi kwa misingi ya itikadi, asili ya mtu, sehemu anayotoka, nasaba, kabila, jinsi, dini au imani yake; Neno ‘kupinga’ limeondolewa – Serikali inawajibu sio tu wa kuzuia na kuondoa bali pia wa kupinga maovu dhidi ya watu wake Neno ‘kupinga’ liongezewe kati ya maneno ‘inazuia; na kuondoa

Pia kuwepo upatanisho wa kisarufi isomeke inazuia, inapinga na inaondoa ….
(ii) kuhakikisha uwepo wa amani na kujenga utamadun wa kuenzi, kuheshimu na kudumisha amani, umoja na utengamano, ushirikiano na uvumilivu wa kisiasa kwa adhumuni ya kukuza maendeleo ya kijamii na kiuchumi;
(b) kuhakikisha kuwepo kwa amani na utulivu na kujenga utamaduni wa kuenzi, kuheshimu na kudumisha uzalendo, amani, umoja, utangamano, ushirikiano na uvumilivu wa kisiasa kwa madhumuni ya kukuza maendeleo ya kijamii na kiuchumi; na Neno jipya la ‘uzalendo’ limeongezewa Uzalendo ni matokeo ya kuwepo kwa amani, umoja, haki ……
(iii) kuhakikisha uwepo wa ulinzi, usalama na ustawi wa watu na mali zao, na kuepuka kufanya jambo lolote litakalohatarisha au kwenda kinyume na lengo hilo;
(c) Kuhakikisha kuwepo kwa usalama na ustawi wa watu na mali zao.
Kuna mabadiliko ambapo – Ibara hii imepunguza maneno – na kuepuka kufanya jambo lolote litakalo hatarisha au kwenda kinyume na lengo hilo Maneno hayo yarudishwe kwenye hiyo ibara; inaonesha kama vile waandishi walikuwa wakiepuka uwajibikaji.
SEHEMU YA TATU
MALENGO YA KIUCHUMI, KIJAMII NA KIUTAMADUNI
13.-(1) Lengo la Katiba hii kiuchumi ni kujenga uchumi wa kisasa utakaowezesha wananchi na Taifa kujitegemea kwa kuzingatia matumizi ya elimu ya sayansi na teknolojia katika nyanja zote za uzalishaji mali kwa kuhimiza mapinduzi ya kilimo, ufugaji na uvuvi, mapinduzi ya viwanda na kujenga sekta muhimu ya nishati, mawasiliano na miundo mbinu. Ibara hii haijaeleza kama njia kuu za uchumi zitakuwa wapi Ibara hii iseme kuwa njia kuu zote za uchumi zitamilikiwa na umma na zitaufaidisha umma wa watanzania
10(3)(c) kiuchumi, Serikali inachukua hatua zinazofaa ili –
(2) Katika kuhakikisha utekelezaji wa lengo hilo, Serikali itachukua hatua zifuatazo:
(i) kuwaletea wananchi maisha bora kwa kuondoa umaskini;
IMEFUTWA Rasimu ya Bunge maalum imeondoa 10(3)(c)(i) Katika ibara hii jukumu la kuwaletea wananchi maisha bora kwa kuondoa umasikini limefutwa Ibara hii irejeshe jukumu la kuwaletea wananchi wa Tanzania maisha bora kwa kuondoa umasikini
Vifungu vyote katika rasimu ya katiba ibara ya 10(3)(c) virudishwe kama vilivyo
(ix) kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa fursa na nafasi za wazi kwa watu wote na kuanzisha shughuli za kiuchumi na kukuza mazingira yaliyo bora kwa ajili ya kuhamasisha sekta binafsi katika uchumi; haionekani
(x) kuhakikisha kuwa kila mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi anapata fursa ya kufanya kazi, kwa maana ya kufanya shughuli yoyote halali inayompatia kipato; IMEFUTWA Ibara irudishwe kwani taifa haliwezi kuendelea ikiwa watu wake hawatajali kazi.
(xiii) kuwezesha na kuendeleza matumizi ya sayansi na teknolojia na kukuza ubunifu katika shughuli za kiuchumi na maendeleo ya Taifa kwa jumla; (a) kuweka na kutekeleza mpango mkakati wa kutoa elimu ya kisasa yenye kusisitiza ubunifu, sayansi na teknolojia kuanzia ngazi ya msingi, sekondari, ufundi na amali hadi vyuo vikuu na katika shughuli za uchumi na maendeleo ya Taifa kwa ujumla; Maneno ya kisiasa kama ‘mpango mkakati’ yanaonesha kuendelezwa kwa ahadi zisizotekelezwa
(iii) kuweka mazingira bora kwa ajili ya kuanzisha na kuendeleza vyombo vya uwakilishi wa wakulima, wafugaji na wavuvi; (b) kuimarisha na kujenga uwezo wa vyama vya ushirika ili viwe vyombo madhubuti vya kueneza maarifa, mbinu na zana bora za kisasa katika kilimo, ufugaji na uvuvi ili kuongeza tija katika uzalishaji, kutoa mikopo, kutafuta na kuendeleza masoko ya mazao yao; Imejumuisha iii); v); vi); vii) Pamoja na kujumuisha huku, bado ibara hizi zimepoteza msisitizo uliokuwepo kwenye rasimu ya tume
(vi) kuweka mazingira bora ya uzalishaji wa mazao kwa wakulima, wafugaji na wavuvi, utafutaji na uendelezaji wa masoko ya mazao yao;
(vii) kuweka utaratibu mzuri wa upangaji na usimamiaji wa mizania ya bei za mazao na pembejeo;
(viii) kuimarisha na kuendeleza uwekezaji wa ndani, upatikanaji wa pembejeo za kilimo, maeneo ya ufugaji na vifaa vya uvuvi;
(c) kuweka utaratibu wa kujenga viwanda mama, viwanda vya kati na viwanda vidogo vitakavyosindika na kuchakata bidhaa za kilimo, ufugaji, uvuvi na madini ili kuziongezea thamani kwa ajili ya mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi; Mpya Serikali inaepuka kuwajibika kwa kutumia lugha rahisi isiyo na masharti – mfano ‘kuweka utaratibu’ badala yake ingesomeka kuwa Serikali itajenga voiwanda vya kati na vidogo na kuhimiza wananchi pia kuvijenga ……kuweka utaratibu ni jambo moja lakini kujenga ndilo jambo la manufaa zaidi
(v) kuweka mazingira bora kwa ajili ya kukuza kilimo, ufugaji na uvuvi kwa kuhakikisha kuwa wakulima, wafugaji na wavuvi wanakuwa na ardhi na nyenzo kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao; (d) kuhakikisha kuwa wakulima, wafugaji na wavuvi wanakuwa na ardhi na nyenzo kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao katika kukuza mazingira yaliyo bora kwa ajili ya kuhamasisha sekta binafsi katika uchumi, upangaji na usimamizi wa mizania ya bei za mazao na pembejeo; Imeandikwa upya Imeandika haki za wakulima, wafugaji na wavuvi
(iv) kuweka mazingira bora ya kufanya biashara na kukuza fursa za uwekezaji; (e) kuweka mazingira bora ya kufanya biashara na kukuza fursa za uwekezaji; Imebaki kama ilivyo Hata hivyo – katiba ingepaswa kuwalinda wananchi dhidi ya sera mbovu za uwekezaji hususan zile zinazopora rasilimali za taifa na zile zinazonyanyasa wananachi
(xi) kuhamasisha uwekezaji wa pamoja baina ya raia na wasio raia katika miundombinu ya uchumi, uvunaji wa rasilimali na maliasili za Taifa; (f) kuhamasisha uwekezaji wa pamoja baina ya raia na wasio raia katika miundombinu ya uchumi, uvunaji wa rasilimali na maliasili za Taifa; Imebaki kama ilivyo Kifungu kiseme kuwa katika uwekezaaji wowote wa pamoja baina ya raia na mgeni – raia wa tananzania atamiliki asilimia 60 ya mradi
Pili Kifungu kiwe wazi kuwa ni marufuku kwa wageni – kama watu binafsi au hata kama wamejisajili kama kampuni kumiliki ardhi hapa Tanzania – wanaweza kuwa na kibali cha kutumia ardhi lakini siyo kumiliki
(ii) kuhakikishakwamba shughuli za Serikali zinatekelezwa kwa njia ambazo zitahakikisha kuwa utajiri wa Taifa unaendelezwa, unahifadhiwa na unatumiwa kwa manufaa ya wananchi wote kwa jumla na pia kuzuia mtu kumnyonya mtu mwingine; (g) kuhakikisha kwamba shughuli za Serikali zinatekelezwa kwa njia ambazo utajiri wa Taifa unatumiwa kwa manufaa ya wananchi wote na kuweka mazingira yatakayochochea maendeleo linganifu na kuwawezesha wananchi kuondokana na umaskini; na Jukumu la kuendeleza na kuhifadhi utajiri limeondolewa – Neno maendeleo linganifu halijafafanuliwa
Maneno – pia kuzuia mtu kumnyonya mtu mwingine yameondolewa! Utajiri usioendelezwa na kuhifadhiwa hauna tija. Matumizi pasopo wajibu ni sawa na ufujaji wa utajiri wa taifa. Ni vema utajiri huo ukawekewa misingi ya uendelevu p- sustainability
(xii) kuweka utaratibu wa usimamizi wa kiuchumi na uandaaji wa mipango, kuwezesha malengo ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu kutekelezwa; (h) kuweka utaratibu wa usimamizi na udhibiti wa huduma za kiuchumi na kijamii ili kuwezesha ushindani wenye haki na ubora wa viwango vya huduma zinazotolewa ili kuwalinda wananchi. Ibara imefanyiwa barekebisho Ni sahihi kutamka wazi kuwa Serikali isimamie na kudhibiti huduma za kiuchumi pia itamke kuwa haki za mtumiaji/mlaji zinalindwa

14.-(1) Lengo la Katiba hii kijamii ni kujenga jamii yenye ustawi na uwezo wa kushiriki katika shughuli za kimaendeleo katika nyanja mbalimbali.
Ibara hii haiendani na sera ya mambo ya nje ya taifa – imeangalia maendeleo ya ndani tu
Pia haijaangali msingi wa jamii yoyote ambao ni familia Ibara imuandae mtanzania kuweza kutoa ushindani wa dhati kimataifa
Pia ibara itoe msisitizo kwa heshma na ulinzi wa familia kama ngazi muhimu zaidi katika jamii yoyote ya kiungwana
10(3)(b)kijamii, Serikali inachukua hatua zinazofaa ili – (2) Katika utekelezaji wa lengo hilo, Serikali itachukua hatua zinazofaa ili:
(i) kuhakikisha kwamba heshima ya binadamu inahifadhiwa na kudumishwa kwa kufuata mila, desturi na Kanuni za Tangazo la Dunia kuhusu Haki za Binadamu na mikataba mingine ya kimataifa iliyoridhiwa na Tanzania; (a) kuhakikisha kwamba heshima ya binadamu inahifadhiwa na kudumishwa kwa kufuata mila, desturi na Kanuni za Tangazo la Dunia kuhusu Haki za Binadamu na mikataba mingine ya kimataifa iliyoridhiwa na Jamhuri ya Muungano; Kuna mabadiliko TZ vz JM Ni vema kukawa na mtiririko sawia – consistency – ikiwa ni kutumia Jamhuri ya Muungano au ni kutumia Tanzania
(ii) kuhakikisha kwamba Serikali na vyombo vyake vyote vya umma vinatoa nafasi na fursa zilizo sawa kwa raia wote, bila ya kujali itikadi, jinsi, rangi, kabila, dini, nasaba, hali ya mtu au mahali alipo; (b) kuhakikisha kwamba Serikali na vyombo vyake vyote vya umma vinatoa nafasi na fursa sawa kwa raia wote, bila ubaguzi; Mabadiliko yamefanyika ambapo Neno ubaguzi ni la jumla sana Maneno katika ibara ya 10(3)(b)(ii) ya Rasimu ya Pili yarudiwe kama yalivyo
Kujenga utamaduni wa kuwepo ushirikiano, maelewano na maridhiano, uvumilivu na kuheshimu mila desturi na imani ya dini ya kila mtu imehamishwa Irudishwe haraka mana hii inhusu sana utengamano wa jamii pampoja na kuwa imepelekwa kwenye malengo ya kiutamaduni
(iv) kuhakikisha kuwa msaada na hifadhi ya jamii inatolewa kwa watu wasiojiweza, wazee, wagonjwa, watoto na watu wenye ulemavu; (c) kuhakikisha kuwa huduma na hifadhi ya jamii inatolewa kwa watu wasiojiweza, wazee, watoto na watu wenye ulemavu; Kuna badiliko ambapo wangonjwa wameondolewa Waandishi hawakujiuliza – mbona kuna Bima ya Afya Tanzania?
(v) kuwezesha upatikanaji na utoaji wa huduma ya msaada wa kisheria kwa wananchi wasiokuwa na uwezo wa kumudu gharama za uwakili; (d) kuwezesha upatikanaji na utoaji wa huduma ya msaada wa kisheria kwa wananchi wasiokuwa na uwezo wa kumudu gharama za mawakili; Hakuna badiliko
(vi) kuweka utaratibu unaofaa kwa ajili ya kufanikisha utekelezaji wa haki ya mtu kujipatia elimu na kuwa huru kupata fursa sawa ya kutafuta elimu katika fani anayoipenda hadi kufikia upeo wowote kulingana na stahili na uwezo wake; (e) kuweka utaratibu unaofaa kwa ajili ya kufanikisha utekelezaji wa haki ya mtu kujipatia elimu na kuwa huru kupata fursa sawa ya kutafuta elimu katika fani anayoipenda. Imefuta kufikia upeo wowote kulingana na stajili na uwezo wake Maneno husika yarudishwe
(f) kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora ya afya kwa watu wote ikiwa ni pamoja na afya ya uzazi salama; Hii ni mpya
(g) kuweka mazingira yatakayowezesha wasanii kutumia fursa zilizopo na vipaji vyao katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na mabadiliko katika jamii; na Hii ni mpya
(h) kuweka utaratibu na mazingira yanayofaa kwa ajili ya kukuza na kuendeleza michezo nchini. Hii ni mpya

15.-(1) Lengo la Katiba hii kiutamaduni ni kukuza, kudumisha na kuhifadhi lugha ya Kiswahili, urithi wa asili na utamaduni wa wananchi.
Ibara hii imepangwa upya – Kiswahili kimepewa kipaumbele kuliko nyanja nyingine za utamaduni Lengo hili lina mtazamo finyu kuwa utamaduni ni lugha tu! Ibara zote katika Rasimu ya Pili zirejeshwe
(d) kiutamaduni, Serikali itachukua hatua zinazofaa ili – (2) Katika kuhakikisha utekelezaji wa lengo hilo, Serikali itachukua hatua zinazofaa ili:
(iii) kutambua, kulinda na kuendeleza lugha ya Kiswahili; na
(a) kulinda na kuendeleza lugha ya Kiswahili; Neno kutambua limefutwa
(i) kulinda na kuhifadhi urithi wa asili, malikale na sehemu zenye umuhimu wa kihistoria au kidini ili kuepuka uharibifu, udhalilishaji, wizi au utoroshaji nje ya nchi; (b) kulinda na kuhifadhi urithi wa asili, malikale na sehemu zenye umuhimu wa kihistoria ili kuepuka uharibifu, wizi au utoroshaji nje ya nchi; Udhalilishaji limefutwa
(ii) kulinda, kuhifadhi na kuendeleza tamaduni za watu wa jamii mbalimbali ambazo zinaendeleza na kukuza utu na hadhi yao kwa namna ambayo haikinzani na Malengo Muhimu, Misingi ya Mwelekeo wa Shughuli za Serikali na Sera za Kitaifa; (c) kulinda, kuhifadhi na kuendeleza utamaduni wa jamii mbalimbali; na Maneno ‘ambazo zinaendeleza na kukuza utu na hadhi yao kwa namna ambayo haikinzani na Malengo Muhimu, Misingi ya Mwelekeo wa Shughuli za Serikali na Sera za Kitaifa;’ yamefutwa
(d) kujenga utamaduni wa kuwepo ushirikiano, maelewano, maridhiano, uvumilivu na kuheshimu mila, desturi na imani ya dini ya kila mtu. Imehamishiwa hapa

SEHEMU YA NNE – UTAFITI, DIRA YA MAENDELEO, MIPANGO NA
UTEKELEZAJI WA MALENGO YA TAIFA – mpya

16. Katika kuweka mipango ya Taifa, Serikali itatoa kipaumbele kwenye shughuli za utafiti na maendeleo kwa lengo la kupata taarifa zitakazowezesha upatikanaji wa maendeleo ya kiuchumi nchini. Mpya
17.-(1) Kutakuwa na Dira ya Taifa ya Maendeleo katika nyanja mbalimbali kwa kuzingatia haki na wajibu wa kila raia kupata maendeleo. Mpya Hakuna uhakika ikiwa dira ya maendeleo itakuwa inahusu mambo yasiyo ya muungano yanayosimamiwa na Zanzibar
(2) Katika kutekeleza ibara ndogo ya (1), Mamlaka za Serikali zitaweka mipango ya kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo. Mpya
18.-(1) Kutakuwa na Tume ya Mipango ya Jamhuri ya Muungano itakayoitwa “Tume ya Mipango” ambayo itakuwa ndicho chombo cha juu cha kupanga na kusimamia utekelezaji wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya Taifa. Mpya – Bali Mipango siyo suala la muungano Tume hii siyo ya muungano – ilipaswa kuhusika na Katiba ya Tanganyika na Katiba ya Zanzibar
(2) Bunge litatunga sheria kwa ajili ya utekelezaji wa Ibara hii.
11.-(1) Malengo ya Taifa yaliyoainishwa ndani ya Katiba hii
yatakuwa ni mwongozo kwa Serikali na mamlaka nyingine na kwa kila mwananchi katika matumizi au kutafsiri masharti ya Katiba hii
au sheria nyingine yoyote na katika utekelezaji wa uamuzi wa kisera
kwa madhumuni ya kujenga jamii iliyo bora, huru na makini. 19.-(1) Malengo ya Taifa yaliyoainishwa ndani ya Katiba hii yatakuwa ni mwongozo kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na kwa wananchi katika matumizi au kutafsiri masharti ya Katiba hii au sheria nyingine yoyote au katika utekelezaji wa maamuzi ya kisera kwa madhumuni ya kujenga jamii iliyo bora, huru na makini. Kuna mabadiliko
(2) Serikali itatoa taarifa Bungeni si chini ya mara moja katika kila mwaka, kuhusu hatua zilizochukuliwa na mamlaka ya nchi ili kuhakikisha utekelezaji wa malengo ya Taifa yaliyoainishwa
katika Katiba hii. (2) Serikali ya Jamhuri ya Muungano itawasilisha katika Bunge mara moja kwa mwaka, taarifa ya hatua ilizozichukua katika utekelezaji wa malengo ya Taifa. Maneno si chini ya mara moja na ili kuhakikisha utekelezaji limefutwa Uwajibikaji ni jambo la msingi – maandishi ya rasimu ya tume yarudishwe ili mamlaka ziwajibikwe kwa wawakilishi wa wananchi kueleza jinsi wanavyotekeleza malengo ya kitaifa
20.-(1) Kutakuwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia ambayo itakuwa ni chombo cha usimamizi, uratibu, utafiti na ushauri kuhusu masuala yote yanayohusu sayansi na teknolojia nchini. Mpya – na sayansi siyo suala la muungano Tume hii siyo ya muungano – ilipaswa kuhusika na Katiba ya Tanganyika na Katiba ya Zanzibar
(2) Muundo, majukumu na mamlaka ya Tume ya Sayansi na Teknolojia yatakuwa kama yatakavyoainishwa na sheria itakayotungwa na Bunge.
21.-(1) Bila kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (2), Serikali, vyombo vyake vyote na watu au mamlaka yoyote yenye kutekeleza madaraka ya utawala, kutunga sheria au ya utoaji haki, vitakuwa na jukumu na wajibu wa kuzingatia na kutekeleza masharti yote ya Sura hii. Mpya Hakuna utaratibu ulioppo ikiwa vyombo vya upande mmoja wa muungano vitakataa kutii mashariti ya ibara hii kama kuna hatua zozote vinaweza kuchukuliwa
(2) Masharti ya Sura hii hayatatiliwa nguvu ya kisheria na Mahakama yoyote. Mahakama yoyote nchini haitakuwa na uwezo wa kuamua juu ya suala kama kutenda au kukosa kutenda jambo kwa mtu au mahakama yoyote au kama sheria au hukumu yoyote inaambatana na masharti ya Sura hii. Imebadilishwa – Rasimu ya tume Masharti kutotiliwa nguvu na mahakama kunafanya vifungu hivi kutokuwa na maana yoyote kwa mwananchi Katika ulimwengu wa sasa kuna uwezekano mkubwa wa kutilia nguvu mashharti yoytote ya kikatiba kuhusu haki za kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.

SEHEMU YA TANO – SERA YA MAMBO YA NJE

12.-(1) Sera ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Muungano
inalenga na kuzingatia maslahi ya Taifa na mamlaka kamili ya nchi
na kwamba sera hiyo inatekelezwa kwa uwazi ili – 22.-(1) Sera ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Muungano inalenga na kuzingatia maslahi ya Taifa na mamlaka kamili ya nchi na kwamba sera hiyo inatekelezwa kwa uwazi ili: Hakuna badiliko

(a) kukuza ujirani mwema, ushirikiano wa kikanda na wa
kimataifa; (a) kukuza ujirani mwema, ushirikiano wa kikanda na wa kimataifa; Hakuna badiliko

(b) kukuza maendeleo na ushirikiano wa kiuchumi wenye tija kwa Taifa na raia wake; (b) kukuza maendeleo na ushirikiano wa kiuchumi wenye tija kwa Taifa na raia wake; Hakuna badiliko

(c) kuunga mkono na kuendeleza jitihada za kuimarisha Umoja wa Afrika, sera ya kutofungamana na upande wowote na ushirikiano na nchi zinazostawi duniani;
(c) kuunga mkono na kuendeleza jitihada za kuimarisha Umoja wa Afrika, sera ya kutofungamana na upande wowote, na kukuza ushirikiano na nchi zinazoendelea duniani;
Hakuna badiliko

(d) kuheshimu sheria za kimataifa; (d) kuheshimu sheria za kimataifa; Hakuna badiliko
(e) kuzingatia mikataba ya kimataifa na ya kikanda yenye maslahi kwa Jamhuri ya Muungano na kutatua migogoro ya kimataifa kwa njia ya majadiliano, usuluhishi, maridhiano au mahakama; (e) kuzingatia mikataba ya kimataifa na ya kikanda yenye maslahi kwa Jamhuri ya Muungano na kutatua migogoro ya kimataifa kwa njia ya majadiliano, usuluhishi, maridhiano au mahakama; Hakuna badiliko

(f) kukuza uzingatiaji wa haki za binadamu na uhuru wa watu; (f) kukuza, kulinda na kuzingatia haki za binadamu na uhuru wa watu; Hakuna badiliko

(g) kupambana na makosa ya kimataifa ya jinai; na (g) kupambana na makosa ya kimataifa ya jinai; na Hakuna badiliko

(h) kuheshimu uhuru wa mataifa mengine. (h) Kuheshimu uhuru wa mataifa mengine. Hakuna badiliko
Kudumisha heshma, amani na uhuru wa taifa la Tanzania nje ya nchi na kuheshimu uhuru wa mataifa mengine
(2) Bunge litatunga sheria, pamoja na mambo mengine,
itakayoelekeza na kusimamia utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje (2) Bunge litatunga sheria, pamoja na mambo mengine, itakayoelekeza na kusimamia utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje.
Hakuna badiliko

Kuna haja ya kuongeza neno (h)….Bunge litatunga sheria pamoja na manbo mengine: kulinda heshima, amani na utulivu na uhureu wa Taifa nje ya nchi na kuheshimu nchi nyingine.

SURA YA TATU.
UCHAMBUZI WA SURA YA 3 NA 4 KATIKA RASIMU YA PILI NA KATIBA INAYOPENDEKEZWA
SURA YA 4
IBARA
RASIMU YA PILI
KATIBA INAYOPENDEKEZWA
28……………. Tofauti Maoni
14(1)(c)
Haushushi hadhi ofisi anayofanyia kazi 29(1)(c) Hauruhusu matumizi ya ofisi ya umma kwa maslai binafsi Kuna tofauti za kiuandishi katika katiba – Kuweka maana ya kufanana katiba katiba pendekezwa na rasimu
– Mambo yote waliyoyatoa kuhusu mamlaka ya wananchi na kuweka mamlaka ya sheria, yamepoteza nguvu na uwezo wa wananchi.
15(1)(2) Zawadi katika utumishi wa umma, kuwa itakuwa ni zawadi ya jamhuri wa Muungano
Zawadi ni kitu chochote chenye thamani atakachopewa kiongozi wa umma katika utekelezaji wa shughuri za umma 29(2)(a) Bunge litatunga sheria itakayo tafsiri neno zawadi, aina,thamani, kiwango na uhifadhi wa zawadi Mantinki ya ibara ya 15 na 29(a)(a) ni tofauti – Zawadi ni mali ya nani? Na sio tafsiri ya neno zawadi
– Tafasili ya neon zawadi imebinywa.

16 Akaunti za nje na mikopo kiongozi wa umma hatofungua na kumilik akaunti za benki nje ya nchi isipokuwa kwa namna sheria za nchi zinaruhusu 29(2)(b)Bunge litatunga sheria kuweka masharti Rasimu iliweka marufuku ya moja kwa moja, lakini katiba pendekezwa imeondoa marufuku hiyo na kusema itatungwa sheria kuweka masharti Mapendekezo ya rasimu ni mazuri na yazingatiwe kwa kuweka mafuruku ya moja kwa moja ili kupunguza mianya ya rushwa na ufisadi
17 Kutangaza mali ndani ya siku thelathini baada ya kupata uongozi 29(2)(c)Bunge litatunga sheria ya kuweka masharti ya kumtaka kiongozi wa umma kutoa tamko la mali na
thamani yake, madeni yake pamoja na ya mwenza wake wa ndoa
(2) Kwa madhumuni ya Katiba hii, Bunge litatunga sheria itakayoweka, pamoja na mambo mengine:

(a) tafsiri ya neno zawadi, aina, thamani, kiwango na uhifadhi wa zawadi ambayo kiongozi anapokea wakati akitekeleza majukumu yake;

(b) masharti ya kufungua akaunti za nje kwa kiongozi wa umma;

(c) masharti ya kumtaka kiongozi wa umma kutoa tamko la mali na thamani yake, madeni yake pamoja na ya mwenza wake wa ndoa na mtoto wake aliye chini ya umri wa miaka kumi na nane;

(d) masharti ya kuzuia kiongozi wa umma kutoshiriki kufanya uamuzi wa jambo au shughuli yoyote ambayo ana maslahi nayo yeye binafsi, mwenza wake wa ndoa, mtoto wake, jamaa au rafiki yake au mtu yeyote wa karibu;

(e) masharti ya matumizi ya mali ya umma;

(f) utaratibu wa utwaaji wa mali za kiongozi wa umma zinazopatikana kwa kukiuka sheria;

(g) utaratibu wa kumwajibisha kiongozi wa umma aliyekiuka maadili na miiko ya uongozi wa umma; na

Katiba pendekezwa haijatoa muda Ni vema suala la muda likazingatiwa ili kumnyima nafasi kiongozi wa umma kujilibikizia mali
21(2)(b)(1) Dhana ya uwajibikaji wa pamoja kwa viongozi wanaohusika Katiba pendekezwa haijazungumzia Lazima katiba pendekezwa isisitize dhana ya uwajibikaji wa pamoja wa viongozi
(iii)Kujilimbikizia mali kinyume na sheria, kusema uongo au kutoa taarifa zisizo na ukweli (iv), kutenganisha biashara na shughuri binafsi na masuala yanayohusiana na uongozi,

Ibara ya 21(1) na (2) ya rasimu ya Pili 30.-(1) Bila kuathiri masharti ya Katiba hii, kiongozi wa umma ataheshimu na kutii maadili ya uongozi wa umma na miiko ya uongozi.
(2) Bunge litatunga sheria itakayoainisha:

(a) miiko inayopaswa kuzingatiwa na viongozi wa umma;

(b) utaratibu wa kumuondoa kazini kiongozi wa umma kutokana na kuvunja miiko na kukiuka maadili ya uongozi wa umma;

(c) vitendo ambavyo kiongozi wa umma hapaswi kuvitenda; na

(d) ngazi au orodha ya viongozi wa umma wanaofungwa na Sehemu hii.

Mamlaka ya wananchi kuwawajibisha viongozi imetolewa Kuna tofauti kubwa za kiuwandishi katika ibara hizi
Katiba haijaweka miiko ya uongozi.
Inaleta ubaguzi na matabaka.

31.-(1) Mtumishi wa umma aliye katika ajira ya kudumu hataruhusiwa kuingia katika ajira nyingine yoyote ya kudumu yenye malipo ya mshahara.
(2) Mtumishi wa umma haruhusiwi kugombea au kuteuliwa kushika nafasi ya madaraka katika chama cha siasa au nafasi ya madaraka ya kisiasa ya aina yoyote chini ya Katiba hii.
(3) Endapo mtumishi wa umma anayefungwa na masharti ya Ibara ya 30(2)(d) ataamua kugombea au atateuliwa kushika:

(a) nafasi ya madaraka ya kisiasa ya aina yoyote chini ya Katiba hii; au

(b) uongozi wa ngazi yoyote katika chama cha siasa,

mtumishi huyo atachukuliwa kuwa utumishi wake umekoma tangu siku ya kuteuliwa kuwa mgombea au kuteuliwa kushika nafasi ya madaraka ya kisiasa au uongozi katika chama cha siasa.

22 23 (1)-Ardhi ndiyo rasilimali kuu ya nchi kiuchumi itakayotumiwa kwa vizazi vya sasa na vijavyo 10(3)(c) (ii) Rasimu inazungumzia kuendeleza na kuhifadhi utajiri wa taifa kwa manufaa ya wote, kuzuia kumyonya mtu mwingine Ardhi siyo jambo la Muungano
Kusisitiza kutumia rasilimali kwa kizazi cha sasa na kijacho, bila kuweka mikakati sitahiki na kuruhusu watu kuchukua ardhi, ni kuifanya ardhi iwe ya watu wachache.

22(2)(a)Haki ya kumiliki ardhi ni kwa raia wa Tanzania pekee Rasimu haijasisitiza jambo hili Mapendekezo ya katiba pendekezwa yaendelee kuungwa mkono kwa hili
22 (2)(b)Asiye raia wa Tanzania kutumia ardhi kwa ajiri ya uwekezaji tuu 10(3)(c)(viii)Uwekezaji wa ndani, pia uwekezaji wa pamoja wa raia na wasio raia 10(3)(c)(xi) Katiba pendekezwa haijazungumzia aina hizi za uwekezaji yaani uwekezaji wa ndani na uwekezaji wa pamoja
Makundi mbalimbali ya kijamii yamepewa fursa kama vile wakulima, wavuvi, wafugaji na makundi madogo Wametajwa katika rasimu Mapendekezo ya katiba pendekezwa yaungwe mkono kwenye hili
Usawa wa kijinsia katika kumili ardhi, Wanawake sawa na wanaume katika kumiliki ardhi
Rasimu haijataja -Mapendekezo ya katiba pendekezwa yaungwe mkono
-Mwanamke kumiliki ardhi ni kuwaadaa wananchi
23 Bunge kutunga sheria itakayosimamia matumizi bora ya ardhi Rasimu inazungumzia kuweka utaratibu mzuri/ kuweka mazingira bora Mapendekezo ya katiba pendekezwa yaungwe mkono
24 Utaratibu bora wa kulipa fidia ambapo eneo litachukuliwa Rasimu haijazungumzia Mapendekezo ya katiba pendekezwa yaungwe mkono
Maliasiri zote kama gesi, mafuta na madini ni mali ya umma zitatumika kwa vizazi vya sasa na vijavyo, serikali zitaweza utaratibu mzuri wa usimamizi Rasimu haijazungumzia Mapendekezo ya katiba pendekezwa yaungwe mkono

25 Kusimamia mazingira taasisi za umma na kiraia zitawajibika katika kusimamia Rasimu ipo kimya Katiba pendekezwa iungwe mkono
26 Haki ya kumiliki rasilimali za kijenetiki ni kwa watanzania pekee kwa manufaa ya taifa lao Rasimu haijazungumza Katiba pendekezwa iungwe mkono kwy hili
Mizania ya bei za mazao na pembejeo Hakuna Kuweka mizania ya bei ya mazao na pembejeo
147(1) Tume ya utumishi wa Bunge ambayo itakuwa na wajumbe wafuatao
(a) Spika wa Bunge la Jamhuri wa ambaye atakuwa mwenyekiti
(b) Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ambaye atakuwa makamu mwenyekiti
(c) Wabunge wawili wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, mmoja kutoka kila upande wa Jamhuri ya Muungano
(d) Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na
(e) Mwanasheria mkuu 155(1) Tume ya Utumishi wa Bunge ambayo itakuwa na wajumbe wafuatao
(a) Spika wa Bunge ambaye atakuwa mwenyekiti
(b) Naibu spika wa Bunge ambaye atakuwa makamu mwenyekiti
(c) Waziri mwenye dhamana ya Bunge
(d) Wabunge watano wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa kuzingatia uwakilishi wa pande mbili za muungano
(e) Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Rasimu inazungumzia wabunge wawili na Mwanasheria mkuu wa serikali na Katiba inapendekeza uwepo wa Waziri mwenye dhamana ya Bunge na wabunge watano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Uwepo wa wabunge wa tano ni mzuri kuongeza uwakilishi Lakini bado haijulikani lengo la kuwepo kwa waziri mwenye dhamana ya Bunge ni nini?

IBARA RASIMU YA PILI KATIBA INAYOPENDEKEZWA TOFAUTI MAONI
Sura ya Nne Imekuwa sura ya Tano

Ibara 23/32 Jina: SURA YA NNE: HAKI ZA BINADAMU, WAJIBU WA RAIA NA MAMALAKA ZA NCHI

Sehenu ya Kwanza Haki za binadamu: Ibara ya 23 hadi 48

Uhuru, utu na
usawa wa
binadamu

23(1) Binadamu wote huzaliwa huru na wote ni sawa

(2)Kila mtu anayo haki ya kuheshimiwa, kutambuliwa na
kuthaminiwa utu wake Jina SURA YA TANO
HAKI ZA BINADAMU, WAJIBU WA RAIA, JAMII NA MAMLAKA ZA NCHI
Sehemu ya Kwanza
Haki za Binadamu
Ibara ya 32 had 59

Uhuru, utu na
usawa wa
binadamu

32.-(1) Binadamu wote huzaliwa huru na wote ni sawa.

(2) Kila mtu anayo haki ya kuheshimiwa, kutambuliwa na
kuthaminiwa utu wake 1. Jina la Sura limeongezewa neno Wajibu wa Raia, Jamii na Mamlaka ya nchi.

1. Ibara ya 23 ambayo ni ibara ya 32 ya Katiba pendekezwa havinatofauti kabisa Jamii imepewa wajibu katika suala la haki za Binadamu

Ibara 24 /33 24. Kila mtu anayo haki ya kuishi na kupata hifadhi ya maisha yake
kutoka katika Serikali na jamii kwa mujibu wa sheria za nchi 33. Kila mtu anayo haki ya kuishi na kupata hifadhi ya maisha yake
kutoka katika Serikali na jamii kwa mujibu wa sheria za nchi. Hakuna tofauti Bado haikidhi matwakwa ya haki ya kuishi kwani haitoi haki madhubuti kwa vile haki hii itatolea kwa mujibu wa sheria
Ibara 25/ 34 Marufuku kuhusu Ubaguzi
25(1)
Watu wote ni sawa Mbele ya sheria na wanayo haki ya kulindwa na kupata
haki sawa mbele ya sheria.
25(2) Ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu, mamlaka ya nchi
au mamlaka yoyote inayotekeleza madaraka yake chini ya sheria yoyote au
katika kutekeleza kazi au shughuli yoyote ya mamlaka ya nchi

(3) Ni marufuku kwa sheria yoyote iliyotungwa na mamlaka yoyote
katika Jamhuri ya Muungano kuweka sharti lolote ambalo ni la ubaguzi ama
wa dhahiri au kwa taathira yake
(4) Haki ya raia, wajibu na maslahi ya kila mtu na jumuiya ya watu
yatalindwa na kuamuliwa na mahakama na vyombo vinginevyo vya mamlaka ya
nchi vilivyowekwa kwa mujibu wa sheria za nchi.
(5) Kwa madhumuni ya masharti ya Ibara hii, neno “kubagua” maana
yake ni kutimiza utashi, haki au mahitaji mengineyo kwa watu mbalimbali
kwa kuzingatia utaifa wao, kabila, mahali walipotokea, maoni yao ya
kisiasa, rangi, dini, jinsi, ulemavu au hali yao katika jamii kwa namna ambayo
watu wa aina fulani wanatendewa au kuhesabiwa kuwa dhaifu au duni na
kuwekewa vikwazo au masharti ya vipingamizi ambapo watu wa aina nyingine
wanatendewa tofauti au wanapewa fursa au faida iliyoko nje ya masharti au sifa
za lazima.
(6) Neno “kubagua” lilivyotumiwa katika ibara ndogo ya (2),
halitafafanuliwa kwa namna ambayo itaizuia mamlaka ya nchi kuchukua hatua
za makusudi zenye lengo la kurekebisha matatizo mahsusi katika jamii.
(7) Kwa madhumuni ya kuhakikisha usawa mbele ya sheria,
mamlaka ya nchi itaweka utaratibu unaofaa na unaozingatia misingi
kwamba:
(a) wakati haki na wajibu kwa mtu yeyote vinapohitajika
kufanyiwa uamuzi na mahakama au mamlaka nyingine
inayohusika, basi mtu huyo atakuwa na haki ya kupewa fursa ya
kusikilizwa kwa ukamilifu na pia atakuwa na haki ya kukata
rufaa au kupata nafuu nyingine ya kisheria kutokana na uamuzi wa
mahakama au mamlaka nyingine inayohusika;
(b) ni marufuku kwa mtu aliyeshtakiwa kwa kosa la jinai
kutendewa kama mtu aliyehukumiwa kwa kutenda kosa hilo
isipokuwa tu kama itathibitika mahakamani kuwa anayo hatia ya
kutenda kosa hilo;
(c) ni marufuku kwa mtu kuadhibiwa kwa sababu ya kitendo
chochote ambacho wakati alipotenda kitendo hicho hakikuwa ni
kosa chini ya sheria;
(d) ni marufuku kwa mtu kupewa adhabu ambayo ni kubwa kuliko
adhabu iliyokuwapo wakati kosa linalohusika lilipotendeka;
(e) kwa ajili ya kuhifadhi haki ya usawa wa binadamu, heshima ya mtu
na faragha italindwa katika shughuli zote zinazohusu upelelezi
wa tuhuma na uendeshaji wa mashtaka ya jinai na katika shughuli
nyingine ambazo mtu anakuwa katika kizuizi cha mamlaka ya
nchi au katika kuhakikisha utekelezaji wa adhabu; na
(f) ni marufuku kwa mtu kuteswa, kufanyiwa ukatili au kupewa adhabu
zinazotweza au kudhalilisha utu wake.
Haki ya
Kutobaguliwa
34.-(1) Watu wote ni sawa na wanayo haki ya kulindwa na kupata
haki sawa mbele ya sheria.

(2) Ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu, mamlaka ya nchi
au mamlaka yoyote inayotekeleza madaraka yake chini ya sheria yoyote au
katika kutekeleza kazi au shughuli yoyote ya mamlaka ya nchi
(3) Ni marufuku kwa sheria yoyote iliyotungwa na mamlaka yoyote
katika Jamhuri ya Muungano kuweka sharti lolote ambalo ni la ubaguzi ama
wa dhahiri au kwa taathira yake.

(4) Haki ya raia, wajibu na maslahi ya kila mtu na jumuiya ya watu
yatalindwa na kuamuliwa na mahakama na vyombo vinginevyo vya mamlaka ya
nchi vilivyowekwa kwa mujibu wa sheria za nchi.
(5) Kwa madhumuni ya masharti ya Ibara hii, neno “kubagua” maana
yake ni kutimiza utashi, haki au mahitaji mengineyo kwa watu mbalimbali
kwa kuzingatia utaifa wao, kabila, mahali walipotokea, maoni yao ya
kisiasa, rangi, dini, jinsi, ulemavu au hali yao katika jamii kwa namna ambayo
watu wa aina fulani wanatendewa au kuhesabiwa kuwa dhaifu au duni na
kuwekewa vikwazo au masharti ya vipingamizi ambapo watu wa aina nyingine
wanatendewa tofauti au wanapewa fursa au faida iliyoko nje ya masharti au sifa
za lazima.
(6) Neno “kubagua” lilivyotumiwa katika ibara ndogo ya (2),
halitafafanuliwa kwa namna ambayo itaizuia mamlaka ya nchi kuchukua hatua
za makusudi zenye lengo la kurekebisha matatizo mahsusi katika jamii.
(7) Kwa madhumuni ya kuhakikisha usawa mbele ya sheria,
mamlaka ya nchi itaweka utaratibu unaofaa na unaozingatia misingi
kwamba:
(a) wakati haki na wajibu kwa mtu yeyote vinapohitajika
kufanyiwa uamuzi na mahakama au mamlaka nyingine
inayohusika, basi mtu huyo atakuwa na haki ya kupewa fursa ya
kusikilizwa kwa ukamilifu na pia atakuwa na haki ya kukata
rufaa au kupata nafuu nyingine ya kisheria kutokana na uamuzi wa
mahakama au mamlaka nyingine inayohusika;
(b) ni marufuku kwa mtu aliyeshtakiwa kwa kosa la jinai
kutendewa kama mtu aliyehukumiwa kwa kutenda kosa hilo
isipokuwa tu kama itathibitika mahakamani kuwa anayo hatia ya
kutenda kosa hilo;
(c) ni marufuku kwa mtu kuadhibiwa kwa sababu ya kitendo
chochote ambacho wakati alipotenda kitendo hicho hakikuwa ni
kosa chini ya sheria;
(d) ni marufuku kwa mtu kupewa adhabu ambayo ni kubwa kuliko
adhabu iliyokuwapo wakati kosa linalohusika lilipotendeka;
(e) kwa ajili ya kuhifadhi haki ya usawa wa binadamu, heshima ya mtu
na faragha italindwa katika shughuli zote zinazohusu upelelezi
wa tuhuma na uendeshaji wa mashtaka ya jinai na katika shughuli
nyingine ambazo mtu anakuwa katika kizuizi cha mamlaka ya
nchi au katika kuhakikisha utekelezaji wa adhabu; na
(f) ni marufuku kwa mtu kuteswa, kufanyiwa ukatili au kupewa adhabu
zinazotweza au kudhalilisha utu wake.
. Kichwa kimebadilika na kutoa haki na si marufuku

Ibara ya 25(1) inatoa msisitizo wa usawa mbele ya sheria na kulindwa na sheria

Katika ibara 34(7)(e) Neno lililokua itahifadhiwa katika rasimu limebadilikika na kuwa Italindwa Ni vyema kuweka haki zaidi ya kinyume chake

Tofauti ya kimaneno inaweza kubadili mantiki kuhusu usawa mbele ya sheria lakini madhara si makubwa kwani usawa upo
Tofauti hii si ya msingi sana kwa kuwa wameepuka kutumia neno hifadhi mara mbili
Ibara ya 26/35 Haki ya kutokuwa
mtumwa

26-(1) Kila mtu ana haki ya kutotendewa au kutotumikishwa kama
mtumwa, kutofanyishwa kazi za kulazimishwa au kutweza, na kwa msingi huo, nimarufuku kwa mtu:
(a) kufanywa au kutendewa kama mtumwa;
(b)kulazimimishwa kufanya kazi bila hiyari yake;au
(c)kusafirishwa kwa nia ya kufanywa mtumwa, kibiashara au kwa faida
ya mtu mwingine.
(2) Biashara haramu ya kusafirisha na kuuza binadamu ni
marufuku katika Jamhuri ya Muungano
Haki ya kutokuwa
mtumwa

35.-(1) Kila mtu ana haki ya kutotendewa au kutotumikishwa kama
mtumwa, kutofanyishwa kazi za kulazimishwa au kutweza, na kwa msingi huo, ni

(a) kufanywa au kutendewa kama mtumwa;
(b) kusafirishwa kwa nia ya kufanywa mtumwa, kibiashara au kwa faida
ya mtu mwingine.
(2) Biashara haramu ya kusafirisha na kuuza binadamu ni
marufuku katika Jamhuri ya Muungano
Kipengele cha 26(1) (b)
Kimeondolewa kilichohusu kulazimishwa kufanya kazi bila hiyari yake Hapakuwa na haja yakuondoa kipengeke hiki kwani kinasisitiza hali ya kazi za kulazimishwa ambazo ni aina y a utumwa usio dhahiri
Ibara 27/35 Uhuru wa mtu
binafsi
27.(1) Kila mtu anayo haki ya kuwa huru na kuishi akiwa mtu huru.
(2) Kwa madhumuni ya kuhifadhi haki ya mtu kuwa huru na kuishi
kwa uhuru, itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kukamatwa, kufungwa,
kufungiwa, kuwekwa kizuizini, kuhamishwa kwa nguvu au kunyang’anywa
uhuru wake vinginevyo, isipokuwa tu katika:
(a) hali na kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria; au
(b) kutekeleza hukumu, amri au adhabu iliyotolewa na
Mahakama kutokana na shauri au kutiwa hatiani kwa kosa la jinai. Uhuru wa mtu
binafsi

36.-(1) Kila mtu anayo haki ya kuwa huru na kuishi akiwa mtu huru.
(2) Kwa madhumuni ya kuhifadhi haki ya mtu kuwa huru na kuishi
kwa uhuru, itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kukamatwa, kufungwa,
kufungiwa, kuwekwa kizuizini, kuhamishwa kwa nguvu au kunyang’anywa
uhuru wake vinginevyo, isipokuwa tu katika:
(a) hali na kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria; au
(b) kutekeleza hukumu, amri au adhabu iliyotolewa na
mahakama kutokana na shauri au kutiwa hatiani kwa kosa la jinai. Kimsingi hakuna tofauti Hakuna tofauti ya kimantiki
Ibara
28/37 Haki ya Faragha na usalama wa mtu

28.-(1) Kila mtu anastahili kuheshimiwa na kupata hifadhi kwa nafsi
yake, maisha yake binafsi na familia yake na nyumbani kwake, na pia
heshima na hifadhi ya maskani yake na mawasiliano yake ya binafsi.
(2) Kwa madhumuni ya kuhifadhi haki ya mtu kwa mujibu wa ibara
hii, mamlaka ya nchi itaweka utaratibu wa sheria kuhusu hali, namna na kiasi ambacho haki ya mtu ya faragha na ya usalama wa nafsi yake, mali na maskani yake, yanaweza kuingiliwa bila kuathiri masharti ya Ibara hii.
kuingiliwa bila kuathiri masharti ya Ibara hii.

Haki ya faragha na usalama wa mtu

37.-(1) Kila mtu anastahili kuheshimiwa na kupata hifadhi kwa nafsi
yake, maisha yake binafsi na familia yake na unyumba wake, na pia
heshima na hifadhi ya maskani yake na mawasiliano yake ya binafsi.
(2) Kwa madhumuni ya kuhifadhi haki ya mtu kwa mujibu wa ibara
hii, mamlaka ya nchi itaweka utaratibu wa sheria kuhusu hali, namna na kiasi ambacho haki ya mtu ya faragha na ya usalama wa nafsi yake, mali na maskani yake, yanaweza kuingiliwa bila kuathiri masharti ya Ibara hii.
kuingiliwa bila kuathiri masharti ya Ibara hii. Ipo tofauti ya neno Nyumbai kwake limebadilishwa na kuw aunyumba wake Hakuna tatizo la kimsingi katika badiliko hili kwani nyumbani kwake ni kama maskani yake ambalo limeshatumika na unyumba ni sual la faragha kama haki inayotolewa ya faragha
29/38 Uhuru wa mtu kwenda anakotaka
29.-(1) Kila raia anayo haki ya kwenda kokote katika Jamhuri ya
Muungano na kuishi katika sehemu yoyote, kutoka nje ya nchi na
kuingia, na pia haki ya kutoshurutishwa kuhama au kufukuzwa kutoka katika
Jamhuri ya Muungano
2) Kitendo chochote halali au sheria yoyote yenye madhumuni ya:
(a) kupunguza uhuru wa mtu kwenda anakotaka na kumweka chini
ya ulinzi au kifungoni; au
(b) kuweka mipaka kwa matumizi ya uhuru wa mtu kwenda
anakotaka ili-
(i) kutekeleza hukumu au amri ya mahakama;
(ii) kumlazimisha kutimiza kwanza wajibu wowote anaotakiwa na
sheria nyingine kuutimiza; au iii) kulinda maslahi ya umma kwa jumla au kuhifadhi maslahi
mahsusi au maslahi ya sehemu fulani ya umma,
hakitahesabiwa au sheria hiyo haitahesabiwa kuwa ni kinyume
cha masharti ya Ibara hii.

Uhuru wa mtu
kwenda anakotaka
38.-(1) Kila raia anayo haki ya kwenda kokote katika Jamhuri ya
Muungano na kuishi katika sehemu yoyote, kutoka nje ya nchi na
kuingia, na pia haki ya kutoshurutishwa kuhama au kufukuzwa kutoka katika
Jamhuri ya Muungano.
(2) Kitendo chochote halali au sheria yoyote yenye madhumuni ya:
(a) kupunguza uhuru wa mtu kwenda anakotaka na kumweka chini
ya ulinzi au kifungoni; au
(b) kuweka mipaka kwa matumizi ya uhuru wa mtu kwenda
anakotaka ili-
(i) kutekeleza hukumu au amri ya mahakama;
(ii) kumlazimisha kutimiza kwanza wajibu wowote anaotakiwa na
sheria nyingine kuutimiza; au
(iii) kulinda maslahi ya umma kwa jumla au kuhifadhi maslahi
mahsusi au maslahi ya sehemu fulani ya umma,
hakitahesabiwa au sheria hiyo haitahesabiwa kuwa ni kinyume
cha masharti ya Ibara hii.

Hakuna tofauti Hakuta tofauti za kimsingi.
Ibara ya 30/39 Uhuru wa
maoni
30-(1) Kila mtu:
(a) ana haki na uhuru wa:
(i) kuwa na maoni na ii) kufanya mawasiliano na kutoingiliwa katika mawasiliano yake;
(iii) masuala mengine muhimu kwa jamii.
(2) Utekelezaji wa haki zilizoainishwa katika ibara ndogo ya(1) Utajumuisha wajibu muhimu kwa wananachi na wajibu huo unaweza kupunguza haki hizo kutokana na
(a) Vita au machafuko ya kisiasa;au
(b) propaganda kuhusu vita ushawishi wa chuki kwa misingi ya rangi, ukabila, jinsi, itikadi , dini au masual yoyote yanayoweza kuleta madhara kwa Taifa
Uhuru wa
maoni
39.-(1) Kila mtu:
(a) ana haki na uhuru wa:
(i) kuwa na maoni na ii) kufanya mawasiliano na kutoingiliwa katika mawasiliano yake; (iii) masuala mengine muhimu kwa jamii.

(2) Utekelezaji wa haki zilizoainishwa katika ibara ndogo ya (1),
hautajumuisha kuchochea vita, machafuko na chuki kwa misingi ya rangi,
ukabila, jinsi, itikadi, dini au masuala yoyote yanayoweza kuleta madhara kwa
Taifa. Kifungu kidogo cha 2 kimebadilishwa na kuwekwa kwa njia ya uhasi zaidi kwani Rasimu ilikua inaweka mipaka ya haki ya uhuru wa maoni kwa kutoa wajibu.
Pia imetoa dhima ya haki na hili linaleta tatizo la kipimo cha haki na uhuru husika Katiba inayopendekzwa imekosa dhima ya sehemu hii kwa kuweka katazo tu nadhani pengine wangeongeza katazo hili juu ya mipaka iliyokua katika rasimu
31/40 Uhuru wa vyombo vya habari

31.-(1) Kila mtu ana haki na uhuru wa:
(a) kutafuta, kupata, kutumia na kusambaza habari na taarifa sahihi; na
(b) kuanzisha vyombo vya habari na njia nyingine za upashanaji wa habari bila kujali mipaka ya nchi
(2) Vyombo vya habari vitakuwa huru na vitakuwa na:
(a) haki ya kupata, kutumia na kusambaza habari na taarifa kwa wananchi; na
(b) wajibu wa:
(i) kusambaza habari na taarifa kwa wananchi;
(ii) kuheshimu na kulinda utu, heshima, uhuru na staha yawananchi dhidi ya habari na taarifa wanazozitumia,wanazozitayarisha na kuzisambaza.
( 3) Serikali na taasisi zake, asasi za kiraia,na watu binafsi watakuwa na wajibu wa kutoa habari kwa umma juu ya shughuli na utekelezaji wa shughuli zao., kwa kadri
itakavyohitajika

Uhuru wa vyombo vya habari

40.-(1) Kila mtu ana haki na uhuru wa:
(a) kutafuta, kupata, kutumia na kusambaza habari na taarifa sahihi; na
(b) kuanzisha vyombo vya habari na njia nyingine za upashanaji wa
habari
(2) Vyombo vya habari vitakuwa huru na vitakuwa na:
(a) haki ya kupata, kutumia na kusambaza habari na taarifa
wanazozipata;
(b) wajibu wa:
(i) kusambaza habari na taarifa sahihi na za ukweli kwa wananchi;
(ii) kuheshimu faragha na kulinda utu, heshima, uhuru na staha ya
wananchi katika habari na taarifa wanazozitumia,wanazozitayarisha na kuzisambaza;
(iii) kuzingatia miiko ya taaluma ya uandishi na utangazaji wa
habari.
(3) Serikali na taasisi zake, zitakuwa na wajibu wa kutoa taarifa kwa
umma kuhusu shughuli za Serikali na utekelezaji wake, kwa kadri
itakavyohitajika.
(4) Bunge litatunga sheria kwa ajili ya kusimamia na kulinda:
(a) haki, wajibu na uhuru wa vyombo vya habari na waandishi wa
habari; na
(b) habari na taarifa kwa madhumuni ya usalama wa Taifa, amani, haki,
staha na uhuru wa watu wengine 1. Ibara ya 40 ya katiba -P imeondoa maneno Bila kujali mipaka ya nchi yaliyokuwepo katika ibara ya 31 ya Rasimu ikitoa haki ya kuanzisha vyombo vya habari na njia nyingine za upashanaji wa habari
2. Katiba inayopendekezwa imeongeza maneno katika ibara yake ya 40 (2)(b) katika wajibu wa kusambaza taarifa ziwe ni sahihi na za ukweli
3. Ibara ya 40(2) (b)(ii) Katiba -P neno Faragha limeongezwa kuheshimu faragha
4. Ibara ya 40(2) (b) imeongeza kifungu kidogo (iii) ambacho hakikuwepo kwenye Rasimu “kuzingatia miiko ya taaluma ya uandishi na utangazaji wa
Habari”.
5.Katikakifungu kidogo ch 3 cha rasimu kilichokua kikitoa wajibu wa kuto ahabari kwa serikali na taasisi zake pamoja ja asasi za kiraia na watu binafsi Katiba P imeondoa wajibu huo kwa makundi hayo na kuuwacha kwa serikali na taasisi zake tu
Pia kigezo cha neon uchochezi kinaweza kutumiwa vibaya na watawala kwa ajili ya kubinya uhuru. Mfano: kisingizio cha neon intelijensia 1. Kwa kuondoa maneno “Bila kujali mipaka ya nchi” uhuru uliotolewa unaweza kuminywa ili uwe ni wa mipaka ya nchi hii tu wakati haki hii inavuka mipaka(Angalia Haki kama ilivyo katika ICCPR]

2. Kwa kuongeza maneno hayo ya usahihi na ukweli inawezakuwa ni vyema kuwa wananchi waweze kupata taarifa sahihi na za ukweli lakini hii pia inaweza kuweka mipaka iwapo watawala wataamua kuitumia vinginevyo maana ukweli na usahihi unaweza kuwa kwa anayeukubali au vinginevyo Hili litahitaji tafsiri ili kuondoa mkanaganyiko au kutumika vibaya

3. Neno faragha lililoongezwa katika Ibara ya 40(2)(b)(ii) Limeongeza ulinzi wa haki katika kutoa wajibu kwa vyombo vya habari

4. Kifungu kilichoongezwa cha kuzingatia miiko ya taaluma ya uandishi na utangaziji wa habari kimeboresha wajibu walio nao vyombo vya habari
5. Si sahihi kuondoa wajibu kwa Asasi za kiraia na kwa mtu binafsi anyeweza kuwa na taarifa kwani wajibu wa kuto ataarifa si wa serikai pekee.

Ibara ya 32/41 Uhuru wa imani ya dini

32.-(1) Kila mtu ana uhuru wa mawazo, imani na uchaguzi
katika mambo ya imani ya dini na anao uhuru pia wa kubadilisha dini, imani
yake au kutokuwa na imani na dini.
(2) Kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni
huru na jambo la hiari kwa mtu binafsi ilimradi hakiuki sheria za nchi.
(3) Shughuli ya uendeshaji wa jumuiya za dini itakuwa nje ya shughuli
za mamlaka ya Serikali.
(4) Hifadhi ya haki zilizotajwa katika Ibara hii itakuwa chini ya taratibu zilikaowekwa na sheria ambazo ni muhimu katika jamii ya kidemokrasia kwa
ajili ya usalama, amani, maadili na umoja wa jamii na wana wa kitaifa na
vitasimamiwa kwa utaratibu utakaoainishwa kwenye sheria za nchi.
(5) Ni marufuku kwa mtu, kikundi au taasisi ya dini kutumia uhuru wa
kutangaza dini kwa namna ambayo italeta uvunjifu wa amani kujenga chuki au
kuchochea vurugu na ghasia kwa madai ya kutetea imani au dini hiyo.
(6) Dini na imani ya dini haitatumika kwa namna yoyote itakayowagawa
wananchi, kuleta uhasama au kuharibu amani miongoni mwa wananchi
(7) Neno “dini” kama lilivyotumika katika Ibara hii litatafsiriwa kwamba
maana yake ni pamoja na madhehebu ya dini, na maneno mengine yanayanayofanana
au kuambatana na neno hilo nayo yatatafsiriwa kwa maana hiyo.
Uhuru wa imani ya
dini
41.-(1) Kila mtu ana uhuru wa mawazo, dhamiri, imani na uchaguzi
katika mambo ya imani ya dini na anao uhuru pia wa kubadilisha dini, imani
yake au kutokuwa na imani na dini.
(2) Kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni
huru na jambo la hiari kwa mtu binafsi ilimradi hakiuki sheria za nchi.
(3) Shughuli ya uendeshaji wa jumuiya za dini itakuwa nje ya shughuli
za mamlaka ya Serikali.
(4) Hifadhi ya haki zilizotajwa katika Ibara hii itakuwa chini ya utaratibu
utakaowekwa na sheria ambazo ni muhimu katika jamii ya kidemokrasia kwa
ajili ya usalama, amani, maadili na umoja wa jamii na wa kitaifa na
vitasimamiwa kwa utaratibu utakaoainishwa kwenye sheria za nchi.
(5) Ni marufuku kwa mtu, kikundi au taasisi ya dini kutumia uhuru wa
kutangaza dini kwa namna ambayo italeta uvunjifu wa amani, kujenga chuki au
kuchochea vurugu na ghasia kwa madai ya kutetea imani au dini hiyo.
(6) Dini na imani ya dini haitatumika kwa namna yoyote itakayowagawa
wananchi, kuleta uhasama au uvunjifu wa amani miongoni mwa wananchi.
(7) Neno “dini” kama lilivyotumika katika Ibara hii litatafsiriwa kwamba
maana yake ni pamoja na madhehebu ya dini, na maneno mengine yanayanayofanana
au kuambatana na neno hilo nayo yatatafsiriwa kwa maana hiyo.

KatikaIbara hii Katiba inatuyopendekezwa Ibara ya 41(1) inayolingana na ibara ya rasimu ya 32 (1) imeongeza neno dhamiri ambalo halikuwepo katika Rasimu
Katka kifungu cha 4 cha ibara ya 40 ya Katiba pendekezwa wamebadili nafsi ya maneno kutoka wingi kwenda umoja badala ya taratibu zilizowekwa wamesema utaratibu utakaowekwa

Kifungu kidogo cha 6 katika katiba Pendekezwa kimebadili maneno katika kifungu kidogo cha 6 katika rasimu yaliyokuwa yanasomeka au kuharibu amani miongoni mwa wananchi na kuwa au uvunjifu wa amani miongoni mwa wananchi
Kuongezeka kwa neno dhamiri ni vizuri tu kwani hakii hiyo imepewa ongezeko
Badiliko la wingi kwenda umoja hali madhara yoyote
Mabadiliko katika ibara ndogo ya 6 si ya msingi sana kubadilisha maana
33/42 Uhuru wa mtu
kujumuika na
kushirikiana na
wengine

33. Kila mtu anastahili kuwa huru bila kuathiri sheria za nchi, kukutana na
watu wengine kwa hiario yake na kwa amani,kujumuika na kushirikiana na watu wengine , kutoa mawazo hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au maslahi yake au
kujiunga na vyama au mashirika yaliyoanzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi
au kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo.
Uhuru wa mtu
kujumuika na
kushirikiana na
wengine

42. Kila mtu anastahili kuwa huru bila kuathiri sheria za nchi, kukutana na
watu wengine kwa hiario yake na kwa amani,kujumuika na kushirikiana na watu wengine , kutoa mawazo hadharani, na kwa ajili hiyo kuanzisha au
kujiunga na vyama au mashirika yaliyoanzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi
au kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo.
. Katia ibara hii ya 42 kunatofauti ndogoya lugha kutoka maneno na hasa zaidi kuwa Kwa ajili hiyo Badiliko hili halina madhara yoyote kimantiki au kimaudhui
34/42 Uhuru wa kushiriki
shughuli za umma

34.-(1) Kila raia wa Jamhuri ya Muungano ana haki ya kushiriki katika
shughuli za utawala wa nchi kwa hiari yake, ama moja kwa moja au kupitia
wawakilishi waliochaguliwa na wananchi, kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa
kwa mujibu wa sheria za nchi.
2) Kila raia wa ana haki na uhuru wa kushiriki
kwa ukamilifu katika kufikia uamuzi juu ya mambo yanayomhusu yeye na , maisha
yake au yanayolihusu Taifa
Uhuru wa kushiriki
shughuli za
utawala wa nchi

43.-(1) Kila raia wa Jamhuri ya Muungano ana haki ya kushiriki katika
shughuli za utawala wa nchi kwa hiari yake, ama moja kwa moja au kupitia
wawakilishi waliochaguliwa na wananchi, kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa
kwa mujibu wa sheria za nchi.
(2) Kila raia wa Jamhuri ya Muungano ana haki na uhuru wa kushiriki
kwa ukamilifu katika kufikia uamuzi juu ya mambo yanayomhusu , maisha
yake au yanayolihusu Taifa.
Kuna badiliko katika haki inayotolewa Rasimu ilitoa haki kushiriki shughuli za umma Katiba P inatoa haki ya kushiriki shughuli za utawala wa nchi tu na siyo shughuli za umma. Badiliko katika haki linaondolea wananchi haki ya ushiriki mpana katika umma inaaki haki yakushiriki katika utawala tu

Inaonekana wameangalia maudhui ya ibara hiyo lakini kwa kichwa hicho ibara ndogo ya pili inayoangalia ushiriki wa uamuzi juu ya mambo yanayohusu maisha yake au yanayolihusu taifa yanakuwa yamebanwa katika utawala tu.
Uhuru wa kushiriki shughuli za umma umebanwa sana, na hivyo kutambua shusguli za kiutawala tu.
35/44 Haki ya kufanaya kazi

35(1) Kila mtu ana haki ya kufanya kazi ya kuajiriwa au kujiajiri
mwenyewe
(2) Kila raia ana haki na fursa sawa kushika nafasi yoyote ya kazi,
uongozi au shughuli yoyote iliyo chini ya mamlaka ya nchi. Haki ya kufanya kazi

44.-(1) Kila mtu ana haki ya kufanya kazi ya kuajiriwa au kujiajiri
mwenyewe na kupata ujira unaostahili.
(2) Kila raia ana haki na fursa sawa kushika nafasi yoyote ya kazi,
uongozi au shughuli yoyote iliyo chini ya mamlaka ya nchi. Katiba Inayopendekezwa katika ibara ya 44 (1) imeongeza maneno kupata ujira unaostahili Hapakuwa na haja ya kuongeza maneno hayo kwani ujira upo hasa kwa waajiriwa na wafanya kazi za ajira na haki hiyo ipo katika ibara ya 36/45
36/45 Haki za Wafanya kazi na Waajiriwa

36.-(1) Kila mfanyakazi ana haki zifuatazo:
(a) kufanya kazi bila ubaguzi wa aina yoyote;
(b) kupata ujira na malipo halali kulingana na kiasi na sifa za kazi
anayofanya;
(c) kuunda au kujiunga na chama cha wafanyakazi mahali pa kazi;
(d) kushiriki katika shughuli za chama cha wafanyakazi; na
(2) Kila chama cha waajiri na wafanyakazi kitakuwa na haki ya:
(a) kuamua kuhusu uongozi, programu na shughuli zake; na
(b) kuanzisha, kujiunga na kusimamia shirikisho lao.
(3) Kila chama cha wafanyakazi kitakuwa na haki ya kufanya majadiliano
ya pamoja na mwajiri na kuingia mikataba ya hali bora ya kazi.
(4) Bunge litatunga sheria itakayoweka masharti kuhusu haki
za wafanyakazi na utaratibu utakaowezesha wafanyakazi kutumia haki zao Haki za Wafanya kazi na Waajiriwa

45.-(1) Kila mfanyakazi ana haki zifuatazo:
(a) kufanya kazi bila ubaguzi wa aina yoyote;
(b) kupata ujira na malipo halali kulingana na kiasi na sifa za kazi
anayofanya;
(c) kuunda au kujiunga na chama cha wafanyakazi mahali pa kazi;
(d) kushiriki katika shughuli za chama cha wafanyakazi; na
(e) kupata hifadhi ya afya na usalama wake katika sehemu ya kazi.
(2) Kila mwajiri ana haki ya kujiunga na chama cha waajiri, shirikisho au
Mashirikisho ya sekta yake.
(3) Kila chama cha waajiri na wafanyakazi kitakuwa na haki ya:
(a) kuamua kuhusu uongozi, programu na shughuli zake; na
(b) kuanzisha, kujiunga na kusimamia shirikisho lao.
(4) Kila chama cha wafanyakazi kitakuwa na haki ya kufanya majadiliano
ya pamoja na mwajiri na kuingia mikataba ya hali bora ya kazi.
(5) Bunge litatunga sheria itakayoweka masharti kuhusu haki za waajiri
na wafanyakazi na utaratibu utakaowezesha waajiri na wafanyakazi kutumia haki zao. Kimeongezwa kipengele (e) katika ibara ya 45 (1) inayotoa haki ya kupata hifadhi ya afya na usalama wake katika sehemu ya kazi.
Ongezeko jingine ni Ibara ndogo ya 2 inayotoa haki kwa mwajiri kujiunga katika chama Hili niongezeko chanya kwani ni muhimu sana kuwa na haki hii kwa waajiriwa
Ongezeko la ibara ndogo ya kwanza hali na shida

Hapakuwa na haja sana ya wajili kujiunga katika chama. Kwani inafahamika bayana kuwa siku zote wamekuwa huru, waliotakiwa kukazaniwa ni Waajiliwa.
Haki ya hifadhi ya afya na usala wake, viwekewe mkakati na kipao mbele ili kunusuru afya na maisha ya waajiliwa

Ibara ya /46 Haki za wakulima, wafugaji, wavuvi na wachimbaji madini

Ibara hii ni mpya haikuwepo kwenye Rasimu Haki za wakulima, wafugaji, wavuvi na wachimbaji madini

46.-(1) Wakulima, wafugaji, wavuvi na wachimbaji madini watakuwa na haki ya:

(a) kumiliki, kutumia na kuendeleza ardhi kwa ajili ya shughuli zao;

(b) kupata taarifa na maarifa kwa lengo la kuboresha kilimo, ufugaji, uvuvi na uchimbaji madini;

(c) kumiliki na kunufaika na rasilimali za kijenetiki za kilimo, mifugo na uvuvi; na

(d) kushirikishwa katika utungaji wa sera, sheria na mipango mbalimbali inayohusu shughuli zao.

(2) Mamlaka ya nchi itaweka utaratibu wa kisheria kwa madhumuni ya kubainisha na kutenga maeneo ya ardhi kwa ajili ya matumizi ya kila kundi lililoainishwa katika ibara ndogo ya (1).

Ibara mpya Haiko wazi hasa wachimbaji madini ni wepi kwani kuna wachimbaji wa dogo na wachiimbaji wakubwa, watanzania wengi ni wachimbaji wadogo je haki hii ni kwao au ni kwa wachimbaji wote?
Hii imekaa kisiasa zaidi. Ni haki inayolenga kuteka hisia za makundi ya watu mbalimbali.
Na makundi hayo yaliyoainishwa kwenye ibara hii yana vipao mbele tofauti tofauti.
Ibara ndogo ya 1.(a) haikom wazi kwani mvuvi hamiliki ardhi kwenye shughuli zake za uvuvi.

37/47 Haki ya Kumiliki Mali

37.-(1) Kila mtu anayo haki ya kumiliki mali na hifadhi ya mali yake
aliyonayo kwa mujibu wa sheria za nchi.
(2) Bila kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (1), itakuwa ni marufuku
kwa mtu yeyote kuchukuliwa mali yake kwa madhumuni ya kuitaifisha au
madhumuni mengine bila ya malipo yanayolingana na thamani halisi ya mali hiyo na yatakayotolewa mapema.
(3) Kwa madhumuni ya masharti ya Ibara hii, haki ya umiliki na hifadhi
ya mali haitahusu mali iliyothibitishwa kwamba haikupatikana kwa njia
halali Haki ya Kumiliki Mali

47.-(1) Kila mtu anayo haki ya kumiliki mali na hifadhi ya mali yake
aliyonayo kwa mujibu wa sheria za nchi.
(2) Bila kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (1), itakuwa ni marufuku
kwa mtu yeyote kunyang’anywa mali yake kwa madhumuni ya kuitaifisha au
madhumuni mengine bila idhini ya sheria ambayo inaweka masharti ya kutoa
fidia inayolingana na thamani halisi.
(3) Kwa madhumuni ya masharti ya Ibara hii, haki ya umiliki na hifadhi
ya mali haitahusu mali iliyothibitishwa kwamba haikupatikana kwa njia
halali 1.Kuna badiliko Ibara ya 37(2)y aRasimu ambayo sasa ni Ibara ya 47(2) ya Katiba-P la msamiati kutoka neno Kuchukuliwa kuwa kunyanga’nywa na
2. kimaudhui katika Ibara hiyo hiyo pale ambapo Katiba Imebadili kwa kutaka idhini ya sheria inayoweka masharti ya kutoa fidia inayolingana na thamani halisi badala ya ilivyokua kuweo na malipo yanayolingana na thamani halisi na yatakayotolewa mapema 1. Mabadiliko ya msamiati hayana madhara yeyote.

2. Badiliko ya kimaudhui linaweza kuwa shida pale ambapo sheria haitatungwa mapema na pia kuondoa suala la fidia kulipwa mapema ni tatizo kwani hilo ndilo tatizo kubwa katika ulipaji fidia.

Siyo tu kutwaa bali kwa kulipa fidia sitahiki na kwa wakati sitahiki.
.Ibara ya 38 Haki ya Uraia
Kila raia ana haki ya kutambuliwa uraia wake na kwa madhumuni haya , mamalaka ya nchi itaweka utaratibu wa sheria utakaowezesha wananchi kupata hati ya kuzaliwa, kitambulisho cha uraia wake bila ya upendeleo na ubaguzi wa aina yoyote, na pale inapohitajika, nyaraka za kumwezesha kusafiri Ibara hii imeondolewa kabisa katika hati za haki za binadamu Haipo kabisa Haki ya uraia ni muhimu kutambulika kikatiba na ni haki ya kila raia kuwa nayo na hasa maelekezo ya kuwa na cheti cha kuzaliwa, kitambulisho cha uraia na hati za kusafiria.

Kuondoa hii haki ni kuwakosesha watanzania walio wengi haki hii muhimu na ukitilia maanani mtu anaweza kujikuta akiambiwa si raia kwa vile tu haki hii kama ilivyowekwa kwenye Rasimu haipo

Ibara ya 39/48 Haki ya Mtuhumiwa na Mfungwa

39. -(1) Mtu aliyekamatwa au aliyewekwa kizuizini anayo haki ya:
(a) kuelezwa kwa lugha anayoifahamu au lugha ya alama:
(i) sababu ya kukamatwa kwake;
(ii) haki ya kutokutoa maelezo yoyote; na
(iii) matokeo ya kutoa maelezo;
(b) Kutoa maelezo
(c) kuwasiliana na wakili au mtu mwingine ambaye msaada wake ni
muhimu kwa mtuhumiwa
(d) kutolazimishwa kutoa maelezo ya kukiri kosa ambayo
yatatumika kama ushahidi dhidi yake (e) kupelekwa mahakamani mapema iwezekanavyo.
(2) Mamalaka za nchi zitaweka utaratibu wa sheria utakaowezesha:
(a) Mtuhumiwa kupata nakala ya mashataka yanayomkabili na kumbukumbu ya mwenendo wa mashtaka;
(b) mtuhumiwa au mfungwa kupata nakala ya mwenendo wa mashtaka na hukumu baada ya shauri kukamilika mahakamani; na
(c) mtuhumiwa au mfungwa kufikishwa mahakamni ilikuthibitisha uwepo wake

Haki ya Mtuhumiwa na Mfungwa

48.-(1) Mtu aliyekamatwa au aliyewekwa kizuizini anayo haki ya:
(a) kuelezwa kwa lugha anayoifahamu:
(i) sababu ya kukamatwa kwake;
(ii) haki ya kutokutoa maelezo yoyote; na
(iii) matokeo ya kutoa maelezo;
(b) kuwasiliana na wakili au mtu mwingine ambaye msaada wake ni
muhimu kwa mtuhumiwa;
(c) kutolazimishwa kutoa maelezo ya kukiri kosa ambayo
yatatumika kama ushahidi dhidi yake;
(d) kufikishwa mahakamani mapema iwezekanavyo kama
itakavyoelekezwa katika sheria;
(e) kuwekwa katika mazingira yanayozingatia haki za binadamu.
(2) Mtu anayetumikia kifungo, anayo haki ya:
(a) kuhifadhiwa katika mazingira yanayozingatia haki za binadamu;
(b) kupata nakala ya mwenendo wa mashtaka na nakala ya hukumu kwa
madhumuni ya kukata rufaa;
(c) kuwasiliana na wakili au mtu mwingine ambaye msaada wake ni
muhimu katika kukata rufaa;
(3) Bunge litatunga Sheria itakayoweka utaratibu utakaowezesha:
(a) mtuhumiwa kupata nakala ya mashtaka yanayomkabili;
(b) mtuhumiwa kufikishwa mahakamani na kuomba dhamana kwa
mujibu wa sheria; na
(c) mfungwa kupata kumbukumbu ya nakala ya mashtaka na hukumu
baada ya shauri kukamilika mahakamani.
(4) Kwa ajili ya kuhifadhi haki zilizotajwa katika ibara hii, mamlaka ya
nchi itazingatia masharti ya Ibara ya 33(7)(e) ya Katiba hii. 1. Ibara 39(1) (a) imebadilishwa kwa kuondoa maneno lugha ya alama
2. Kipengele (b) cha ibara ya 39(1) kimeondolewa kabisa

3. Katika ibara hii kipengeke cha (e) kuna mabadiliko ya msamiati neno kupelekwa limebadilika kuwa kufikishwa
3.Pamoja na mabadiliko ya kisarufi pia yapo mabadiliko ya nyongeza ya vifungu na haki.
Kifungu (e) katika ibara hiikimeongeza haki ya mtuhumiwa kuwekwa katika mazingira yanyozingatia haki.
Kifungu cha (2) katika Katiba-P kimeainisha haki (a)ya mfungwa kuhifadhiwa katika mazingira yanayozingatia haki
(b) Kupata mwenendo wa mashataka na nakala ya hukumu
(c) kuwasiliana na wakili u mtu mwingine muhimu katika kukata rufaa
Kipengeke cha (3) Kimeongeza haki ya dhamana kwa mtuhumiwa
Ibara ndogo ya (4) Imetoa msisistizo wa haki zilizotolew kuzingatia haki ya kutokubaguliwa kama ilivyo katika ibara 33(7)(e) ya katiba pendekezi. 1. Waliobadili wanaweza kuona kuwa lugha ya alama ni kama ziada kwa vile imeshasemekana kwa lugha anayoifahamu lakini kwa kufahamu kuwa lugha ya alama haifahamiki sana ni vyema katiba ikiitaja ili kuwa msisistizo kwa vyombo husika.
Lugha ya alama haikuwa sahihi kuitoa kwani watu wenye mahitaji hao nao ni watanzania na wote wanaumuhimu sawa na wengine.
2. Kuondolewa kwa kipengele (b) cha ibara ya 39(1) kunaweza kusiwe na madhara kwani kutoa maelezo inaweza isitafsiriwe kama haki bali wajibu
3. Nyongeza ya kipengele (e) ni uboreshaji wa rasimu kwa kuongeza haki kwa mtuhumiwa.
Mabadiliko yote yaliyofanyiwa katika ibara hii ni ya kuboresha yametofautisha mfungwa na mtuhumiwa kwa kuweka haki za kila mmoja bayana,ila hakiya mtuhumiwa kupata nakala ya mashataka na kumbukumbu y a mwenendo wa mashataka imeondolewa,Hii ni haki muhimu ya mtuhumiwa ambayo isingeondolewa kwani wengi ndipo wanapokiukiwa haki hiyo
Ibara ya 40/49 Haki ya mtu aliye
chini ya ulinzi au
kizuizi

40.-(1) Mtu aliye katika
kizuizi au ulinzi ataendelea kuwa na haki zote
za msingi zilizoainishwa katika Katiba hii kwa kiwango anachostahiki
katika mazingira ya kuwekwa kizuizini au katika ulinzi.
(2) Mtu aliye katika kizuizi au ulinzi ana haki ya kuiomba
mahakama ili mamlaka ya nchi inayomuhifadhi kueleza sababu za yeye
kuwekwa au kuendelea kuwa katika kizuizi au ulinzi.
(3) Raia wa Jamhuri ya Muungano hatapelekwa katika nchi ya nje yoyote
kujibu mashtaka au kufanyiwa mahojiano ya aina yoyote kinyume cha ridhaa
yake, isipokuwa kwa mujibu wa sheria za nchi na mikataba ya kimataifa na wajibu wa nchi katika uhusiano wa kimataifa Haki ya mtu aliye
chini ya ulinzi au
kizuizi

49.-(1) Mtu aliye katika kizuizi au ulinzi ataendelea kuwa na haki zote
za msingi zilizoainishwa katika Katiba hii kwa kiwango anachostahiki
katika mazingira ya kuwekwa kizuizini au katika ulinzi.
(2) Mtu aliye katika kizuizi au ulinzi ana haki ya kuiomba
mahakama ili mamlaka ya nchi inayomuhifadhi kueleza sababu za yeye
kuwekwa au kuendelea kuwa katika kizuizi au ulinzi.
(3) Raia wa Jamhuri ya Muungano hatapelekwa katika nchi ya nje yoyote
kujibu mashtaka au kufanyiwa mahojiano ya aina yoyote kinyume cha ridhaa
yake, isipokuwa kwa mujibu wa sheria za nchi na mikataba ya kimataifa na wajibu wa nchi katika uhusiano wa kimataifa. Hakuna badiliko lolote Iwapo tunapinga sheria ya kuweka kizuizini ibara hii haipaswo jkuwepo kwani inaonekana kutambua uwekwaji kizuizini.Kila mtu anayepatikamana na shutumaapeleke mahakamani kwa utaratibu wa kawaida.

Sheria ya kumweka mtu kizuizini nimbaya sana kwani mara nyingi hutumiwa na watawala kuwakamata watu na kuwaweka kizuizini kwa kusingizia uvunjifu wa amani au usala wan chi, kitu ambacho siyo kweli.

Hivyo ibara hii aitakiwi kuwepo.
Ibara ya 41/50 Uhuru na haki ya
mazingira safi na
salama
41.-(1) Kila mtu anayeishi katika Jamhuri ya Muungano ana haki ya
kuishi katika mazingira safi, salama na ya kiafya.
(2) Haki ya kuishi katika mazingira safi, salama na ya kiafya
inahusisha haki kwa kila mtu kutumia maeneo ya umma au sehemu
mbalimbali za mazingira yaliyotengwa kwa madhumuni ya burudani, elimu,
afya, ibada, utamaduni na shughuli za kiuchumi.
(3) Mtu yeyote anayeishi Tanzania anao wajibu wa kutunza na kuendeleza, mazingira na kutoa taarifa kwa mamlaka za nchi kuhusu
shughuli au jambo lolote ambalo ni la hatari au lina uwezekano mkubwa wa
kuharibu au kuathiri mazingira. Uhuru na haki ya
mazingira safi na
salama
50.-(1) Kila mtu anayeishi katika Jamhuri ya Muungano ana haki ya
kuishi katika mazingira safi, salama na ya kiafya.
(2) Haki ya kuishi katika mazingira safi, salama na ya kiafya
inahusisha haki kwa kila mtu kutumia maeneo ya umma au sehemu
mbalimbali za mazingira yaliyotengwa kwa madhumuni ya burudani, elimu,
afya, ibada, utamaduni na shughuli za kiuchumi.
(3) Mtu yeyote anayeishi Tanzania anao wajibu wa kutunza, kulinda
Na kuhifadhi mazingira na kutoa taarifa kwa mamlaka za nchi kuhusu
shughuli au jambo lolote ambalo ni la hatari au lina uwezekano mkubwa wa
kuharibu au kuathiri mazingira. Katika ibara hii ibara ndogo ya (3) neno kuendeleza limeondolewa na badala yake yamewekwa maneno mawili kulinda na kuhifadhi Mabadiliko haya ni ya kiushindani wa maneno zaidi ya kubadili mantiki ya haki kwani neno lililotangulia Kutunza lina weza kubeba maana ya kulinda na kuhifadhi lakini neno Kuendeleza lina maana tofauti kwani mtu anaweza kutunza bila kuendeleza.
Ibara /51 Haki ya afya na maji safi na salama
Hizi ni haki mpya hazikuwepo katika rasimu Haki ya afya na maji safi na salama
51.-(1) Kila mtu ana haki ya kupata huduma ya afya na maji safi na salama.
(2) Mamlaka ya nchi itahakikisha kwamba huduma zilizorejewa katika ibara ndogo ya (1) zinapatikana kwa urahisi kwa kuzingatia mahitaji ya nchi na rasilimali zilizopo.

Ni haki mpya kabisa Haki hizi zililalamikiwa sana kutokuwepo kwake kwa hiyo imekua vizuri sana kuwa zimewekwa ila kifungu kidogo cha 2 kinaifunga haki hii kwa maneno kuwa zitapatikana kwa urahisi kwa kuzingatia mahitaji na rasilimali zilizopo.

Neno kuzingatia mahitaji ya nchi na rasilimali zilizopo, ina iondolea serikali kuwajibika katika kuhakikisha kuwaletea wananchi haki zao.
Ibara 42/52 Haki ya Elimu na Kujifunza
42.-(1) Kila mtu ana haki ya:
(a) Kupata fursa ya kupata elimu bora bila ya vikwazo
(b) kupata elimu bora ya msingi
inayomtayarisha kikamilifu kuendelea na elimu ya ngazi inayofuatia au kuweka
msingi wa kuanza kujitegemea.
(c) Kupata elimu bora inayotolewa nje ya utaratibu wa umma kwa gharama nafuu
(d) kupata fursa sawa ya kupata elimu ya juu ilimradi ana sifa stahiki kupata elimu hiyo, bila ubaguzi wa aina yoyote
(2) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (1), kila mtu ana haki ya
kuchagua taaluma na ajira anayoitaka kwa mujibu wa elimu yake na ujuzi
alionao.

Haki ya elimu
52.-(1) Kila mtu ana haki ya kupata elimu bora ya msingi
inayomtayarisha kikamilifu kuendelea na elimu ya ngazi inayofuatia au kuweka
msingi wa kuanza kujitegemea.
(2) Kila mtu ana fursa ya kupata elimu ya juu ilimradi ana sifa stahiki.
(3) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (2), kila mtu ana haki ya
kuchagua taaluma na ajira anayoitaka kwa mujibu wa elimu yake na ujuzi
alionao.
(4) Serikali itahakikisha kuwepo kwa mfumo wa elimu unaozingatia
uwezo na mahitaji ya Taifa.

1. Kichwa cha habari kimebadilishwa kwa kuondoa neno Kujifunza imebaki haki ya ELIMU
2. Katiba -P imeacha kifungu katika rasimu kinachotoa haki ya kupata fursa ya kupata elimu bora bila vikwazo
3. Rasimu pendekezwa imeacha kipengele (c) katika rasimu ibara y a41 (1) kinachotoa haki ya kupata elimu bora inayotolewa nje ya utaratibu wa umma kwa gharama nafuu
4. Rasimu -P imeongeza kipengele cha 4 kuwa serikali itazingatia uwezo na mahitaji ya taifa kwenye uwepo wa fumo wa elimu 1. Kwa mujibu wa randama ibara hii iliwekewa haki ya kujifunza kwa kutambua kuwa kuna haja ya kutoa fursa ya kujifunza nje ya mfumo rasmi wa elimu na kuwa elimu haina mwisho ingefaa kufahamukwa nini Katiba pendekezwa imeliacha neno hili
2. Kuondoa kipengekle hiki Katiba Inayopendekezwahaikutilia maanani hali ilivyo ya upatikanaji wa elimu kwani kuna wenye fursa zaidi ya wengine na ndio maan rasimu iliweka haki ya kupata fursa.

3. Kuondoa kipengele kinachotoa haki ya kupata elimu nje ya utaratibu wa umma kwa gharama nafuu hakukuzingatia hali halisi ya shule nje ya mfumo wa umma zinazotoza gharama kubwa sana na kufanya pawepo na matabaka hapa nchini katika
4. Kipengele hiki (4) kinachoweka suala la kuzingatia uwezo na mahitaji ya taifa katika elimu ni kifungu kinachominya haki ya elimu.Sijui ni mahitaji gani ya Taifa yanayozingatiwa katika elimu kwani elimu inapaswa kupatikana kwa kila mtu na ukiweka suala la uwezo maana yake uwezo usipokuwepo basi kuna watakaokosewa haki hiyoi na je ni nani hao wanaostahili kukosa haki hii ya elimu?.
Neno mfumo wa elimu unao zingatia uwezo na
Ibara ya 43/53 Haki ya mtoto

43.-(1) Kila mtoto ana haki ya:
(a) kupewa jina, uraia na ;
(b) kutoa mawazo, kusikilizwa na kulindwa dhidi ya uonevu, ukatili,
udhalilishaji,
(c) kucheza na kupata elimu ya msingi;
d) kuhifadhiwa katika mazingira mazuri, kwa walio katika
ukinzani na sheria;
(e) kupata lishe bora, huduma ya afya, makaazi na mazingira
Yanayomjenga kimaadili;
(f) kushiriki katika shughuli zinazolingana na umri alionao; na
(g) kupata malezi na ulinzi kutoka kwa wazazi, walezi, au
mamlaka ya nchi
(2) Mamalaka ya nchi itaweka utaratibu wa sheria utakaowezwsha utekelezaji na usimamizi wa haki za mtoto kwa kufuata msingi wakutoa kipaumbele kwa maslahi na manufaa ya mtoto
(3) Itakuwa ni wajibu wa kila mzazi, mlezi, jamii na mamlaka ya nchi kuhakikisha kuwa watoto wanalelewa katika maadili stahiki kwa umri wao.
Haki za mtoto

53.-(1) Kila mtoto ana haki ya:
(a) kupewa jina, uraia na kusajiliwa;
(b) kutoa mawazo, kusikilizwa na kulindwa dhidi ya uonevu, ukatili,
udhalilishaji, utumikishwaji na mila potofu;
(c) kuwekewa mazingira bora ya kucheza na kupata elimu ya msingi;
d) kuhifadhiwa katika mazingira mazuri, kwa walio katika
ukinzani na sheria;
(e) kupata lishe bora, huduma ya afya, makaazi na mazingira
yanayomjenga kimwili, kiakili na kimaadili;
(f) kushiriki katika shughuli zinazolingana na umri alionao; na
(g) kupata malezi na ulinzi kutoka kwa wazazi, walezi, jamii au
mamlaka ya nchi, bila ya ubaguzi wowote.
(2) Itakuwa ni wajibu wa kila mzazi, mlezi, jamii na mamlaka ya nchi kuhakikisha kuwa watoto wanalelewa katika maadili stahiki kwa umri wao.
(3) Kwa madhumuni ya Ibara hii “mtoto” maana yake ni mtu mwenye
umri wa chini ya miaka kumi na nane.

1. Kichwa kuna tofauti ya wingi katika Katiba Inayopendekezwainaongelea haki za mtoto na Rasimu inaongela haki ya Mtoto
2. Katiba pendekezwa
imeongeza hakiya mtoto kusajiliwa ambayo haikuwepo katika 3.Rasimu
Katiba-P imeongezea ulinzi wa mtoto dhidi ya utumikishwaji na mila potofu
4. Katiba -P imebadili maudhui ya kifungu kidogo cha (1) (c) katika ibara hii kwa kuweka haki ya kuwekewa mazingira bora ya kucheza n a kupata elimu ya msingi ambapo Rasimu ilitoa haki kucheza na kupata elimu.
5. Katiba P Imeboresha kifungu (!) (e) kwa kuongeza maneno Kimwili na kiakili katika kipengele (e) cha ibara hii kifungu kidogo cha (1) katika haki ya kupata lishe bora– namazingira yanayomjenga mtoto.
6.Katiba Inayopendekezwa kifungu kidogo (1) (g) kimeongeza jamii katika malezi na ulinzi wa mtoto na pia yatafanyika bila ubaguzi wowote
7 .Kifungu kidogo 3 katika ibara hiikimeweka tafsiri ya mtoto.
8. Ibara ndogo ya(2) katika Rasimu iliyokua inaweka wajibu kwa mamlaka ya ncho kuweza kutekeleza na kusimamia haki za mtoto kwa kufuata msingi wa kutoa kipaumbele kwa maslahi na manufaa ya mtot kimeondolewa kabisa. 1. Ni sawa kuongelea haki za mtoto kwa vile ni nyingi.
2. Ni vyema haki ya mtoto ya kusajiliwa kutambulika katika Katiba
3. Ulinzi uliowekwa unaimarisha hai za mtoto
4. Mabadilio haya ya kimaudhui katik ibara hii kipengele (1)(c) yatahitaji sheria itakayoonyesha mazingira hayo ya kucheza na kupata elimu yatakuwaje.Pia imepunguza haki kwa kuifunga kwenye elimu ya msingi tu
5 Hili ni badiliko chanya kutambua kuwa mtot ana haki kujengwa si kimaadili tu bali kimwili na kiakili.
6. Maboresho katika ibara hii kipengee (1) (g) ni chanya
7. Kuwekwa tafsiri ya mtot ni suala chanya

8.Kuondoa kifungu kinachoweka utaratibu wa kutekeleza haki zilizomo katika ibara hii kumepoteza uwezekanao wa haki hizi kuhakikishiwa utekelezaji wake kikatiba.
9. Mila potofu haisitaili kuwepo kwani kila jamii ina jinsi inavyo tafasili mila husika. Neno sitahiki lililo takiwa kuendelea kubaki ni uzalilishaji.
Ibara 44/54 Haki na wajibu wa
Vijana

44.-(1) Kila kijana ana haki na wajibu wa kushiriki kikamilifu katika
shughuli za maendeleo ya Jamhuri ya Muungano pamoja na jamii kwa ujumla,
na kwa mantiki hiyo, Serikali ya Jamhuri ya Muungano na jamii zitahakikisha
kuwa vijana wanawekewa mazingira mazuri ya kuwa raia wema na kupatiwa
fursa za kushiriki kikamilifu katika nyanja za kisiasa, kiuchumi, kijamii na
kiutamaduni.

Haki na wajibu wa
vijana

54.-(1) Kila kijana ana haki na wajibu wa kushiriki kikamilifu katika
shughuli za maendeleo ya Jamhuri ya Muungano pamoja na jamii kwa ujumla,
na kwa mantiki hiyo, Serikali ya Jamhuri ya Muungano na jamii zitahakikisha
kuwa vijana wanawekewa mazingira mazuri ya kuwa raia wema na kupatiwa
fursa za kushiriki kikamilifu katika nyanja za kisiasa, kiuchumi, kijamii na
kiutamaduni.
(2) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (1), Bunge litatunga sheria
itakayosimamia, pamoja na mambo mengine, uanzishwaji, muundo, majukumu
na uendeshaji wa Baraza la Vijana la Taifa. Katiba -P imeongeza kifungu kidogo (2) kinachoweka mazingira ya kuwepo kwa baraza la vijana Hili badiliko linatoa nafasi kwa vijana kuwa na baraza lao
Baraza hili kimantiki halina tija kwa vijana kwani itakuwa aina maana kuwaundia baraza la vijana kisha kuwatengenezea masharti na kuwachagulia viongozi wao badala ya kuwaacha wao wakijitawala kwa mjibu wa sheria.

Ni ingizo ambalo limelenga malengo ya kisiasa zaidi badala ya utetezi wa vijana katika kukuza msitakabali wa Taifa.

Kilio cha vijana ni ajira na siyo kuundiwa baraza ambalo mwisho wa siku hawatafanufaika nalo.
Ibara 45/52 Haki za Watu wenye ulemavu

45(1) Mtu mwenye ulemavu anastahiki:
(a) kuheshimiwa, kutambuliwa na kutendewa kwa namna ambayo haishushi utu wake
(b) kupata elimu kwa kutumia vifaa maalum na kushiriki katika shughuli za kijamii;
(c) kuwekewa miundo mbinu na mazingira yatakayowezesha kwenda anapotaka,kutumia vyombo vya usafiri
na kupata habari;
(d) kutumia lugha ya kutumia lugha ya alama, maandishi ya nukta nundu,
maandishi yaliyokuzwa au njia nyingine zinazofaa;
(e) kusoma,kujifunza na kuchanganyika na watu wengine; na
(f) kupata ajira na kugombea nafsi za uongozi katika nyadhifa mbalimbali kwa usawa;
(2) Mamlaka ya nchi itaweka utaratibu wa sheria utakaowezesha watu wenye ulemavu kushiriki katika nafasi za uwakilishi.
Haki za watu
wenye ulemavu

55. Mtu mwenye ulemavu ana haki ya:
(a) kuheshimiwa, kutambuliwa na kulindwa dhidi ya vitendo
vinavyoshusha utu wake ikiwemo ubaguzi, uonevu, ukatili na mila
potofu;
(b) kupata elimu kwa kutumia vifaa maalum na kushiriki katika nafasi
za uwakilishi na shughuli za kijamii;
(c) kuwekewa miundo mbinu na mazingira yanayofaa
yatakayomwezesha kwenda anapotaka, kutumia vyombo vya usafiri
na kupata habari;
(d) kutumia lugha ya kutumia lugha ya alama, alama mguso, maandishi ya nukta nundu,
maandishi yaliyokuzwa au njia nyingine zinazofaa;
(e) kupata ajira na kufanya kazi; na
(f) kupata huduma bora za afya, uzazi salama, marekebisho na
utengemano 1. Ibara hii kifungu cha (1)(a) kimefanya mabadiliko katika lugha na kuigeuza kuweka hakiya kulindwa badala ya haki ya kutendewa namna ambayo haishushi utu na hivyo kutaja vitendo hivyo vonavyoweza kushusha utu.
2. Katika kipengele (c) cha kifungu cha 1 neno yanayofaa limongezwa katika mazingira ya miundo mbinu
3. Katika kipengele (d) maneno alama mguso yameongezewa katika hai ya kutumia lugha
4. Kipengele (e) katika ibara 45(1) ibara ya Rasimu kimeondolewa kabisa
5. Kipengele (f) katika rasimu kimepunguzwa haki kugombea nafsi za uongozi katika nyadhifa mbalimbali kwa usawa 1. Badiliko hili limeweka bayana zaidi haki hiyo ila si badiliko ambalo lisingekuwepo kungekua na ukosefu wa haki hiyo.
2. Nyingeza ya neno yanayofaa limeongeza msisitizo katika sehemu hiyo.
3. Ongezeko hilo la alama mguso kama ina tofauti na lugha ya alama itakua imepanua wigo wa aina za lugha kwa watu wenye ulemavu
4. Kuondolewa kwa kipengele hiki kumepunguza msisitizo wa hai ambazo katika mazingira ya watu wnye ulemav ilifaa zisisitizwe.Inaweezekana sehemu hii ikaonekana ni sawa na kipenge (b) kinachohusu kupata elimu lakini hapa msisitizo ni kujifunza,kusoma na kuchanganyika na wengine.
5. Kwa kuondoa sehemu hii ni kupunguza haki ya watu wenye ulemavu katika masuala ya uongozi inawezekana kuwa maneno yaliyoongezwa katika kipengele (b) kushiriki katika uwakilishi yakaonekana yamekidhi haja ya kuondoa maneno katika kipengele hiki.Kwa mazingira ya hali ya watu wenye ulemavu na jinsi wanavyochukuliwa na jamii lugha katika Rasimu ilikua inaweka bayana haki hii ya kugombea nafasi kwa usawa.
Pia haki ya kupata ajira ilifaa isisitizwe bayana
Ibara ya 46/56 Haki za
makundi madogo katika
jamii

46.(1) Mamlaka ya nchi
itaweka utaratibu wa sheria utakaowezesha makundi madogo katika jamii:
a) kushiriki katika uongozi wa mamlaka za nchi;
(b) kupewa fursa maalum za elimu na fursa za kujiendeleza kiuchumi na fursa za ajira; na
(c) kutengewa maeneo ya ardhi ambayo kwa desturi, makundi hayo
huyatumia kama maeneo ya kuishi na kupata riziki ya chakula
(2) Serikali na mamlaka ya nchi itachukua hatua za makusudi za kukuza
na kuendeleza shughuli za kiuchumi na kuweka miundombinu ya makazi, elimu,
maji na afya kwa ajili ya kizazi cha sasa na vijavyo vya jamii ya watu walio
katika makundi madogo.
(3) Kwa madhumuni ya Ibara hii, “makundi madogo” maana yake ni
jamii za watu wanaoishi kwa kutegemea uoto wa asili na mazingira
yanayowazunguka kwa ajili ya chakula, malazi na mahitaji mengine ya maisha.

Haki za
makundi madogo katika
jamii

56.-(1) Mamlaka ya nchi kwa kuzingatia rasilimali na uwezo wa nchi,
itaweka utaratibu wa sheria utakaowezesha makundi madogo katika jamii:

(a) kushiriki katika uongozi wa mamlaka za nchi;
(b) kupewa fursa maalum za elimu kujiendeleza kiuchumi na ajira; na
(c) kutengewa maeneo ya ardhi ambayo kwa desturi, makundi hayo
huyatumia kama maeneo ya kuishi na kupata riziki ya chakula.
(2) Serikali na mamlaka ya nchi itachukua hatua za makusudi za kukuza
na kuendeleza shughuli za kiuchumi na kuweka miundombinu ya makazi, elimu,
maji na afya kwa ajili ya kizazi cha sasa na vijavyo vya jamii ya watu walio
katika makundi madogo.
(3) Kwa madhumuni ya Ibara hii, “makundi madogo” maana yake ni
jamii za watu wanaoishi kwa kutegemea uoto wa asili na mazingira
yanayowazunguka kwa ajili ya chakula, malazi na mahitaji mengine ya maisha.

1. Katika ibara hii kuna nyongeza ya maneno katika kifungu cha 56(1) cha Katiba-P “kwa kuzingatia rasilimali na uwezo wa nchi” katika kuwezesha makundi madogo katika jamii 1. Maneno yaliyoongezwa huktumika sana kwa watawala kutokutekeleza haki kwani haki huweza kutotekelezwa kwa kigezo kuwa hakuna uwezo au rasilimali haziruhusu kwa hiyo haki hii ni kama tu haipo.

Maneno haya hutumiwa na watawala katika kukwepa majukumu yao. Hivyo ni maneno ambayo hayawawajibishi watawala.
Ibara ya 47/57 Haki za wanawake

47.(1) Kila mwanamke ana haki ya:
(a) kuheshimiwa utu wake ,
(b) kuwa salama dhidi ya unyonyaji na ukatili;
c) kushiriki bila ya ubaguzi katika uchaguzi na ngazi zote za
maamuzi;
(d) kupata fursa na ujira sawa na mwanaume katika kazi zenye sifa
zinazofanana

(e) Kulindwa dhidi ya ubaguzi, uonevu na mila zenye madhara;
(f) ) kulindwa ajira yake wakati wa ujauzito na pale anapojifungua
(g) kupata huduma bora ya afya na
(2) Mamlaka za nchi zitaweka utaratibu wa kisheria utakaosimamia masuala yanayousu utekelezaji wa masharti ya ibara hii ikiwa nipamoja na kukuza utu , heshima, usalama na fursa za wanawake wakiwemo wajane
Haki za wanawake

57. Kila mwanamke ana haki ya:
(a) kuheshimiwa, kuthaminiwa na kutambuliwa utu wake;
(b) kulindwa dhidi ya ubaguzi, udhalilishaji, dhuluma, unyanyasaji,
ukatili wa kijinsia na mila potofu;
(c) kushiriki bila ya ubaguzi katika uchaguzi na ngazi zote za
maamuzi;
(d) kupata fursa na ujira sawa na mwanaume katika kazi zenye sifa
zinazofanana;
(e) kulindwa ajira yake wakati wa ujauzito na pale anapojifungua;
(f) kupata huduma bora ya afya ikiwemo afya ya uzazi salama; na
(g) kumiliki mali.
1. Kipengele (a) katika Ibara ya 57 iliyo sawa na ibara ya 47 ya Rasimu kimeongeza maneno kuthaminiwa na kutambuliwa katika maneno ya awali ya kuheshimiwa utu wamwanamke.
2. Kipengele (b) katika Katiba -kimeongeza ulinzi dhidi ya dhuluma,,udhalilishaji na ukatili wa kijinsia
3. Kipengele (f) katika Katiba-P kimeongeza haki ya afya ya uzazi salama
Na kipengele (g) kimeongeza haki ya kumiliki mali
4. Katiba -P imefuta kifungu cha 2 katika rasimu kilichohusu kuwekwa kwa utaratiu wa kisheria utakaosimamia masuala yanayohusu utekelezaji wa masharti ya ibara hii na kusisitiza heshima nausalama na fursa za wanawake wakiwemo wajane 1. Ongezeko la maneno haya hakuna athari yoyote . Na ni mazuiri kwao yanatoa fursa na uwezo wa mwanamke kujitambua na kutambuliwa pia.
2. Ongezeko hili katika kipengele (b) kimeboresha ulinzi kwa mazingira ya hali ya wananwake nchini hasa ukatili wa kijinsia .Kimeboresha kipenge (e) cgha Rasimu kilichokua na ulinzi dhidi ya ubaguzi, uonevo na mila zenye madhara. Lugha ya madhara iliyo kwenye rasimu ingekuwa bora zaidi ya mila potofu.
3. Nyongeza hizi zimeboresha haki zilizokuwepo katika rasimu
4. Kuondolewa kwa kipengele hiki kunaondoa uwezekanowa seheku hii kutekelezeka na pia kumepunguza utambuzi wa wajane ambao ni kundi linalodhulumika san kaytika jamii.
Ibara ya 48/58 Haki za Wazee

48: Mamlaka ya nchi itaweka utaratibu utakaowezesha wazee kupata
fursa ya:
(a) kushiriki katika shughuli za kijamii
(b) Kuendeleza maisha yao
(c) Kutambuliwa utu wao na kuheshimiwa pasipo kudharauliwa;na
(d) kupata mahitaji ya msingi kutoka kwenye familia,zao, jamii na mamlaka ya nchi Haki za wazee

58. Mamlaka ya nchi itaweka utaratibu utakaowezesha wazee kupata
fursa ya:
(a) kushiriki katika shughuli za kimaendeleo na kijamii;
(b) kuendesha maisha yake na kujiendele
za kulingana na uwezo wake
ikiwa ni pamoja na kufanya kazi;
(c) kupata huduma za matibabu;
(d) kulindwa dhidi ya unyonyaji, vitendo vya ukatili ikiwemo mateso na
mauaji;
(e) kuwekewa miundombinu na mazingira bora yatakayowawezesha
kwenda wanakotaka na kutumia vyombo vya usafiri wa umma kwa
gharama nafuu; na
(f) kupata mahitaji ya msingi kutoka kwenye familia yake, jamii na
inapobidi mamlaka ya nchi.
1. Ibara ya 58 kipengle (a) kimeongezewa neno kimaendeleo katika ushiriki wa wazee katika shughuli za kijamii.
2. Kifungu (b) katika katiba -P kimetoa ufafanuzi zaidi katika kifungu cha rasimu kilichotoa haki ya wazee kuendesha maisha yao kwa maneno
” kujiendele
za kulingana na uwezo wake
ikiwa ni pamoja na kufanya kazi”
3. Kingele (c) na (d) Vimeongezwa katika haki ya ulinzi kwa wazee dhidi ya unyonyaji, ukatili na mateso pi akuweka miundo mbinu waweze kwenda watakapo kwa usafiri wa umma kwa bei nafuu 1. Ongezeko hili halina athari sana kwani shughuli za kijamii huweza pia kuwa za kimaendeleo
2. Kwa kutambua uhali ya wazee wa Tanzania kifungi kilichoongezewa ni kama shere kwani mzee kutakiwa kujiendeleza kwa kadri ya uwezo wakati ni wazi kuwa uwezo wa wazee pamoja na kufanya kazi ni kuwatwika mzigio na si kuwapa haki.
3. Nyongeza katika kipengele (c) na (d0 vieboresha haki za wazee ila vitahitaji uwepowa sheria ya kuwezeshautekelezaji wake.
4. Wazee wanataka kuthaminiwa na kusaidiwa katika mambo ya msingi na siyo kuwatengenezea mazingira ya wao kuhangaika. Kwani hali za Wazee hapa Tanzania ni mbaya, wanahitaji maradhi, chakula na matibabu na si kuwatengenezea mazingira.
Ulinzi wa wazee (Hifadhi ya jamii) haipo.

Ibara /59 Hii ibara haikuwepo katika Rasimu ya pili Uhuru wa taaluma,
ubunifu, ugunduzi
na usanii
59.-(1) Kila mtu atakuwa na uhuru wa kushiriki kwenye mambo
yanayoendeleza na kukuza sanaa, taaluma, ubunifu na ugunduzi.
(2) Kila mtu ata kuwa na uhuru wa kujifunza, kufundisha, kutafiti na
kueneza matumizi ya matokeo ya utafiti kulingana na kanuni za kitaaluma na za
kiutafiti.
(3) Serikali itakuza na kuendeleza utafiti, ubunifu na ugunduzi katika
sanaa, sayansi na teknolojia kwa kutunga sheria ambazo:
(a) zitalinda hakimiliki na hataza na haki za wabunifu, watafiti na zitalinda hakimiliki na hataza na haki za wabunifu, watafiti na
wasanii;
(b) zitawezesha taasisi za elimu na za utafiti kutumia ugunduzi wao kwa
manufaa ya taifa;
(c) zitasimamia uhamishaji wa sayansi na teknolojia;
(d) zitawezesha kukuza rasilimali watu kwenye nyanja za kitaaluma,
sayansi, teknolojia na ubunifu;
(e) zitalinda na kusimamia ubora wa taaluma, utafiti na matumizi ya
ugunduzi na ubunifu; na
(f) zitafafanua mambo mengine yanayohusu hakimiliki na hataza.

Ongezeko hili ni Jipya Ongezeko la ibara hii ni bora katika uwanja huo wa sayansi na teknolojia na utafiti na ubunifu ikiwemo hati miliki.

Linahitaji kuwekewa mazingira weseshi ili kuwapa fursa za ugunduzi, utafiti na nk.

SURA YA 7 & 8
IBARA
RASIMU YA PILI KATIBA INAYOPENDEKEZWA TOFAUTI MAONI
Ibara ya 73.
Muundo wa muungano 60. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itakuwa na muundo wa shirikisho lenye serikali tatu ambazo ni :
a) Serikali ya Jamhuri ya Muungano
b) Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
c) Serikali ya Tanganyika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itakuwa na muundo wa Serikali
mbili ambazo ni:
(a) Serikali ya Jamhuri ya Muungano; na
(b) Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Kuondolewa kwa muundo wa muungano wa serikali tatu na kuwa mbili Maoni ya wananchi kuhusu muundo wa muungano wa serikali tatu hayajazingatiwa.
Kilio cha watanzania ni kuondoa au kupunguza kero za muungano.
Hivyo kurudisha serikali 2 badala ya 3 ni kuzidi kuwatumbukiza wananchi katika kero za muungano.
Ibara ya 74.
Utekelezaji wa shughuli za mamlaka ya nchi 60 (2) Shughuli za Jamhuri ya muungano zitatekelezwa na kusimamiwa na;
a) Serikali ya jamhuri ya muungano
b) Bunge la jamhuri ya muungano
c) Mahakama ya jamhuri ya muungano Shughuli zote za Mamlaka ya Nchi katika Jamhuri ya Muungano
zitatekelezwa na kudhibitiwa na vyombo viwili vyenye mamlaka ya utendaji,
vyombo viwili vyenye mamlaka ya utoaji haki, na pia vyombo viwili vyenye
mamlaka ya kutunga sheria na kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma.

a) Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
b) Mahakama ya Jamhuri ya Muungano na Mahakama Kuu ya Zanzibar.
c) Bunge na Baraza la Wawakilishi. Kuongezwa kwa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar, mahalama kuu ya Zanzibar na baraza la wawakilishi katika shughuli zote za Jamhuri ya Muungano. Maoni ya rasimu ya pili kuhusu shughuli za jamhuri ya muungano hayajazingatiwa.

**************

Ibara ya 75.
Mamlaka ya serikali ya jamhuri ya muungano 62. Serikali ya jamhuri itakuwa na mamlaka ya utekelezaji kwa mambo yote yaliyoorodheshwa kuwa mambo ya muungano kwa kuzingatia mamlaka itakayopewa chini ya katiba hii. Serikali ya Jamhuri ya Muungano itakuwa na mamlaka ya utekelezaji
katika Jamhuri ya Muungano kwa Mambo ya Muungano na kwa mambo yote
yasiyo ya Muungano yanayohusu Tanzania Bara.
Ukuu wa serikali ya muungano kutekeleza mambo yasiyo ya muungano yahusuyo Tanzania bara.

Kumezwa kwa Tanzania bara Madaraka makubwa ya serikali ya muungano kwa mambo yahusuyo Tanzania bara pekee.

Wameturudisha kama tulivyokuwa awali.

Tanzania bara (Tanganyika) imebaki kuvaa koti la Muungano.

Mambo ya muungano yamezidi kuongezeka badala ya kupunguzwa kama ilivyokuwa imependekezwa na Tume.

Ibara ya 76.
Mamlaka ya
Serikali ya
Mapinduzi ya
Zanzibar kwa
mambo yasiyo ya
Muungano
Ibara hii haikuwepo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itakuwa na mamlaka na haki juu ya mambo yasiyo ya Muungano yanayohusu Zanzibar.

Ibara hii ni mpya.

Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kuwa na mamlaka yake kamili katika mambo yasiyo ya muungano yanayohusu Zanzibar. Zanzibar imepewa mamlaka kamili kuhusu mambo yake wakatiTanzania bara haina.

Zanzibar imezidi kuonekana wakati Tanganyika imemezwa ndani ya Muungano.
Ibara ya 77.
Mahusiano kati ya serikali ya jamhuri ya muungano na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar. Ibara hii haikuwepo katika rasimu ya pili Katika kutekeleza majukumu yake katika maeneo mbalimbali,
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itazingatia misingi ya kushirikiana na kushauriana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa lengo la kukuza na kulinda maslahi ya Taifa na maendeleo ya wananchi. Iko vizuri kwani inaweka misingi ya kushirikiana na serikali ya Mapinduzi .
Ibara ya 78.
Wajibu wa viongozi wakuu kulinda muungano 69. Viongozi Wakuu wanaohusika na masharti ya Ibara hii ni:
(a) Rais wa Jamhuri ya Muungano;
(b) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano;
(c) Rais wa Tanganyika; na
(d) Rais wa Zanzibar.
Viongozi wakuu wanaohusika na masharti ya Ibara hii ni:
(a) Rais wa Jamhuri ya Muungano;
(b) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano;
(c) Rais wa Zanzibar;
(d) Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano; na
(e) Makamu wa Rais wa Zanzibar. Kufutwa kwa rais wa Tanganyika.
Kuongezwa kwa waziri mkuu wa jamhuri ya muungano na makamu wa rais wa Zanzibar. Cheo cha waziri mkuu kimerudishwa.
Kitendo cha Waziri Mkuu kuwa Makamu wa pili wa raisi ni kumfanya awe raisi wa Tanganyika.

Dhana hii inaifanya Tanganyika kutambuliwa ila kwa kufichwa.

Na hali hii inaifanya Tanzania kuwa shirikisho la nchi mbili Tanganyika na Zanzibar, japo Tanganyika inazidi kuwa mafichoni.

Ibara ya 79.
Serikali ya jamhuri ya muungano. 70. Kutakuwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano ambayo itaundwa na Rais, Makamu wa Rais na Mawaziri wa Jamhuri ya Muungano.
Kutakuwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano ambayo itaundwa
na Rais, Makamu wa Rais na Baraza la Mawaziri. Uwepo wa baraza la mawaziri Iko vizuri
Ibara ya 80.
Rais wa jamhuri ya muungano. 71. Kutakuwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano.
(2) Rais wa Jamhuri ya Muungano atakuwa Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu na:
(a) atakuwa alama na taswira ya Jamhuri ya Muungano na watu wake;
(b) atakuwa alama ya umoja, uhuru wa nchi na mamlaka yake; na
(c) atakuwa na dhamana ya kukuza na kuhifadhi umoja wa kitaifa.
Kutakuwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano.
(2) Rais wa Jamhuri ya Muungano atakuwa Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Amiri Jeshi Mkuu na atakuwa:
(a) alama na taswira ya Jamhuri ya Muungano na watu wake; na
(b) alama ya umoja, uhuru wa nchi na mamlaka yake.
Hakuna mabadiliko hakuna
Ibara ya 81.
Madaraka na majukumu ya Rais 72. Majukumu ya Rais yameainishwa vizuri Rais atatekeleza mamlaka ya Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa
Serikali, Amiri Jeshi Mkuu kwa mujibu wa Katiba hii na atakuwa na madaraka na majukumu kama yatakavyoainishwa kwenye sheria zitakazotungwa na Bunge.

Pia majukumu ambayo hayakuainishwa katika Katiba hii na ambayo hayakiuki Katiba hii na sheria zitakazotungwa na Bunge.
Madaraka ya rais yaliyokuwa yameainishwa katika rasimu ya pili yameondolewa. Ni vizuri madaraka ya rais yakatajwa bayana kuliko kuacha ombwe.

Hali hii ya kutokuweka bayana madalaka ya rais yanazidi kutengeneza mwanya wa rais kuamua atakavyo na si kw akuongozewa na misingoi ya sheria.
Ibara ya 82.
Utekelezaji wa madaraka ya Rais 73. Katika utekelezaji wa madaraka ya Rais kwa mujibu wa Sura hii na kwa kuzingatia masharti ya ibara ndogo ya (3), Rais ana mamlaka ya kuanzisha au kufuta nafasi za madaraka katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano. Katika utekelezaji wa madaraka ya Rais kwa mujibu wa Sura hii,
Rais atakuwa na mamlaka ya kuanzisha au kufuta nafasi za madaraka katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
Kimeondolewa kipengele cha rais kuzingatia masharti kuhusu uthibitisho wa Bunge katika nafasi za madaraka na vile vile ushauri wa mamlaka za Serikali, Bunge au Mahakama zilizopewa madaraka ya kumshauri katika kufanya uteuzi, kuanzisha au kufuta nafasi za madaraka katika utumishi wa Serikali. Madaraka ya Rais yameongezwa.

Hali hii inazidi kumfanya Raisi awe mtawala badala ya kuwa kiongozi.
Kipengele cha rais kuzingatia ushauri atakaopewa kimeondolewa. Hii ni kutengeneza mazingira ya rais kutokuwajibishwa.
Ibara ya 83.
Rais kuzingatia ushauri 74. Rais atakuwa na wajibu wa kufuata na kuzingatia ushauri atakaopewa na mamlaka za nchi, na endapo hakubaliani na ushauri aliopewa, sharti atoe sababu katika Baraza la Mawaziri kuhusu sababu ya kutokubaliana na ushauri aliopewa.
Katika kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Katiba na Sheria, Rais atakuwa huru katika utendaji wa kazi na shughuli zake na hatalazimika kufuata au kuzingatia ushauri atakaopewa na mtu yeyote au mamlaka yoyote
isipokuwa pale tu anapotakiwa na Katiba hii au sheria nyingine yoyote kufanya jambo lolote kulingana na ushauri anaopewa na mtu au mamlaka yoyote. Rais kuwa huru katika utendaji wa kazi na kutozingatia ushauri atakaopewa. Madaraka na uhuru wa rais umeongezwa jambo ambalo ni hatari.
Ibara ya 84.
Rais kushindwa kumudu majukumu yake 75. Endapo Baraza la Mawaziri litaridhika kuwa Rais hawezi kumudu kazi zake kwa sababu ya maradhi, linaweza kuwasilisha kwa Jaji Mkuu azimio la kumwomba Jaji Mkuu athibitishe kwamba Rais, kwa sababu ya maradhi, hawezi kumudu kazi zake.
Endapo Baraza la Mawaziri litaridhika kuwa Rais hawezi
kumudu kazi zake kwa sababu ya maradhi ya mwili au akili linaweza kuwasilisha kwa Jaji Mkuu azimio la kumwomba Jaji Mkuu athibitishe kwamba Rais, kwa sababu ya maradhi ya mwili au akili hawezi kumudu kazi
zake. Hakuna mabadiliko Iko vizuri
Ibara ya 85.
Utaratibu wa kujaza nafasi ya Rais kabla ya kumaliza muda wake. 76 (2)…………
(b) kwa Rais aliyepatikana kwa utaratibu wa mgombea huru, baada ya kushauriana na Baraza la Ulinzi na Usalama wa Taifa, atapendekeza jina la mtu atakayekuwa Makamu wa Rais na uteuzi huo utathibitishwa na Bunge kwa kura zaidi ya asilimia hamsini ya Wabunge wote. 85 (2)………
(b) kwa Rais aliyepatikana kwa utaratibu wa mgombea huru, baada ya kushauriana na Tume Huru ya Uchaguzi, atapendekeza jina la mtu atakayekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais na uteuzi
huo utathibitishwa na Bunge kwa wingi wa kura za Wabunge wote. Mgombea huru wa urais kushauriana na Tume ya uchaguzi badala ya baraza la ulinzi na usalama wa taifa.

Uteuzi kuthibitishwa kwa wingi wa kura za wabunge wote badala ya kura zaidi ya 50% ya wabunge wote.

Hii ni mbaya kwani ni raisi raisi kutokukubalia na wengi lakini kwa kigezo cha wingi wa kura akashinda. Masharti ya kumpata makamu wa rais na uthibitishaji wa kura yamepunguzwa.

Kutakuwa na ugumu wa rais atakaye kuwa mgombea huru, upatikanaji wa makamu wa rais itakuwa ni shida, kwa mjibu wa mtililiko wa mlengo huu waerikali 2 badala ya 3.
Ibara ya 86.
Utekelezaji wa majukumu ya Rais akiwa hayupo. 77.-(1) Ikitokea kwamba nafasi ya madaraka ya Rais iko wazi kutokana na: (c) kutokuwepo katika Jamhuri ya Muungano, kazi na shughuli za Rais zitatekelezwa na mmoja wapo wa wafuatao, kwa kufuata orodha kama ilivyopangwa –

(ii) Waziri Mwandamizi

86.-(1) Ikitokea kwamba nafasi ya madaraka ya Rais iko wazi
kutokana na:
(c) kutokuwepo katika Jamhuri ya Muungano, kazi na shughuli za Rais zitatekelezwa na mmoja wa wafuatao, kwa kufuata orodha kama ilivyopangwa-

(ii) Waziri Mkuu. Kurudishwa kwa cheo cha waziri mkuu Maoni ya rasimu ya pili hayajazingatiwa
Ibara ya 87.
Uchaguzi wa rais 78.-(1) Rais atachaguliwa na wananchi kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii na kwa mujibu wa sheria za nchi.
(2) Nafasi ya madaraka ya Rais itakuwa wazi na uchaguzi wa Rais utafanyika baada ya Rais kumaliza muda wake wa kuwa madarakani kwa mujibu wa Katiba hii. 87.-(1) Rais atachaguliwa na wananchi kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii na kwa mujibu wa sheria.

(2) Nafasi ya madaraka ya Rais itakuwa wazi na uchaguzi wa Rais utafanyika baada ya Rais kumaliza muda wake wa kuwa madarakani kwa mujibu wa Katiba hii.
Hakuna mabadiliko Hakuna
Ibara ya 88.
Sifa za rais 79.-(1) …………….
(e) anayo shahada ya chuo cha elimu ya juu kinachotambuliwa kwa mujibu wa sheria za nchi;
(g) sera zake au sera za chama chake si za mrengo wa kuligawa Taifa kwa misingi ya ukabila, dini, rangi au jinsi; na
(h) ni mwadilifu, anayeheshimu haki za binadamu, asiyedharau wala kubagua watu kwa misingi ya kabila, dini, jinsi, maumbile au hali zao katika jamii na anafuata maadili ya viongozi na mwenendo wake hautiliwi shaka na jamii.
88.-(1) …………..
(e) anayo shahada ya chuo cha elimu ya juu kinachotambuliwa kwa mujibu wa sheria, au awe na ujuzi na uzoefu wa uongozi katika ngazi ya taifa utakaomwezesha kumudu madaraka ya Rais;
Kipengele (g) na (h) kimeondolewa.

Kumeongezwa option ya awe na ujuzi na uzoefu wa uongozi katika ngazi ya taifa utakaomwezesha kumudu madaraka ya Rais;
Kuondolewa kwa kipengele kinachohusu maadili ya rais kunaweza kuleta rais asiye muadilifu.

Kigezo cha shahada kuwa cha lazima ni kizuri kwani kiongozi mkuu wan chi anatakiwa awe na ujuzi au uelewa zaidi.

Uzoefu wa uongozi ngazi ya Taifa ni kuzidi kuleta nyufa na kuwabana watu kama siyo kuleta matabaka.
Uzoefu wa ngazi ya Taifa ni mgumu sana
Ibara ya 89.
Utaratibu wa uchaguzi wa Rais 80 (1) Katika Uchaguzi wa Rais, kila chama cha siasa kinachopenda kushiriki katika uchaguzi wa Rais kitawasilisha kwa Tume Huru ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano, kwa mujibu wa sheria za nchi, jina la mwanachama mmoja anayependekezwa kwa nafasi ya madaraka ya Rais.
89.-(1) Katika uchaguzi wa Rais kila chama cha siasa kitakachotaka kushiriki katika uchaguzi wa Rais, kitawasilisha kwa Tume Huru ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano, kwa mujibu wa sheria, jina la mwanachama mmoja anayependekezwa kwa nafasi ya madaraka ya Rais.
Hakuna mabadiliko hakuna
Ibara ya 90.
Malalamiko kuhusu uhalali wa uchaguzi wa Rais. 81 (2) Malalamiko ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Rais yatawasilishwa Mahakama ya Juu ndani ya muda uliowekwa na sheria ya nchi baada ya siku ya kutangazwa kwa matokeo ya Uchaguzi wa Rais.
(3) Mahakama ya Juu itasikiliza na kutoa uamuzi wa shauri la kupinga matokeo ya uchaguzi wa Rais ndani ya muda utakaoainishwa na sheria ya nchi tangu kupokea malalamiko yaliyowasilishwa kwa mujibu wa ibara ndogo ya (2) na uamuzi huo utakuwa wa mwisho.
90 (2) Malalamiko ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Rais yatawasilishwa Mahakama ya Juu ndani ya muda wa siku saba baada ya siku ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa Rais.

(3) Mahakama ya Juu itasikiliza na kutoa uamuzi wa shauri la
kupinga matokeo ya uchaguzi wa Rais ndani ya siku kumi na nne tangu kupokea malalamiko yaliyowasilishwa kwa mujibu wa ibara ndogo ya (2) na uamuzi huo utakuwa wa mwisho. Muda wa kufungua shauri la kupinga matokeo ni ni siku 7 na uamuzi wa kupinga matokeo ni ndani ya siku 14. Kuweka muda wa kupeleka shauri mahakama ni jambo chanya.

Kuweka mda maalumu ni kulenga kuleta umuhimu wa raia kujuana kutambua kazi na kutambua umuhimu wa kuthamini taasisi nyingine kama
Ibara ya 91.
Kiapo cha rais na muda wa kushika madaraka. 82.-(1) Rais Mteule ataapishwa na Jaji Mkuu na atashika nafasi ya madaraka ya Rais mapema iwezekanavyo baada ya kutangazwa kwamba amechaguliwa kuwa Rais, lakini kwa hali yoyote, hatashika madaraka kabla ya kupita siku thelathini kutoka siku matokeo ya Uchaguzi wa Rais yalipotangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi au siku ya kuthibitishwa na Mahakama ya Juu.
91.-(1) Rais Mteule ataapishwa na Jaji Mkuu au Naibu Jaji Mkuu
endapo Jaji Mkuu hayupo na atashika nafasi ya madaraka ya Rais siku saba baada ya kutangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi au mara baada ya
kuthibitishwa na Mahakama ya Juu.
Rais kushika madaraka baada ya siku 7 tangu kutangazwa matokeo na sio 30. Kuapishwa kwa rais kumeharakishwa mno bila kuzingatia muda uliowekwa wa kupeleka shauri mahakani kupinga matokeo.
Ibara ya 92.
Haki ya kuchaguliwa tena 83 (3) Mtu aliyewahi kuwa Rais wa Tanganyika au Zanzibar hatapoteza sifa za kugombea na kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa sababu aliwahi kushika nafasi ya madaraka ya Rais wa Tanganyika au Rais wa Zanzibar.
92 (3) Bila kuathiri masharti ya Katiba hii, mtu aliyewahi kuwa Rais wa Zanzibar hatapoteza sifa za kugombea na kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano. Kuondolewa kwa kipengele cha rais wa Tanganyika. Muundo wa serikali 3 umeondolewa.
Ibara ya 93.
Madaraka ya kutangaza vita 84.-(1) Kwa kuzingatia masharti ya Ibara hii, Rais atakuwa na mamlaka ya kutangaza kuwepo kwa vita kati ya Jamhuri ya Muungano na nchi nyingine au kundi lolote lile baada ya kupata idhini ya Bunge.
93.-(1) Kwa kuzingatia masharti ya Ibara hii, Rais atakuwa na mamlaka ya kutangaza kuwepo kwa vita kati ya Jamhuri ya Muungano na nchi nyingine au kundi lolote lile baada ya kupata idhini ya Bunge.
Hakuna mabadiliko hakuna
Ibara ya 94.
Madaraka ya rais kutangaza hali ya hatari. 85.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii au sheria za nchi, Rais anaweza, baada ya kushauriana na Baraza la Ulinzi na Usalama wa Taifa, kutangaza hali ya hatari au hali ya kuzingirwa kwa eneo fulani la
Jamhuri ya Muungano au katika sehemu yake yoyote. 94.-(1) Bila kuathiri masharti ya Katiba hii au sheria, Rais anaweza, baada ya kushauriana na Baraza la Usalama la Taifa, kutangaza hali ya hatari au hali ya kuzingirwa kwa eneo fulani la Jamhuri ya Muungano au katika sehemu yake yoyote.
Hakuna mabadiliko hakuna
Ibara ya 95.
Mamlaka ya rais kutoa msamaha. 86. Hakuna mabadiliko
******** IBARA HII NI YA KUANGALKIA ZAIDI 95. Hakuna mabadiko

Hakuna mbadiliko hakuna
Ibara ya 96.
Kinga ya mashtaka dhidi ya rais 87.-(1) Wakati Rais akiwa madarakani, hatashitakiwa wala mtu yeyote hataendesha mashtaka ya aina yoyote dhidi yake mahakamani kwa ajili ya kosa lolote la jinai.
96.-(1) Wakati Rais akiwa madarakani, hatashtakiwa wala mtu yeyote hataendesha mashtaka ya aina yoyote dhidi yake mahakamani kwa ajili ya kosa
lolote la jinai. Hakuna mabadiliko hakuna
Ibara ya 97.
Bunge kumshtaki rais 88 (2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Ibara hii, hoja yoyote ya kumshtaki Rais haitatolewa isipokuwa tu kama itadaiwa kwamba Rais ametenda mojawapo ya makosa yafuatayo:
(d) uhaini;
Kipengele cha uhaini kimeondolewa Kipengele cha uhaini kimeondolewa Kitendo cha kuondoa kosa la uhaini ni makosa. Ikumbukwe kwamba rais anaweza kuandaa genge la watu na kustengeza njia ya wao kupindua nchi kwa masilai binafsi.
Ibara ya 98.
Maslahi ya rais 89.-(1) Rais atalipwa mshahara na malipo mengineyo kama yatakavyoainishwa na Tume ya Utumishi wa Umma na atakapostaafu atapokea malipo ya uzeeni na stahili nyingine kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina.
98.-(1) Rais atalipwa mshahara na malipo mengine, na atakapostaafu
atapokea malipo ya uzeeni, kiinua mgongo au posho kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina.

(3) Bunge litatunga sheria kwa ajili ya utekelezaji wa masharti ya Ibara hii.
Kimeongezwa kipengele cha Bunge litatunga sheria kwa ajili ya utekelezaji wa masharti ya Ibara hii. Wabunge nao ni watumishi wa umma hivyo kitendo cha kujiondoa katika Tume ya Utumishi wa Umma siyo jambo jema jema kwa msikabari wa Taifa.
Mshahara wa rais ni vizuri ukaratibiwa Tumme ya Utumishi ili kukuza utawazi na uwajibija

Ibara ya 99.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano. 90.-(1) Kutakuwa na Makamu wa Rais ambaye atakuwa ndiye Msaidizi Mkuu wa Rais kuhusu mambo yote ya Jamhuri ya Muungano kwa jumla
99. Kutakuwa na Makamu wa Rais watatu ambao watakuwa:
(a) Makamu wa Kwanza wa Rais;
(b) Rais wa Zanzibar ambaye atakuwa Makamu wa Pili wa Rais; na
(c) Waziri Mkuu ambaye atakuwa Makamu wa Tatu wa Rais. Kuongezwa kwa makamu wa rais watatu Majukumu ya rais wa Zanzibar na waziri mkuu hayajaainishwa.
Ibara ya 100.
Upatikanaji wa makamu wa kwanza wa Rais 91.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ya 76, Makamu wa Rais atapatikana kwa kuchaguliwa katika uchaguzi pamoja na Rais, baada ya kupendekezwa na chama chake au mgombea huru wakati ule ule anapopendekezwa mgombea wa nafasi ya madaraka ya Rais na watapigiwa kura kwa pamoja.
100 (3) Chama cha siasa chochote au mtu yeyote anayekusudia kugombea nafasi ya madaraka ya Rais, akiwa mgombea huru, hatazuiwa kumpendekeza mtu yeyote kuwa mgombea nafasi ya madaraka ya Makamu wa Kwanza wa Rais kwa sababu tu kwamba mtu huyo kwa wakati huo ameshika kiti cha Rais wa
Zanzibar.
Ibara ya 101.
Majukumu ya makamu wa kwanza ya Rais Ibara hii haikuwepo ila majukumu hayo yameainishwa katika ibara ya 90. 101. Makamu wa Kwanza wa Rais atakuwa ni Msaidizi Mkuu wa Rais kuhusu mambo yote ya Jamhuri ya Muungano na:
(a) atafanya kazi zote atakazoagizwa na Rais;
(b) atafanya kazi za Rais kama Rais hayupo kazini au yupo nje ya nchi
kwa kuzingatia masharti ya Ibara ya 83(3); na
(c) atakuwa Mwenyekiti wa Tume ya Usimamizi na Uratibu wa Mambo
ya Muungano. Majukumu ya makamu wa rais yametengewa ibara yake. Iko vizuri.
Lengo lake ni kutoa mwanga na taswira ya jinsi gani wananchi wapate kujua na kufahamu shughuli zake.
Ibara ya 102.
Muda wa makamu wa kwanza wa Rais kushika madaraka 94.-(1) Makamu wa Rais atashika nafasi ya madaraka ya Makamu wa Rais siku hiyo hiyo Rais anaposhika madaraka.
102.-(1) Makamu wa Kwanza wa Rais atashika nafasi ya madaraka ya Makamu wa Kwanza wa Rais mara tu Rais anaposhika madaraka yake baada ya kuwa ameapishwa. Hakuna mabadiliko Iko vizuri. Inaweka wazi mda na taratibu za makamu wa raisi kushika nyazifa.
Mda wa siku 7 au 14 unafaa kabisa kwa mtu aliyechaguliwa kujipanga. Na pia kuheshimu uhamzi halali wa Mahakama.
Ibara ya 103.
Bunge kumshtaki makamu wa kwanza wa Rais 95.-(1) Bunge litakuwa na mamlaka ya kumshtaki na kumuondoa Makamu wa Rais madarakani kwa utaratibu unaotumika kumshtaki Rais kwa mujibu wa Katiba hii, isipokuwa kwamba, hoja yoyote ya kumshtaki Makamu wa Rais itatolewa tu iwapo:
103.-(1) Bunge litakuwa na mamlaka ya kumshtaki na kumuondoa Makamu wa Kwanza wa Rais madarakani kwa utaratibu unaotumika kumshtaki
Rais kwa mujibu wa Katiba hii, isipokuwa kwamba, hoja yoyote ya kumshtaki Makamu wa Kwanza wa Rais itatolewa tu iwapo: Hakuna mabadiliko Hakuna mabadiliko
Ibara ya 104.
Makamu wa Kwanza wa Rais kushindwa kumudu majukumu yake
Ibara hii haikuwepo 104. Endapo Makamu wa Kwanza wa Rais hawezi kumudu kazi zake kwa sababu ya maradhi ya mwili au akili, Rais anaweza, baada ya kushauriana na Baraza la Mawaziri, kuwasilisha kwa Jaji Mkuu azimio la kumwomba Jaji Mkuu athibitishe kwamba Makamu wa Kwanza wa Rais, kwa sababu ya maradhi ya mwili au akili hawezi kumudu kazi zake na masharti mengine ya Ibara ya 84 yatatumika. Iko vizuri Iko vizuri
Ibara ya 105.
Upatikanaji wa makamu wa kwanza wa rais wakati nafasi hiyo inapokuwa wazi. 96. Endapo nafasi ya madaraka ya Makamu wa Rais iko wazi kutokana na masharti yaliyomo katika Ibara ya 94 na 95, basi mapema iwezekanavyo na kwa vyovyote vile ndani ya siku zisizozidi kumi na nne tokea kifo au baada ya kuachia madaraka, Rais atamteua mtu atakayekuwa Makamu wa Rais na uteuzi huo utathibitishwa na Bunge kwa kura za Wabunge zaidi ya asilimia hamsini ya Wabunge wote.
105. Endapo nafasi ya Madaraka ya Makamu wa Kwanza wa Rais iko wazi kutokana na masharti yaliyomo katika Ibara ya 99 na 100, basi mapema iwezekanavyo na kwa vyovyote vile ndani ya siku zisizozidi kumi na nne tokea
kifo au baada ya kuachia madaraka, Rais atamteua mtu atakayekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais na uteuzi huo utathibitishwa na Bunge kwa wingi wa kura za Wabunge wote. Kipengele cha kura za wabunge kuwa zaidi ya 50% kimeondolewa. Idadi ya kura za wabunge inatakiwa kuzidi 50% na sio wingi wa kura tu.
Suala hili la wingi wa kura ni suala la kisiasa, kwani halina mshiko katika mkutadha wa haki na uhalisia.

Ni lengo lenye kutaka kukidhi haja za watawala.
Ibara ya 106.
Kiapo cha makamu wa kwanza wa Rais. 93. Makamu wa Rais, kabla ya kushika madaraka yake ataapishwa na Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, kiapo cha uaminifu na pia kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi yake kitakachowekwa kwa mujibu wa sheria za nchi.
106. Makamu wa Rais, kabla ya kushika madaraka yake ataapishwa na Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano au Naibu Jaji Mkuu endapo Jaji Mkuu
hayupo, kiapo cha uaminifu na kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi yake kitakachowekwa kwa mujibu wa Sheria. Hakuna mabadiliko Hakuna mabadiliko
Ibara ya 107.
Makamu wa pili wa rais Ibara hii haikuwepo 107.-(1) Makamu wa Pili wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye ni Rais wa Zanzibar, pamoja na majukumu mengine yaliyoainishwa katika Katiba ya Zanzibar, ataanza kushika nafasi ya madaraka ya Makamu wa Pili wa Rais mara baada ya kuapishwa na Rais. Ibara hii imeongezwa Majukumu yake hayajaainishwa.
Ni kiongozi anayekula viapo viwili.
Na ni suala ambalo linazidisha gharama za uendeshaji wa serikali badala ya kupunguza matumizi ya serikali.

Jambo hili litazidi kuwalemea wananchi wa Tanzania amabo ndiyo walipa kodi za kulipa mishahala na malupulupi ya viongozi.
Ibara ya 108.
Makamu wa tatu wa rais Ibara hii haikuwepo 108.-(1) Makamu wa Tatu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye ni Waziri Mkuu, pamoja na majukumu mengine yaliyoainishwa katika Katiba hii,
atashika madaraka baada ya kuapishwa na Rais. Ibara hii imeongezwa Majukumu ya waziri mkuu yameongezwa.

Ni nafazi ambayo inazidi kuleta mkanganyiko hasa katika utendaji. Wakati upi atafanya kazi kama Makamu wa tatu wa rais na akiwa Waziri Mkuu.

Ni nafasi inayozidi kuibinya Zanzibar kwani ni nafasi inayomtambua kuwa kiongozi wa Jamhuri ya Muungano na siyo rais ya Zanzibar

Ibara ya 109.
Maslahi ya Makamu wa Rais Ibara hii haikuwepo 109.-(1) Makamu wa Rais atalipwa mshahara na malipo mengine, na atakapostaafu atapokea malipo ya uzeeni, kiinua mgongo au posho kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina. Iko vizuri Ibara hii haina masilahi kwa Watanzania. Kwani ni nafasi inayozidi kuongeza gharama zaidi ya kuzipunguza.

Ibara ya 110.
Waziri mkuu wa jamhuri ya muungano Ibara hii haikuwepo (2) Mshahara na malipo Cheo cha waziri mkuu kimerudishwa. Maoni ya rasimu ya pili hayajazingatiwa.
Ibara ya 111.
Kazi na mamlaka ya waziri mkuu Ibara hii haikuwepo 111.-(1) Waziri Mkuu atakuwa na madaraka juu ya udhibiti, usimamizi na utekelezaji wa siku hadi siku wa kazi na shughuli za Serikali ya Jamhuri ya Muungano. Madaraka ya waziri mkuu kama yalivyokuwa kwenye Katiba ya 1977 yamerudishwa. Maoni ya rasimu ya pili hayajazingatiwa.
Ibara ya 112.
Uwajibikaji wa serikali Ibara hii haikuwepo 112. Bila kuathiri masharti ya Katiba hii, Waziri Mkuu atawajibika kwa Rais kuhusu utekelezaji wa madaraka yake.
Madaraka ya waziri mkuu kama yalivyokuwa kwenye Katiba ya 1977 yamerudishwa. Maoni ya rasimu ya pili hayajazingatiwa.
Kwani Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilipendekeza
Ibara ya 113.
Kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu Ibara hii haikuwepo 113.-(1) Bila ya kujali masharti ya Ibara ya 105 ya Katiba hii, Bunge linaweza kupitisha azimio la kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu endapo itatolewa hoja kupendekeza hivyo na ikapitishwa kwa mujibu wa masharti ya Ibara hii. Madaraka ya waziri mkuu kama yalivyokuwa kwenye Katiba ya 1977 yamerudishwa. Maoni ya rasimu ya pili hayajazingatiwa
Ibara ya 114.
Baraza la mawaziri 97.-(1) Kutakuwa na Baraza la Mawaziri la Jamhuri ya Muungano litakalokuwa na wajumbe wafuatao:
(a) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano; na
(b) Waziri Mwandamizi na Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
(4) Baraza la Mawaziri ndicho chombo kikuu cha kumshauri Rais kuhusu mambo yanayohusu utekelezaji wa madaraka na matumizi ya mamlaka ya Rais. 114.-(1) Kutakuwa na Baraza la Mawaziri la Jamhuri ya Muungano ambalo litakuwa na wajumbe wafuatao:
(a) Rais;
(b) Makamu wa Kwanza wa Rais;
(c) Rais wa Zanzibar ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais;
(d) Waziri Mkuu ambaye ni Makamu wa Tatu wa Rais; na
(e) Mawaziri wote wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano. Kuongezwa kwa kipengele cha wajumbe kama rais, rais wa Zanzibar, waziri mkuu na mawaziri wote wa serikali ya jamhuri ya muungano.

Kipengele cha mamlaka ya baraza la mawaziri kimeondolewa. Kuongezwa kwa wajumbe hao kutalifanya baraza la mawaziri kuwa na sura ya serikali zaidi.

Mamlaka ya baraza la mawaziri yamepunguzwa.

Pia Tume ilipendekeza kuwa Baraza la Mawaziri kiwe ndio chombo mhimu cha kumshauri rais. Katiba Inayopendekezwaimeondoa na hivyo kuwafanya wawe ni sehemu moja na rais hivyo kukosa ufanisi katka utendaji kazi za serikali.
Ibara ya 115.
Uteuzi wa mawaziri na naibu mawaziri. 98.-(1) Kutakuwa na Mawaziri na Naibu Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano watakaoteuliwa na Rais kwa kushauriana na Makamu wa Rais na baadaye kuthibitishwa na Bunge.
(2) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (1), idadi ya Mawaziri na Naibu Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano haitazidi kumi na tano.
(4) Uteuzi wa Mawaziri na Naibu Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano utazingatia uwakilishi wa Nchi Washirika. 115.-(1) Kutakuwa na Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano watakaoteuliwa na Rais kwa kushauriana na Makamu wa Rais.

(2) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (1), idadi ya Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano haitazidi thelathini.

(4) Pamoja na Mawaziri waliotajwa katika ibara ndogo ya (1), Rais aweza, baada ya kushauriana na Waziri Mkuu, kuwateua Naibu Mawaziri kutegemeana na mahitaji ya Serikali. Uteuzi wa mawaziri na manaibu mawaziri kutothibitishwa na bunge.

Ongezeko la idadi ya mawaziri wa serikali ya jamhuri ya muungano kuwa 30 bila manaibu mawaziri wao.

Uteuzi wa naibu mawaziri kutozingatia uwakilishi wa nchi washirika bali mahitaji ya serikali.
Mamlaka ya rais kuteua mawaziri na naibu mawaziri yameongezwa.

Ukubwa wa baraza la mawaziri ni mzigo.

Uteuzi wa naibu mawaziri bili
kuzingatia uwakilishi wan chi washirika unaweza kusababisha upendeleo.
Kazi ya kuwateua ingelifanywa na Tume ya Uteuzi kisha rais kuchagua na kuwapeleka Bungeni kuithinishwa. Hili limeondolewa na hivyo kuzidi kumrundikia raisi kazi nyingi sana.
Ibara ya 116.
Sifa za waziri na naibu waziri 101.-(1) Mtu atateuliwa kuwa Waziri au Naibu Waziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano ikiwa:
(b) awe na shahada ya chuo cha elimu ya juu kinachotambulika kwa mujibu wa sheria za nchi; na
(2) Watu wafuatao hawatakuwa na sifa ya kuteuliwa kuwa Mawaziri au Naibu Mawaziri katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano:
(a) Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Wabunge wa Bunge la Tanganyika, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la
Zanzibar au madiwani katika Nchi Washirika; 116.-(1) Mtu atateuliwa kuwa Waziri au Naibu Waziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano ikiwa:

(b) ana shahada ya chuo cha elimu ya juu kinachotambulika kwa mujibu wa sheria au ana elimu inayolingana;

(d) ni mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano. Kipengele cha elimu inayolingana na shahada ya chuo kikuu kimeongezwa.

Kipengele cha sifa cha kutokuwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Wabunge wa Bunge la Tanganyika, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la
Zanzibar au madiwani katika Nchi Washirika kimeondolewa. Maoni ya rasimu ya pili kuwa waziri na naibu waziri kutokuwa wanasiasa hayajazingatiwa.
Hii itazidi kuleta mkanganyiko hasa katika utendaji kazi wao.

Tume iliamua kutenganisha uwaziri na ubunge kwa ajili ya kuleta ufanisi. Kitendo cha kuwachanganya ni kuzolotesha utendaji kazi na kuweka ugumu wa uwajibikaji
Ibara ya 117.
Kiapo, muda na masharti ya kazi ya waziri na naibu waziri 102 (3) Kila Waziri anawajibika binafsi na kwa pamoja kwa Rais katika utekelezaji wa majukumu na katika kutumia nafasi ya madaraka ya Waziri.
Kipengele hiki kimeondolewa. Kipengele hiki kimeondolewa. Ni muhimu kipengele cha uwajibikaji kiwepo ili kumbana waziri na naibu waziri katika utendaji kazi.

Kwani bila kuwajibika hawatakuwa tayari kufanya kazi kwa ajili ya uzalendo na kutanguliza maslahi mapana ya Taifa
Ibara ya 118.
Mwanasheria mkuu wa serikali 104. kipengele cha mwanasheria mkuu kuwa mbunge hakikuwepo 118 (4) Mwanasheria Mkuu atakuwa Mbunge kutokana na wadhifa wake na atashika madaraka yake mpaka….. kipengele cha mwanasheria mkuu kuwa mbunge hakikuwepo Inaongeza idadi ya wabunge kwa serikali itayokuwa madarakani.

Imeizinisha Mwanasheria Mkuu kuwa mbunge. Hii ni kuzidi kulimbikiza madaraka mengi kwa mtu mmoja. Na hii itafanya kuzorotesha ufanisi na utendaji kazi za serikali.

Kitendo cha mwanasheria mkuu wa serikali juteuliwa na rais bila kudhinishawa na Bunge ni kupokonya madaraka ya wananchi kupitia uwakilishi wao wa Bungeni.
Ibara ya 119.
Naibu mwanasheria mkuu Ibara hii haikuwepo 119.-(1) Kutakuwa na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali
atakayeteuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watu wenye sifa zilizoainishwa katika ibara ndogo ya (2) ya Ibara ya 113. Uteuzi wa naibu mwanasheria mkuu wa serikali Iko vizuri
Ibara ya 120.
Mkurugenzi wa mashtaka Ibara hii haikuwepo 120.-(1) Kutakuwa na Mkurugenzi wa Mashtaka ambaye atateuliwa na Rais, kutoka miongoni mwa watumishi wa umma wenye sifa ya kufanya kazi ya uwakili au mtu mwenye sifa ya kusajiliwa kuwa wakili na amekua na sifa hizo mfululizo kwa muda usiopungua miaka kumi. Utararatibu na majukumu yake yatatungiwa sheria na bunge. Iko vizuri kiutendaji. Japokuwa upatikanaji wake ni wakutilia shaka.

Katibu Mkuu Kiongozi hakupaswa kuteuliwa moja kwa moja na rais kwani kwa kufanya hivyo ni kupokonya madaraka ya Bunge.

Bunge linatakiwa kumuidhinisha kutokana na ufanisi, weledi, ujuzi na sifa nyinginezo. Na baada ya kumuidhinisha rais angelimchagua au kukataa kumchagua nah ii ifanyike kwa sifa ya uwazi na si vinginevyo.
Ibara ya 121.
Katibu Mkuu
Kiongozi 105.-(1) Kutakuwa na Katibu Mkuu Kiongozi atakayeteuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watumishi waandamizi watatu katika utumishi wa umma watakaopendekezwa na Tume ya Utumishi wa Umma
na kuthibitishwa na Bunge. 121.-(1) Kutakuwa na Katibu Mkuu Kiongozi atakayeteuliwa na Rais kutoka miongoni mwa Maafisa Waandamizi walio katika nafasi ya uteuzi katika Utumishi wa Umma. Kipengele cha kuthibitishwa na bunge kimeondolewa. Madaraka ya rais katika nafasi za uteuzi yameongezwa.
Ibara ya 122.
Sekretarieti ya Baraza la Mawaziri 108.-(1) Kutakuwa na Sekretarieti ya Baraza la Mawaziri ambayo itakuwa na jukumu la kuhudumia Baraza la Mawaziri, Kamati Maalum ya Makatibu Wakuu na kutekeleza majukumu mengine kama itakavyopangiwa na Katibu wa Baraza la Mawaziri. 122.-(1) Kutakuwa na Sekretarieti ya Baraza la Mawaziri ambayo itakuwa na jukumu la kuhudumia Baraza la Mawaziri na kutekeleza majukumu mengine kama itakavyopangiwa na Katibu wa Baraza la Mawaziri. Hakuna mabadiliko Iko vizuri
Ibara ya 123.
Ibara hii haikuwepo 123.-(1) Kutakuwa na Mkuu wa Mkoa kwa kila mkoa katika Jamhuri ya Muungano ambaye, bila kuathiri ibara ndogo ya (3), atakuwa ni kiongozi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano. Ibara hii ingeweza kuingia kwenye katiba za nchi washirika.
Wakuu wa Mikoa ana wilaya si sehemu ya Muungano. Bali nafasi hizi zijadiliwe kwenye katiba za nchi washirika.
Ibara ya 124.
Serikali za Mitaa Ibara hii haikuwepo 124.-(1) Kutakuwa na Serikali za Mitaa katika kila mkoa, manispaa, wilaya, mji na kijiji katika Jamhuri ya Muungano ambazo zitakuwa za aina na majina yatakayowekwa na sheria itakayotungwa na Bunge au na Baraza la Wawakilishi. Maoni ya rasimu ya pili ya katiba hajazingatiwa. Ibara hii ingeweza kuingia kwenye katiba za nchi washirika
Ibara ya 125.
Mamlaka ya
Serikali za Mitaa Ibara hii haikuwepo Majukumu ya serikali za mitaa yameainishwa Ibara hii ingeweza kuingia kwenye katiba za nchi washirika
Ibara ya 126.
Uongozi katika Serikali za Mitaa Ibara hii haikuwepo 126. Uongozi katika Serikali za Mitaa utakuwa na uwakilishi wa
wananchi, na viongozi wa Serikali za Mitaa watapatikana kupitia mchakato wa uchaguzi au uteuzi kwa mujibu wa sheria itakayotungwa na Bunge au Baraza la Wawakilishi. Ibara hii ingeweza kuingia kwenye katiba za nchi washirika

SURA YA 9 Katiba Inayopendekezwa Na SURA 8 Rasimu ya Pili ya Katiba:
Ibara Rasimu ya Pili Katiba Inayopendekezwa Tofauti Maoni
Kichwa cha Habari UHUSIANO NA URATIBU WA SERIKALI UHUSIANO NA URATIBU WA MAMBO YA MUUNGANO Katika rasimu ya pili ya katiba kichwa cha habari kinalenga kuangalia mahusiano ya serikali za nchi washirika na katiba inayopendekezwa inaangalia uratibu wa mambo ya Muungano Ni mambo mawili tofauti yasiyofanana. Serikali za nchi washirika na mambo ya Muungano haviwezi kuwa na uzito sawa
109 (1) sasa 122(1) 109(1) Kutakuwa na Tume ya kusimamia na kuratibu mahusiano baina ya Serikali ya Muungano na Serikali za nchi Washirika an Kusimamia na kuratibu uhusiano baina ya Serikali za Nchi washirika, ambayo itajulikana kwa kifupi kama “Tume ya Uhusiano na Uratibu wa Serikali” 122.-(1) Kutakuwa na Tume ya Usimamizi na Uratibu wa Mambo ya Muungano ambayo itajulikana kwa kifupi kama “Tume ya Mambo ya Muungano”. Tofauti ni kwamba; Katiba inayopendekezwa inaunda tume ya mambo ya Muungano na rasimu ya pili inaunda tume ya uhusiano na uratibu wa serikali. Hivyo basi tume ya kuratibu mambo ya Muungano inayopendekezwa itakuwa haina nguvu kama serikali hazina chombo kinachokuza mahusiano na kuratibu utendaji wake. Tume inayopendekezwa ya mambo ya Muungano haina tofaouti na tume nyingi za mambo ya Muungano zilizowahi kuundwa kabla katika mfumo wa sasa mpaka kuwa na wizara kabisa ya mambo ya Muungano lakini bado kuna kero nyingi za Muungano Inapendekezwa tuwe na tume ya kuratibu serikali kama ilivyo kwenye rasimu ya pili kwa sababu ni ngazi ya juu ki utawala endapo serikali zitaratibiwa ili kukuza mahusiano kati ya pande mbili za Muungano.
Tume ilipendekeza kuwepo na serikali 3. Jamhuri ya Muungano, Jamhuri ya watu wa Zanzibar na Tanganyika. Hivyo kuyaacha mabo hayo ya msingi ni kuidhalau Tume.
109(2) sasa 122(2) Tume ya Uhusiano na Uratibu wa Serikali itakuwa na wajumbe wafuatao
(a) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye atakuwa Mwenyekiti; (b) Rais wa Tanganyika; (c) Rais wa Zanzibar (d) Mawaziri wakaazi (e) Waziri mwenye dhamana ya mambo ya nje wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano. (2) Tume ya Mambo ya Muungano itakuwa na wajumbe wafuatao: (a) Makamu wa Kwanza wa Rais ambaye atakuwa Mwenyekiti; (b) Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano; (c) Kiongozi wa shughuli za Serikali katika Baraza la Wawakilishi; na (d) Mawaziri wenye dhamana ya masuala ya Muungano. Katika katiba inayopendekezwa viongozi wanaounde tume ya uratibu wa mambo ya Muungano watakuwa na mgongano mkubwa wa maslahi kwani makamu wa rais, waziri mkuu wote ni viongozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wenye mamlaka katika pande zote za Muungano. Upande mmoja wa Muungano hautawakilishwa kwa uwiano ulio sawa.
Pia viongozi wanaopendekezwa katika nafasi za uratibu hawana maamuzi ya mwisho kwani ni mawaziri watahitaji ridhaa ya rais.
Bado mfumo unaopendekwa na rasimu ya pili ya katiba una tija kwa taifa kwa sababu kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano (Makamu wa Rais) atakaa na viongozi (marais) wawili wa nchi washirika na kufikia maamuzi.
Utaratibu unaopendekezwa utachelewesha maamuzi na kuongeza kero za Muungano na si kutoa utatuzi wa mara moja
122(3)
(3) Mwenyekiti wa Tume ya Mambo ya Muungano anaweza kumwalika mtu yeyote atakayeona anafaa kwa ajili ya kufafanua jambo kwenye Tume kabla ya kufikia uamuzi. Ibara Mpya Ni ibara isiyo na tija kwa taifa kwani imetoa mwanya kwa mtu yeyote bila kuanisha sifa mathalani mtu yeyote anaweza kuwa raia wa nje ya Tanzania
110(1) sasa 123(1) Tume ya Uhusiano na Uratibu wa Serikali itakuwa na jukumu maalum la kuwezesha uratibu na ushirikiano katika kutekeleza masharti ya katiba hii, sera, sheria, mipango na mikakati baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali za Nchi Washirika na baina ya Serikali za Nchi Washirika na pia itakuwa chombo maalum kwa ajili ya
(a) Kushauriana na kushirikiana baina ya-(i) Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali za Nchi Washirika; na (ii) Serikali za Nchi Washirika zenyewe katika masuala yasiyo ya Muungano 123.-(1) Tume ya Mambo ya Muungano itakuwa na jukumu maalum la kuwezesha uratibu na ushirikiano katika kutekeleza masharti ya Katiba hii, sera, sheria, mipango na mikakati baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na pia itakuwa chombo maalum kwa ajili ya: (a) kuweka utaratibu bora na endelevu wa kushauriana na kushirikiana baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar;
(b) kusimamia, kuratibu na kuhakikisha kwamba kuna kuwiana kwa sera na sheria za Nchi Washirika katika mambo yasiyo ya Muungano; (b) kuweka mazingira wezeshi kwa ajili ya kuratibu na kusimamia, utekelezaji wa Mambo ya Muungano kwa manufaa ya ustawi wa wananchi wote;
(c) Kushauriana na kushirikiana baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na taasisi za kimataifa kwa niaba ya Nchi Washirika; (c) kupendekeza na kusimamia utaratibu utakaowezesha uwakilishi wa pande zote mbili za katika maeneo na masuala mbalimbali kwa nia ya kukuza umoja na mshikamano katika utekelezaji wa Mambo ya Muungano;
(d) usimamizi na ukuzaji wa masuala yenye maslahi kwa Taifa; (d) kukuza na kuwezesha uratibu na ushirikiano baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika Mambo yasiyo ya Muungano kwa lengo la kuwezesha kufanana kwa kiwango cha utoaji huduma kwa wananchi wote;
(e) usuluhuhishi na utatuzi wa migogoro baina ya – (i) Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali za Nchi Washirika; na (ii) Serikali za Nchi Washirika katika mambo yasiyo ya Muungano (e) kuratibu masuala yenye maslahi kwa Taifa; na (f) kusimamia uwakilishi wa pande zote mbili za Muungano katika masuala ya ajira katika utumishi wa Jamhuri ya Muungano.
(2) Kwa madhumuni ya Ibara ndogo ya (1)(e), endapo upande wowote katika mgogoro hautaridhika na uamuzi wa Tume ya uhusiano na uratibu wa Serikali, unaweza kulipeleka suala hilo katika Mahakama ya Juu na uamuzi wa mahakama hiyo utakuwa ni wa mwisho (2) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (1)(f), Tume ya Mambo ya Muungano itaweka utaratibu utakaowezesha uteuzi wa viongozi na watumishi katika taasisi au wizara za Muungano. (3) Bunge litatunga sheria itakayofafanua: (a) utaratibu wa utekelezaji wa majukumu ya Tume; (b) uanzishwaji, muundo na majukumu ya Sekretarieti ya Tume ya Mambo ya Muungano; na (c) mambo mengine yote yanayohusu Tume ya Mambo ya Muungano.
(3) Bunge litatunga sheria kwa ajili ya-
(a) kusimamia uhusiano na uratibu baina ya Serikali za Nchi Washirika na kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali za Nchi Washirika; na (b) kuweka utaratibu wa utatuzi wa migogoro kwa mujibu wa Ibara hii. Imefutwa
112 (rasimu ya pili) 112(1) Kutakuwa na Sekretariati ya Tume ya Uhusiano na Uratibu wa Serikali itakayoongozwa na Katibu akisaidiwa na Naibu Katibu ambao watateuliwa na Rais. (2) Mtu atateuliwa kuwa Katibu au Naibu Katibu ikiwa ana sifa zifuatazo: (a) ni mtumishi mwandamizi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano au Serikali za nchi washirika; (b)ana shahada kutoka chuo cha elimu ya juu kinachotambulika kwa mujibu wa sheria za nchi; na (c) ana mwenendo usiotiliwa shaka na jamii (3) Katibu na Naibu Katibu watawajibika kwa Tume na watafanya kazi na kutekeleza majukumu ya Sekretarieti. (4) Uteuzi wa Katibu na Naibu Katibu wa Tume utafanywa kwa kuzingatia msingi kwamba endapo Katibu atateuliwa kutoka upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano, basi Naibu Katibu atateuliwa kutoka upande wa pili wa Jamhuri ya Muungano

madhumuni ya ibara ndogo ya (1)(f), Tume ya Mambo ya Muungano itaweka utaratibu utakaowezesha uteuzi wa viongozi na watumishi katika taasisi au wizara za Muungano. (3) Bunge litatunga sheria itakayofafanua: (a) utaratibu wa utekelezaji wa majukumu ya Tume; (b) uanzishwaji, muundo na majukumu ya Sekretarieti ya Tume ya Mambo ya Muungano; na (c) mambo mengine yote yanayohusu Tume ya Mambo ya Muungano.

SURA YA 10 (BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO:
Ibara Rasimu ya Pili Katiba Inayopendekezwa Tofauti Maoni
SEHEMU YA KWANZA: MUUNDO NA MADARAKA YA BUNGE
113(1) sasa 129(1) Bunge 113(1) Kutakuwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano 129.-(1) Kutakuwa na Bunge ambalo litakuwa na sehemu mbili, yaani Rais na Wabunge. Rais kufanywa kuwa sehemu ya bunge Pendekezo la Katiba inayopendekezwa la kumfanya rais kuwa sehemu ya bunge ni kinyume na utawala wa sheria hasa mgawanyo wa madaraka. Rais ni sehemu ya serikali hivyo hakutakuwa na mgawanyo wa madaraka na mamlaka. Rais ataingilia sana utendaji wa Bunge. Mfano sheria ya mabadiliko ya katiba imerudishwa mara kadhaa bungeni kwa matakwa ya Rais na bunge kushindwa kusimamia mamlaka yake ya kibunge
113(2) sasa 129(2) Wajumbe wa Bunge watakuwa watakuwa wa aina zifuatazo
(a) Wabunge sabini wa kuchaguliwa kupitia majimbo ya uchaguzi, hamsini kutoka Tanganyika na ishirini kutoka Zanzibar, na (b) Wabunge watano wenye ulemavu watakaoteuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watu wenye sifa za kuchaguliwa kuwa wabunge kuwakilisha watu wenye ulemavu kwa kuzingatia uwakilishi wa Nchi Washirika na jinsi. (2) Kutakuwa na aina zifuatazo za Wabunge: (a) wabunge wa kuchaguliwa kupitia majimbo ya uchaguzi yatakayotangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi; (b) wabunge watano wenye ulemavu watakaoteuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watu wenye sifa za kuchaguliwa kuwa wabunge; (c) wabunge wasiozidi kumi watakaoteuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watu wenye sifa za kuwa wabunge; (d) Spika iwapo hatakuwa amechaguliwa kutoka miongoni mwa Wabunge; na (e) Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Rasimu ya pili inapendekeza aina na idadi za wabunge katika shirikisho la Jamhuri ya Muungano wakati Katiba inayopendekezwa inazungumzia aina za wabunge katika Jamhuri ya Muungano Mfumo unaopendekezwa na aina za wabunge wanaopendekezwa hauna tofauti na mfumo katika katiba ya sasa; Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 ambapo kumekuwa na malalamiko mengi kwamba kwanini wabunge wa kutoka upande wa Zanzibar wanatunga sheria zisizotumika Zanzibar, zile zinazotumika Zanzibar hupaswa kupitishwa tena na Baraza la Wawakilishi, lakini pia kazi ya usimamizi wa serikali ina mkinzano baina ya wabunge kutoka upande wa Zanzibar kuisimamia serikali ya Muungano hata katika kupanga na kupitisha bajeti inayotekelezwa upande mmoja wan chi. Hivyo basi mfumo uliopendekezwa kwenye rasimu ya pili ulikuwa bora zaidi ya huu unaopendekezwa kwenye katiba inayopendekezwa.
Tume ilipendekeza spika na naibu wasiwe wabunge.
Pia kuna tofauti katika Muundo.
Kwa muundo wa Bunge hili litazidi kuongeza idadi ya Wabunge. Tofauti na inavyo semwa na wajumnbe wa Bunge maalumu kuwa muundo wa Bunge hili litapunguza idadi ya wabunge bungeni siyo kweli.
113(3) Katika kila jimbo la uchaguzi kutakuwa na nafasi mbili za ubunge, moja kwa ajili ya mwanamke na moja kwa ajili ya mwanamme 129(4) Bla kuathiri masharti ya Ibara hii, msingi wa uwakilishi katika ibara ndogo ya (2)(a), utazingatia uwakilishi ulio sawa kati ya wabunge wanawake na wanaume Rasimu ya pili inatoa mchakato wa kupata asilimia; wakati Katiba inayopendekezwa haitoi namna ya jinsi huo uwiano utakavyopatika Ibara ya 66(1)(b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ni bora zaidi ya ibara hii katika Katiba inayopendekezwa kwa sababu inatoa maelekezo ya namna ya kuleta uwiano walau kwa asilimia thelathini ya wabunge wote. Lugha ya kuzingatia inaweza kutafsiriwa uwakilishi wa idadi yoyote ile ya wanawake na ikawa sasa hii kwa sababu dhana ya usawa katika uwakilishi kwa sasa haiangalii namba (idadi) bali uwepo wa wanawake (quota system). Hivyo Ibara hii inanyima fursa ya 50/50 kama ilivyopendekezwa kwenye Rasimu ya Pili.
113(4) Wabunge kutoka kila jimbo la Uchaguzi watapatikana kwa kupigiwa kura na wananchi kwa mujibu wa masharti ya katiba hii na sheria inayoweka utaratibu kuhusu mambo ya uchaguzi I29(3) Wabunge waliotajwa katika ibara ndogo ya (2)(a) watapatikana kwa kupigiwa kura na wananchi kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii na sheria itakayotungwa na Bunge. Hakuna Ipo sawa
(5) Bila kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (2), idadi ya wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano waliochaguliwa au kuteuliwa haitazidi mia tatu na sitini.
(6) Bunge litatunga sheria itakayoainisha utaratibu wa utekelezaji wa masharti ya Ibara hii. Mpya Idadi ya wabunge inayopendekezwa kwenye katiba inayopendekezwa bado ni kubwa kwani idadi ya sasa pia inapigiwa kelele na wananchi kwamba ni kubwa ipunguzwe.
114 sasa
130 Muda wa Bunge 114(1) Bila kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, maisha ya kila Bunge yatakuwa ni muda wa miaka mitano 130(2)Bila kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, maisha ya kila Bunge yatakuwa ni muda wa miaka mitano Hakuna Ipo sawa
114(2) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (1), maneno “maisha ya Bunge” maana yake ni muda wote unaoanzia tarehe ambapo Bunge Jipya litaitishwa ili kukutana kwa mara ya kwanza baada ya uchaguzi wa wabunge na kuishia tarehe ya kuvunjwa kwa Bunge kwa ajili ya kuwezesha uchaguzi mwingine kufanyika (2) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (1), maneno “maisha ya Bunge” maana yake ni muda wote unaoanzia tarehe ambapo Bunge Jipya litaitishwa ili kukutana kwa mara ya kwanza baada ya uchaguzi wa wabunge na kuishia tarehe ya uchaguzi mwingine wa wabunge. Hakuna hakuna
115 sasa 131 Madaraka ya Bunge 115(1) Bunge ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano chenye madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu 131 (2) Sehemu ya Pili ya Bunge ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano chenye madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii.
Ukuu wa bunge (parliamentary supremacy) kwenye rasimu ya pili imeelezwa bayana wakati katiba inayopendekezwa ina toa ukuu wa nchi kwenye Serikali (Executive) Katika nchi za kidemokrasia Parliamentary Supremacy ndio msingi mkuu wa uongozi lakini kwenye utawala wa kidikteta basi Executive huwa na nguvu zaidi ya Bunge. Hivyo mfumo unaopendekezwa kwenye katiba inayopendekezwa hauna tija kwa taifa linalokuza demokrasia kama msingi wa uongozi.
Pia Hayati mwalimu Nyerere aliwahi kusema kwa katiba hii tuliyonayo ambayo kwa pendekezo katika Ibara hii zinafanana sana kwamba anaweza kuwa dikteta
Hakuna (1) Rais kama sehemu ya Bunge atatekeleza mamlaka yote aliyokabidhiwa kwa mujibu wa Katiba hii. Mpya Rais (Serikali) haipaswi kuwa chombo kikuu katika nchi isipokuwa bunge kuwa chombo kikuu. Hivyo napendekeza kwa ajili ya uwajibikaji Rais asiwe sehemu ya bunge
(2) Katika kutekeleza majukumu yake, Bunge litakuwa na madaraka yafuatayo: (a) kutunga sheria pale ambapo utekelezaji unahitaji kutungiwa sheria; (b) kujadili na kutoa ushauri katika mambo yote yenye maslahi kwa Taifa na umma wa Watanzania; (c) kumuuliza Waziri yeyote suala lolote kuhusu mambo ya umma katika Jamhuri ya Muungano ambayo yako katika wajibu wake; (d) kujadili mgawanyo na kuidhinisha matumizi ya fedha kwa Wizara, taasisi na mashirika ya Serikali; (e) kujadili utekelezaji wa majukumu ya kila Wizara wakati wa Mkutano wa Bunge wa kila mwaka wa bajeti; (f) kujadili na kuidhinisha mpango wowote wa muda mrefu, muda wa kati au muda mfupi unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali katika Jamhuri ya Muungano; (g) kujadili na kuridhia mikataba ya kimataifa inayohusu Jamhuri ya Muungano na ambayo kwa masharti yake inahitaji kuridhiwa; na (h) kujadili na kuridhia mikataba yote inayohusisha rasilimali zinazosimamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano (3) Katika kutekeleza majukumu yake, Bunge litakuwa na madaraka yafuatayo: (a) kutunga sheria pale ambapo utekelezaji unahitaji kutungiwa sheria; (b) kujadili na kutoa ushauri katika mambo yote yenye maslahi kwa Taifa na umma wa Watanzania; (c) kumuuliza Waziri yeyote suala lolote kuhusu mambo ya umma katika Jamhuri ya Muungano ambayo yako katika wajibu wake; (d) kujadili mgawanyo na kuidhinisha matumizi ya fedha kwa Wizara, taasisi na mashirika ya Serikali; (e) kujadili utekelezaji wa majukumu ya kila Wizara wakati wa Mkutano wa Bunge wa kila mwaka wa bajeti; (f) kujadili na kuidhinisha mpango wowote wa muda mrefu, muda wa kati au muda mfupi unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali katika Jamhuri ya Muungano; (g) kujadili na kuridhia mikataba ya kimataifa inayohusu Jamhuri ya Muungano na ambayo kwa masharti yake inahitaji kuridhiwa; na (h) kuthibitisha mapendekezo ya uteuzi wa viongozi kwa mujibu wa Katiba hii na Sheria. Katiba inayopendekeza imefuta kabisa ibara hii ambayo ni muhimu sana (h) kujadili na kuridhia mikataba yote inayohusisha rasilimali zinazosimamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano badala yake wameweka ibara hii (h) kuthibitisha mapendekezo ya uteuzi wa viongozi kwa mujibu wa Katiba hii na Sheria. Ambayo katika ibara nyingine wamempa mamlaka rais kuteua bila kuwa na sharti la kuidhinishwa na bunge Ibara hii ni muhimu ikarejeshwa kwani sasa kuna uporaji mkubwa wa rasilimali za taifa letu la Tanzania.
Suala la Mbunge kuwa na mamlaka ya kumhoji Waziri ni utata. Kama waziri anatokana na wabunge, na kwa hali ya kawaida siyo raisi kuwajibishwa na watu ambao wako chini yake kiutendaji.

Kipengele cha Bunge kujadili na kuridhia mikataba kimeondolewa. Kitendo hiki hakikubariki hata kidogo, kwani Bunge lina kazi na majukumu makubwa ya kulinda mali ya Taifa letu. Kuondoa jukumu hili kwa wabunge ni kuwapokonya wajibu wao wa kikatiba. Na hali hii itachangia au kupelekea bunge kushindwa kuiwajibisha serikali.
116 sasa 132 Mipaka ya Bunge katika kutumia madaraka yake 116.-(1) Katika kutekeleza madaraka ya kuisimamia Serikali kwa mujibu wa Katiba hii, wajibu wa Bunge utakuwa ni kuishauri Serikali na endapo Bunge halitaridhishwa na hatua zilizochukuliwa na Serikali katika utekelezaji wa suala lililotolewa ushauri, basi Bunge litakuwa na haki ya kuiwajibisha Serikali kwa mujibu wa madaraka lililopewa katika Katiba hii. (2) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (1), Bunge halitachukua hatua yoyote ya kiutendaji ambayo, kwa desturi ni shughuli za Serikali, na halitatoa maagizo yoyote ya kiutendaji kwa Serikali na watumishi wa umma: Isipokuwa kwamba, Bunge litashauri kuhusu suala lolote lililo katika dhamana ya Waziri anayehusika. 132.-(1) Katika kutekeleza madaraka ya kuisimamia Serikali kwa mujibu wa Katiba hii, wajibu wa Bunge utakuwa ni kuishauri Serikali na endapo Bunge halitaridhishwa na hatua zilizochukuliwa na Serikali katika utekelezaji wa suala lililotolewa ushauri, basi Bunge litakuwa na haki ya kuiwajibisha Serikali kwa mujibu wa madaraka lililopewa katika Katiba hii. (2) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (1), Bunge halitachukua hatua yoyote ya kiutendaji ambayo, kwa desturi ni shughuli za Serikali, na halitatoa maagizo yoyote ya kiutendaji kwa Serikali na watumishi wa umma: Isipokuwa kwamba, Bunge litashauri kuhusu suala lolote lililo katika dhamana ya Waziri anayehusika. Hakuna Bunge linapaswa kuwa na masilahi mapana na ulinzi wa maliasili na Taifa kwa ujumla wake.Hivyo bila kikwazo chochote linapaswa kuwa na mamlaka na uwezo wa kuhoji na kushauri serikali.
117 sasa 133 Madaraka ya kutunga sheria 117(1) Madaraka ya kutunga sheria kwa mambo yote yanayohusu Jamhuri Muungano yatakuwa chini ya Bunge la jamhuri ya Muungano. 133.-(1) Mamlaka yote ya kutunga sheria juu ya mambo mengine yote yahusuyo Tanzania Bara, yatakuwa mikononi mwa Bunge.
Matumizi ya neno “Mamlaka na Madaraka” Matumizi ya maneno yawekwe bayana ili kuleta ufanisi wa kiutendaji.
(2)Madaraka ya kutunga sheria katika Tanganyika kwa mambo yote yasiyo ya Muungano yatakuwa chini ya Bunge la Tanganyika na madaraka ya kutunga sheria katika Zanzibar kwa mambo yote yasiyo ya Muungano yatakuwa chini ya Baraza la wawakilishi la Zanzibar (2) Mamlaka yoyote ya kutunga sheria katika Zanzibar juu ya mambo yote yasiyo ya Muungano yatakuwa mikononi mwa Baraza la Wawakilishi.

Matumizi ya neno “Mamlaka na Madaraka” Ipo haja ya kuendelea kupigani haki hii kwa upande wa Tanganyika kuwa na bunge lake kama ilivyo upande wa Zanzibar
(3) Endapo sheria iliyotungwa na Bunge inahusu jambo lolote ambalo liko chini ya mamlaka ya Bunge la Tanganyika au Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, sheria hiyo itakuwa batili na itatenguka (3) Endapo sheria yoyote iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi inahusu jambo lolote katika Zanzibar ambalo liko chini ya mamlaka ya Bunge, sheria hiyo itakuwa batili na itatanguka na pia endapo sheria yoyote iliyotungwa na Bunge inahusu jambo lolote ambalo liko chini ya mamlaka ya Baraza la Wawakilishi, sheria hiyo itakuwa batili na itatanguka. Sheria itakayotenguka ni ile itakayotungwa na baraza la wawakilishi Ukuu wa katiba ya Zanzibar baaada ya mabadiliko 2010 inapaswa kutiliwa maanani je? Zanzibar itakubaliana na Ibara hii? Zipo sheria nyingi upande wa Zanzibar zinakinzana na katiba ya Jamhuri lakini hakuna utashi wa kutatua utata huo. Mfano Sheria ya Mzanzibari, 1985 ni sheria ya kibaguzi lakin haijawahi kutenguliwa.
Hali hii itazidi kuleta utata.
(4) Endapo sheria iliyotungwa na Bunge la Tanganyika au Baraza la Wawakilisha la Zanzibar inahusu jambo lolote ambalo liko chini ya mamlaka ya Bunge la Jamhuri ya Muungano, Sheria hiyo itakuwa batili na itatenguka
(4) Sheria yoyote iliyotungwa na Bunge kuhusu jambo lolote haitatumika Zanzibar isipokuwa kwa mujibu wa masharti yafuatayo: (a) Sheria hiyo iwe imetamka wazi kwamba itatumika Tanzania Bara na vilevile Zanzibar au iwe inabadilisha, kurekebisha au kufuta sheria inayotumika Zanzibar; (b) Sheria hiyo iwe inabadilisha au kurekebisha au kufuta sheria iliyokuwa inatumika tangu zamani Tanzania Bara ambayo ilikuwa inatumika pia Zanzibar kwa mujibu wa Mapatano ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ya mwaka 1964, au kwa mujibu wa sheria yoyote ambayo ilitamka wazi kwamba itatumika Tanzania Bara na vilevile Zanzibar; au (c) Sheria hiyo iwe inahusu Mambo ya Muungano, na kila inapotajwa Tanzania katika Sheria yoyote ifahamike kuwa sheria hiyo itatumika katika Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa ufafanuzi uliotolewa na masharti ya Ibara hii.
Kwa nini tunakuwa na Bunge la Wawakilishi katika bunge la Muungano na wakati Tanganyika imevaa koti la muungano.
(5)Bila kuathiri kutumika kwa katiba ya Tanganyika na Katiba ya Zanzibar, Katiba hii itakuwa na nguvu ya Kisheria katika Jamhuri ya Muungano kwa mambo yanayohusu Muungano na endapo sheria nyingine yoyote itakiuka masharti yaliyomo katika katiba hii, basi sheria hiyo nyingine, kwa kiasi kinachokiuka katiba hii, itakuwa batili. (5) Bila kuathiri kutumika kwa Katiba ya Zanzibar kwa mujibu wa Katiba hii kuhusu mambo yote ya Zanzibar yasiyo Mambo ya Muungano, Katiba hii itakuwa na nguvu ya sheria katika Jamhuri nzima ya Muungano na endapo sheria nyingine yoyote itakiuka masharti yaliyomo katika Katiba hii, Katiba ndiyo itakuwa na nguvu, na sheria hiyo nyingine, kwa kiasi inachokiuka Katiba, itakuwa batili. Ukuu wa Katiba ya Jamhuri dhidi ya katiba ya Zanzibar wakati ibara ya rasimu ya pili iliyopendekeza serikali tatu ilikuwa inazungumzia ukuu wa katiba ya jamhuri dhidi ya katiba za Tanganyika na Zanzibar Kurudisha mamlaka ya bunge la Tanganyika ili kuwa na usawa katika Muungano, inaqweza kuwa surauhisho kwani aiingii akilini baraza la wawakilishi-Zanzibar waingie kwenye bunge la jamhuri kujadili mambo ya Tanzania bara ambayo kwa kiasi kikubwa hayawahusu.
118 sasa 134 Uratibu wa kubadilisha katiba 118(1) Bunge linaweza kutunga sheria kwa ajili ya kubadilisha masharti yoyote ya Katiba hii. 134(1) Bunge linaweza kutunga sheria kwa ajili ya kubadilisha masharti yoyote ya Katiba hii kwa kufuata kanuni zifuatazo:
(a) Muswada wa sheria kwa ajili ya kubadilisha masharti ya Katiba hii au masharti yoyote ya sheria yanayohusu jambo lolote isipokuwa mambo yanayohusu aya ya (b) au (c), utapitishwa kwa kuungwa mkono kwa wingi wa kura za Wabunge wote; (b) Muswada wa sheria kwa ajili ya kubadilisha masharti yoyote ya
Katiba hii au masharti yoyote ya sheria yoyote yanayohusika na jambo lolote kati ya mambo yaliyotajwa katika Nyongeza ya Pili, utapitishwa tu iwapo utaungwa mkono kwa kura za wabunge ambao idadi yao haipungui theluthi mbili ya Wabunge wote wa Tanzania Bara na theluthi mbili ya Wabunge wote wa Zanzibar;
Imeboreshwa kwa kuweka utaratibu juu ya uwakilishi na uwiano wa maamuzi katika kufanya mabadiliko ya katiba
Neno kuungwa mkono kwa zaidi ya nusu halali za kura zilkizopigwa na wananchi ni neno la kisiasa zaidi. Katiba itamke wazi kuwa kura za kupitisha maamuzi mhimu kama hayo iwe ni zaidi ya asilimia 50 kutoka kila upande wa Jamuhuri ya Muungano
Uhalali wa jambo hili upimwe kwa idadi ya kura kwa kuvuka asilia hamsini (50) ya kura zote halali.
(2) Muswada wa Sheria wa kubadili katiba utahesabiwa kuwa umepitishwa na Bunge iwapo utaungwa mkono kwa kura za Wabunge wasiopungua theluthi mbili ya Wabunge wote kutoka Tanganyika na wasiopungua theluthi mbili ya Wabunge wote kutoka Zanzibar Inafanana na Ibara 132(1) Hakuna tofauti Kuwepo na uwazi na utashi. Na pale panapohitajika basi kusiwepo na vikwazo au vizingiti kutoka kwa watawala.
(3) Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti ya ibara ndogo ya (1) kubadilisha masharti ya Katiba hii maana yake ni pamoja na kurekebisha au kusahihisha masharti haya au kufuta na kuweka masharti mengine badala yake au kusisitiza au kubadilisha matumizi ya masharti hayo (2) Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti ya ibara ndogo ya (1) kubadilisha masharti ya Katiba hii maana yake ni pamoja na kurekebisha au kusahihisha masharti haya au kufuta na kuweka masharti mengine badala yake au kusisitiza au kubadilisha matumizi ya masharti hayo. Hakuna Ni sawa kwani hiyo ndiyo njia sitahiki kisheria.
119 sasa 134(1)(c) Bunge halitaweza kufanya mabadiliko ya Katiba kuhusu (a) Masharti yaliyomo katika Sura ya Kwanza, Sura ya Pili na Sura ya nne; (b) masharti ya Ibara ya 60; (c) masharti ya Ibara ya 79; (d) kuongeza au kupunguza jambo lolote la Muungano; (e) uwepo wa Jamhuri ya Muungano; (f) masharti ya Ibara hii,
Hadi kwanza maabadiliko hayo yaungwe mkono na theluthi mbili ya wananchi wa Jamhuri ya Muungano kutoka kila upande wa Jamhuri ya Muungano kwa Kura ya Maoni itakayoendeshwa na kusimamiwa na Tume Huru ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa sheria za nchi. (c) Muswada wa sheria kwa ajili ya kubadilisha masharti yoyote yanayohusika na jambo lolote kati ya mambo yaliyotajwa katika Nyongeza ya Tatu iliyoko mwishoni mwa Katiba hii, utapitishwa tu iwapo utaungwa mkono kwa zaidi ya nusu ya kura halali zilizopigwa
na wananchi wa Tanzania Bara, na zaidi ya nusu ya kura halali
zilizopigwa na wananchi wa Tanzania Zanzibar katika kura ya maoni itakayoendeshwa na kusimamiwa na Tume Huru ya Uchaguzi kwa mujibu wa sheria Ibara hii imebadilishwa sana kwanza; hakuna katazo kama Ibara ya 119(a)-(f) pili; Kura za wananchi rasimu ya pili ilipendekeza theluthi bili ya wananchi katiba inayopendekezwa inasema zaidi ya nusu Theluthi mbili inayopendekezwa na rasimu ya pili ni muhimu zaidi kwa sababu mabadiliko ya katiba lazima yashirikishe wananchi kwa mapana yake. Na wananchi kwa utashi wao ndiyo wawe na maamzi ya dhati juu ya jambo hilo. Na hapa ifahamike kuwa theluthi mbili zinazozungumziwa ndiyo uwe uzibitisho tosha kuwa wananchi wengi wameridhia au wamekataa.
120 sasa 135 Utaratibu wa Kutunga sheria 120(1) Bunge litatumia madaraka yake ya kutunga sheria kwa kujadili na kupitisha Muswada wa Sheria ambao utawekwa saini na Rais 135(1) Bunge litatumia madaraka yake ya kutunga sheria kwa kujadili na kupitisha muswada wa sheria Maneno “Muswada wa Sheria ambao utawekwa saini na Rais” yameondolewa Ni muhimu yakarudishwa ili kuleta ufanisi. Na kwa kufanya hivyo tutakuwa tunajenga Taifa lenye kutambua na kuthamin uwazi.
(2)Bila kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (3), Muswada wa Sheria unaweza kuandikwa na Serikali, Kamati ya Bunge au kikundi cha Wabunge. (2) Bila kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (3), muswada wa sheria unaweza kuandikwa na Serikali, Kamati ya Bunge, kikundi cha Wabunge au Mbunge.
Imeboreshwa kwa kuongeza Mbunge Imeboreshwa ni ibara iliyojenga mazingira shirikishi na rafiki na nah ii pia ni njia ya kidemokrasia.

(3) Wakati wa kuandaa Muswada wa Sheria kuhusu jambo lolote la Muungano, Serikali ya Jamhuri ya Muungano itahakikisha kwamba inawashirikisha wananchi kwa ajili ya kupata maoni na mapendekezo juu ya muswada huo. (3) Wakati wa kuandaa muswada wa sheria, Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Kamati ya Bunge, Kikundi cha Wabunge au Mbunge atahakikisha kwamba anawashirikisha wananchi kwa ajili ya kupata maoni na mapendekezo juu ya muswada huo. Rasimu inazungumzia jambo lolote la Muungano; Katiba inayopendekezwa inazungumzia Serikali ya Jamhuri ya Muungano hivyo mambo yote ya Muungano na yasiyo ya Muungano Katiba inayopendekezwa inatakiwa kuwa mahususi kwenye mambo ya Muungano tu ndio ipelekwe pande zote. Na mambo yasiyo ya Muungano ambayo ni maoni, na matakwa ya wananchi wa upande mmoja wa Muungano yaani Tanganyika yatapelekwa wapi?
(4) Muswada wa sheria utahesabiwa kuwa umepitishwa na Bunge iwapo utaungwa mkono kwa kura za wabunge wasiopungua theluthi mbili ya wabunge wote kutoka Tanganyika na wasiopungua theluthi mbili ya Wabunge wote kutoka Zanzibar. (4) Bila kuathiri masharti ya Ibara ya 134, muswada utahesabiwa kuwa umepitishwa na Bunge iwapo utaungwa mkono kwa wingi wa kura za Wabunge wote.
Rasimu ya Pili ya katiba inapendekeza muswada ili upitishwe lazima na theluthi mbili wakati katiba inayopendekezwa inataka wingi wa kura Maoni ya rasimu ya Katiba yatasaidia kuongeza mahudhurio ya wabunge kwenye bunge la Jamhuri ya Muungano; kwa sasa kuna changamoto ya mahudhurio hivyo pendekezo kwenye katiba kunaibeba hali hiyo.
Ni vema katiba ikatamka bayana kuwa uamzi utafikiwa kwa kwa maamzi ya theluthi mbili ya wabunge wote.
(5) Bila kuathiri masharti ya Ibara ndogo ya (4), Bunge litatunga Kanuni za Kudumu zitakazoweka utaratibu wa:- (a)kuwasilisha, kujadili na kupitisha Muswada wa Sheria; na (b) utekelezaji bora wa masharti ya ibara ndogo (3) (5) Bunge litatunga kanuni za kudumu zitakazoweka utaratibu wa: (a) kuwasilisha, kujadili na kupitisha muswada wa sheria; na (b) utekelezaji bora wa masharti ya ibara ndogo ya (3). Hakuna Hakuna shida kwani ni suala la utaratibu kama ulivyo utaratibu mwingine.
121 sasa 136 Utaratibu wa kutunga sheria kuhusu mambo ya fedha 121(1)Bunge halitashughulikia jambo lolote kati ya mambo yanayohusika na Ibara hii isipokuwa kama Rais amependekeza kwamba jambo hilo lishughulikiwe na Bunge na pendekezo hilo la Rais liwe limewasilishwa kwenye Bunge na Waziri 136.-(1) Bunge halitashughulikia jambo lolote kati ya mambo yanayohusika na Ibara hii isipokuwa kama Rais amependekeza kwamba jambo hilo lishughulikiwe na Bunge na pendekezo hilo la Rais liwe limewasilishwa kwenye Bunge na Waziri Hakuna Hakuna
(2) Muswada wa Sheria kwa ajili ya jambo lolote kati ya mambo yafuatayo: (i) Kutoza kodi au kubadilisha kodi kwa namna nyingine yoyote isipokuwa kupunguza; (ii) kuagiza kwamba malipo au matumizi ya fedha yafanywe kutokana na Mfuko Mkuu wa Hazina au mfuko mwingine wowote wa Serikali au kubadilisha kiwango hicho na namna nyingine yoyote isipokuwa kupunguza;
(b) kuagiza kwamba malipo au matumizi ya fedha yafanywe kutokana na Mfuko Mkuu wa Hazina au mfuko mwingine wowote wa Serikali wakati ikifahamika kwamba fedha iliyomo katika mifuko hiyo haikupangiwa itolewe kwa ajili ya malipo au matumizi hayo, au kuagiza kwamba malipo au matumizi yanayofanywa kutokana na mifuko hiyo yaongezwe; (c) kufuta au kusamehe deni lolote linalotakiwa lilipwe kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano; au (d) hoja au mabadiliko yoyote ya hoja kwa ajili ya lolote kati ya mambo yaliyoelezwa katika aya ya (a) ya Ibara hii ndogo . (2) Mambo yanayohusika na Ibara hii ni yafuatayo: (a) muswada wa sheria kwa ajili ya jambo lolote kati ya mambo yafuatayo:(i) kutoza kodi au kubadilisha kodi kwa namna nyingine yoyote isipokuwa kupunguza;(ii) kuagiza kwamba malipo au matumizi ya fedha yafanywe kutokana na Mfuko Mkuu wa Hazina au mfuko mwingine wowote wa Serikali au kubadilisha kiwango hicho na namna nyingine yoyote isipokuwa kupunguza; (b) kuagiza kwamba malipo au matumizi ya fedha yafanywe kutokana na Mfuko Mkuu wa Hazina au mfuko mwingine wowote wa Serikali wakati ikifahamika kwamba fedha iliyomo katika mifuko hiyo haikupangiwa itolewe kwa ajili ya malipo au matumizi hayo, au kuagiza kwamba malipo au matumizi yanayofanywa kutokana na mifuko hiyo yaongezwe; (c) kufuta au kusamehe deni lolote linalotakiwa lilipwe kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano; au(d) hoja au mabadiliko yoyote ya hoja kwa ajili ya lolote kati ya mambo yaliyoelezwa katika aya ya (a). Hakuna mabadiliko ya kimantiki isipokuwa kiuandishi hata hivyo haiathiri dhana ya ibara nzima Ni maboresho yanayolenga kuimarisha maamzi mhimu na yasiyokuwa na chuki.

Taratibu na sheria kali juu ya ubadhilifu wa fedha hasa benki kuu utakomeshwa kwa kuweka sheria kali. Hivyo kuwekwa kwa ibara hii itasaidia kupunguza wizi wa fedha za walipakodi.
122 sasa 137 Madaraka ya Rais kuhus muswada wa sheria 122(1) Muswada wa Sheria uliopitishwa na Bunge Sharti kupata saini ya Rais, ili kuthibitisha kukubaliwa kwake na Rais 137.-(1) Bila kuathiri masharti mengineyo yaliyomo katika Katiba hii, Bunge litatumia madaraka yake ya kutunga sheria kwa kufuata utaratibu wa kujadili na kupitisha miswada ya sheria, na muswada hautakuwa sheria mpaka uwe umepitishwa na Bunge na kukubaliwa na Rais kwa mujibu wa masharti ya Ibara hii. Maelezo kwenye katiba inayopendekezwa yameboreshwa Ibara hii kimantiki ni nzuri ikiwa nia na utashi wa Taifa vitawekwa mbele kwanza.
(2) Muswada wa Sheria uliyowasilishwa kwa Rais kwa ajili ya kupata kibali utawekewa saini na Rais ndani ya siku zisizozidi thelathini kutoka siku ambayo Muswada huo uliwasilishwa na kupokelewa na Katibu wa Baraza la Mawaziri (2) Muswada wa sheria uliowasilishwa kwa Rais kwa ajili ya kupata kibali utawekewa saini na Rais ndani ya siku zisizozidi thelathini kutoka siku ambayo muswada huo uliwasilishwa na kupokelewa na Katibu wa Baraza la 50 Mawaziri.
Hakuna Kunma haja ya kuendelea kushikilia idadi ya siku 30, kwani kwa kufanya hivyo kutazidisha utendaji wao.
(3) Baada ya Muswada wa Sheria kuwasilishwa kwa Rais kwa ajili ya kupata kibali chake, Rais anaweza kukubali au kukataa Muswada huo basi ataurudisha Bungeni pamoja na maelezo ya sababu za kukataa Muswada huo (3) Baada ya muswada wa sheria kuwasilishwa kwa Rais kwa ajili ya kupata kibali chake, Rais anaweza kukubali au kukataa muswada huo, na iwapo Rais atakataa kuukubali Muswada huo basi ataurudisha Bungeni pamoja na maelezo ya sababu za kukataa Muswada huo. Hakuna Kataika hali ya kawaida, ibara hii ni nzuri kwani inalenga kuchochea shughuli mbali mbali na kuleta ufanisi wa utendaji wa kazi za serikal.
(4) Baada ya Muswada wa Sheria kurudishwa Bungeni na Rais kwa mujibu wa masharti ya Ibara hii, Muswada huo hautapelekwa tena kwa Rais kwa ajili ya kupata kibali chake kabla ya kumalizika muda wa siku sitini tangu uliporudishwa Bungeni (4) Baada ya muswada wa sheria kurudishwa Bungeni na Rais kwa mujibu wa masharti ya Ibara hii, muswada huo hautapelekwa tena kwa Rais kwa ajili ya kupata kibali chake kabla ya kumalizika muda wa miezi sita tangu uliporudishwa Bungeni. Katiba inayopendekezwa imetoa kipindi cha miezi sita wakati rasimu ya pili imependekeza siku sitini Siku sitini zilizopendekezwa ni nzuri zaidi katika kuonyesha uwajibikaji
(5) Endapo katika kujadiliwa tena Bungeni kabla haujapelekwa tena kwa Rais, Muswada uliorudishwa Bungeni na Rais umeungwa mkono na Wabunge ambao idadi yao haipungui theluthi mbili ya Wabunge wote, basi Muswada huo unaweza kuwasilishwa mapema zaidi kwa Rais (5) Endapo katika kujadiliwa tena Bungeni kabla haujapelekwa tena kwa Rais, muswada uliorudishwa Bungeni na Rais umeungwa mkono na Wabunge ambao idadi yao haipungui theluthi mbili ya Wabunge wote, basi muswada huo unaweza kuwasilishwa mapema zaidi kwa Rais. Hakuna Hakuna
(6) Iwapo Muswada uliorudishwa Bungeni na Rais na katika kuujadili ukaungwa mkono na Wabunge ambao idadi yao haipungui theluthi mbili ya Wabunge wote na kupelekwa tena kwa Rais kwa ajili ya kupata kibali chake, basi Rais atatakiwa kuukubali Muswada husika kabla ya kumalizika muda wa siku sitini, na endapo siku sitini zitapita tangu Muswada huo ulipopelekwa tena kwa Rais pasipo Rais kuukubali, basi Katibu wa Bunge ataandika Hati kuthibitisha kuwa Muswada huo umekuwa sheria. (6) Iwapo muswada uliorudishwa Bungeni na Rais na katika kuujadili ukaungwa mkono na Wabunge ambao idadi yao haipungui theluthi mbili ya Wabunge wote na kupelekwa tena kwa Rais kwa ajili ya kupata kibali chake, basi Rais atatakiwa kuukubali muswada husika kabla ya kumalizika muda wa miezi sita na endapo miezi sita itafika tangu muswada huo ulipopelekwa tena kwa Rais pasipo Rais kuukubali, basi Rais atatakiwa kuukubali muswada huo la sivyo itabidi alivunje Bunge. • Katiba inayopendekezwa imetoa kipindi cha miezi sita wakati rasimu ya pili imependekeza siku sitini
• Pia Rasimu inapendekeza kama muswada umeungwa mkono na theluthi mbili au zaidi na baada ya siku sitini kupita katibu wa wabunge ataandika hati ya kuthibitisha kuwa muswada huo umekuwa sheria wakati rasimu inayopendekezwa inapendekeza bunge kuvunjwa Siku sitini zilizopendekezwa ni nzuri zaidi katika kuonyesha uwajibikaji
Pendekezo la Rasimu ya Pili la Katiba linatoa wigo mpana wa demokrasia; pia inashawishi ofisi ya Rais (Serikali) kuwa makini ili bunge lisiingilie kazi za serikali
123 sasa 138 Kupitishwa kwa Bajeti ya Serikali 123(1) Endapo Bunge halitaridhishwa na mchanganuo au mgawanyo wa hoja ya Bajeti ya Serikali, Bunge linaweza kurudisha hoja ya Bajeti ya Serikali pamoja na mapendekezo mahsusi kuhusiana na upungufu uliobainika 138-(1) Endapo Bunge halitaridhishwa na hoja kuhusu Bajeti ya Serikali, Bunge linaweza kurudisha hoja hiyo pamoja na mapendekezo mahsusi kuhusiana na upungufu uliobainika.
Haina shida, kama dhamila na utashi wa dhati vitazingatiwa lengo linakuwa ni kuboresha.
(2) Serikali itawajibika kuyafanyia kazi mapendekezo ya Bunge kwa kadri itakavyowezekana na kasha kuwasilisha tena Bungeni hoja husika pamoja na maelezo ya utekelezaji wa maelekezo ya Bunge na endapo Bunge litakataa kwa mar ya pili hoja kuhusu Bajeti ya Serikali, basi hoja hiyo itahesabika kuwa imepitishwa na Bunge. (2) Serikali inawajibika kuyafanyia kazi mapendekezo ya Bunge kwa kadri itakavyowezekana na kuiwasilisha tena hoja hiyo Bungeni pamoja na maelezo ya utekelezaji wa mapendekezo ya Bunge na endapo Bunge litaikataa kwa mara ya pili basi Rais atalivunja Bunge na kuitisha Uchaguzi Mkuu. Rasimu inaangalia maamuzi ya wengi kupitia wabunge kama inavyopendekezwa na bunge na pia pendekezo la kuvunja bunge ni tofauti na pendekezo la uwezo wa wabunge kupitisha hoja hiyo Pendekezo la kuvunja bunge serikali inaweza ikatumia vibaya kupitisha hoja za serikali kwa hofu ya kupoteza ubunge, hivyo inalipa bunge mamlaka kusimamia mambo ya wananchi kuliko kuburuzwa na serikali kufikia maamuzi kwa kitisho kwamba bunge litavunjwa.
Kwa lugha nyingine hiki ni kiini macho cha kutaka kuumanisha umma kuwa bunge linawajibika. Katika hili sababu moja kubwa ni kwamba wabunge ni sehemu ya mawaziri, hivyo hapa kunakosekana mfumo wa uwajibishanaji.
SURA YA PILI: WABUNGE (a) Uchaguzi wa Wabunge
124 sasa 139 Uchaguzi wa Wabunge 124(1) Kila baada ya Bunge kumaliza muda wake wa kipindi cha miaka mitano, kutakuwa na uchaguzi wa wabunge katika majimbo ya uchaguzi kama itakavyotangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi utakaofanyika kwa mujibu wa sheria za nchi. 139 (1) Kila baada ya Bunge kumaliza muda wa maisha yake, kutakuwa na uchaguzi wa Wabunge katika majimbo ya uchaguzi kama itakavyotangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi utakaofanyika kwa mujibu wa sheria. Hakuna Hakuna
(2) kutakuwa na uchaguzi wa Mbunge katika jimbo la uchaguzi ikiwa kiti cha Mbunge aliyechaguliwa kuwakilisha jimbo la uchaguzi kwa utaratibu wa mgombea huru, kitakuwa wazi kwa sababu nyingine yoyote isiyohusika na Bunge kumaliza muda wake (2) Kutakuwa na uchaguzi wa mbunge katika Jimbo la Uchaguzi ikiwa kiti cha Mbunge aliyechaguliwa kuwakilisha jimbo la uchaguzi kitakuwa wazi kwa sababu nyingine yoyote isiyohusika na Bunge kumaliza muda wake. Ibara hii katika rasimu ya pili inapendekeza uchaguzi mdogo ufanyike pindi mgombea huru kwa namna moja atakuwa hayupo kwenye kiti cha ubunge; lakini Katiba inayopendekezwa inapendekeza uchaguzi mdogo kwa wabunge wote hata wa vyama vya siasa Ili kupunguza gharama za chaguzi ndogo vyama vipendekeze vichague mbunge atakayewakilisha jimbo hilo la uchaguzi kupitia tiketi ya chama chao bila kufanya uchaguzi mdogo
(3) Endapo tarehe ya Bunge kumaliza muda wake imetangazwa au inafahamika, hakutakuwa na uchaguzi mdogo wa Mbunge kwa mujibu wa ibara ndogo ya (2) ndani ya kipindi cha miezi kumi na miwili kabla ya tarehe hiyo. (3) Endapo tarehe ya Bunge kumaliza muda wake imetangazwa au inafahamika, hakutakuwa na uchaguzi mdogo wa Mbunge kwa mujibu wa ibara ndogo ya (2) ndani ya kipindi cha miezi kumi na miwili kabla ya tarehe hiyo. Hakuna Hakuna
(4) Endapo Mbunge anayetokana na chama cha siasa atapoteza sifa za kuwa Mbunge kwa sababu yoyote isiyokuwa ya Bunge kumaliza muda wake, Tume Huru ya Uchaguzi, kwa mujibu wa masharti yatakayowekwa na sheria za nchi kwa ajili hiyo, itamteua na kumtangaza kuwa mbunge mtu mwingine kutoka kwenye orodha ya majina ya wagombea iliyowasilishwa na chama hicho kwa mujibu wa ibara ndogo ya 5 Imefutwa
(5) Orodha ya majina ya wagombea kutoka kila chama cha siasa iliyowasilishwa kwa Tume huru ya Uchaguzi katika Uchaguzi Mkuu ndiyo itakayotumiwa na Tume Huru ya Uchaguzi baadea ya kushauriana an chama cha Siasa kinachohusika, kwa madhumuni ya kujaza nafasi ya mbunge inapotokea kuwa wazi, wakati wowote wa Maisha ya Bunge Imefutwa
125 sasa 140 Sifa ya kuchaguliwa kuwa mbunge 125 (1) Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara hii, mtu yeyote atakuwa na sifa za kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa mbunge endapo: (a) ni raia wa Jamhuri ya Muungano aliyetimiza umri wa miaka ishirini na moja wakati wa kugombea; (b)anajua kusoma na kuandika lugha ya Kiswahili au Kiingereza na ana elimu isiyopungua kidato cha nne; (c)ni mwanachama aliyependekezwa na chama cha siasa au mgombea huru; (d) ni mwadilifu na anayeheshimu haki za binadamu na asiyedharau wala kubagua watu kwa misingi ya kabila, dini, jinsi, maumbile au hali zao katika jamii; na (1) Bila kuathiri masharti yaliyomo katika Ibara hii, mtu yeyote atakuwa na sifa za kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa mbunge endapo:(a) ni raia wa Jamhuri ya Muungano aliyetimiza umri wa miaka ishirini na moja wakati wa kugombea; (b) anajua kusoma na kuandika lugha ya Kiswahili au Kingereza; na(c) ni mwanachama aliyependekezwa na chama cha siasa au mgombea huru. Katiba inayopendekezwa inafuta kigezo cha kidato cha nne Elimu walau kidato cha nne ingefaa kwa sababu sasa shule za sekondari zipo katika ngazi ya kata hivyo fursa ya kupata elimu ni kubwa kuliko ilivyokuwa;
Hivyo ongezeko la kigezo hiki cha elimu ya sekondari halina tija na mantiki katika ulimwengu wa sasa
Lakini pia mijadala ya bungeni inahitaji upeo mkubwa zaidi hivyo mtu aliyefika kidato cha nne walau anakuwa na upeo wa ziada ukilinganisha na Yule ambaye anajua kusoma tu kama inavyopendekezwa
(2) Mtu hatakuwa na sifa za kugombaea kuchaguliwa kuwa Mbunge ikiwa-
(a) mtu huyo aliwahi kuwa Mbunge kwa vipindi vitatu vya miaka mitano; au (b) imethibitishwa rasmi kwamba mtu huyo ana ugonjwa wa akili (c)mtu huyo amehukumiwa na Mahakama yoyote katika jamhuri ya Muungano na kupwewa adhabu ya kifo au kufungwa gerezani kwa muda usiozidi miezi sitat kwa kosa lolote; (d)katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya uchaguzi amepata kuhukumiwa na kupewa adhabu ya kifungo kwa kosa linaloambatana na kukosa uaminifu au kwa kuvunja sheria inayohusiana na Maadili ya Uongozi; (e) mtu huyo ana maslahi yoyote aliyowekewa miiko maalum kwa mujibu wa sheria za nchi, na iwapo amekiuka miiko hiyo; au (f)Mtu huyo anashika madaraka ya ofisa mwandamizi katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano au Nchi Washirika (g) kwa mujibu wa sheria ya nchi inayoshulikia makosa yanayohusika na uchaguzi wa auinba yoyote, mtu huyo amezuiliwa kujiandikisha kama mpiga kura au kupiga kura katika uchaguzi wa wabunge; au (h) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe aya uchaguzi amewahi kutiwa hatiani katika mahakama kwa kosa la kukwepa kulipa kodi yoyote ya Serikali au makosa yanayohusu kukosa uaminifu. (2) Mtu hatakuwa na sifa za kugombea au kuchaguliwa kuwa mbunge
ikiwa:
(a) Imethibitishwa rasmi na Bodi ya Utabibu kwamba ana ugonjwa wa akili; (b) mtu huyo amehukumiwa na mahakama yoyote katika Jamhuri ya Muungano na kupewa adhabu ya kifo au ya kifungo gerezani kwa muda unaozidi miezi sita kwa kosa lolote linalohusu kukwepa kulipa kodi. (c) Katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya uchaguzi amepata kuhukumiwa na kupewa adhabu ya kifungo kwa kosa linaloambatana na kukosa uaminifu au kwa kuvunja sheria inayohusiana na maadili ya uongozi. Ibara hii imefutwa (a) mtu huyo aliwahi kuwa Mbunge kwa vipindi vitatu vya miaka mitano; Ukomo wa ubunge ni muhimu kwani hata rais naye ana ukomo wa vipindi 2
(3) Bunge linaweza kutunga sheria kwa ajili ya kuweka masharti yatakayomzuia mtu asichaguliwe kuwa Mbunge wa kuwakilisha Jimbo la Uchaguzi ikiwa mtu huyo ni mwenye madaraka yanayohusika na
shughuli za kuongoza au kusimamia uchaguzi wa Wabunge au shughuli
za uandikishaji wa wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Wabunge. (3) Bunge linaweza kutunga sheria itakayoweka masharti yatakayomzuia mtu asichaguliwe kuwa mbunge wa kuwakilisha jimbo la uchaguzi ikiwa mtu huyo ni mwenye madaraka yanayohusika na shughuli za kuongoza au kusimamia uchaguzi wa wabunge au shughuli za uandikishaji wa wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa wabunge. Hakuna Hakuna
4) Katika aya ya (e) ya ibara ndogo ya (2) ya Ibara hii “mkataba wa Serikali” maana yake ni mapatano yoyote ya mkataba ambayo mmojawapo wa walioshiriki ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano au Serikali ya Mapinduzi Zanzibar au Serikali ya Tanganyika, Idara au Taasisi yoyote ya Serikali yoyote kati ya hizo au mtumishi yeyote wa Serikali aliyeshiriki katika majadiliano ya mkataba husika kwa niaba ya Serikali yoyote miongoni mwa hizo. Imefutwa
(5) Watu wenye nyadhifa zifuatazo katika Utumishi wa Umma hawatakuwa na sifa ya kuwa Wabunge: (a) Rais na Makamu wa Rais; (b) Rais wa Tanganyika na Rais wa Zanzibar na Makamu wao; (c) Spika na Naibu Spika wa Bunge; (d) Waziri na Naibu Waziri; (e) Mwanasheria Mkuu wa Serikali; (f) Katibu Mkuu Kiongozi, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu; (g) Viongozi na watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama; (h) mtu ambaye ameajiriwa katika vyombo vya dola kama askari; (i) Jaji Mkuu, Jaji au Hakimu wa Mahakama, Wakili wa Serikali na Ofisa Sheria Katika Serikali ya Jamhuri ya
Muungano au Serikali za Washirika; (j) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali; (k) Mjumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi; na (l) mtu yeyote aliyeajiriwa, kuteuliwa au kuchaguliwa katika
utumishi wa umma. imefutwa
6) Kwa madhumuni ya kutoa fursa ya kukata rufani kwa mtu yeyote: (a) aliyethibitishwa rasmi kisheria kuwa ana ugonjwa wa akili; (b) aliyehukumiwa na kupewa adhabu ya kifo au kifungo; au (c) aliyepatikana na hatia ya kosa lolote lililotajwa katika sheria kwa mujibu wa ibara ndogo ya (2), mamlaka ya nchi itaweka utaratibu wa sheria kwa ajili ya kuweka masharti kwamba hukumu inayopingwa haitakuwa na nguvu kwa ajili ya utekelezaji wa masharti ya ibara ndogo ya (2) hadi upite muda uliotajwa
katika sheria hiyo. 4) Kwa madhumuni ya kutoa fursa ya kukata rufani kwa mtu yeyote:(a) aliyethibitishwa rasmi kisheria kuwa ana ugonjwa wa akili;(b) aliyehukumiwa na kupewa adhabu ya kifo au kifungo; au (c) aliyepatikana na hatia ya kosa lolote lililotajwa katika sheria kwa mujibu wa ibara ndogo ya (2), mamlaka ya nchi itaweka utaratibu wa sheria kwa ajili ya kuweka masharti kwamba hukumu inayopingwa haitakuwa na nguvu kwa ajili ya utekelezaji wa masharti ya ibara ndogo ya (2) hadi upite muda uliotajwa katika sheria hiyo.
126 sasa 141 Utaratibu wa uchaguzi wa wabunge Wabunge. 126.-(1) Wabunge wanaowakilisha majimbo ya uchaguzi watachaguliwa na wananchi kwa kufuata masharti ya Katiba hii na sheria
za nchi kwa mujibu wa Katiba hii, inayoweka masharti kuhusu uchaguzi wa Wabunge. 141.-(1) Wabunge wanaowakilisha majimbo ya uchaguzi, watachaguliwa na wananchi kwa kufuata masharti ya Katiba hii na sheria kwa mujibu wa Katiba hii, inayoweka masharti kuhusu uchaguzi wa Wabunge. Hakuna Hakuna
(2) Wagombea uchaguzi katika majimbo ya Uchaguzi watatakiwa kuwasilisha majina yao kwa Tume Huru ya Uchaguzi kwa mujibu wa
utaratibu uliowekwa na sheria za nchi. (2) Wagombea uchaguzi katika majimbo ya Uchaguzi, watatakiwa kuwasilisha majina yao kwa Tume Huru ya Uchaguzi kwa mujibu wa utaratibu utakaowekwa na sheria. Hakuna Hakuna
127 sasa 142 Kiapo na masharti ya kazi ya Ubunge 127.-(1) Kila Mbunge ataapishwa kiapo cha uaminifu na Spika katika Bunge kabla hajaanza kushiriki katika shughuli za Bunge, lakini Mbunge anaweza kushiriki katika uchaguzi wa Spika hata kabla hajaapishwa. 142.-(1) Kila Mbunge ataapishwa kiapo cha uaminifu na Spika katika Bunge kabla hajaanza kushiriki katika shughuli za Bunge, lakini Mbunge anaweza kushiriki katika uchaguzi wa Spika hata kabla hajaapishwa. Hakuna Hakuna
(2) Mbunge atashika madaraka kwa mujibu wa Katiba hii, na atalipwa mshahara, posho na malipo mengine kama yatakavyopangwa na Tume ya Utumishi wa Umma kwa mujibu wa sheria za nchi. (2) Mbunge atashika madaraka kwa mujibu wa Katiba hii, na atalipwa mshahara, posho na malipo mengine kwa mujibu wa sheria. Tume ya Utumishi wa Umma imetolewa kupanga malipo ya mbunge Inatakiwa tume hii irejeshwe ili kuondoa mtindo wa ofisi ya spika ya bunge kupendekeza na kuidhinisha kupanda kwa malipo katika historia ya bunge la jamhuri katika nyakati tofauti
(3) Wakati wowote wa madaraka yake, Mbunge atawajibika moja kwa moja kwa wapiga kura wake. Imefutwa Hakuna uwajibikaji moja kwa moja kwa wapiga kura wake Ibara muhimu irudishwe ili kuleta uwajibikaji na dhana nzima ya uwakilishi ni kwa wananchi waliomchagua
128 sasa 143 Kupoteza sifa ya ubunge 128.-(1) Mbunge atakoma kuwa Mbunge ikiwa litatokea lolote kati ya mambo yafuatayo: (a) tukio lolote ambalo, kama asingekuwa Mbunge lingemfanya
asiwe au apoteze sifa za kuchaguliwa au kuteuliwa kwa
mujibu wa masharti ya Katiba hii; (b) atakosa kuhudhuria Mikutano ya Bunge miwili mfululizo bila ya ruhusa ya Spika; (c) itathibitishwa kwamba amevunja masharti ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma; (d) atashindwa kufanya kazi za Mbunge kwa muda wa miezi sita mfululizo kutokana na maradhi au kizuizi ndani ya gereza; (e) atashindwa kutoa tamko rasmi kuhusu sifa za kuwa Mbunge au taarifa rasmi kuhusu mali kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii katika muda uliowekwa mahsusi na sheria za nchi; (f) atajiuzulu ubunge;
(g) kwa ridhaa yake atajiondoa au kujivua uanachama wa chama chake cha siasa, atafukuzwa au kuvuliwa uanachama na chama chake cha siasa; (h) ataondolewa madarakani kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii; (i) kufariki dunia. 143.-(1) Mbunge atakoma kuwa Mbunge ikiwa litatokea lolote kati ya
mambo yafuatayo: (a) tukio lolote ambalo, kama asingekuwa Mbunge lingemfanya asiwe au apoteze sifa za kuchaguliwa au kuteuliwa kwa mujibu wa masharti ya 52 Katiba hii; (b) atakosa kuhudhuria Mkutano mmoja wa Bunge bila ya ruhusa ya Spika; (c) itathibitishwa kwamba amevunja masharti ya sheria inayohusu maadili ya viongozi wa umma;(d) atashindwa kufanya kazi za Mbunge kwa muda wa miezi sita mfululizo kutokana na kizuizi ndani ya gereza;(e) atashindwa kutoa tamko rasmi kuhusu sifa za kuwa Mbunge au taarifa rasmi kuhusu mali kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii katika muda uliowekwa mahsusi na sheria; (f) atajiuzulu ubunge; (g) kwa ridhaa yake atajiondoa au kujivua uanachama wa chama chake cha siasa, atafukuzwa au kuvuliwa uanachama na chama chake cha siasa; (h) Mbunge aliyetokana na mgombea huru, atajiunga na chama chochote (i) ataondolewa madarakani kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii; au(j) kufariki dunia. Rasimu inapendekeza kutohudhuria vikao viwili wakati Katiba Inayopendekezwainasema kikao kimoja
Kama ni mgombea binafsi akijiunga na chama cha siasa basi itakuwa sababu ya kukoma ubunge

Sababu ya mbunge kukoma kuwa mbunge kwa kisingizio cha kutohudhulia mkutano mmoja wa bunge bila ruhusa ya spika ni uonevu na haitekelezeki. Zipo sababu nyingi za kuamini kuwa kifungu hiki hakitekelezeki.
Moja ni tabia iliyozuka ya kura kupigwa kwa internet, simu na hata nukshi. Jambo ambalo limepingwa vikali sana lakini watawala wakalifumbia macho.
Pili mfumo uliopo ni wa kulindana, hivyo ni nai atakuwa tayari kumfunga paka kengere?
Mambo ya msingi ya kumwondoa mbunge katika nafasi yake yameachwa:
Mfano
Suala la maadili na mbunge kutokukaa jimboni kwake. Hivi ndivyo vilio vikuu vya wananchi kuhusu sababu siatahiki za kumtoa mbunge madarakani.
(2) Mbunge anaweza kukata rufani mahakamani kupinga hukumu ya kuthibitishwa kwake kuwa ana maradhi au kupinga adhabu ya kufungwa gerezani, au kupinga kupatikana kwake na hatia kwa kosa la aina iliyotajwa katika ibara ndogo ya (1). (2) Mbunge anaweza kufungua shauri mahakamani kupinga uamuzi wa kuthibitishwa kwake kuwa ana ugonjwa wa akili au kupinga kufukuzwa au kuvuliwa uanachama wake wa chama cha siasa au kupatikana na hatia kwa kosa la aina iliyotajwa katika ibara ndogo ya (1). Hakuna Hakuna
129 sasa Imefutwa 129.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii, wananchi watakuwa na haki ya kumuondoa Mbunge wao madarakani, endapo Mbunge atafanya moja wapo au zaidi ya mambo yafuatayo: (a) kuunga mkono sera ambazo zinaenda kinyume na maslahi ya wapiga kura au kinyume na maslahi ya Taifa; (b) kushindwa kuwasilisha au kutetea kwa dhati hojainazotokana na kero za wapiga kura wake;
(c) kuacha kuishi au kuhamisha makaazi yake kutoka eneo la
Jimbo la Uchaguzi kwa zaidi ya miezi sita bila sababu za
msingi; au
(d) mambo mengine yatakayoainishwa kwenye sheria ya nchi. (2) Bunge litatunga sheria kuweka masharti ya kuendesha uchunguzi kwa Mbunge atakayeshindwa kutekeleza majukumu yake kwa
wapiga kura wake na utaratibu wa kumuondoa katika Ubunge. Imefutwa Wananchi hawana nguvu ya kumuondoa mbunge wao ambaye hawajibiki Ibara muhimu inafaa kurudishwa
130 sasa 144 Uamuzi wa suala kama mtu ni Mbunge 130.-(1) Kila shauri kwa ajili ya kupata uamuzi juu ya suala –
(a) kama uchaguzi wa Mbunge ulikuwa halali au sivyo; au (b) kama Mbunge amekoma kuwa Mbunge na nafasi ya madaraka
ya Ubunge iko wazi au hapana,
Litafunguliwa na kusikilizwa kwanza katika Mahakama Kuu. (1) Kila shauri kwa ajili ya kupata uamuzi kama: (a) uchaguzi wa Mbunge ulikuwa halali au sivyo; au (b) Mbunge amekoma kuwa Mbunge na nafasi ya madaraka ya Ubunge iko wazi au hapana, litafunguliwa na kusikilizwa kwanza katika Mahakama Kuu. Hakuna Hakuna
(2) Bunge linaweza kutunga sheria kwa ajili ya kuweka masharti kuhusu mambo yafuatayo: (a) watu wanaoweza kufungua shauri katika Mahakama Kuu kwa ajili ya kupata uamuzi juu ya suala lolote kwa mujibu wa masharti ya Ibara hii; (b) sababu na nyakati za kufungua shauri la namna hiyo, utaratibu wa kufungua shauri na masharti yanayotakiwa yatimizwe kwa kila shauri kama hilo; na (c) kutaja mamlaka ya Mahakama Kuu juu ya shauri kama hilo na kueleza utaratibu wa kusikiliza shauri lenyewe. (2) Bunge linaweza kutunga sheria kwa ajili ya kuweka masharti kuhusu mambo yafuatayo: (a) watu wanaoweza kufungua shauri katika Mahakama Kuu kwa ajili ya kupata uamuzi juu ya suala lolote kwa mujibu wa masharti ya Ibara hii; (b) sababu na nyakati za kufungua shauri la namna hiyo, utaratibu wa kufungua shauri na masharti yanayotakiwa yatimizwe kwa kila shauri kama hilo; na (c) kutaja mamlaka ya Mahakama Kuu juu ya shauri kama hilo Hakuna Hakuna
131 sasa 145 Tamko rasmi la Mbunge kuhusu mali na madeni 131.-(1) Kila Mbunge kabla ya kumalizika siku thelathinin tangu aapishwe kushika nafasi ya madaraka ya Mbunge sharti
awasilishe kwa Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji nakala mbili za tamko rasmi kwamba hajapoteza sifa za kuwa mbunge kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii. 145.-(1) Kila Mbunge kabla ya kumalizika siku thelathini tangu aapishwe kushika nafasi ya madaraka ya Mbunge sharti awasilishe kwa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma nakala mbili za tamko rasmi kuhusu mali na madeni kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii. Hakuna Ni jambo zuri kwani linatoa fursa ya watu kufahamu mali zake na kisha kuweza kudadisi uhalisia wa kipato chake.
(2) Tamko rasmi lililotajwa katika ibara ndogo ya (1),
Litatolewa katika fomu maalum itakayoandaliwa kwa mujibu wa sheria za nchi. (2) Tamko rasmi lililotajwa katika ibara ndogo ya (1), litatolewa katika fomu maalum itakayoandaliwa kwa mujibu washeria. Hakuna Hakuna

SEHEMU YA TATU: Uongozi wa Bunge (a) Spika na Naibu Spika
132 sasa 146 Spika na mamlaka yake 132.-(1) Kutakuwa na Spika wa Bunge ambaye atachaguliwa na Wabunge na atakuwa ndiye Kiongozi wa Bunge na atawakilisha Bunge katika vyombo na vikao vingine vyote nje ya Bunge. 146.-(1) Kutakuwa na Spika wa Bunge ambaye atachaguliwa na Wabunge kutoka miongoni mwa watu ambao ni Wabunge au wenye sifa za kuwa Wabunge na atakuwa ndiye Kiongozi wa Bunge na atawakilisha Bunge katika vyombo na vikao vingine vyote nje ya Bunge. Katiba inayopendekezwa inapendekeza spika kuchaguliwa miongoni mwa wabunge wakati rasimu ya pili inataka spika kutokuwa mbunge kabisa Ni vyema spika akawa sio mbunge ili aweze kutenda kazi zake kwa haki zaidi. Pia majukumu ya Spika ni makubwa hivyo atashindwa kuwakilisha vyema wananchi wake
(2) Waziri, Naibu Waziri, Mbunge au mtu mwenye madaraka ya aina nyingine yoyote yatakayotajwa na sheria za nchi kwa madhumuni ya Ibara hii, hataweza kuchaguliwa kuwa Spika. (2) Waziri, Naibu Waziri au mtu mwenye madaraka ya aina nyingine yoyote yatakayotajwa na sheria kwa madhumuni ya Ibara hii, hataweza kuchaguliwa kuwa Spika Hakuna Hakuna
(3) Mtu yeyote atakayechaguliwa kuwa Spika atatakiwa, kabla ya kumaliza siku thelathini tangu kuchaguliwa kwake, kuwasilisha kwa Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji tamko rasmi kwamba hajapoteza sifa za uchaguzi kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii, tamko hilo litatolewa katika fomu maalum itakayoandaliwa kwa mujibu wa
sheria za nchi. (3) Mtu yeyote atakayechaguliwa kuwa Spika atatakiwa, kabla ya kumaliza siku kumi na tano tangu kuchaguliwa kwake, kuwasilisha kwa Rais tamko rasmi kwamba hajapoteza sifa za uchaguzi kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii na Tamko hilo litatolewa kwa kutumia fomu maalum itakayowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge. Katiba inayopendekezwa inatoa siku kumi na tano za Spika mteule za kuwasilisha tamko rasmi kwamba hajapoteza sifa za uchaguzi; Rasimu inayopendekezwa inamtaka ndani ya siku 30 kuwasilisha tamko hilo kwenye Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji Rais ana mamlaka makubwa hawezi kutenda haki kama spika anatokana na chama chake cha siasa hivyo pendekezo la kwenda kwenye tume huru inayopendekezwa katika rasimu ya pili ni muhimu
133 sasa 147 Ukomo wa Spika 133.-(1) Spika atakoma kushika nafasi ya madaraka ya Spika litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo: (a) atachaguliwa kuwa Mbunge; (b) kutatokea jambo lolote ambalo, kama asingekuwa Spika, lingemfanya mtu huyo asiwe na sifa za uchaguzi au apoteze sifa za uchaguzi wa Spika; (c) ataondolewa kwenye madaraka ya Spika kwa Azimio la Bunge lililoungwa mkono na Wabunge ambao idadi yao haipungui theluthi mbili ya Wabunge wote; (d) atashindwa kuwasilisha tamko rasmi kuhusiana na mali na madeni yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii; (e) atapatikana na hatia kwa kosa la kutoa habari za uongo, kwa kiapo kinyume cha sheria kuhusu tamko rasmi lolote lililotolewa kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii; (f) atashindwa kuwasilisha taarifa ya mali kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii kabla ya kumalizika muda uliowekwa kwa ajili hiyo; (g) itathibitika kuwa amevunja masharti ya sheria inayohusu maadili ya uongozi wa umma; au (h) kufariki dunia. 147.-(1) Spika atakoma kushika nafasi ya madaraka ya Spika iwapo: (a) kutatokea jambo lolote ambalo, kama asingekuwa Spika, lingemfanya mtu huyo asiwe na sifa za uchaguzi au apoteze sifa za uchaguzi wa Spika; (b) ataondolewa kwenye madaraka ya Spika kwa Azimio la Bunge lililoungwa mkono na Wabunge ambao idadi yao haipungui theluthi mbili ya Wabunge wote; (c) atashindwa kuwasilisha tamko rasmi kuhusiana na mali na madeni yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii;
(d) atapatikana na hatia kwa kosa la kutoa habari za uongo, kwa kiapo kinyume cha sheria kuhusu tamko rasmi lolote lililotolewa kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii; (e) atashindwa kuwasilisha tamko la mali na madeni kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii kabla ya kumalizika muda uliowekwa kwa ajili hiyo;(f) itathibitika kuwa amevunja masharti ya sheria inayohusu maadili ya uongozi wa umma; (g) atajiuzulu; au(h) atafariki dunia Hakuna Hakuna
(2) Isipokuwa shughuli ya kumchagua Spika, hakuna shughuli yoyote itakayotekelezwa katika Bunge wakati wowote ambao nafasi ya madaraka ya Spika itakuwa wazi. (2) Hakuna shughuli yoyote itakayotekelezwa katika Bunge wakati wowote ambao nafasi ya madaraka ya Spika itakuwa wazi, isipokuwa shughuli ya kumchagua Spika. Mpangilio wa sentensi katika lugha Mantiki imebakia kuwa sawa
134 sasa 148 Naibu Spika 134.-(1) Kutakuwa na Naibu Spika wa Bunge ambaye atachaguliwa na Wabunge. 148.-(1) Kutakuwa na Naibu Spika wa Bunge ambaye atachaguliwa na Wabunge kutoka miongoni mwao. Katiba inayopendekezwa inasema kabisa naibu spika atachaguliwa miongoni mwao wakati rasimu ya pili ipo kimya inasema tu kutakuw na naibu spika atakayechaguliwa na wabunge Ibara hii ni vyema ikasema wazi kwamba naibu spika hatachaguliwa miongoni mwa wabunge . Hii itasaidia kuleta ufanisi na uwazi katika kazi zake bila kushurutishwa na mtu au kikundi cha watu.
(2) Waziri, Naibu Waziri, Mbunge au mtu mwenye madaraka ya aina nyingine yoyote yatakayotajwa na sheria za nchi kwa madhumuni ya Ibara hii, hataweza kuchaguliwa kuwa Naibu Spika. (2) Waziri, Naibu Waziri au mtu mwenye madaraka ya aina nyingine yoyote yatakayotajwa na sheria kwa madhumuni ya Ibara hii, hataweza kuchaguliwa kuwa Naibu Spika. Hakuna Hii ni sawa kwani kwa kufanya hivyo ni kutenganisha miavuli ya madaraka.
(3) Wabunge watamchagua Naibu Spika nyakati zifuatazo:
(a) Bunge litakapokutana kwa mara ya kwanza baada ya Uchaguzi Mkuu au mapema iwezekanavyo baada ya wakati
huo; na (b) katika kikao cha kwanza cha Bunge baada ya nafasi ya madaraka ya Naibu Spika, kuwa wazi kwa sababu yoyote isiyohusika na Bunge kuvunjwa au mapema iwezekanavyo baada ya kikao hicho. (3) Wabunge watamchagua Naibu Spika nyakati zifuatazo:
(a) Bunge litakapokutana kwa mara ya kwanza baada ya Uchaguzi Mkuu au mapema iwezekanavyo baada ya wakati huo; na (b) katika kikao cha kwanza cha Bunge baada ya nafasi ya madaraka ya Naibu Spika, kuwa wazi kwa sababu yoyote isiyohusika na Bunge kuvunjwa au mapema iwezekanavyo baada ya kikao hicho Hakuna Hakuna
(4) Naibu Spika atakoma kushika nafasi ya madaraka ya Naibu
Spika litokeapo lolote kati ya mambo yaliyoainishwa katika Ibara ya (4) Naibu Spika atakoma kushika nafasi ya madaraka ya Naibu Spika litokeapo lolote kati ya mambo yaliyoainishwa katika Ibara ya 147(1).
135 sasa 149 Sifa ya mtu kuchaguliwa kuwa Spika au Naibu Spika 135.(1) Mtu atastahili kuchaguliwa kuwa Spika au Naibu Spika endapo atakuwa na sifa zifuatazo – (a) angalau awe na elimu ya shahada ya chuo cha elimu ya juu kinachotambulika kwa mujibu wa sheria za nchi; (b) wakati wa kugombea, awe mwenye umri usiopungua miaka arobaini; (c) bila ya kuathiri masharti ya aya ya (a) na (b), awe na sifa za kumuwezesha kuchaguliwa kuwa Mbunge; na
(d) asiwe kiongozi au amewahi kuwa kiongozi wa juu wa chama cha siasa katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya kuomba kuchaguliwa kushika nafasi ya madaraka ya Spika au
Naibu Spika. 149. Mtu atastahili kuchaguliwa kuwa Spika au Naibu Spika endapo wakati wa kugombea, atakuwa mwenye umri usiopungua miaka arobaini na usiozidi miaka sabini. Sifa za elimu, uongozi katika chama, sifa za kuwa mbunge kama zinavyopendekezwa katika rasimu zimeachwa katika katiba inayopendekezwa Ni sifa muhimu anazopaswa kuwa nazo naibu spika hivyo zinapaswa kurudishwa
2) Kwa madhumuni ya aya ya (d), kiongozi wa juu wa chama cha siasa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu au Mjumbe wa chombo chochote cha kitaifa chenye mamlaka katika chama cha siasa. imefutwa Ibara muhimu irudishwe
136 sasa 150 Utaratibu wa uchaguzi na kiapo cha Spika na Naibu Spika 136.-(1) Kutakuwa na uchaguzi wa Spika katika kikao cha kwanza cha Mkutano wa Kwanza wa Bunge Jipya, na katika kikao cha kwanza chochote mara baada ya kutokea nafasi ya madaraka ya Spika kuwa wazi. 150.-(1) Kutakuwa na uchaguzi wa Spika katika kikao cha kwanza cha Mkutano wa Kwanza wa Bunge Jipya, na katika kikao cha kwanza chochote mara baada ya kutokea nafasi ya madaraka ya Spika kuwa wazi Hakuna Hakuna
(2) Kutakuwa na uchaguzi wa Naibu Spika wakati wowote katika Mkutano wa Kwanza wa Bunge Jipya na vile vile katika kikao cha kwanza cha Bunge kitakachofuata mara baada ya kutokea nafasi ya madaraka ya Naibu Spika kuwa wazi.

(3) Uchaguzi wa Spika na Naibu Spika, utafanywa kwa kura ya siri, na utaendeshwa kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Kanuni za Bunge. (2) Kutakuwa na uchaguzi wa Naibu Spika wakati wowote katika Mkutano wa Kwanza wa Bunge Jipya na vile vile katika kikao cha kwanza cha Bunge kitakachofuata mara baada ya kutokea nafasi ya madaraka ya Naibu Spika kuwa wazi.

(3) Uchaguzi wa Spika na Naibu Spika, utafanywa kwa kura ya siri, na utaendeshwa kwa kufuata utaratibu utakaowekwa na kanuni za Bunge. Hakuna Hakuna
(4) Spika na Naibu Spika watachaguliwa kwa misingi kwamba, endapo Spika atatoka upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano, Naibu Spika atatoka upande wa pili wa Jamhuri ya Muungano. (4) Spika na Naibu Spika watachaguliwa kwa misingi kwamba, endapo Spika atatoka upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano, Naibu Spika atatoka upande wa pili wa Jamhuri ya Muungano hakuna hakuna
(5) Isipokuwa kama ataacha madaraka yake, Spika na Spika watakaa madarakani kwa vipindi visivyozidi viwili vya mitano. (5) Isipokuwa kama ataacha madaraka yake, Spika na Naibu Spika watakaa madarakani kwa vipindi visivyozidi viwili vya miaka mitano hakuna Hakuna
(6) Mtu yeyote atakayechaguliwa kuwa Spika au Naibu atatakiwa, kabla ya kuanza kutekeleza madaraka yake, kuapishwa Bunge kiapo cha uaminifu. (6) Mtu yeyote atakayechaguliwa kuwa Spika au Naibu Spika atatakiwa, kabla ya kuanza kutekeleza madaraka yake, kuapa kiapo cha uaminifu. hakuna

Hakuna
137 sasa 151 Katibu wa Bunge 137.-(1) Kutakuwa na Katibu wa Bunge ambaye atateuliwa na Rais kutoka miongoni mwa majina matatu ya watu wenye madaraka ya juu katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano yatakayopendekezwa na Tume ya Utumishi wa Umma. 151.-(1) Kutakuwa na Katibu wa Bunge ambaye atateuliwa na Rais. Rasimu ya pili ya katiba inapendekeza kuwa katibu ateuliwe miongoini kutoka miongoni mwa majina matatu ya watu wenye madaraka ya juu katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano yatakayopendekezwa na Tume ya Utumishi wa Umma. Kwa kigezo kuwa Katibu mkuu wa bunge, ndiye mtendaji mkuu wa bunge ni sahii kuwa na katibu mwenye uzoefu
(2) Katibu wa Bunge atakuwa ndiye Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Bunge na atawajibika kwa utendaji bora wa shughuli za Bunge kwa kuzingatia masharti ya Katiba hii na sheria za nchi. (2) Katibu wa Bunge atakuwa ndiye Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Bunge na atawajibika kwa utendaji bora wa shughuli za Bunge kwa kuzingatia masharti ya Katiba hii na sheria. Hakuna Hakuna
138 sasa 152 Sekretarieti ya Bunge 138.(1) Kutakuwa na Sekretarieti ya Bunge itakayokuwa na watumishi kutoka pande zote za Jamhuri ya Muungano kwa kuzingatia
ngazi za utumishi kwa mujibu wa mahitaji ya shughuli za Bunge kama itakavyoamuliwa na Tume ya Utumishi ya Bunge. 152.-(1) Kutakuwa na Sekretarieti ya Bunge itakayokuwa na watumishi kutoka pande zote za Jamhuri ya Muungano kwa kuzingatia sifa za kitaaluma na ngazi za utumishi kwa mujibu wa mahitaji ya shughuli za Bunge kama itakavyoamuliwa na Tume ya Utumishi wa Bunge. Hakuna Hakuna
(2) Sekretarieti ya Bunge chini ya uongozi wa Katibu wa Bunge, itatekeleza kazi na shughuli zote zilizowekwa au zitakazokuwa ni muhimu kwa ajili ya kuhakikisha utekelezaji bora wa shughuli za Bunge,
Wabunge na madaraka ya Bunge. (2) Sekretarieti ya Bunge chini ya uongozi wa Katibu wa Bunge, itatekeleza kazi na shughuli zote zilizowekwa au zitakazokuwa ni muhimu kwa ajili ya kuhakikisha utekelezaji bora wa shughuli za Bunge, Wabunge na madaraka ya Bunge. Hakuna Hakuna

SURA YA KUMI NA MOJA
SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR, BARAZA LA MAPINDUZI LA ZANZIBAR NA BARAZA LA WAWAKILISHI LA ZANZIBAR
SEHEMU YA KWANZA
(a) Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
Haikuwepo kwenye Rasimu ya Pili 163(1) Kutakuwa na Serikali ya Zanzibar itakayojulikana kama “Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar” ambayo itakuwa na mamlaka katika Zanzibar juu ya
mambo yote yasiyo ya Muungano kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii. Rasimu ya Pili ya Katiba iliyotolewa na Tume haikuwa na Ibara hii. Masuala yanayohusu Serikali ya Mapinduzi Zanzibar si suala la Muungano na haikupaswa kuwa katika Katiba Pendekezi.

(2) Bila kuathiri masharti yaliyomo katika ibara hii na katika ibara zifuatazo
katika Sura hii, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaundwa na kutekeleza
madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii na Katiba ya Zanzibar ya
1984. Kuna haja ya kuangalia vizuri Katiba ya Zanzibar. Kwani kwa mjibu wa Tume kila nchi mshirika anatakiwa na Katina yake inayojihusisha na mambo yasiyohusu Muungano. Hivyo mamabo ya Zanzibar yaratibiwe na serikali ya Zanzibar.
(b) Rais wa Zanzibar
164.-(1) Kutakuwa na Rais wa Zanzibar ambaye atakuwa Kiongozi Mkuu
wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
la Zanzibar atakayechaguliwa kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya 1984.
(2) Rais wa Zanzibar kabla ya kushika madaraka yake ataapa mbele ya
Jaji Mkuu wa Zanzibar kiapo cha kuilinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya
Muungano, na kiapo kingine chochote kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar
kinachohusika na utendaji wa kazi yake, kisha atashika na kutekeleza madaraka
hayo kwa mujibu wa Katiba hii na Katiba ya Zanzibar ya 1984. Kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984, Rais wa Zanzibar ataapa kuitetea na kuilinda Katiba ya Zanzibar; na kwa mujibu wa Katiba hii ya Zanzibar kuna mambo mengi sana ambayo yanakinzana moja kwa moja na Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Hivyo basi ibara hii inaleta mgongano mkubwa.
Na kama anaapa kuilinda katiba ya Zanzibar na kew awakarti mwingine kuapa kuilinda katiba ya Muungano hapa pia bado kuna sintofahamu. Iko wapi katiba ya Tanganyika inayounda muungano?
(c) Baraza la Mapinduzi Zanzibar
165.-(1) Kutakuwa na Baraza la Mapinduzi la Zanzibar litakalokuwa na
wajumbe wa aina na idadi itakayowekwa kwa mujibu wa masharti ya Katiba ya
Zanzibar ya 1984. Hatuna tatizo nalo kwani ni chombo halali kwa serikali ya mapinduzi nya zanibar. Isipokuwa hakitakiwi kuratibiwa na serikali ya muungano. Badala yake iwe chini ya serikali ya mapinduzi ya Zanzibar.
(2) Bila kuathiri madaraka ya Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kama
Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Baraza la Mapinduzi litakuwa ndicho
chombo kikuu cha kumsaidia na kumshauri Rais wa Zanzibar katika masuala ya
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kuratibu utekelezaji wa shughuli za Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar na pia utekelezaji wa madaraka yake juu ya shughuli
za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuhusu mambo yote yasiyo Mambo ya
Muungano, kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii na yale ya Katiba ya Zanzibar
ya 1984.
SEHEMU YA PILI
BARAZA LA WAWAKILISHI LA ZANZIBAR
166 166.-(1) Kutakuwa na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar kama
litakavyoundwa kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya 1984.
166 (2) Madaraka yote ya kutunga sheria katika Zanzibar juu ya mambo yote
yasiyo Mambo ya Muungano yatakuwa mikononi mwa Baraza la Wawakilishi la
Zanzibar.

SURA YA KUMI NA MBILI
MAHAKAMA YA JAMHURI YA MUUNGANO
SEHEMU YA KWANZA
MSINGI YA UTOAJI HAKI NA UHURU WA MAHAKAMA
167.-(1) Kutakuwa na Mahakama ya Jamuhuri ya Muungano 167.-(1) Kutakuwa na Mahakama ya Jamhuri ya Muungano. Hakuna tofauti
Mahakama ya Jamuhuri ya Muungano kupitia katiba hii, itakuwa na mamlaka kutoka kwa wananchi na itatekeleza maamlaka yake kupitia Mahakama ya juu na Mahakama ya Rufani (2) Mahakama ya Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa Katiba hii
na sheria nyingine yoyote, itatekeleza mamlaka yake kupitia Mahakama ya Juu
na Mahakama ya Rufani. Mamlaka ya Mahakama ya Jamuhuri ya Muungano yametolewa toka kwa wananchi.
Kuongeza kifungu ambacho kinatoa nguvu kutungwa kwa sheria itakayoongoza mamlaka ya Mahakama ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mamlaka ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inatakiwa yatokane na Katiba na si vinginevyo hasa. Lengo la Ibara hii inatakiwa kuwa ni kutoa ulinzi wa Kikatiba kwa uwepo wa Mahakama ya Jamuhuri ya Muungano.
Mahakama ya Jamuhuri ya Muungano ni moja ya mihimili ya Dola; na kwa hivyo mamlaka yake inatakiwa kuwa inatokana na wananchi na si vinginevyo.
Mahakama ya Jamhuri ya Muungano itakuwa ni chombo chenye
mamlaka ya mwisho ya utoaji haki katika Jamhuri ya Muungano. (3) Mahakama ya Jamhuri ya Muungano itakuwa ni chombo chenye
mamlaka ya mwisho ya utoaji haki katika Jamhuri ya Muungano. HAKUNA Ikiwa ndio chombo cha juu cha utoaji haki katika Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania, mamlaka ya Mahakama ya Jamuhuri ya Muungano inatakiwa ipate nguvu ya Kikatiba, tofauti na Ibara ya 161 (2) ya Katiba Inayopendekezwa ilivyoainisha.
Hivyo ni jambo la kuangalia kwa jicho la kipekee kwani kuna mambo kuna masuala mengine hayaruhusiwi kujadiliwa Zanzibar.

Katika kutoa uamuzi wa mashauri ya madai na jinai kwa kuzingatia sheria, Mahakama ya Jamuhuri ya Muungano itafuata kanuni zifuatazo, yaani:
(a) Kutenda haki kwa wote bila kujali hali ya mtu kijamii, kisiasa, kiutamaduni au kiuchumi;
(b) Kutochelewesha haki bila sababu za msingi;
(c) Kutoa fidia ipasavyo kwa watu wanaoathirika kutokana na makosa ya watu wengine, na kwa mujibu wa sheria za nchi zilizotungwa mahususi kwa ajili hiyo;
(d) Kukuza na kuendeleza usuluhishi baina ya wanaohusika katika migogoro; na
(e) Kutenda haki bila kufungwa na masharti ya kiufundi. 168. Katika kutoa uamuzi wa mashauri ya madai na jinai kwa kuzingatia
sheria, Mahakama ya Jamhuri ya Muungano itafuata kanuni zifuatazo:
(a) kutenda haki kwa wote bila ubaguzi wowote;
(b) kutochelewesha haki bila sababu ya msingi;
(c) kutoa fidia ipasayo kwa watu wanaoathirika kutokana na makosa ya
watu wengine, na kwa mujibu wa sheria zilizotungwa mahususi kwa
ajili hiyo;
(d) kuendeleza usuluhishi baina ya wanaohusika katika migogoro; na
(e) kutenda haki bila kufungwa na masharti ya kiufundi yanayoweza
kukwamisha haki kutendeka. Kutokuainishwa kwa misingi ya utoaji haki kwenye Ibara ya 168(a).
Ibara ya 163(d) kukosa msisitizo wa kukuza na kuendeleza; huwezi kuendeleza usuluhishi bila kukuza usuluhishi huu pia.
Kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi juu ya upendeleo unaoonekana kufanywa na Mahakama za nchi; hivyo basi ni muhimu sana kwa misingi ya utoaji haki ina haja kubwa ya kuainishwa ili kuondoa shaka katika uendeshaji na utoaji haki.
Kuna ombwe kubwa sana hasa katika misingi ya utoaji haki. Na hii inatokana na jinsi watendaji wa mahakama wanavyopatikana. Kwa upatikanaji wa kuteuliwa tu, tusitegemee katiba hii kuwa na tija.
1649(1) Katika kutekeleza mamlaka ya utoaji haki, Mahakama ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania itaongozwa na masharti ya Katiba hii na haitaingiliwa ama kwa kudhibitiwa, kushinikizwa au kupewa maelekezo na mtu au chombo chochote. 169.-(1) Katika kutekeleza mamlaka ya utoaji haki, Mahakama zote
zitaongozwa na masharti ya Katiba hii na hazitaingiliwa ama kwa kudhibitiwa,
kushinikizwa au kupewa maelekezo na mtu au chombo chochote. Ibara kuongeleza Mahakama zote badala ya mahakama ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania;
Siyo mahakama zote zinahusu muungano. Hivyo ingeoanishwa ni mahakama ipi inayozungumziwa ili kuondoa mtafaruku. Mahakama kuu ya Zanzibar inazungumziwa badala ya mahakama ya muungano.
Nafasi ya madaraka ya Jaji wa Mahakama ya Juu au Mahakama ya Rufani haitafutwa wakati wowote ule ikiwa kuna mtu kw awakati huo anashikilia nafasi hiyo. (2) Nafasi ya madaraka ya Jaji wa Mahakama ya Juu, Mahakama ya
Rufani au Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano haitafutwa wakati wowote
ule ikiwa kuna mtu ambaye kwa wakati huo anashikilia nafasi hiyo. Kuongezwa kwa Mahakama Kuu ya Jamuhuri ya Muungano. Mahakama Kuu si suala la Muungano pamoja na kuwa inaitwa Mahakama Kuu ya Jamuhuri ya Muungano; kwani madaraka yake yanaishia Tanzania Bara peke yake.;
Mishahara na malipo mengine ya Majaji wa Mahakama ya Juu na
Mahakama ya Rufani yatalipwa
kutoka katika Mfuko Mkuu wa Hazina. (3) Mishahara na malipo mengine ya Majaji wa Mahakama ya Juu,
Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano yatalipwa
kutoka katika Mfuko Mkuu wa Hazina. Kuongezwa kwa Mahakama Kuu ya Jamuhuri ya Muungano. Mahakama Kuu ya Jamuhuri ya Muungano si suala la Muungano pamoja na kuwa inaitwa Mahakama Kuu ya Jamuhuri ya Muungano; kwani madaraka yake yanaishia Tanzania Bara peke yake.
Mshahara na malipo mengine yanayolipwa kwa Jaji wa Mahakama ya
Juu na Mahakama ya Rufani
hayatabadilishwa kwa maana ya kumuondolea faida Jaji husika. (4) Mshahara na malipo mengine yanayolipwa kwa Jaji wa Mahakama ya
Juu, Mahakama ya Rufani au Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano
hayatabadilishwa kwa maana ya kumuondolea faida Jaji husika. Kuongezwa kwa Mahakama Kuu ya Jamuhuri ya Muungano. Mahakama Kuu ya Jamuhuri ya Muungano si suala la Muungano pamoja na kuwa inaitwa Mahakama Kuu ya Jamuhuri ya Muungano; kwani madaraka yake yanaishia Tanzania Bara peke yake.;
Malipo ya mafao ya kustaafu ya Jaji wa Mahakama ya Juu au Jaji wa Mahakama
ya Rufani hayatabadilishwa kwa
maana ya kumuondolea faida Jaji husika wakati wote wa uhai wake. (5) Malipo ya mafao ya kustaafu ya Jaji wa Mahakama ya Juu, Mahakama
ya Rufani au Mahakamu Kuu ya Jamhuri ya Muungano hayatabadilishwa kwa
maana ya kumuondolea faida Jaji husika wakati wote wa uhai wake. Kuongezwa kwa Mahakama Kuu ya Jamuhuri ya Muungano. Mahakama Kuu ya Jamuhuri ya Muungano si suala la Muungano pamoja na kuwa inaitwa Mahakama Kuu ya Jamuhuri ya Muungano; kwani madaraka yake yanaishia Tanzania Bara peke yake.
Jaji wa Mahakama ya Juu au Jaji wa Mahakama ya Rufani hatashtakiwa kwa jambo
lolote alilolifanya au kutolifanya kwa nia njema katika utekelezaji wa shughuli ya
utoaji haki kwa mujibu wa sheria za nchi. (6) Jaji wa Mahakama ya Juu, Mahakama ya Rufani, Mahakamu Kuu ya
Jamhuri ya Muungano au Mahakama Kuu ya Zanzibar hatashtakiwa kwa jambo
lolote alilolifanya au kutolifanya kwa nia njema katika utekelezaji wa shughuli ya
utoaji haki kwa mujibu wa Katiba hii na sheria. Kuongezwa kwa Mahakam Kuu ya Jamuhuri ya Muungano; na Mahakama kuu ya Zanzibar. Mahakama Kuu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mahakama Kuu ya Zanzibar; si masuala ya muungano, kwani kila moja ya Mahakama hizi ina mamlaka yake mahususi inayoishia katika upande husika wa Muungano.

MUUNDO WA MAHAKAMA
(a) Mahakama ya Jamhuri ya Muungano

170 (1) Bila kuathiri masharti yoyote yaliyotangulia katika Sehemu hii, kutakuwa na muundo wa Mahakama katika Jamuhuri ya Muungano utakaokuwa kama ifuatavyo:
(a) Mahakama ya Juu; na
(b) Mahakama ya Rufani.
(2) mahakama Kuu ya Tanganyika na Mahakama Kuu ya Zanzibar zitakuwa na mamlaka sawa ya kusikiliza katika ngazi ya awali, mashauri ya madai na jinai kuhusu Mambo ya Muungano katika maeneo ya utawala ya Nchi Washiriki. 170.-(1) Bila kuathiri masharti yoyote yaliyotangulia katika sehemu hii,
kutakuwa na Muundo wa Mahakama katika Jamhuri ya Muungano utakaokuwa
kama ifuatavyo:
(a) Mahakama ya Juu;
(b) Mahakama ya Rufani; na
(c) Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano.
(2) Bila kuathiri masharti ya Katiba hii au sheria nyingine yoyoye
iliyotungwa na Bunge, iwapo sheria yoyote iliyotungwa na Bunge inayotumika
Tanzania Bara na vile vile Zanzibar imekabidhi madaraka yoyote kwa Mahakama
Kuu ya Jamhuri ya Muungano, basi Mahakama Kuu ya Zanzibar yaweza
kutekeleza madaraka hayo kwa kiasi kile kile inavyoweza kutekeleza Mahakama
Kuu ya Jamhuri ya Muungano. i. Kichwa cha Habari cha Sehemu hii ya Katiba Inayopendekezwa kuongele Mahakama ya Jamuhuri ya Muungano badala ya Mahakama za Jamuhuri ya Muungano;
ii. Kutokutambuliwa kwa Mahakama Kuu ya Tanganyika; wala Mahakama Kuu ya Zanzibar;

(b) Mahakama ya Juu ya Jamhuri ya Muungano

154(1) kutakuwa na Mahakama ya Juu ya Jamuhuri ya Muungano au kwa kifupi itaitwa “Mahakama ya Juu” ambayo itakuwa na:
(a) Jaji Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano ambaye atakuwa Rais wa Mahakama ya Juu;
(b) naibu Jaji Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano ambaye atakuwa Makamu wa Rais wa Mahakama ya Juu; na
(c) Majaji wengine wa Mahakama ya Juu wasiopungua saba.
(2) Uteuzi wa Majaji wa Mahakama ya Juu utazingatia sifa zilizoainishwa katika Katiba hii na uwakilishi wa sehemu mbili za Jamuhuri ya Muungano.
171. Kutakuwa na Mahakama ya Juu ya Jamhuri ya Muungano au kwa
kifupi kama “Mahakama ya Juu” na ambayo itakuwa na:
(a) Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ambaye atakuwa Rais wa
Mahakama ya Juu;
(b) Naibu Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ambaye atakuwa
Makamu wa Rais wa Mahakama ya Juu; na
(c) Majaji wengine wa Mahakama ya Juu wasiopungua saba. i. Kutokuwekwa kwa kifungu kinachoelezea kuwa sifa za uteuzi wa Majaji wa Mahakama ya Juu utaainishwa na Katiba;
ii. Kutokuwepo kwa kifungu kinachoainisha kuwa uteuzi wa Majaji wa Mahakama ya Juu utazingatia uwakilishi wa sehemu mbili za Jamuhuri ya Muungano.

Kuna haja ya kuwa na ulinzi wa Kikatiba wa sifa za uteuzi wa Majaji wa Mahakama ya Juu na pia kuzingatiwa kwa uwakilishi wa pande mbili za jamuhuri ya Muungano.

155(1) Akidi ya kikao cha Mahakama ya Juu itakuwa ni Majaji wa Mahakama ya Juu watano. 172.-(1) Akidi ya kikao cha Mahakama ya Juu itakuwa ni Majaji wa
Mahakama ya Juu watano. HAKUNA
(2) Kila shauri na rufani inayohitaji uamuzi wa Mahakama ya Juu
itaamuliwa kwa kufuata kauli ya walio wengi kati ya Majaji wa Mahakama ya
Juu waliosikiliza shauri au rufani hiyo. (2) Kila shauri na rufani inayohitaji uamuzi wa Mahakama ya Juu
itaamuliwa kwa kufuata kauli ya walio wengi kati ya Majaji wa Mahakama ya
Juu waliosikiliza shauri hilo. KUTOKUTAJWA KWA “RUFANI” KWENYE KIPENGELE CHA MWISHO CHA KIFUNGU. Kwa vile Ibara ndogo inaongelea masuala yote mawili; “shauri” na “rufani” kutokutajwa kwa rufani kunaleta mkanganyiko katika utekelezaji.
.
(2) Akidi ya Majaji katika kikao cha Mahakama ya Juu kwa madhumuni ya kusikiliza shauri linalohusu masuala yaliyoainishwa katika Ibara ya 156(1) (a), (b), (c) na (e) itazingatia uwakilishi wa sehemu mbili za Jamuhuri ya Muungano. KIFUNGU HIKI HAKIPO Katiba inayopendekezwa pia inataja taja neno rufani na kutambua uwakilishi wa serikali mbili
156(1) Mahakama ya Juu itakuwa ni ngazi ya mwisho ya rufani katika Jamuhuri ya Muungano na itakuwa na madaraka ya:
(a) Pekee na ya awali ya kusikiliza na kuamua mashauri yanayohusu matokeo yuchaguzi wa Rais wa Jamuhuri wa Muungano;
(b) Kusikiliza na kuamua mashauri yatakayowakilishwa na wananchi, Serikali au Serikali za Nchi Wasirika kuhusu tafsiri au utekelezaji wa Katiba hii;
(c) Kusikiliza na kuamua migogoro baina ya Nchi Washiriki au baina ya Nchi Msiriki na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano;
(d) Kusikiliza na kuamua rufani kutoka Mahakama ya Rufani;
(e) Kutoa ushauri kwa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano au Serikali za nchi Washirika, pale itakapoomb wa;
(f) Kusikiliza na kuamua shauri lolote litakaloletwa mbele yake kwa mujibu wa Katiba hii au sheria nyingine yoyote itakayoipa Mahakama hiyo mamlaka.
173.-(1) Mahakama ya Juu itakuwa ni ngazi ya mwisho ya rufani katika
Jamhuri ya Muungano na itakuwa na madaraka ya:
(a) pekee na ya awali ya:
(i) kusikiliza na kuamua mashauri yanayohusu matokeo ya
uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano;
(ii) kusikiliza, kusuluhisha na kuamua mashauri yatakayowasilishwa
na Serikali ya Jamhuri ya Muungano au Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar kuhusu tafsiri au utekelezaji wa Katiba hii;
(b) kusikiliza na kuamua rufani kutoka Mahakama ya Rufani;
(c) kutoa ushauri kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano au Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar, pale itakapohitajika; na
(d) kusikiliza na kuamua shauri lolote litakalowasilishwa mbele yake kwa
mujibu wa Katiba hii au sheria nyingine yoyote itakayoipa Mahakama
hiyo mamlaka. i. Kuondolewa uwezo wa wananchi kuwasilisha mashauri kuhusu tafsiri au utekelezaji wa Katiba kwenye Mahakama ya Juu;
ii. Kuiondolea Mahakama ya Juu mamlaka ya kuamua migogoro baina ya Nchi Washiriki au baina ya Nchi Mshiriki na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano;
iii. Ushauri kwa Serikali husika kutolewa “itakapohitajika” na sio “itakapoombwa”. Mambo mengi ya msingi yameondolewa. Nahaya ndiyo yaliyokua kilio cha watu wengi, wakati wa kuratibu na kunkusanya maoni ya katiba mpya.
Uwezo wa wananchi au mwananchi mmoja mmoja kupeleka shauri au mashauri mahakamani kuhusu tafsiri au utekelezajii wa katiba hii umeondolewa. Jambo hili ni kwa ajili ya manufaa ya watawala lakini kwa msitakabali wa usitawi wa utawala wa sheria na demokrasia ni kupokonya mamlaka ya wananchi na kubaka uhuru wa raia.
(1) Mahakama ya Rufani na Mahakama za Nchi washirika, isipokuwa Mahakama ya Juu, zitalazimika kufuata maamuzi ya Mahakama ya juu. (2) Mahakama ya Rufani, Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano na
Mahakama Kuu ya Zanzibar, zitalazimika kufuata maamuzi ya Mahakama ya
Juu. KUTAJWA KWA MAHAKAMA KUU YA JAMUHURI YA MUUNGANO NA MAHAKAMA KUU YA ZANZIBAR Mahakama kuu ya Jamuhuri ya Muungano na Mahakama Kuu ya Zanzibar sio suala la Muungano.
(3) Bila kujali masharti ya ibara ndogo ya (2), Mahakama ya Juu
haitafungwa na uamuzi wake wa awali.
Katika utawala wa kisheria na ukuu au utawala wa kimahakama ni sawa mahakani za chini kufuata uamzi wa mahakama ya juu. Japo kuna mkanganyiko kwani Mahakama kuu ya Zanzibar na Mahakama kuu ya Tanganyika siyo mabo ya muungano.
(4) Bunge linaweza kutunga sheria itakayoweka masharti zaidi kuhusu uendeshaji wa Mahakama ya juu. (4) Bunge litatunga sheria itakayoweka utaratibu zaidi kuhusu uendeshaji
wa Mahakama ya Juu. UWEZO WA BUNGE KUTUNGA SHERIA KUHUSU “UTARATIBU ZAIDI” BADALA YA “MASHARTI ZAIDI”
(3) Mahakama ya juu itaandaa Kanuni kwa ajili ya utekelezaji wa mamlaka yake. (5) Mahakama ya Juu itaandaa kanuni kwa ajili ya utekelezaji wa
mamlaka yake. HAKUNA
156(1) Jaji wa Mahakama ya Juu atakuwa na madaraka ya kusikiliza na kuamua shauri lolote katika Mahakama ya Juu. 174.-(1) Jaji wa Mahakama ya Juu atakuwa na madaraka ya
kusikiliza na kuamua shauri lolote katika Mahakama ya Juu. HAKUNA. Marginal notes imebadilika kutoka Mamlaka ya Mahakama ya Juu na Kuwa Mamlaka ya Mahakama ya Juu.
(2) Bila kujali masharti ya ibara ndogo ya (1), iwapo Jaji wa Mahakama ya Juu, kabla ya kuteuliwa kwake alikuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani au Mahakama kuu ya Nchi washirika, jaji huyo anaweza kuendelea kufanya kazi zake katika Mahakama aliyotoka hadi amalize kutayarisha na kutoa hukumu au hadi akamilishe shughuli nyingine yoyote inayohusika na mashauri ambayo alikwishaanza kuyasikiliza kabla hajateuliwa kuwa jaji wa Mahakama ya Juu. (2) Bila kujali masharti ya ibara ndogo ya (1), iwapo Jaji wa Mahakama
ya Juu, kabla ya kuteuliwa kwake alikuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani au
Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano au Mahakama Kuu ya Zanzibar, Jaji
huyo anaweza kuendelea kufanya kazi zake katika Mahakama aliyotoka hadi
amalize kutayarisha na kutoa hukumu au hadi akamilishe shughuli nyingine
yoyote inayuhusika na mashauri ambayo alikwishaanza kuyasikiliza kabla
hajateuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Juu. KUTAJWA KWA MAHAKAMA KUU YA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA MAHAKAMA KUU YA ZANZIBAR Mahakama Kuu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Mahakama Kuu ya Zanzibar sio masuala ya Muungano.
(3) Kwa kuzingatia masharti ya ibara ndogo ya (2), itakuwa ni halali
kwa Jaji wa Mahakama ya Juu kutoa hukumu au uamuzi mwingine wowote
unaohusika kwa kutumia na kutaja nafasi ya madaraka aliyokuwa akishika kabla
ya kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Juu na endapo hukumu hiyo au
uamuzi huo utapingwa kwa njia ya rufani itakayofikishwa mbele ya
Mahakama ya Juu, Jaji huyo hatakuwa na madaraka ya kusikiliza rufani hiyo. (3) Kwa kuzingatia masharti ya ibara ndogo ya (2), itakuwa ni halali
kwa Jaji wa Mahakama ya Juu kutoa hukumu au uamuzi mwingine wowote
unaohusika kwa kutumia na kutaja nafasi ya madaraka aliyokuwa akishika kabla
ya kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Juu na endapo hukumu hiyo au
uamuzi huo utapingwa kwa njia ya rufani itakayofikishwa mbele ya
Mahakama ya Juu, Jaji huyo hatakuwa na madaraka ya kusikiliza rufani hiyo. HAKUNA
(c) Uteuzi wa Jaji wa Mahakama ya Juu

158 (1) Jaji Mkuu atateuliwa na Rais kutoka orodha ya majina ya watu
watatu yaliyopendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama na kabla ya kuapishwa jina lake litawasilishwa Bungeni kwa ajili ya kuthibitishwa na Bunge. 175.-(1) Jaji Mkuu atateuliwa na Rais kutoka orodha ya majina ya watu
watatu yaliyopendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama. Jina la jaji Mkuu baada ya kuteuliwa na Rais kuwasilishwa Bungeni kwa ajili ya Bunge kuthibitisha. Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilipendekeza kuwa Mbunge kama mwakilishi wa wananchi liwe na mamlaka ya kuidhinisha uteuzi wa jaji mkuu. Kidendo cha kufuta ibara hii ni kupokonya wabunge madalaka yao na kuliifanya bunge liwe ni sehemuya kutekeleza na kulinda maslahi ya watawala kwani kwa kushindwa kuwahoji au kuwawajibisha ni kubariki kila kitu chao.
(2) Jaji Mkuu ndiye atakuwa Mkuu wa Mhimili wa Mahakama katika
Jamhuri ya Muungano. (2) Jaji Mkuu ndiye atakuwa Mkuu wa Mhimili wa Mahakama katika
Jamhuri ya Muungano. HAKUNA
(3) Mtu ataweza kuteuliwa kuwa Jaji Mkuu endapo atakuwa
amefikisha umri wa miaka arobaini na tano au zaidi na mwenye sifa ya
uadilifu na uaminifu katika utekelezaji wa majukumu yake na awe:
(a) ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano;
(b) na shahada ya sheria kutoka chuo cha elimu ya juu
kinachotambuliwa na mamlaka inayoshughulikia elimu ya juu katika
Jamhuri ya Muungano;

(i) amefanya kazi ya Ujaji katika Mahakama ya Rufani, Mahakama
Kuu ya Jamhuri ya Muungano au Mahakama Kuu ya Zanzibar; au
(ii) amefanya kazi ya utumishi wa umma katika Jamhuri ya
Muungano au ana utaalamu akiwa na sifa ya kusajiliwa kuwa
wakili na amekuwa na sifa hizo mfululizo kwa muda usiopungua
miaka ishirini. i. Tabia njema haijatajwa kama sifa mojawapo;
ii. Kutajwa kwa Mahakama Kuu ya Jamuhuri wa Muungano na Mahakama Kuu ya Zanzibar;
iii. Kutumiwa neon “utaalam” badala ya neon”uanataaluma” katika ibara 158(c) (ii). Ibara ya 176(1) inataja “tabia mbaya” kama sababu mojawapo inayoweza kumsababisha Jaji wa Mahakama ya Juu kuondolewa katika madaraka yake.; hivyo basi ni busara pia “tabia njema” ikawa ni mojawapo ya sifa ya mtu kuwa na uwezo wa kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Juu;

Neno tabia njema limeondolewa. Tabia njema kwa watawala wetu limeonekana kuwa mwiba na ndiyo maana wamelipania mpaka wakalitoa. Tabia njema ndiyo mara nyingi kipimo kikuu cha kufanya kazi.
Hata kama una weledi mkubwa kiasi gani, au unauzoefu mkubwa sana kama huna tabia njema ujue wewe ni wakutilia shaka tu hasa katika shughuli kubwa hizi za umma.
159.-(1) Naibu Jaji Mkuu atateuliwa na Rais kutoka orodha ya majina ya
watu watatu yaliyopendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama na kabla ya kuapishwa jina lake litawasilishwa Bungeni kwa ajili ya kuthibitishwa na Bunge. 176.-(1) Naibu Jaji Mkuu atateuliwa na Rais kutoka orodha ya majina ya
watu watatu yaliyopendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama. Jina la Naibu Jaji Mkuu baada ya kuteuliwa na Rais kuwasilishwa Bungeni kwa ajili ya Bunge kuthibitisha. Tume ilipendekeza Jaji mkuu na Naibu jaji mkuu wathibitishwe na bunge. Hapa tunaona mamlaka ya bunge kuthibitisha uteuzi wa Naibu Jaji Mkuu umeondolewa. Jambo hili si la kuunga mkono hata kidogo kwani pasipokuwepo na taasisi kama ya Bunge kuthibitisha uteuzi, kasumba ya kupeana vyeo itazidi kushamili.
(2) Mtu atateuliwa kuwa Naibu Jaji Mkuu endapo atakuwa na sifa
zilizoainishwa katika Ibara ya 158 na kwa kufuata msingi kwamba endapo Jaji Mkuu atatoka upande mmoja wa Muungano, basi Naibu Jaji Mkuu atatoka upande wa pili wa Jamhuri ya Muungano. (2) Mtu atateuliwa kuwa Naibu Jaji Mkuu endapo atakuwa na sifa
zilizoainishwa katika Ibara ya 170. Kutozingatiwa kwa msingi kwamba endapo Jaji Mkuu atatoka upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano basi Naibu Jaji Mkuu atatoka upande wa pili wa Jamhuri ya Muungano.
(3) Naibu Jaji Mkuu atakuwa ndiye Msaidizi Mkuu wa Jaji Mkuu katika
utekelezaji wa majukumu yake. (3) Naibu Jaji Mkuu atakuwa ndiye Msaidizi Mkuu wa Jaji Mkuu katika
utekelezaji wa majukumu yake. HAKUNA
-(1) Majaji wa Mahakama ya Juu watateuliwa na Rais kutoka miongoni mwa
majina yatakayopendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama. 177.-(1) Jaji wa Mahakama ya Juu atateuliwa na Rais kutoka miongoni mwa
majina yatakayopendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama. Matumizi ya umoja katika kumtamka Jaji. Wameondoa mamlaka ya Bunge kuthibitisha uteuzi wa Majaji wa Mahakama ya juu. Hii ni kulipokonya Bunge mamlaka yake. Tume ya mabadiliko ya Katina ilipendekeza kuwa ili kuleta ufanisi katika kazi za umma ni vizuri viongozi wakuu na waandamizi wa serikalini wakathibitishwa na Bunge, kwani Bunge ndicho chombo maalumu cha kuwawakilisha wananchi.
-(2) mtu anaweza kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Juu endapo atakuwa na sifa zifuatazo:
(a) Awe ni raia wa kuzaliwa wa Jamuhuri ya Muunganomwenye tabia njema, uadilifu na uaminifu;
(b) Awe na shahada ya sheria kutika chuo cha elimu ya juu kinachotambuliwa na mamlaka inayoshughulikia elimu ya juu katika Jamhuri ya Muungano; na
i. Awe amefanya kazi ya ujaji katika Mahakama ya Rufani au Mahakama kuu za Nchi washirika; au
ii. Awe wakili, mtumishi wa umma au mwanataaluma akiwa na sifa ya kusajiliwa kuwa wakili na amekuwa na sifa hizo mfululizo kwa muda usiopungua miaka kumu na tano. (2) Mtu ataweza kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Juu endapo
atakuwa ni Jaji wa Mahakama ya Rufani na awe:
(a) ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano mwenye, uadilifu na
uaminifu;
(b) na shahada ya sheria kutoka chuo cha elimu ya juu kinachotambuliwa
na mamlaka inayoshughulikia elimu ya juu katika Jamhuri ya
Muungano; na
(i) awe amefanya kazi ya ujaji katika Mahakama ya Rufani au
Mahakama Kuu; au
(ii) awe wakili, mtumishi wa umma au mwana taaluma akiwa na
sifa ya kusajiliwa kuwa wakili na amekuwa na i. Sifa za mtu aweze kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Juu itabidi awe ni Jaji wa Mahakama ya Rufani;
ii. Tabia njema haijatajwa kama sifa mojawapo ya mtu kuweza kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Juu;
iii. Kutajwa kwa Mahakama Kuu Neno tabia njema limeondolewa. Pengine hii inaweza ikawa ni agenda ya watawala kuwachagua viongozi wasiofaa ili kuridhia matakwa yao.
161. Jaji Mkuu, Naibu Jaji Mkuu au Jaji wa Mahakama ya Juu atashika
61
madaraka yake mara tu atakapokuwa ameapishwa na Rais kiapo cha uaminifu na
kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi kitakachowekwa kwa
mujibu wa sheria za nchi. 178. Jaji Mkuu, Naibu Jaji Mkuu au Jaji wa Mahakama ya Juu atashika
madaraka yake mara tu atakapokuwa ameapishwa na Rais kiapo cha uaminifu na
kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi kitakachowekwa kwa
mujibu wa sheria. HAKUNA
162-(1) Jaji Mkuu atashika nafasi ya madaraka ya Jaji Mkuu hadi
atakapofikisha umri wa miaka sabini, isipokuwa tu kama:
(a) atajiuzulu;
(b) atashindwa kutekeleza majukumu yake kutokana na maradhi;
(c) atafariki dunia; au
(d) atavuliwa madaraka ya Jaji Mkuu kwa mujibu wa Katiba hii. 179.-(1) Jaji Mkuu atashika nafasi ya madaraka ya Jaji Mkuu hadi
atakapofikisha umri wa miaka sabini, isipokuwa tu kama:
(a) atajiuzulu;
(b) atashindwa kutekeleza majukumu yake kutokana na maradhi;
(c) atafariki dunia; au
(d) atavuliwa madaraka ya Jaji Mkuu kwa mujibu wa Katiba hii. HAKUNA
(2) Masharti ya ibara ndogo ya (1) yatatumika pia kwa Naibu Jaji Mkuu
na Jaji wa Mahakama ya Juu. (2) Masharti ya ibara ndogo ya (1) yatatumika pia kwa Naibu Jaji Mkuu
na Jaji wa Mahakama ya Juu. HAKUNA
(3) Bila kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (1) na ya (2), Jaji Mkuu,
Naibu Jaji Mkuu na Jaji wa Mahakama ya Juu aliyetimiza umri wa kustaafu
atalazimika kuendelea kufanya kazi baada ya kutimiza umri huo hadi amalize
kutayarisha na kutoa hukumu au hadi akamilishe shughuli nyingine yoyote
inayohusika na mashauri ambayo alikwishaanza kuyasikiliza kabla hajatimiza
umri wa kustaafu. (3) Bila kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (1) na ya (2), Jaji Mkuu,
Naibu Jaji Mkuu na Jaji wa Mahakama ya Juu aliyetimiza umri wa kustaafu
atalazimika kuendelea kufanya kazi baada ya kutimiza umri huo hadi amalize
kutayarisha na kutoa hukumu au hadi akamilishe shughuli nyingine yoyote
inayohusika na mashauri ambayo alikwishaanza kuyasikiliza kabla hajatimiza
umri wa kustaafu. HAKUNA
(4) Bila kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (3), Jaji Mkuu au Naibu Jaji
Mkuu aliyetimiza umri wa kustaafu, ataachia nafasi ya madaraka yake, isipokuwa
ataendelea kutekeleza shughuli ambazo hajazikamilisha akiwa katika nafasi ya
madaraka ya Jaji wa Mahakama ya Juu hadi atakapokamilisha shughuli hizo. (4) Bila kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (3), Jaji Mkuu au Naibu Jaji
Mkuu aliyetimiza umri wa kustaafu, ataachia nafasi ya madaraka yake, isipokuwa
ataendelea kutekeleza shughuli ambazo hajazikamilisha akiwa katika nafasi ya
madaraka ya Jaji wa Mahakama ya Juu hadi atakapokamilisha shughuli hizo. HAKUNA
163.-(1) Iwapo itatokea kwamba:
(a) nafasi ya madaraka ya Jaji Mkuu itakuwa wazi;
(b) Jaji Mkuu hayupo katika Jamhuri ya Muungano; au
(c) Jaji Mkuu atashindwa kumudu kutekeleza kazi zake kwa sababu
yoyote iliyoainishwa katika Katiba hii,

Naibu Jaji Mkuu atatekeleza kazi za Jaji Mkuu hadi atakapoteuliwa
Jaji Mkuu mwingine au hadi Jaji Mkuu ambaye alikuwa hayupo au
alikuwa hamudu kazi zake atakaporejea kazini. 180.-(1) Iwapo itatokea kwamba:
(a) nafasi ya madaraka ya Jaji Mkuu itakuwa wazi;
(b) Jaji Mkuu hayupo katika Jamhuri ya Muungano; au
(c) Jaji Mkuu atashindwa kumudu kutekeleza kazi zake kwa sababu
yoyote iliyoainishwa katika Katiba hii,
(d) Naibu Jaji Mkuu atatekeleza kazi za Jaji Mkuu hadi atakapoteuliwa
Jaji Mkuu mwingine au hadi Jaji Mkuu ambaye alikuwa hayupo au
alikuwa hamudu kazi zake atakaporejea kazini.
(2) Ikitokea kwamba nafasi ya madaraka ya Jaji wa Mahakama ya Juu
itakuwa wazi au endapo Jaji wa Mahakama ya Juu yeyote ameteuliwa kutekeleza
kazi za Naibu Jaji Mkuu au kama Jaji wa Mahakama ya Juu atashindwa
kutekeleza kazi zake kwa sababu yoyote, au Jaji Mkuu atamshauri Rais kuwa
kazi za Mahakama ya Juu zilivyo kwa wakati huo zinahitaji ateuliwe Kaimu Jaji
wa Mahakama ya Juu, basi Rais anaweza kumteua Kaimu Jaji wa Mahakama ya
Juu kutoka miongoni mwa watu wanaoweza kuteuliwa kuwa Majaji wa
Mahakama ya Juu watakaopendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama. (2) Ikitokea kwamba nafasi ya madaraka ya Jaji wa Mahakama ya Juu
itakuwa wazi au endapo Jaji wa Mahakama ya Juu yeyote ameteuliwa kutekeleza
kazi za Naibu Jaji Mkuu au kama Jaji wa Mahakama ya Juu atashindwa
kutekeleza kazi zake kwa sababu yoyote, au Jaji Mkuu atamshauri Rais kuwa
kazi za Mahakama ya Juu zilivyo kwa wakati huo zinahitaji ateuliwe Kaimu Jaji
wa Mahakama ya Juu, basi Rais anaweza kumteua Kaimu Jaji wa Mahakama ya
Juu kutoka miongoni mwa watu wanaoweza kuteuliwa kuwa Majaji wa
Mahakama ya Juu watakaopendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama. HAKUNA
(3) Mtu atakayeteuliwa kuwa Kaimu Jaji wa Mahakama ya Juu atafanya
kazi kama Kaimu Jaji wa Mahakama ya Juu kwa muda wote utakaotajwa kwenye
hati ya kuteuliwa kwake. (3) Mtu atakayeteuliwa kuwa Kaimu Jaji wa Mahakama ya Juu atafanya
kazi kama Kaimu Jaji wa Mahakama ya Juu kwa muda wote utakaotajwa kwenye
hati ya kuteuliwa kwake. HAKUNA
(4) Bila kujali masharti ya ibara ndogo ya (2), mtu aliyeteuliwa kuwa
Kaimu Jaji wa Mahakama ya Juu ataendelea kufanya kazi kama Kaimu Jaji wa
Mahakama ya Juu hadi amalize kutayarisha na kutoa hukumu au hadi amalize
shughuli nyingine yoyote inayohusika na rufani au mashauri mengine ambayo
alikwishaanza kuyasikiliza kabla ya muda wake wa uteuzi haujamalizika au
uteuzi wake haujafutwa. (4) Bila kujali masharti ya ibara ndogo ya (2), mtu aliyeteuliwa kuwa
Kaimu Jaji wa Mahakama ya Juu ataendelea kufanya kazi kama Kaimu Jaji wa
Mahakama ya Juu hadi amalize kutayarisha na kutoa hukumu au hadi amalize
shughuli nyingine yoyote inayohusika na rufani au mashauri mengine ambayo
alikwishaanza kuyasikiliza kabla ya muda wake wa uteuzi haujamalizika au
uteuzi wake haujafutwa. HAKUNA
(5) Kwa madhumuni ya masharti ya Ibara hii, Kaimu Jaji wa Mahakama
ya Juu atakuwa na mamlaka kamili ya Jaji wa Mahakama ya Juu na atatekeleza
kazi zote za Jaji wa Mahakama ya Juu na kwamba idadi ya Majaji wa Mahakama
ya Juu iliyotajwa katika Ibara ya 167 haitaathirika kwa sababu tu mmoja au zaidi
ya Majaji wa Mahakama ya Juu katika kikao chochote ni Kaimu Jaji wa
Mahakama ya Juu. (5) Kwa madhumuni ya masharti ya Ibara hii, Kaimu Jaji wa Mahakama
ya Juu atakuwa na mamlaka kamili ya Jaji wa Mahakama ya Juu na atatekeleza
kazi zote za Jaji wa Mahakama ya Juu na kwamba idadi ya Majaji wa Mahakama
ya Juu iliyotajwa katika Ibara ya 167 haitaathirika kwa sababu tu mmoja au zaidi
ya Majaji wa Mahakama ya Juu katika kikao chochote ni Kaimu Jaji wa
Mahakama ya Juu. HAKUNA
164.-(1) Jaji wa Mahakama ya Juu ataondolewa katika nafasi ya madaraka
ya Jaji wa Mahakama ya Juu kwa sababu ya kushindwa kutekeleza madaraka
yake ama kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote au kwa sababu ya
tabia mbaya inayoathiri maadili ya kazi ya Jaji au sheria inayohusu maadili ya
uongozi wa umma, na hataondolewa madarakani isipokuwa kwa mujibu wa
masharti ya ibara ndogo ya (2). 181.-(1) Jaji wa Mahakama ya Juu ataondolewa katika nafasi ya madaraka
ya Jaji wa Mahakama ya Juu kwa sababu ya kushindwa kutekeleza madaraka
yake ama kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote au kwa sababu ya
tabia mbaya inayoathiri maadili ya kazi ya Jaji au sheria inayohusu maadili ya
uongozi wa umma, na hataondolewa madarakani isipokuwa kwa mujibu wa
masharti ya ibara ndogo ya (2). HAKUNA Katika ibara ya 175 “tabia njema” iliondolewa kama sifa mojawapo ya mtu anyeweza kuteuliwa kuwa jaji wa Mahakama ya Juu. Katika ibara “tabia mbaya” inatajwa kama sababu mojawapo inayoweza kumfanya Jaji wa Mahakama ya juu akaondolewa katika madaraka yake hayo. Hii ni kupingana ibara tofauti za Katiba.
(2) Endapo Rais anaona kuwa suala la kumuondoa Jaji madarakani
linahitaji kuchunguzwa, basi katika hali hiyo utaratibu utakuwa kama ifuatavyo:
(a) Rais anaweza, baada ya kushauriana na Jaji Mkuu, kumsimamisha
kazi Jaji huyo;
(b) Rais atateua Tume ambayo itakuwa na Mwenyekiti na Wajumbe
wengine wasiopungua wawili na angalau nusu ya wajumbe hao wawe
ni Majaji wa Mahakama ya Juu au Mahakama ya Rufani kutoka nchi
yoyote iliyomo kwenye Jumuiya ya Madola; na
(c) Tume hiyo itachunguza shauri hilo kisha itatoa taarifa kwa Rais
kuhusu maelezo ya shauri hilo na itamshauri Rais kama Jaji huyo
anayehusika aondolewe madarakani kwa mujibu wa masharti ya
Ibara hii kwa sababu ya kushindwa kufanya kazi kutokana na
maradhi au sababu nyingine yoyote au kwa sababu ya tabia mbaya. (2) Endapo Rais anaona kuwa suala la kumuondoa Jaji madarakani
linahitaji kuchunguzwa, basi katika hali hiyo utaratibu utakuwa kama ifuatavyo:
(a) Rais anaweza, baada ya kushauriana na Jaji Mkuu, kumsimamisha
kazi Jaji huyo;
(b) Rais atateua Tume ambayo itakuwa na Mwenyekiti na Wajumbe
wengine wasiopungua wawili na angalau nusu ya wajumbe hao wawe
ni Majaji wa Mahakama ya Juu au Mahakama ya Rufani kutoka nchi
yoyote iliyomo kwenye Jumuiya ya Madola; na
(c) Tume hiyo itachunguza shauri hilo kisha itatoa taarifa kwa Rais
kuhusu maelezo ya shauri hilo na itamshauri Rais kama Jaji huyo
anayehusika aondolewe madarakani kwa mujibu wa masharti ya
Ibara hii kwa sababu ya kushindwa kufanya kazi kutokana na
maradhi au sababu nyingine yoyote au kwa sababu ya tabia mbaya. HAKUNA Katika ibara ya 170 “tabia njema” iliondolewa kama sifa mojawapo ya mtu anyeweza kuteuliwa kuwa jaji wa Mahakama ya Juu. Katika ibara “tabia mbaya” inatajwa kama sababu mojawapo inayoweza kumfanya Jaji wa Mahakama ya juu akaondolewa katika madaraka yake hayo. Hii ni kupingana ibara tofauti za Katiba.
(3) Jaji aliyesimamishwa kazi kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya
(2), ataendelea kulipwa mshahara na maslahi yake mengine hadi Jaji huyo
atakapoondolewa kazini na Rais chini ya masharti ya ibara ndogo ya (4). (3) Jaji aliyesimamishwa kazi kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya
(2), ataendelea kulipwa mshahara na maslahi yake mengine hadi Jaji huyo
atakapoondolewa kazini na Rais chini ya masharti ya ibara ndogo ya (4). HAKUNA
(4) Endapo Tume iliyoteuliwa kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya
(2) itamshauri Rais kwamba Jaji ambaye mwenendo wake umechunguzwa na
Tume hiyo aondolewe kazini kwa sababu ya kushindwa kufanya kazi kutokana na
maradhi au sababu nyingine yoyote au kwa sababu ya tabia mbaya, Rais atamuondoa kazini Jaji huyo na
utumishi wake utakuwa umekoma. (4) Endapo Tume iliyoteuliwa kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya
(2) itamshauri Rais kwamba Jaji ambaye mwenendo wake umechunguzwa na
Tume hiyo aondolewe kazini kwa sababu ya kushindwa kufanya kazi kutokana na
maradhi au sababu nyingine yoyote, Rais atamuondoa kazini Jaji huyo na
utumishi wake utakuwa umekoma. Tabia mbaya haikutajwa kama sababu inayoweza kumfanya Rais kumuondoa Jaji katika madaraka yake hayo, kama Tume iliyoundwa itagundua kuwa jaji huyo anashindwa kufanya kazi kwa sababu ya tabia mbaya. ibara hii ndogo inapingana na ibara ya 176 (1) na (2) ambayo inaainisha kuwa “tabia mbaya” inaweza kuwa mojawapo ya sababu za Jaji kuondolewa katika mdaraka yake hayo.
(5) Endapo Tume iliyoteuliwa kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya
(2) itamshauri Rais kwamba Jaji ambaye mwenendo wake umechunguzwa na
Tume hiyo asiondolewe, Rais atafuta uamuzi wa kumsimamisha kazi na utumishi
wa Jaji huyo utaendelea. (5) Endapo Tume iliyoteuliwa kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya
(2) itamshauri Rais kwamba Jaji ambaye mwenendo wake umechunguzwa na
Tume hiyo asiondolewe, Rais atafuta uamuzi wa kumsimamisha kazi na utumishi
wa Jaji huyo utaendelea. HAKUNA
(6) Masharti ya Ibara hii hayatawahusu watu walioteuliwa kukaimu nafasi
ya ujaji. (6) Masharti ya Ibara hii hayatawahusu watu walioteuliwa kukaimu nafasi
ya ujaji. HAKUNA
(d) Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano

165.-(1) Kutakuwa na Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya
Muungano, itakayojulikana kwa kifupi kama “Mahakama ya Rufani” na
ambayo itakuwa na:
(a) Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani;
(b) Makamu Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani; na
(c) Majaji wengine wasiopungua kumi na saba.
182.-(1) Kutakuwa na Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya
Muungano, itakayojulikana kwa kifupi kama “Mahakama ya Rufani” na
ambayo itakuwa na:
(a) Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani;
(b) Makamu Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani; na
(c) Majaji wengine wasiopungua kumi na saba.
HAKUNA
(2) Majaji wa Mahakama ya Rufani watateuliwa kwa kuzingatia sifa
zitakazoainishwa katika Katiba hii na uwakilishi wa kila upande wa Jamhuri ya
Muungano. (2) Jaji wa Mahakama ya Rufani atateuliwa kwa kuzingatia sifa
zitakazoainishwa katika Katiba hii na uwakilishi wa kila upande wa Jamhuri ya
Muungano. Kutumika kwa umoja kwenye neno Jaji;
(3) Sheria zitakazotungwa kwa mujibu wa Katiba za Nchi Washirika zitaweka masharti kuhusu utaratibu wa kuwasilisha rufani mbele ya Mahakama ya Rufani. (3) Bunge litatunga sheria itakayoweka masharti kuhusu utaratibu wa
Kuwasilisha rufaa mbele ya Mahakama ya Rufani. Sheria zitatungwa na Bunge.
166.-(1) Akidi ya kila kikao cha Mahakama ya Rufani itakuwa ni Majaji
wa Mahakama ya Rufani watatu. 183.-(1) Akidi ya kila kikao cha Mahakama ya Rufani itakuwa ni Majaji
wa Mahakama ya Rufani watatu. HAKUNA
(2) Kila shauri linalohitaji uamuzi wa Mahakama ya Rufani litaamuliwa
kwa kufuata kauli ya walio wengi kati ya Majaji wa Mahakama ya Rufani
waliosikiliza shauri au rufani husika. (2) Kila shauri linalohitaji uamuzi wa Mahakama ya Rufani litaamuliwa
kwa kufuata kauli ya walio wengi kati ya Majaji wa Mahakama ya Rufani
waliosikiliza shauri husika. Kutokutajwa kwa neno rufani.
HAKUNA (3) Jaji mmoja wa Mahakama ya Rufani anaweza kutekeleza madaraka
yoyote ya Mahakama ya Rufani ambayo hayahusiki na uamuzi juu ya rufani,
isipokuwa kwamba:
(a) katika rufaa ya jinai, iwapo Jaji wa Mahakama ya Rufani aliyeombwa
kutekeleza madaraka hayo atatoa uamuzi ambao mwombaji
hataridhika nao, basi mwombaji atakuwa na haki kutaka maombi yake
yaamuliwe na Mahakama ya Rufani; au
(b) katika rufaa ya madai, Mahakama ya Rufani yaweza kubatilisha au
kubadilisha amri, agizo au uamuzi wa namna nyingine yoyote
uliotolewa na Jaji mmoja wa Mahakama ya Rufani kwa mujibu wa
masharti ya Ibara hii. imefutwa
167.-(1) Mahakama ya Rufani itakuwa na mamlaka ya:
(a) Kusikiliza na kuamua juu ya kila rufani inayowasilishwa mbele ya Mahakama ya Rufani kutokana na hukumu au uamuzi wowote wa Mahakama Kuu za Nchi Washirika au Mahakama yoyote ya chini iliyopewa mamlaka maalum ya kusikiliza mashauri amabayo kwa kawaida husikilizwa na Mahakama Kuu;
(b) kufanya mapitio ya maamuzi ya Mahakama Kuu za Nchi Washirika au Mahakama yoyote ya chini iliyopewa mamlaka maalum ya kusikiliza mashauri ambayo kwa kawaida husikilizwa na Mahakama Kuu; na
(c) kufanya jambo jingine kama itakavyoainishwa kwenye sheria za nchi
184.-(1) Mahakama ya Rufani itakuwa na mamlaka ya:
(a) kusikiliza na kuamua kuhusu rufaa inayowasilishwa mbele ya
Mahakama ya Rufani kutokana na hukumu au uamuzi wowote wa
Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano au Mahakama Kuu ya
Zanzibar au Mahakama yoyote ya chini iliyopewa mamlaka maalum
ya kusikiliza mashauri ambayo kwa kawaida husikilizwa na
Mahakama Kuu;
(b) kufanya mapitio ya maamuzi ya Mahakama Kuu ya Jamhuri ya
Muungano au Mahakama Kuu ya Zanzibar au Mahakama yoyote ya
chini iliyopewa mamlaka maalum ya kusikiliza mashauri ambayo kwa
kawaida husikilizwa na Mahakama Kuu; na
(c) kufanya jambo jingine kama itakavyoainishwa katika sheria iliyotungwa na Bunge.
Kutajwa kwa Mahakama Kuu ya Muungano na Mahakama Kuu ya Zanzibar
(2) Mahakama ya Rufani itaandaa kanuni kwa ajili ya utekelezaji wa
mamlaka yake. (2) Mahakama ya Rufani itaandaa kanuni kwa ajili ya utekelezaji wa
mamlaka yake. Hakuna
(3) Bunge linaweza kutunga sheria itakayoweka masharti zaidi kuhusu uendeshaji
wa Mahakama ya Rufani. (3) Bunge litatunga sheria itakayoweka masharti zaidi kuhusu uendeshaji
wa Mahakama ya Rufani. Ulazima wa Bunge kutunga sheria itakayoweka masharti zaidi.
168.-(1) Jaji wa Mahakama ya Rufani atakuwa na madaraka ya kusikiliza
na kuamua shauri lolote katika Mahakama ya Rufani. 185.-(1) Jaji wa Mahakama ya Rufani atakuwa na madaraka ya kusikiliza
na kuamua rufaa yoyote katika Mahakama ya Rufani. Mahakama ya rufaa kuamua kuhusu rufaa tu na sio shauri lolote.
(2) Bila ya kujali masharti ya ibara ndogo ya (1), iwajo Jaji wa Mahakama ya Rufani kabla ya kuteuliwa kwake alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Nchi Washirika, Jaji huyo anaweza kuendelea kufanya kazi katika mahakama aliyotoka hadi amalize kutayarisha na kutoa hukumu au hadi akamilishe shughuli nyingine yoyote inayohusika na mashauri ambayo alikwishaanza kuyasikiliza kabla ya hajateuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. (2) Bila ya kujali masharti ya ibara ndogo ya (1), iwapo Jaji wa
Mahakama ya Rufani kabla ya kuteuliwa kwake alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu
ya Jamhuri ya Muungano au Mahakama Kuu ya Zanzibar, Jaji huyo anaweza
kuendelea kufanya kazi katika Mahakama aliyotoka hadi amalize kutayarisha na
kutoa hukumu au hadi akamilishe shughuli nyingine yoyote inayohusika na
mashauri ambayo alikwishaanza kuyasikiliza kabla hajateuliwa kuwa Jaji wa
Mahakama ya Rufani. Hakuna
(3) Kwa kuzingatia masharti ya ibara ndogo ya (2), itakuwa ni halali kwa
Jaji wa Mahakama ya Rufani kutoa hukumu au uamuzi mwingine wowote
unaohusika kwa kutumia na kutaja nafasi ya madaraka aliyokuwa akiishika kabla
ya kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani na endapo hukumu hiyo au
uamuzi huo utapingwa kwa njia ya rufani itakayowasilishwa mbele ya Mahakama
ya Rufani, Jaji huyo hatakuwa na mamlaka ya kusikiliza rufani hiyo. (3) Kwa kuzingatia masharti ya ibara ndogo ya (2), itakuwa ni halali kwa
Jaji wa Mahakama ya Rufani kutoa hukumu au uamuzi mwingine wowote
unaohusika kwa kutumia na kutaja nafasi ya madaraka aliyokuwa akiishika kabla
ya kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani na endapo hukumu hiyo au
uamuzi huo utapingwa kwa njia ya rufani itakayowasilishwa mbele ya Mahakama
ya Rufani, Jaji huyo hatakuwa na mamlaka ya kusikiliza rufani hiyo.
(e) Uteuzi wa Jaji wa Mahakama ya Rufani

169.-(1) Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani atateuliwa na Rais kutoka orodha ya majina ya watu watatu yatakayopendekezwa na
Tume ya Utumishi wa Mahakama.
186.-(1) Kutakuwa na Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani ambaye
atateuliwa na Rais kutoka orodha ya majina ya watu watatu yaliyopendekezwa na
Tume ya Utumishi wa Mahakama. i. Kutumika kwa neno kutaakuwa na Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani

(2) Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani atakuwa ndiye Mkuu wa
Mahakama ya Rufani na msaidizi wa Jaji Mkuu katika utendaji wa kazi katika
Mahakama ya Rufani, na katika madaraka hayo, Mwenyekiti wa Mahakama ya
Rufani atatekeleza kazi na shughuli atakazopangiwa mara kwa mara na Jaji
Mkuu. (2) Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani atakuwa ndiye Mkuu wa
Mahakama ya Rufani na msaidizi wa Jaji Mkuu katika utendaji wa kazi katika
Mahakama ya Rufani, na katika madaraka hayo, Mwenyekiti wa Mahakama ya
Rufani atatekeleza kazi na shughuli atakazopangiwa mara kwa mara na Jaji
Mkuu. Hakuna
(3) Mtu anaweza kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani
endapo atakuwa na sifa zifuatazo:
(a) awe ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano mwenye tabia
njema, uadilifu na uaminifu;
(b) awe na shahada ya sheria kutoka chuo cha elimu ya juu
kinachotambuliwa na mamlaka inayoshughulikia elimu ya juu katika
Jamhuri ya Muungano; na
(i) awe amefanya kazi ya ujaji katika Mahakamu Kuu za Nchi Washirika; au
(ii) awe wakili, mtumishi wa umma au mwanataaluma akiwa na
sifa ya kusajiliwa kuwa wakili na amekuwa na sifa hizo
mfululizo kwa muda usiopungua miaka kumi na tano. (3) Mtu anaweza kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani
endapo atakuwa na sifa zifuatazo:
(a) awe ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano mwenye tabia
njema, uadilifu na uaminifu;
(b) awe na shahada ya sheria kutoka chuo cha elimu ya juu
kinachotambuliwa na mamlaka inayoshughulikia elimu ya juu katika
Jamhuri ya Muungano; na
(i) awe amefanya kazi ya ujaji katika Mahakamu Kuu ya Jamhuri
ya Muungano au Mahakama Kuu ya Zanzibar; au
(ii) awe wakili, mtumishi wa umma au mwanataaluma akiwa na
sifa ya kusajiliwa kuwa wakili na amekuwa na sifa hizo
mfululizo kwa muda usiopungua miaka kumi na tano. Kutajwa kwa Mahakama Kuu ya Muungano na Mahakama Kuu ya Zanzibar
170.-(1) Makamu Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani atateuliwa na
Rais kutoka katika orodha ya majina ya watu watatu yatakayopendekezwa na
Tume ya Utumishi wa Mahakama na atakuwa ndiye Msaidizi Mkuu wa
Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani. 187.-(1) Makamu Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani atateuliwa na
Rais kutoka katika orodha ya majina ya watu watatu yatakayopendekezwa na
Tume ya Utumishi wa Mahakama na atakuwa ndiye Msaidizi Mkuu wa
Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani. Hakuna
(2) Mtu atateuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani
endapo atakuwa na sifa zilizoainishwa katika Ibara ya 169(3). (2) Mtu atateuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani
endapo atakuwa na sifa zilizoainishwa katika Ibara ya 186(3). Hakuna
(2) Uteuzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani utafanywa kwa msingi kwamba, endapo Mwenyekiti atateuliwa kutoka upande mmoja wa Jamuhuri ya Muungano, basi Makamu Mwenyekiti atateuliwa kutoka upande wa pili wa Jamuhuri ya Muungano. Ibara haipo. Ibara hii haipo. Ibara imeshindwa kuzingatia mgawanyo wa kimadaraka kati ya pande mbili za muungano.
171.-(1) Jaji wa Mahakama ya Rufani atateuliwa na Rais kutoka miongoni
mwa majina yatakayopendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama. 188.-(1) Jaji wa Mahakama ya Rufani atateuliwa na Rais kutoka miongoni
mwa majina yatakayopendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama. Hakuna
(2) Mtu anaweza kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani endapo
atakuwa na sifa zilizoainishwa katika Ibara ya 169(3). (2) Mtu anaweza kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani endapo
atakuwa na sifa zilizoainishwa katika Ibara ya 181(3). Hakuna
172.- Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani, Makamu Mwenyekiti au Jaji
wa Mahakama ya Rufani atashika madaraka yake mara tu atakapoapishwa na
Rais kiapo cha uaminifu na kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa
kazi kitakachowekwa kwa mujibu wa sheria. 189. Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani, Makamu Mwenyekiti au Jaji
wa Mahakama ya Rufani atashika madaraka yake mara tu atakapoapishwa na
Rais kiapo cha uaminifu na kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa
kazi kitakachowekwa kwa mujibu wa sheria. Hakuna
173.-(1) Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani
atashika nafasi ya madaraka ya Ofisi ya Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani hadi atakapofikisha umri wa miaka sabini,
isipokuwa kama:
(a) atajiuzulu;
(b) atashindwa kumudu kazi kutokana na maradhi;
(c) ataondolewa katika nafasi ya madaraka ya Mwenyekiti wa Mahakama
ya Rufani kwa mujibu wa Katiba hii; au
(d) atafariki dunia. 190.-(1) Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani
atashika nafasi ya madaraka yake hadi atakapofikisha umri wa miaka sabini,
isipokuwa kama:
(a) atajiuzulu;
(b) atashindwa kumudu kazi kutokana na maradhi;
(c) ataondolewa katika nafasi ya madaraka ya Mwenyekiti wa Mahakama
ya Rufani kwa mujibu wa Katiba hii; au
(d) atafariki dunia. Kuwekwa pamoja kwa vifungu vya kuondolewa madarakni kwa Mwenyekiti na Makamu wa Mwenyekiti
(2) Makamu Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani
atashika nafasi ya madaraka yake hadi atakapofikisha umri wa miaka sabini,
isipokuwa kama:
(a) atajiuzulu;
(b) atashindwa kumudu kazi kutokana na maradhi;
(c) ataondolewa katika nafasi ya madaraka ya Mwenyekiti wa Mahakama
ya Rufani kwa mujibu wa Katiba hii; au
(d) atafariki dunia. Ibara haipo Kuwekwa pamoja kwa vifungu vya kuondolewa madarakni kwa Mwenyekiti na Makamu wa Mwenyekiti
(3) Jaji aliyetimiza umri wa kustaafu atalazimika kuendelea kufanya kazi
baada ya kutimiza umri huo hadi amalize kutayarisha na kutoa hukumu au hadi
akamilishe shughuli nyingine yoyote inayohusika na mashauri ambayo
alikwishaanza kuyasikiliza kabla hajatimiza umri wa kustaafu. (2) Jaji aliyetimiza umri wa kustaafu atalazimika kuendelea kufanya kazi
baada ya kutimiza umri huo hadi amalize kutayarisha na kutoa hukumu au hadi
akamilishe shughuli nyingine yoyote inayohusika na mashauri ambayo
alikwishaanza kuyasikiliza kabla hajatimiza umri wa kustaafu. Hakuna

(4) Bila ya kujali masharti ya ibara ndogo ya (2), Mwenyekiti au Makamu
Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani aliyetimiza umri wa kustaafu, ataachia
nafasi ya madaraka ya Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti wa Mahakama ya
Rufani, isipokuwa ataendelea kutekeleza shughuli ambazo hajazikamilisha akiwa
katika nafasi ya madaraka ya Jaji wa Mahakama ya Rufani hadi atakapokamilisha
shughuli hizo. (3) Bila ya kujali masharti ya ibara ndogo ya (2), Mwenyekiti au Makamu
Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani aliyetimiza umri wa kustaafu, ataachia
nafasi ya madaraka ya Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti wa Mahakama ya
Rufani, isipokuwa ataendelea kutekeleza shughuli ambazo hajazikamilisha akiwa
katika nafasi ya madaraka ya Jaji wa Mahakama ya Rufani hadi atakapokamilisha
shughuli hizo. Hakuna
174.-(1) Iwapo itatokea kwamba:
(a) nafasi ya madaraka ya Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani ipo wazi;
(b) Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani hayupo katika Jamhuri ya
Muungano; au
(c) Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani ameshindwa kutekeleza kazi
kwa mujibu wa Katiba hii,
Makamu Mwenyekiti atatekeleza kazi za Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani
hadi atakapoteuliwa Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani mwingine au hadi
Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani ambaye alikuwa hayupo nchini au alikuwa
hawezi kumudu kazi zake kutokana na maradhi atakaporejea kazini. 191.-(1) Iwapo itatokea kwamba:
(a) nafasi ya madaraka ya Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani ipo wazi;
(b) Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani hayupo katika Jamhuri ya
Muungano; au
(c) Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani ameshindwa kutekeleza kazi
kwa mujibu wa Katiba hii,
Makamu Mwenyekiti atatekeleza kazi za Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani
hadi atakapoteuliwa Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani mwingine au hadi
Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani ambaye alikuwa hayupo nchini au alikuwa
hawezi kumudu kazi zake kutokana na maradhi atakaporejea kazini. Hakuna
(2) Endapo ufanisi wa kazi za Mahakama ya Rufani utahitaji ateuliwe
Kaimu Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jaji Mkuu
atamshauri Rais kumteua Kaimu Jaji wa Mahakama ya Rufani. (2) Endapo ufanisi wa kazi za Mahakama ya Rufani utahitaji ateuliwe
Kaimu Jaji wa Mahakama ya Rufani, Tume ya Utumishi wa Mahakama
itamshauri Rais kumteua Kaimu Jaji wa Mahakama ya Rufani. Ushauri wa kuteuliwa kwa Kaimu Jaji wa Mahakama ya Rufani kuwekwa chini ya Tume ya Utumishi wa Mahakama.
(3) Endapo Rais ataridhika na ushauri wa Jaji Mkuu, atamteua Kaimu Jaji wa Mahakama ya Rufani kutoka miongoni mwa
watu wanaoweza kuteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani. (3) Endapo Rais ataridhika na ushauri wa Tume ya Utumishi wa
Mahakama, atamteua Kaimu Jaji wa Mahakama ya Rufani kutoka miongoni mwa
watu wanaoweza kuteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani. Ushauri wa kuteuliwa kwa Kaimu Jaji wa Mahakama ya Rufani kuwekwa chini ya Tume ya Utumishi wa Mahakama.
(4) Mtu atakayeteuliwa kuwa Kaimu Jaji wa Mahakama ya Rufani
atafanya kazi kama Kaimu Jaji wa Mahakama ya Rufani kwa muda wote
utakaotajwa wakati wa kuteuliwa kwake, au kama muda haukutajwa, basi hadi
uteuzi utakapofutwa na Rais. (4) Mtu atakayeteuliwa kuwa Kaimu Jaji wa Mahakama ya Rufani
atafanya kazi kama Kaimu Jaji wa Mahakama ya Rufani kwa muda wote
utakaotajwa wakati wa kuteuliwa kwake, au kama muda haukutajwa, basi hadi
uteuzi utakapofutwa na Rais. Hakuna
(5) Bila kujali masharti ya ibara ndogo ya (4), mtu aliyeteuliwa kuwa
Kaimu Jaji wa Mahakama ya Rufani ataendelea kufanya kazi kama Kaimu Jaji
wa Mahakama ya Rufani hadi amalize kutayarisha na kutoa hukumu au hadi
amalize shughuli nyingine yoyote inayohusika na rufani au mashauri mengine
ambayo alikwishaanza kuyasikiliza kabla ya muda wake wa kazi haujamalizika
au uteuzi wake haujafutwa. (5) Bila kujali masharti ya ibara ndogo ya (4), mtu aliyeteuliwa kuwa
Kaimu Jaji wa Mahakama ya Rufani ataendelea kufanya kazi kama Kaimu Jaji
wa Mahakama ya Rufani hadi amalize kutayarisha na kutoa hukumu au hadi
amalize shughuli nyingine yoyote inayohusika na rufani au mashauri mengine
ambayo alikwishaanza kuyasikiliza kabla ya muda wake wa kazi haujamalizika
au uteuzi wake haujafutwa. Hakuna
(6) Kwa madhumuni ya Ibara hii, Kaimu Jaji wa Mahakama ya Rufani
atakuwa na mamlaka kamili ya Jaji wa Mahakama ya Rufani na atatekeleza kazi
zote za Jaji wa Mahakama ya Rufani. (6) Kwa madhumuni ya Ibara hii, Kaimu Jaji wa Mahakama ya Rufani
atakuwa na mamlaka kamili ya Jaji wa Mahakama ya Rufani na atatekeleza kazi
zote za Jaji wa Mahakama ya Rufani. Hakuna
175.-(1) Jaji wa Mahakama ya Rufani anaweza kuondolewa katika nafasi ya jaji wa mahakama ya Rufani kwa sababu ya kushindwa kutekeleza kazi yake kutokana na:
(a) maradhi;
(b) kukiuka kanuni za maadili ya Majaji wa Mahakama ya Rufani;
(c) Kutokuwa na uwezo wa kumudu kazi za Jaji; au
(d) tabia mbaya au mwenendo unaokiuka maadili ya uongozi wa umma.
192. Kwa mujibu wa Katiba hii, masharti kuhusu utaratibu wa
kushughulikia nidhamu ya Jaji wa Mahakama ya Rufani, utakuwa kama
ulivyoainishwa katika Ibara ya 181 inayoweka masharti na utaratibu wa nidhamu
ya Jaji wa Mahakama ya juu. Kutokuainishwa kwa utaratibu wa kushughulikia nidhamu ya Jaji wa Mahakama ya Rufani; badala yake kuhusisha utaratibu na utaratibu wa nidhamu ya Jaji wa Mahakama ya Juu. Ingekuwa vizuri sana katiba itamke wazi njia za kumwajibisha Jaji wa Mahakama ya Rufani. Hii ikiwekwa bayana italeta hofu ya utii wa sheria lakini mda mwingine kama funzo kwa viongozi wengine.
(2) Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani, Makamu mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani au Jaji wa Mahakama ya Rufani anaweza kuondolewa katika nafasi ya madaraka ya Jaji kwa kufuata utaratibu unaofanana na ule uliowekwa kwa ajili ya kumuondoa kazini Jaji Mkuu, Naibu Jaji Mkuu au Jaji wa Mahakama ya Juu kama ulivyoelezwa. Haipo Ibara hii kwa upande wa Rasimu, umewataja Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani, Makamu Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani au Jaji wa Mahakama ya Rufani; na kuelezea utaratibu wa kuondolewa kwao madarakani. Ukiangalia ibara ya 187, imetaja utaratibu tu wa kushughulikia nidhamu ya Jaji wa Mahakama ya Rufani, bila kuainisha kama utaratibu huo utahusisha pia Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani.
(f)Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano

HAIPO 193.-(1) Kutakuwa na Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano,
itakayojulikana kwa kifupi kama “Mahakama Kuu”, ambayo mamlaka yake
yatakuwa kama ilivyoelezwa katika Katiba hii au katika sheria nyingine yoyote.

(2) Iwapo Katiba hii au sheria nyingine yoyote haikutamka wazi kwamba
shauri la aina iliyotajwa mahsusi litasikilizwa kwanza katika Mahakama ya ngazi
iliyotajwa mahsusi kwa ajili hiyo, basi Mahakama Kuu itakuwa na mamlaka ya
kusikiliza kila shauri la aina hiyo.
(3) Hali kadhalika, Mahakama Kuu itakuwa na uwezo wa kutekeleza
shughuli yoyote ambayo kwa mujibu wa mila za kisheria zinazotumika Tanzania,
shughuli ya aina hiyo kwa kawaida hutekelezwa na Mahakama Kuu:
Isipokuwa kwamba masharti ya ibara hii ndogo yatatumika bila kuathiri
mamlaka ya Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano kama ilivyoelezwa
katika Katiba hii au katika sheria nyingine yoyote.
194.-(1) Bila kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (2), mtu aweza tu
kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ikiwa ana sifa maalum, kama
ilivyofafanuliwa katika ibara ndogo ya (2), na awe mtu ambaye amekuwa na mojawapo ya sifa maalum kwa muda usiopungua miaka kumi.
(2) Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa ibara ndogo ya (3), (9) na (10) za
Ibara hii, “sifa maalum” maana yake ni mtu aliye na shahada ya sheria toka chuo
cha elimu ya juu kinachotambulika kwa mujibu wa sheria na:
(a) amekuwa hakimu;
(b) amefanya kazi katika utumishi wa umma akiwa na sifa za kufanya
kazi ya uwakili au ni wakili wa kujitegemea;
(c) ana sifa ya kusajiliwa kuwa wakili; au
(d) amekuwa na sifa hizo mfululizo kwa muda usiopungua miaka kumi.
(3) Iwapo Rais ataridhika kwamba ijapokuwa mtu mwenye sifa mojawapo
ya hizo sifa maalum hakuwa na sifa hiyo kwa muda usiopungua miaka kumi,
lakini mtu huyo ana uwezo, ujuzi na kwa kila hali anafaa kukabidhiwa madaraka
ya Jaji wa Mahakama Kuu na kuna sababu za kumfanya mtu huyo astahili
kukabidhiwa madaraka hayo, basi Rais aweza kutengua lile sharti la kuwa na sifa
maalum kwa muda usiopungua miaka kumi, na baada ya kushauriana na Tume ya
Utumishi wa Mahakama, Rais aweza kumteua mtu huyo kuwa Jaji wa Mahakama
Kuu.
(4) Ikitokea kwamba kiti cha Jaji yeyote kitakuwa wazi au ikiwa Jaji
yeyote atateuliwa kuwa Kaimu Jaji au kama atashindwa kutekeleza kazi zake kwa
sababu yoyote, au kama Jaji Mkuu atamshauri Rais kuwa kazi za Mahakama Kuu
zilivyo wakati huo zahitaji ateuliwe Kaimu Jaji, basi Rais aweza, baada ya
kushauriana na Jaji Mkuu kama kawaida, kumteua Kaimu Jaji kutoka miongoni
mwa watu wenye sifa maalum:
Isipokuwa kwamba:
(a) mtu hatahesabiwa kuwa hastahili kuteuliwa kwa mujibu wa masharti
ya ibara hii ndogo kwa sababu tu kwamba ametimiza umri uliotajwa
katika ibara ndogo ya (1) ya Ibara ya 190 ya Katiba hii;
(b) kwa madhumuni ya kumteua Kaimu Jaji kwa mujibu wa masharti ya
ibara hii ndogo, Rais aweza kutengua lile sharti la kuwa na sifa
maalum kwa muda usiopungua miaka kumi kwa sababu kama zile
zilizotajwa katika ibara ndogo ya (3) ya Ibara hii.
(5) Mtu yeyote atakayeteuliwa kuwa Kaimu Jaji kwa mujibu wa masharti
ya ibara ndogo ya (4), ataendelea kufanya kazi kama Kaimu Jaji kwa muda
wowote utakaotajwa wakati wa kuteuliwa kwake au, kama muda haukutajwa,
mpaka uteuzi wake utakapofutwa na Rais, lakini bila ya kujali kwamba muda
wake wa kazi umemalizika au kwamba uteuzi wake umefutwa, mtu huyo aweza
kuendelea kufanya kazi kama Kaimu Jaji mpaka amalize kutayarisha na kutoa
hukumu au mpaka akamilishe shughuli nyingine yoyote inayohusika na mashauri
ambayo alikwisha anza kuyasikiliza kabla muda wake wa kazi haujamalizika au
kabla ya uteuzi wake haujafutwa.
(6) Kutakuwa na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, ambaye katika ibara
zifuatazo kwenye Katiba hii atatajwa tu kwa kifupi kama “Jaji Kiongozi”, na
Majaji wengine wa Mahakama Kuu wasiopungua thelathini watakaoteuliwa na
Rais baada ya kushauriana na Tume ya Utumishi wa Mahakama.
(7) Bila kuathiri masharti ya Katiba hii au sheria nyingine yoyote kuhusu
madaraka ya Jaji Mkuu aliyetajwa katika Ibara ya 170, Jaji Kiongozi atakuwa ndiye msaidizi maalum wa Jaji Mkuu katika utendaji wa kazi katika Mahakama
Kuu na Mahakama nyinginezo zote za ngazi ya chini yake, na katika madaraka
hayo Jaji Kiongozi atatekeleza kazi na shughuli atakazoagizwa au kuelekezwa
mara kwa mara na Jaji Mkuu, na kwa madhumuni ya Ibara hii, Jaji Kiongozi
atakuwa mkuu wa Mahakama Kuu.
(8) Mbali ya madaraka yake ya kawaida ya Jaji wa Mahakama Kuu kama
Majaji wengine wote wa Mahakama Kuu, Jaji Kiongozi atakuwa pia na mamlaka
ya kutekeleza kazi na shughuli zote zinazoambatana na mamlaka ya Mahakama
Kuu ambazo kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii au ya sheria nyingine yoyote
au kufuatana na mila za kisheria zinazotumika Tanzania hutakiwa zitekelezwe na
Mkuu wa Mahakama Kuu:
Isipokuwa kwamba masharti ya ibara hii ndogo hayatatumika kwa ajili ya
utekelezaji wa kazi au shughuli ambazo kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii au
ya Sheria nyingine yoyote au kufuatana na mila za kisheria zinazotumika
Tanzania zimetajwa mahsusi au zinafahamika kuwa ni kazi au shughuli
zinazotakiwa kutekelezwa tu na Jaji Mkuu.
(9) Kwa madhumuni ya kuondoa mashaka juu ya ufafanuzi au utekelezaji
wa masharti ya ibara ndogo ya (7) na (8), inatamkwa rasmi hapa kwamba
isipokuwa kama masharti ya Katiba hii au ya sheria nyingine yoyote yameagiza
vinginevyo, Jaji Mkuu atakuwa na uwezo wa kutoa kwa Jaji Kiongozi mara kwa
mara maagizo au maelekezo kuhusu utendaji wa kazi na shughuli zake kama
Mkuu wa Mahakama Kuu; vile vile, Jaji Mkuu atakuwa na uwezo wa kukasimu
kwa Jaji Kiongozi baadhi ya madaraka yake ya uongozi na usimamizi juu ya
utekelezaji wa kazi katika Mahakama Kuu na Mahakama nyinginezo zote za
ngazi ya chini yake, na kila inapohitajika, Jaji Mkuu anaweza kutekeleza yeye
mwenyewe moja kwa moja madaraka yake yoyote aliyoyakasimu kwa Jaji
Kiongozi.
(10) Ikitokea kwamba kiti cha Jaji Kiongozi kitakuwa wazi au kwamba
Jaji Kiongozi atashindwa kutekeleza kazi zake kwa sababu yoyote, basi kazi hizo
zitatekelezwa na Jaji mmojawapo atakayeteuliwa na Rais kwa ajili hiyo, na Jaji
huyo atatekeleza kazi hizo mpaka atakapoteuliwa Jaji Kiongozi mwingine na
kushika madaraka ya kiti cha Jaji Kiongozi au mpaka Jaji Kiongozi mwenyewe
ambaye alikuwa hamudu kazi zake atakaporejea kazini.
195.-(1) Kila Jaji wa Mahakama Kuu atalazimika kuacha kazi yake
atakapotimiza umri wa miaka sitini na tano, lakini masharti ya ibara hii ndogo
yatatumika bila kuathiri masharti katika Ibara hii.
(2) Jaji yeyote wa Mahakama Kuu anaweza kustaafu kazi katika utumishi
wa umma wa Jamhuri ya Muungano wakati wowote baada ya kutimiza umri wa
miaka sitini, isipokuwa kama Rais ataagiza kwamba asistaafu na iwapo Rais
ataagiza hivyo, basi huyo Jaji atakayehusika na maagizo hayo ya Rais hatakuwa
na haki ya kustaafu mpaka upite kwanza muda wowote utakaotajwa na Rais kwa
ajili hiyo.
(3) Iwapo Rais ataona kuwa kwa ajili ya manufaa ya umma inafaa Jaji
aliyetimiza umri wa miaka sitini na tano aendelee kufanya kazi, na huyo Jaji
mwenyewe anakubali kwa maandishi kuendelea kufanya kazi, basi Rais aweza kuagiza kuwa Jaji huyo aendelee kufanya kazi kwa muda wowote utakaotajwa na
Rais.
(4) Bila ya kujali kwamba Jaji ametimiza umri ambao analazimika kuacha
kazi kwa mujibu wa masharti ya Ibara hii, mtu anayefanya kazi ya Jaji wa
Mahakama Kuu aweza kuendelea kufanya kazi baada ya kutimiza umri huo
mpaka amalize kutayarisha na kutoa hukumu au mpaka akamilishe shughuli
nyingine yoyote inayohusika na mashauri ambayo alikwishaanza kuyasikiliza
kabla hajatimiza umri huo wa kuacha kazi.
196.-(1) Utaratibu wa kushughulikia nidhamu ya Jaji, kwa sababu mbali
na zile zilizoainishwa katika ibara ndogo ya (2), utakuwa kama
utakavyoelekezwa na sheria itakayotungwa na Bunge.
(2) Jaji wa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano aweza tu
kuondolewa katika madaraka ya kazi kwa sababu ya kushindwa kutekeleza kazi
yake ama kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote au kwa sababu ya
tabia mbaya inayoathiri maadili ya kazi ya Jaji au sheria inayohusu maadili ya
uongozi wa umma, na hataondolewa madarakani isipokuwa kwa mujibu wa
masharti ya ibara ndogo ya (4).
(3) Iwapo Rais anaona kuwa suala la kumuondoa Jaji madarakani
linahitaji kuchunguzwa, basi katika hali hiyo utaratibu utakuwa kama ifuatavyo:
(a) Rais anaweza, baada ya kushauriana na Jaji Mkuu, kumsimamisha
kazi Jaji huyo;
(b) Rais atateua Tume ambayo itakuwa na Mwenyekiti na Wajumbe
wengine wasiopungua wawili na huyo Mwenyekiti na angalau nusu ya
wajumbe wengine wa Tume hiyo itabidi wawe watu ambao ni Majaji
wa Mahakama ya Juu au Mahakama ya Rufani kutoka nchi yoyote
iliyomo kwenye Jumuiya ya Madola; na
(c) Tume hiyo itachunguza shauri lote kisha itatoa taarifa kwa Rais
kuhusu maelezo ya shauri hilo na itamshauri Rais kama huyo Jaji
anayehusika aondolewe kazini kwa mujibu wa masharti ya Ibara hii
kwa sababu ya kushindwa kufanya kazi kutokana na maradhi au
sababu nyingine yoyote au kwa sababu ya tabia mbaya.
(4) Ikiwa Tume iliyoteuliwa kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya
(3), itamshauri Rais kwamba Jaji ambaye habari zake zimechunguzwa na hiyo
Tume aondolewe kazini kwa sababu ya kushindwa kufanya kazi kutokana na
maradhi au sababu nyingine yoyote au kwa sababu ya tabia mbaya, basi Rais
atamuondoa kazini Jaji huyo anayehusika na utumishi wa Jaji huyo utakuwa
umekoma.
(5) Ikiwa suala la kumuondoa Jaji kazini limepelekwa kweye Tume kwa
ajili ya uchunguzi kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (3), Rais anaweza
kumsimamisha kazi Jaji huyo anayehusika, na Rais aweza wakati wowote kufuta
uamuzi huo wa kumsimamisha kazi Jaji huyo, na kwa hali yoyote uamuzi huo
utabatilika ikiwa Tume itamshauri Rais kwamba Jaji huyo asiondolewe kazini.
(6) Masharti ya Ibara hii yatatumika bila kuathiri masharti ya ibara ndogo
ya (10) ya Ibara ya 189.
197. Jaji wa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano atashika madaraka
yake mara tu atakapokuwa ameapishwa na Rais kiapo cha uaminifu na kiapo
kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi kitakachowekwa kwa mujibu
wa sheria.
(g) Mahakama Kuu ya Zanzibar

198.-(1) Kutakuwa na Mahakama Kuu ya Zanzibar itakayoanzishwa kwa
mujibu wa Katiba ya Zanzibar.
(2) Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa Sura hii ya Katiba hii, ifahamike
kwamba masharti yaliyomo katika Sura hii hayazuii kuendelea kuwapo au
kuanzishwa, kwa mujibu wa sheria zinazotumika Zanzibar, kwa Mahakama Kuu
ya Zanzibar au mahakama zilizo chini ya Mahakama Kuu ya Zanzibar.
199.-(1) Bila kuathiri masharti ya Ibara ya 139, mamlaka ya Mahakama
Kuu ya Zanzibar yatakuwa kama itakavyoelezwa katika sheria zinazotumika
Zanzibar.
(2) Bila kuathiri masharti ya Katiba hii au sheria nyingine yoyote
iliyotungwa na Bunge, iwapo sheria yoyote iliyotungwa na Bunge inayotumika
Tanzania Bara na vile vile Zanzibar imekabidhi madaraka yoyote kwa Mahakama
Kuu ya Jamhuri ya Muungano, basi Mahakama Kuu ya Zanzibar yaweza
kutekeleza madaraka hayo kwa kiasi kile kile inavyoweza kutekeleza Mahakama
Kuu ya Jamhuri ya Muungano.
(h)Usimamizi wa Shughuli za Mahakama

176.-(1) Kutakuwa na Msajili Mkuu wa Mahakama ya Jamhuri ya
Muungano atakayeitwa “Msajili Mkuu wa Mahakama”, atakayeteuliwa na Rais
kufuatia mapendekezo ya Tume ya Utumishi wa Mahakama.
200.-(1) Kutakuwa na Msajili Mkuu wa Mahakama ya Jamhuri ya
Muungano atakayeitwa “Msajili Mkuu wa Mahakama”, atakayeteuliwa na Rais
kufuatia mapendekezo ya Tume ya Utumishi wa Mahakama. Hakuna.
(2) Mtu anaweza kuteuliwa kuwa Msajili Mkuu wa Mahakama endapo
atakuwa na sifa zifuatazo:
(a) awe ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano mwenye sifa ya
uadilifu, tabia njema na uaminifu; na
(b) awe na shahada ya sheria kutoka chuo cha elimu ya juu
kinachotambuliwa na mamlaka inayoshughulikia elimu ya juu katika
Jamhuri ya Muungano; na
(i) awe amefanya kazi ya uhakimu katika Mahakama za Nchi Washirika; au
(ii) amekuwa mtumishi wa umma katika Jamhuri ya Muungano,
na amekuwa na sifa hizo mfululizo kwa muda usiopungua miaka kumi. (2) Mtu anaweza kuteuliwa kuwa Msajili Mkuu wa Mahakama endapo
atakuwa na sifa zifuatazo:
(a) awe ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano mwenye sifa ya
uadilifu, tabia njema na uaminifu; na
(b) awe na shahada ya sheria kutoka chuo cha elimu ya juu
kinachotambuliwa na mamlaka inayoshughulikia elimu ya juu katika
Jamhuri ya Muungano; na
(i) awe amefanya kazi ya uhakimu katika Mahakama za Jamhuri
ya Muungano; au
(ii) amekuwa mtumishi wa umma katika Jamhuri ya Muungano,
na amekuwa na sifa hizo mfululizo kwa muda usiopungua miaka kumi. Kutajwa kwa “Mahakama za Jamuhuri ya Muungano”,
177.-(1) Msajili Mkuu wa Mahakama atakuwa na majukumu yafuatayo:
(a) kusimamia utekelezaji wa shughuli za kimahakama;
(b) kuratibu masuala ya kimahakama; na
(c) majukumu mengine atakayopangiwa na Jaji Mkuu. 201.-(1) Msajili Mkuu wa Mahakama atakuwa na majukumu yafuatayo:
(a) kusimamia utekelezaji wa shughuli za Mahakama;
(b) kuratibu masuala ya Mahakama; na
(c) majukumu mengine atakayopangiwa na Jaji Mkuu. -kutajwa kwa neno “shughuli za Mahakama”, badala ya “shughuli za kimahakama’.

(2) Katika kutekeleza majukumu yake, Msajili Mkuu wa Mahakama atawajibika kwa Jaji Mkuu. (2) Katika kutekeleza majukumu yake, Msajili Mkuu wa Mahakama ya
Tanzania atawajibika kwa Jaji Mkuu. Kuongezwa kwa neno Mahakam “ya Tanzania”
178.- Kutakuwa na Mtendaji Mkuu wa Mahakama atakayeteuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watumishi wa umma na kufuatia mapendekezo ya Tume ya Utumishi wa Umma na kuidhinishwa na Bunge. 202.-(1) Kutakuwa na Mtendaji Mkuu wa Mahakama atakayeteuliwa na
Rais kutoka miongoni mwa majina matatu ya watumishi wa umma
yaliyopendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama. i. Kuwekwa ukomo wa majina matatu yanayohitajika kuteuliwa na Rais;
ii. Kuondolewa kwa kipengele cha jina litakaloteuliwa kuthibitishwa na Bunge.
iii. Jina linalopendekezwa litapendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama. Sifa ya jina la mtu anayependekezwa ni mtu huyo kutoka miongoni mwa watumishi wa umma; hivyo ni busara kwa Tume ya Utumishi wa Umma kupendekeza jina hilo.
(2) Mtu hatateuliwa kushika nafasi ya Mtendaji Mkuu wa Mahakama
isipokuwa tu kama ni:
(a) mtumishi mwandamizi wa umma;
(b) mwenye weledi na uzoefu katika masuala ya utawala na mambo ya
fedha; na
(c) mwadilifu na mwenye tabia na mwenendo usiotiliwa shaka na jamii. (2) Mtu hatateuliwa kushika nafasi ya Mtendaji Mkuu wa Mahakama
isipokuwa tu kama ni:
(a) mtumishi mwandamizi wa umma;
(b) mwenye weledi na uzoefu katika masuala ya utawala na mambo ya
fedha; na
(c) mwadilifu na mwenye tabia na mwenendo usiotiliwa shaka na jamii. Hakuna
179.-(1) Mtendaji Mkuu wa Mahakama atakuwa na majukumu yafuatayo:
(a) Katibu wa Tume ya Utumishi wa Mahakama;
(b) Ofisa Masuuli wa Mahakama;
(c) msimamizi mkuu wa Mfuko wa Mahakama;
(d) msimamizi wa masuala ya utawala ya Mahakama; na
(e) kutekeleza kazi nyingine atakazopangiwa na Jaji Mkuu. 203.-(1) Mtendaji Mkuu wa Mahakama atakuwa na majukumu yafuatayo:
(a) Katibu wa Tume ya Utumishi wa Mahakama;
(b) Ofisa Masuuli wa Mahakama;
(c) msimamizi mkuu wa Mfuko wa Mahakama;
(d) msimamizi wa masuala ya utawala ya Mahakama; na
(e) kutekeleza kazi nyingine atakazopangiwa na Jaji Mkuu. Hakuna
(2) Katika kutekeleza majukumu yake, Mtendaji Mkuu wa Mahakama
atawajibika kwa Jaji Mkuu. (2) Katika kutekeleza majukumu yake, Mtendaji Mkuu wa Mahakama
atawajibika kwa Jaji Mkuu. Hakuna

SEHEMU YA TATU
TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA NA MFUKO WA MAHAKAMA
(a)Tume ya Utumishi wa Mahakama

180.-(1) Kutakuwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama ambayo itakuwa
na wajumbe nane watakaoteuliwa na Rais kama ifuatavyo:
(a) Jaji Mkuu ambaye atakuwa Mwenyekiti;
(b) Mwanasheria
(c) Jaji mmoja wa Mahakama ya Juu;
Mkuu wa Serikali;
(d) Jaji mmoja wa Mahakama ya Rufani;
(e) Mwakilishi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika;
(f) Mwakilishi wa Chama cha Wanasheria Zanzibar;
(g) Wawakilishi wawili wa vitivo vya sheria kutoka vyuo vikuu, mmoja
kutoka Tanzania Bara na mmoja kutoka Zanzibar watakaopendekezwa na vyuo vya elimu ya juu husika; na
(h) Mtendaji Mkuu wa Mahakama ambaye atakuwa Katibu. 204.-(1) Kutakuwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama ambayo itakuwa
na wajumbe kumi na moja watakaoteuliwa na Rais kama ifuatavyo:
(a) Jaji Mkuu ambaye atakuwa Mwenyekiti;
(b) Mwanasheria Mkuu wa Serikali;
(c) Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani;
(d) Jaji Mkuu wa Zanzibar;
(e) Jaji mmoja wa Mahakama ya Juu;
(f) Jaji mmoja wa Mahakama ya Rufani;
(g) Jaji Kiongozi;
(h) Mwakilishi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika;
(i) Mwakilishi wa Chama cha Wanasheria Zanzibar;
(j) Wawakilishi wawili wa vitivo vya sheria kutoka vyuo vikuu, mmoja
kutoka Tanzania Bara na mmoja kutoka Zanzibar watakaopendekezwa
na vyuo vya elimu ya juu husika; na
(k) Mtendaji Mkuu wa Mahakama ambaye atakuwa Katibu. i. Kuongezewa kwa idadi ya wajumbe kutoka nane mpaka kumi na moja.
Wajumbe walioongezwa ni
a. Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani
b. Jaji Mkuu wa Zanzibar
c. Jaji Kiongozi
ii. kuondolewa kwa neno Tanganyika na badala yake kuwekwa neno Tanzania Bara

Jambo hili halikubariki kabisa, kwani badala ya kupunguza nafasi wao wanaongeza nafasi. Hali hii ikiruhusiwa ni kulitumbukiza Taifa kwenye ulipaji wa mishahala isiyo na tija na kuzidi kuwaumiza wananchi walipakodi.
(2) Tume inaweza kumualika mtu mwingine
yeyote mwenye utaalamu mahsusi kushiriki katika kikao chochote cha Tume,
isipokuwa mtu huyo hatakuwa na haki ya kupiga kura. (2) Tume ya Utumishi wa Mahakama inaweza kumualika mtu mwingine
yeyote mwenye utaalamu mahsusi kushiriki katika kikao chochote cha Tume,
isipokuwa mtu huyo hatakuwa na haki ya kupiga kura.
(3) Tume itaweka utaratibu wa kuendesha vikao vyake. (3) Tume ya Utumishi wa Mahakama itaweka utaratibu wa kuendesha
vikao vyake.
181.-(1) Tume ya Utumishi wa Mahakama itakuwa na wajibu wa
kuendeleza na kuwezesha uhuru na uwajibikaji wa Mahakama na utoaji haki
wenye ufanisi, mafanikio na uwazi. 205.-(1) Tume ya Utumishi wa Mahakama itakuwa na wajibu wa
kuendeleza na kuwezesha uhuru na uwajibikaji wa Mahakama na utoaji haki
wenye ufanisi, mafanikio na uwazi. Hakuna
(2) Tume ya Utumishi wa Mahakama itakuwa na wajibu wa:
(a) kupendekeza kwa Rais majina ya watu wanaofaa kuteuliwa kuwa
Jaji Mkuu, Naibu Jaji Mkuu, Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani,
Makamu Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani, Majaji wa
Mahakama ya Juu na Mahakama ya Rufani;
(b) kupitia na kupendekeza masharti ya utumishi wa Majaji, Wasajili,
Mahakimu na watumishi wengine wa Mahakama ikiwemo masuala
yanayohusu nidhamu na maslahi yao;
(c)kuteua wasajili na kuajiri watumishi wengine wa Mahakama, kupokea malalamiko dhidi yao na kuwachukulia hatua za kinidhamu kwa mujibu wa sheria za nchi;
(d) kuandaa na kutekeleza mipango ya kujiendeleza kielimu kwa Majaji na watumishi wengine wa Mahakama;
(e) kupendekeza Serikalini hatua za kuimarisha Mahakama ili
kuongeza ufanisi katika utoaji haki;
(f) kutoa fursa ya majadiliano kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Mahakama ya Jamuhuri ya Muungano na hivyo kumsaidia Jaji Mkuu katika kutekeleza majukumu yake kwa malengo ya kuleta ufanisi na mafanikio katika utoaji haki; na
(g) kutekeleza majukumu yoyote itakayopewa kwa mujibu wa Katiba
hii au sheria. (2) Tume ya Utumishi wa Mahakama itakuwa na wajibu wa:
(a) kupendekeza kwa Rais majina ya watu wanaofaa kuteuliwa kuwa
Jaji Mkuu, Naibu Jaji Mkuu, Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani,
Makamu Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani, Majaji wa
Mahakama ya Juu, Mahakama ya Rufani na Majaji wa Mahakama
Kuu;
(b) kupitia na kupendekeza masharti ya utumishi wa Majaji, Wasajili,
Mahakimu na watumishi wengine wa Mahakama ikiwemo masuala
yanayohusu maadili, nidhamu na maslahi yao;
(c) kupendekeza Serikalini hatua za kuimarisha Mahakama ili
kuongeza ufanisi katika utoaji haki; na
(d) kutekeleza majukumu yoyote itakayopewa kwa mujibu wa Katiba
hii au sheria. -Kuongezwa kwa Majaji wa Mahakam Kuu
– Kuongezwa kwa “maadili” kama masharti yaliyo chini ya Tume ya Mahakama
– Kupunguzwa kwa wajibu wa Tume, kutoka saba mpaka. Orodha ya wajibu ulioondolewa ni ule wa ibara ya 181(2) c,d na f ya Rasimu.

Maudhui ya Ibara hii ndogo yamewekwa katika Ibara ndogo ya 4. (3) Katika kutekeleza majukumu yake, Tume ya Utumishi wa
Mahakama inaweza kukasimu madaraka yake kwa kamati mbalimbali
zitakazoundwa kwa mujibu wa sheria.
(4) Katika kutekeleza majukumu yake, Tume ya Utumishi wa
Mahakama inaweza kukasimu madaraka yake kwa kamati mbalimbali
zitakazoundwa kwa mujibu wa sheria. Maudhui ya Ibara hii ndogo yamewekwa katika Ibara ndogo ya 3.
(3) Katika kuekeleza majukumu take, Tume itazingatia:
(a) Uwazi katika mchakato wa uteuzi wa Majaji na Ajira ya watumishi wengine wa Mahakama ya Jamuhuri ya Muungano;
(b) Uwakilishi wa kila upande wa Jamuhuri ya Muungano;
(c) Uwakilishi wa Kijinsia; HAIPO KIFUNGU CHOPTE KIMEONDOLEWA
(5) Bila kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (2)(b), mapendekezo
ya maslahi kwa Majaji na watumishi wengine wa Mahakama
yatawasilishwa kwenye chombo chenye jukumu la kusimamia maslahi ya
watumishi wa umma. (4) Bila kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (2)(b), mapendekezo
ya maslahi kwa Majaji, mahakimu na watumishi wengine wa Mahakama
yatawasilishwa kwenye chombo chenye jukumu la kusimamia maslahi ya
watumishi wa umma. Kuongezwa kwa neno mahakimu.
(6) Bunge litatunga sheria itakayoweka masharti ya utekelezaji wa
majukumu ya Tume. (5) Bunge litatunga sheria itakayoweka masharti ya utekelezaji wa
majukumu ya Tume ya Utumishi wa Mahakama. Kuongezwa kwa maneno Tume “ya Utumishi wa Mahakama”
182.- Itakuwa ni marufuku kwa Jaji wa Mahakama ya Juu, Jaji wa Mahakama ya Rufani, Msajili Mkuu wa Mahakama, Msajili wa ngazi yoyote na Mtendaji Mkuu wa Mahakama kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa, isipokuwa atakuwa na haki ya kupiga kura kuchagua viongozi katika vyombo vya uwakilishi. 206. Itakuwa ni marufuku kwa Jaji wa Mahakama ya Juu, Jaji wa
Mahakama ya Rufani, Jaji wa Mahakama Kuu, Msajili Mkuu wa Mahakama,
Hakimu, na Mtendaji Mkuu wa Mahakama kuwa mwanachama wa chama
chochote cha siasa, isipokuwa atakuwa na haki ya kupiga kura kuchagua
viongozi katika vyombo vya uwakilishi. -kuongezwa kwa Jaji wa Mahakama Kuu na Hakimu katika marufuku ya kuwa mwanachama wa chama cha siasa
-kuondolewa kwa Msajili wa ngazi yoyote katika marufuku
(b)Mfuko wa Mahakama
183.-(1) Kutakuwa na Mfuko wa Mahakama ya Jamhuri ya
Muungano ambao utakuwa chini ya usimamizi wa Mtendaji Mkuu wa
Mahakama. 207.-(1) Kutakuwa na Mfuko wa Mahakama ya Jamhuri ya
Muungano ambao utakuwa chini ya usimamizi wa Mtendaji Mkuu wa
Mahakama. Hakuna
(2) Mfuko wa Mahakama ya Jamhuri ya Muungano utatumika kwa ajili ya
kugharamia shughuli za utawala na uendeshaji wa Mahakama ya Jamhuri ya
Muungano na shughuli nyingine muhimu katika utekelezaji wa majukumu ya
Mahakama. (2) Mfuko wa Mahakama ya Jamhuri ya Muungano utatumika kwa ajili ya
kugharamia shughuli za utawala na uendeshaji wa Mahakama ya Jamhuri ya
Muungano na shughuli nyingine muhimu katika utekelezaji wa majukumu ya
Mahakama. Hakuna
(3) Serikali itahakikisha kwamba katika kila bajeti ya mwaka wa fedha
wa Serikali, inatenga kwa kiwango kinachotosha fedha ambazo zitaingizwa
katika Mfuko wa Mahakama ya Jamhuri ya Muungano. (3) Serikali itahakikisha kwamba katika kila bajeti ya mwaka wa fedha
wa Serikali, inatenga kwa kiwango kinachotosha fedha ambazo zitaingizwa
katika Mfuko wa Mahakama ya Jamhuri ya Muungano. Hakuna
(4) Bunge litatunga sheria itakayoweka masharti kuhusu
73
uendeshaji wa Mfuko wa Mahakama ya Jamhuri ya Muungano. (4) Bunge litatunga sheria itakayoweka masharti kuhusu
uendeshaji wa Mfuko wa Mahakama ya Jamhuri ya Muungano. Hakuna

SURA YA 11 Ibara ya 184 ya Rasimu ya pili ya Katiba—SURA YA 13 Ibara ya 208 ya Katiba inayopendekezwa Misingi mikuu ya utumishi wa umma

184.-(1) Kutakuwa na utumishi wa umma katika Jamhuri ya
Muungano utakaozingatia misingi na kanuni zifuatazo:
(a) kwamba utumishi wa umma ni dhamana kutoka kwa wananchi
na hivyo mtumishi anatakiwa kutumikia wananchi kwa uadilifu,
uaminifu na unyenyekevu;
(b) umuhimu wa kudumisha na kukuza viwango vya juu vya maadili ya kitaaluma;
(c) umuhimu wa kuzingatia matumizi bora na yenye tija ya
rasilimali;
(d) kutoa huduma kwa umma kwa njia ya haki, usawa na bila
upendeleo;
(e) kuhamasisha wananchi kushiriki katika maandalizi ya sera
mbalimbali za nchi;
(f) kuitikia matakwa na mahitaji ya watu kwa haraka na kwa
wakati unaofaa;
(g) kujitolea katika utekelezaji wa sera na mipango ya kitaifa;
(h) uwajibikaji wa viongozi kwa makosa yanayofanyika chini yao;
(i) kuhamasisha na kutekeleza sera ya uwazi katika kutoa habari za
kweli kwa umma na kwa wakati unaofaa; na
(j) kuhakikisha kwamba uteuzi na uajiri katika nafasi mbalimbali
kwa kuzingatia uwezo wa kitaaluma, weledi, maarifa, ujuzi na
uzoefu wao katika eneo husika.
(2) Misingi na Kanuni za Utumishi wa Umma zilizoainishwa katika
Ibara hii zitazingatiwa na kutumika katika uteuzi wa kushika nafasi za madaraka ya uongozi katika:
(a) mamlaka katika mihimili ya dola;
(b) taasisi na idara zote za Serikali; na
(c) mashirika, makampuni na wakala wa Serikali.
(3) Bunge litatunga sheria kuweka masharti ya utekelezaji wa misingi ya utumishi iliyoainishwa katika ibara ndogo ya (1). 208 (1)Kutakuwa na utumishi wa umma katika Jamhuri ya Muungano
utakaozingatia misingi mikuu ifuatayo:
(a) kwamba utumishi wa umma ni dhamana kutoka kwa wananchi na
hivyo mtumishi anatakiwa kutumikia wananchi kwa uadilifu, uaminifu
na unyenyekevu;
(b) kutoa huduma kwa umma kwa wakati, kwa njia ya haki, usawa na bila
upendeleo; na
(c) kuhakikisha kwamba uteuzi na ajira katika nafasi mbalimbali
unazingatia uwezo wa kitaaluma, weledi, maarifa, ujuzi, usawa wa
kijinsia na uzoefu katika eneo husika na fursa kwa watu wenye
ulemavu.
(2) Misingi ya utumishi wa umma iliyoainishwa katika Ibara hii
itazingatiwa na kutumika katika uteuzi wa kushika nafasi za madaraka ya uongozi
katika:
(a) mamlaka katika mihimili ya dola;
(b) taasisi na idara zote za Serikali; na
(c) mashirika, makampuni na wakala wa Serikali.
(3) Bunge litatunga sheria kuweka masharti ya utekelezaji wa misingi ya
utumishi iliyoainishwa katika ibara ndogo ya (1).

Baadhi ya fasili zimeondolewa ambavyo awali zilikuwa kwenye Rasimu ya ya pili ya Katiba kama ifuatavyo:
b)Umuhimu wa kudumisha na kukuza viwango vya juu vya maadili ya kitaaluma
C) umuhimu wa kuzingatia matumizi bora na yenye tija ya rasilimali
e) Kuhamasisha wananchi kushiriki katika maandalizi ya sera mbalimbali za nchi
f) Kuitikia matakwa na mahitaji ya watu kwa haraka na kwa wakati unaofaa.
g) Kujitolea katika utakelezaji wa sera na mipango ya kitaifa
h) uwajibikaji wa viongozi kwa makosa yanayofanyika chini yao
i) Kuhamasisha na kutekeleza sera ya uwazi katika kutoa habari za kweli kwa umma na kwa wakati unaofaa.
Ibara ndogo zilizoondolewa bado zinastahili kuwepo. Utumishi wa umma ni nguzo muhimu ya serikali hivyo ni budi kukuzwa, kuimarishwa na kusimamiwa kikatiba.

Ibara hii pia imepunguza sana madaraka ya wananchi ambayo walipewa katika rasimu ya pili kwa mfano;
e) Kuhamasisha wananchi kushiriki katika maandalizi ya sera mbalimbali za nchi.

Pia dhana ya uwajibikaji na uwazi kwa viongozi imeondolewa.

IBARA RASIMU YA PILI KATIBA INAYOPENDEKEZWA TOFAUTI MAONI
SURA YA 11 Ibara ya 184 ya Rasimu ya pili ya Katiba—

SURA YA 13 Ibara ya 208 ya Katiba inayopendekezwa Misingi mikuu ya utumishi wa umma

184.-(1) Kutakuwa na utumishi wa umma katika Jamhuri ya
Muungano utakaozingatia misingi na kanuni zifuatazo:
(a) kwamba utumishi wa umma ni dhamana kutoka kwa wananchi
na hivyo mtumishi anatakiwa kutumikia wananchi kwa uadilifu,
uaminifu na unyenyekevu;
(b) umuhimu wa kudumisha na kukuza viwango vya juu vya maadili ya kitaaluma;
(c) umuhimu wa kuzingatia matumizi bora na yenye tija ya
rasilimali;
(d) kutoa huduma kwa umma kwa njia ya haki, usawa na bila
upendeleo;
(e) kuhamasisha wananchi kushiriki katika maandalizi ya sera
mbalimbali za nchi;
(f) kuitikia matakwa na mahitaji ya watu kwa haraka na kwa
wakati unaofaa;
(g) kujitolea katika utekelezaji wa sera na mipango ya kitaifa;
(h) uwajibikaji wa viongozi kwa makosa yanayofanyika chini yao;
(i) kuhamasisha na kutekeleza sera ya uwazi katika kutoa habari za
kweli kwa umma na kwa wakati unaofaa; na
(j) kuhakikisha kwamba uteuzi na uajiri katika nafasi mbalimbali
kwa kuzingatia uwezo wa kitaaluma, weledi, maarifa, ujuzi na
uzoefu wao katika eneo husika.
(2) Misingi na Kanuni za Utumishi wa Umma zilizoainishwa katika
Ibara hii zitazingatiwa na kutumika katika uteuzi wa kushika nafasi za madaraka ya uongozi katika:
(a) mamlaka katika mihimili ya dola;
(b) taasisi na idara zote za Serikali; na
(c) mashirika, makampuni na wakala wa Serikali.
(3) Bunge litatunga sheria kuweka masharti ya utekelezaji wa misingi ya utumishi iliyoainishwa katika ibara ndogo ya (1). 208 (1)Kutakuwa na utumishi wa umma katika Jamhuri ya Muungano
utakaozingatia misingi mikuu ifuatayo:
(a) kwamba utumishi wa umma ni dhamana kutoka kwa wananchi na
hivyo mtumishi anatakiwa kutumikia wananchi kwa uadilifu, uaminifu
na unyenyekevu;
(b) kutoa huduma kwa umma kwa wakati, kwa njia ya haki, usawa na bila
upendeleo; na
(c) kuhakikisha kwamba uteuzi na ajira katika nafasi mbalimbali
unazingatia uwezo wa kitaaluma, weledi, maarifa, ujuzi, usawa wa
kijinsia na uzoefu katika eneo husika na fursa kwa watu wenye
ulemavu.
(2) Misingi ya utumishi wa umma iliyoainishwa katika Ibara hii
itazingatiwa na kutumika katika uteuzi wa kushika nafasi za madaraka ya uongozi
katika:
(a) mamlaka katika mihimili ya dola;
(b) taasisi na idara zote za Serikali; na
(c) mashirika, makampuni na wakala wa Serikali.
(3) Bunge litatunga sheria kuweka masharti ya utekelezaji wa misingi ya
utumishi iliyoainishwa katika ibara ndogo ya (1).

Baadhi ya fasili zimeondolewa ambavyo awali zilikuwa kwenye Rasimu ya ya pili ya Katiba kama ifuatavyo:
b)Umuhimu wa kudumisha na kukuza viwango vya juu vya maadili ya kitaaluma
C) umuhimu wa kuzingatia matumizi bora na yenye tija ya rasilimali
e) Kuhamasisha wananchi kushiriki katika maandalizi ya sera mbalimbali za nchi
f) Kuitikia matakwa na mahitaji ya watu kwa haraka na kwa wakati unaofaa.
g) Kujitolea katika utakelezaji wa sera na mipango ya kitaifa
h) uwajibikaji wa viongozi kwa makosa yanayofanyika chini yao
i) Kuhamasisha na kutekeleza sera ya uwazi katika kutoa habari za kweli kwa umma na kwa wakati unaofaa.
Ibara ndogo zilizoondolewa bado zinastahili kuwepo. Utumishi wa umma ni nguzo muhimu ya serikali hivyo ni budi kukuzwa, kuimarishwa na kusimamiwa kikatiba.

Ibara hii pia imepunguza sana madaraka ya wananchi ambayo walipewa katika rasimu ya pili kwa mfano;
e) Kuhamasisha wananchi kushiriki katika maandalizi ya sera mbalimbali za nchi.

Pia dhana ya uwajibikaji na uwazi kwa viongozi imeondolewa.
185 ya rasimu ya pili na ibara ya 209 ya Katiba iliyopendekezwa Ajira na uteuzi wa kiongozi na mtumishi wa umma katika taasisi za muungano

Serikali. 185.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii, ajira katika utumishi
wa umma na uteuzi katika nafasi za madaraka ya uongozi katika Serikali ya
Jamhuri ya Muungano na taasisi zake, itatolewa na kufanyika kwa
kuzingatia:
-(a) taaluma na uweledi; na
(b) uwakilishi wa kila upande wa Jamhuri ya Muungano.
(2) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (1), uteuzi wa viongozi
katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano utafanyika kwa kuzingatia ushiriki
wa kila upande wa Jamhuri ya Muungano.

209 (1)Bila kuathiri masharti ya Katiba hii, ajira katika utumishi wa
umma na uteuzi katika nafasi za madaraka ya uongozi na utumishi katika Serikali
ya Jamhuri ya Muungano na taasisi zake, itatolewa na kufanyika kwa kuzingatia
taaluma, uadilifu na weledi.
(2) Bila kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (1), uteuzi wa kiongozi na
mtumishi katika taasisi au wizara ya Muungano utafanyika kwa kuzingatia
uwakilishi wa pande mbili za Muungano, usawa wa jinsia na watu wenye ulemavu. Katiba iliyopendekezwa imeongeza katika Ibara ndogo ya pili, usawa wa jinsia na watu wenye ulemavu Ibara hii imeboreshwa zaidi kwa kuongeza usawa wa jinsia na watu wenye ulemavu hivyo makundi maalumu katika jamii yamepewa nafasi zaidi katika Ibara hii.
186 ya rasimu ya pili na 210 ya Katiba inayopendekezwa Tume ya Utumishi wa Umma

186.-(1) Kutakuwa na Tume ya Utumishi wa Umma itakayokuwa
na Mwenyekiti na wajumbe wengine sita watakaoteuliwa na Rais na kuidhinishwa na Bunge.
(2) Katika kuteua wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Umma, Rais
atazingatia Kanuni za Utumishi wa Umma zilizoainishwa katika Katiba
hii.
(3) Sifa za Mwenyekiti na Mjumbe wa Tume ya Utumishi wa Umma
zitakuwa kama ifuatavyo:
(a) awe ni raia wa Jamhuri ya Muungano;
(b) awe na shahada ya chuo cha elimu ya juu kinachotambulika kwa
mujibu wa sheria za nchi;
(c) awe na uzoefu wa utumishi wa umma, upeo mkubwa katika
mambo ya utumishi, utawala na mambo ya jamii kwa kipindi
kisichopungua miaka kumi; na
(d) awe na heshima, uweledi, uaminifu, uadilifu na asiye na tabia au
mwenendo wenye kutiliwa shaka na jamii. 210 (1)Kutakuwa na Tume ya Utumishi wa Umma itakayokuwa na
Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wengine watano watakaoteuliwa
na Rais.
(2) Katika kuteua wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Umma, Rais
atazingatia misingi ya utumishi wa umma iliyoainishwa katika Ibara ya 208.
(3) Sifa za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Mjumbe wa Tume ya
Utumishi wa Umma zitakuwa kama ifuatavyo:
(a) awe ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano;
(b) awe na shahada ya chuo cha elimu ya juu kinachotambulika kwa
mujibu wa sheria;
(c) awe na uzoefu wa utumishi wa umma, upeo mkubwa katika mambo ya
utumishi, utawala na mambo ya jamii kwa kipindi kisichopungua
74
miakamiaka kumi, isipokuwa kwa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti
wawe na uzoefu huo kwa kipindi kisichopungua miaka kumi na tano;
na
(d) awe na heshima, weledi, uaminifu, uadilifu na asiye na tabia au
mwenendo wenye kutiliwa shaka na jamii.
Katibu wa Tume
ya Utumishi wa
Umma
Watumishi wa tume ya utumishi wa umma Kuidhinishwa na bunge imeondolewa .

Tofauti ipo katika Ibara ndogo ya pili ya Katiba iliyopendekezwa, katika kuteua wajumbe wa Tume ya Utumishi wa umma, Rais atazingatia misingi ya utumishi iliyoanishwa katika Ibara ya 208. Bunge limepunguziwa madaraka ya kuidhinisha watumishi umma.Bado madaraka ya Rais yanaendelea kuwa makubwa.
Jambo hili la kuwazuia wabunge wasiidhinishe watumishi wa umma ni kuwanyima wananchi haki yao ya kumkubari mtu kupitia nafasi zao za uwakilishi.

Kwa kusema katika kuteua wajumbe wa Tume ya Utumishi wa umma, Rais atazingatia misingi ya utumishi iliyoanishwa katika Ibara ya 208 na sio kwa mujibu wa Katiba hii, imewekwa ukomo/masharti katika misingi ya utumishi wa umma ambayo itatumika katika uchaguzi.
Ibara ya 187 ya Rasimu ya pili na Ibara ya 211 ya Katiba inayopendekezwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma.
187.-(1) Kutakuwa na Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma ambaye atateuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano au Serikali za Nchi Washirika baada ya kuidhinishwa na Bunge.
(2) Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma atakuwa ndiye Mkuu wa Sekretarieti ya Utumishi wa Umma, Mtendaji Mkuu na mtekelezaji wa majukumu ya kila siku ya Tume.
211 (1)Kutakuwa na Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma ambaye
atateuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watumishi wa umma katika Jamhuri ya
Muungano.
(2) Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma atakuwa ndiye Mkuu wa
Sekretarieti ya Utumishi wa Umma, Mtendaji Mkuu na mtekelezaji wa majukumu
ya kila siku ya Tume.
Kutakuwa na Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma ambaye atateuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watumishi wa Serikali ya jamhuri ya Muungano au Serikali za nchi washirika baada ya kuidhinishwa na bunge Katika Ibara hii Rais ameendelea kupewa madaraka makubwa ya kuteua viongozi wa umma.
Kwa katiba hii rais anazidi kufanywa Mungu mtu. Maana kazi ya kuwateua viongozi wakuu ameachiwa yeye.

Wananchi wameendelea kunyimwa madaraka ya kuidhinisha uteuzi wa viongozi wa umma kupitia wawakilishi wao bungeni.
Ibara ya 188 ya Rasimu ya pili ya Katiba na Ibara ya 212 ya Katiba inayopendekezwa Mamlaka na Majukumu ya Tume ya Utumishi wa Umma.
188.-(1) Tume ya Utumishi wa Umma itakuwa ni chombo cha juu katika utumishi wa umma chenye mamlaka ya kusimamia na kuratibu mambo yote kuhusu utumishi wa umma.
(2) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (1), majukumu ya Tume ya Utumishi wa Umma yatakuwa ni: (a) kumshauri Rais juu ya uteuzi wa viongozi katika nafasi mbalimbali kwa mujibu wa Katiba hii; (b) kutoa miongozo mbalimbali na kusimamia mchakato wa ajira katika utumishi wa umma kwa kuzingatia vigezo stahiki; (c) kuteua watu kuhudumu au kushikilia ofisi kwa muda katika utumishi wa umma, kuidhinisha uteuzi na kudhibiti nidhamu na kuwaondoa watumishi wanaohudumu au kushikilia ofisi hizo; (d) kusimamia na kuhamasisha utekelezaji wa misingi na kanuni za utumishi katika sekta zote za utumishi wa umma; (e) kushughulikia rufanizinazowasilishwa na watumishi wa umma dhidi ya uamuzi wa mamlaka mbalimbali za nidhamu katika utumishi wa umma; (f) kutekeleza majukumu mengine yoyote kama yatakavyoainishwa katika sheria za nchi juu ya masuala ya utumishi wa umma na sheria nyingine za nchi; (g) kuunda na kupanga ngazi za mishahara na marupurupu ya watumishi wa umma, ikiwemo, viongozi wa kisiasa, watumishi katika Utumishi wa Serikali, Utumishi wa Bunge na Utumishi wa Mahakama; na (h) kudurusu na kusawazisha mishahara na marupurupu ya watumishi wa umma ikiwemo viongozi wa kisiasa, watumishi katika Utumishi wa Serikali, Utumishi wa Bunge na Utumishi wa Mahakama.

212-(1) Tume ya Utumishi wa Umma itakuwa ni chombo cha juu chenye
mamlaka ya nidhamu na uratibu wa mambo yote kuhusu utumishi wa umma.
(2) Majukumu ya Tume ya Utumishi wa Umma yatakuwa ni:
(a) kuhamasisha utekelezaji wa misingi ya utumishi wa umma;
(b) kushughulikia rufaa zinazowasilishwa na watumishi wa umma dhidi
ya uamuzi wa mamlaka mbalimbali za nidhamu katika utumishi wa
umma; na
(c) kutekeleza majukumu mengine yoyote kwa kadri yatakavyoainishwa
katika sheria kuhusu masuala ya utumishi wa umma.
(3) Bunge litatunga sheria itakayoainisha utaratibu wa kuweka masharti ya
utekelezaji wa kazi za Tume ya Utumishi wa Umma.
a) Kumshauri Rais juu ya uteuzi wa viongozi katika nafasi mbalimbali kwa mujibu wa katiba hii
b) Kutoa miongozo mbalimbali na kusimamia mchakato wa ajira katika utumishi wa umma kwa kuzingatia vigezo stahiki
c) Kuteua watu kuhudumu au kushikilia ofisi kwa muda katika utumishi wa umma, kuidhinisha uteuzi na kudhibiti nidhamu na kuwaondoa watumishi wanaohudumu au kushikilia ofisi hizo;
d) kuunda na kupanga ngazi za mishahara na marupurupu ya watumishi wa umma, ikiwemo, viongozi wa kisiasa, watumishi katika Utumishi wa Serikali, Utumishi wa Bunge na Utumishi wa Mahakama; na (h) kudurusu na kusawazisha mishahara na marupurupu ya watumishi wa umma ikiwemo viongozi wa kisiasa, watumishi katika Utumishi wa Serikali, Utumishi wa Bunge na Utumishi wa Mahakama.

Fasili ya Ibara ya rasimu ya pili ya Katiba zilizoondolewa bado zilitakiwa kuendelea kuwepo kama ibara inavyosema kwamba Tume ya Utumishi wa umma ndio kitakuwa chombo cha juu kabisa chenye mamlaka ya nidhamu na uratibu wa mambo yote kuhusu utumishi wa umma.
Mamlaka makuu ya Tume yameondolewa. Tume ya mabadiliko ya katiba ilipendekeza kuwa Tume ya Utumishi wa umma kiwe chombo cha:
Kumshauri rais
Kuteua watu wa kushika nafasi mbalimbali.
Kupandisha ngazi za mishahara na kudurusu mishahara
Kuajili n.k
Ibara ya 213 ya Katiba inayopendekezwa Haikuwepo
Tume ya Mishahara
213 (1) Kutakuwa na Tume ya Mishahara na maslahi ambayo
itashughulikia mishahara na maslahi ya watumishi wa umma.
(2) Bunge litatunga sheria itakayoweka masharti kuhusu muundo,
majukumu na mambo mengine kuhusu utekelezaji wa Tume ya Mishahara

Ni Ibara mpya katika Katiba inayopendekezwa ambayo haikuwepo katika rasimu ya pili. Kuongeza tume ya mishahara ni kuiongezea serikali gharama za uendeshaji wa tume.
Na pia jambo hili linaweza kuchukuliwa kama ni sehemu ya watawala ya kupeana vyeo na pia hata kutumika kama geiti ya kuoroshea hela za ummna
Jukumu la Mishahala linatakiwe liwe chini ya Tume ya Utumishi wa Umma.
Jambo hili pia litazidi kuleta mkanganyiko katika ulipaji wa mshahala. Kwani kuna Tume ya Utumishi wa Umma. Pia kuna mfuko maalumu wa ulipaji mishahala ya rais, makamu, waziri mkuu etc
Ibara ya 214 ya Katiba inayopendekezwa Haikuwepo Tume ya Kisekta
214. Kutakuwa na Tume mbalimbali za kisekta zitakazoanzishwa kwa mujibu wa sheria zitakazotungwa na Bunge kwa ajili ya usimamizi, uratibu na utoaji wa huduma za jamii.
Ibara mpya katika Katiba inayopendekezwa ambayo haikuwepo katika rasimu ya pili Kuongezwa kwa Ibara hii ni jambo chanya kwani ni tume ambazo zitakuwa zikishughulikia utoaji wa huduma ya jamii, hivyo kutakuwa na uboreshaji wa huduma kwa jamii.
SURA YA 12 Ibara ya 189 ya Rasimu ya Pili na SURA YA 14 Ibara ya 215 ya Katiba inayopendekezwa Ushiriki katika uchaguzi na kura ya maoni

189.-(1) Kila raia wa Jamhuri ya Muungano mwenye umri wa miaka kumi na nane au zaidi mwenye akili timamu ana haki ya kupiga kura na haki ya kuandikishwa na kushiriki kupiga kura katika uchaguzi au kura ya maoni. (2) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (1), mamlaka ya kusimamia uchaguzi itazingatia misingi kwamba: (a) wananchi wanatumia haki ya kisiasa kwa mujibu wa Katiba hii; (b) watu wenye ulemavu wanapewa fursa za uwakilishi; (c) kunakuwa na haki ya kila raia kupiga kura moja kufuatana na utashi wa uwakilishi na kura sawa; na
(d) uchaguzi unakuwa huru na wa haki ambao – (i) ni wa kura ya siri; (ii) hauna matumizi ya nguvu, vitisho, vishawishi wala rushwa; (iii) hauna matamshi au vitendo vinavyoashiria ukabila,ukanda, udini, dharau na kashfa kwa jinsi au unyanyapaa kwa walemavu au makundi madogo katika jamii; (iv) unaendeshwa na kusimamiwa na chombo huru; na (v) unaendeshwa bila upendeleo au kuegemea upande wowote, ulio makini na unaoonyesha uwajibikaji wa watendaji. (3) Katika kutekeleza masharti ya ibara ndogo ya (1) na (2),mamlaka ya nchi itaweka utaratibu wa sheria utakaowezesha: (a) mamlaka zinazosimamia uchaguzi kutangaza majimbo kwa madhumuni ya uchaguzi wa wabunge; (b) uteuzi wa wagombea;
(c) uandikishaji wa wapiga kura; (d) kuendesha na kusimamia uchaguzi na kura ya maoni; (e) kuweka utaratibu wa kuandikisha raia wa Jamhuri ya Muungano wanaoishi nje kuweza kupiga kura katika uchaguzi au kura ya maoni; na (f) utaratibu wa kufanya uchaguzi kuwa mwepesi, wazi na unaozingatia mahitaji ya watu wenye mahitaji maalum.
(4) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (2) na kwa kuzingatia masharti kuhusu kupinga matokeo ya uchaguzi wa Rais, kila mpiga kura ana haki ya kufungua shauri Mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi, anayoamini yamekiuka masharti ya Katiba hii au sheria za nchi.

215.-(1) Kila raia wa Jamhuri ya Muungano mwenye umri wa miaka
kumi na nane au zaidi na mwenye akili timamu ana haki ya kupiga kura na
haki ya kuandikishwa na kushiriki kupiga kura katika uchaguzi au kura
ya maoni.
(2) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (1), mamlaka ya
kusimamia uchaguzi itazingatia misingi kwamba:
(a) wananchi wanatumia haki ya kisiasa kwa mujibu wa Katiba
hii;
(b) watu wenye ulemavu wanapewa fursa za uwakilishi;
(c) kunakuwa na haki ya kila raia kupiga kura kufuatana na utashi wa
uwakilishi na kura sawa; na
(d) uchaguzi unakuwa huru na wa haki ambao-
(i) ni wa kura ya siri;
(ii) hauna matumizi ya nguvu, vitisho, vishawishi wala rushwa;
(iii) hauna matamshi au vitendo vinavyoashiria ukabila, ukanda,
udini, dharau na kashfa kwa jinsi au unyanyapaa kwa
watu wenye ulemavu au makundi madogo katika jamii;
(iv) unaendeshwa na kusimamiwa na chombo huru; na
(v) unaendeshwa bila upendeleo au kuegemea upande wowote,
ulio makini na unaoonyesha uwajibikaji wa watendaji.
(3) Katika kutekeleza masharti ya ibara ndogo ya (1) na (2), mamlaka
ya nchi itaweka utaratibu utakaowezesha:
(a) mamlaka zinazosimamia uchaguzi kutangaza majimbo kwa
madhumuni ya uchaguzi wa wabunge;
(b) uteuzi wa wagombea;
(c) uandikishaji wa wapiga kura;
(d) kuendesha na kusimamia uchaguzi na kura ya maoni; na
(e) utaratibu wa kufanya uchaguzi kuwa mwepesi, wazi na
unaozingatia mahitaji ya watu wenye mahitaji maalum.
(4) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (2) na kwa kuzingatia masharti
kuhusu kupinga matokeo ya uchaguzi wa Rais, mgombea urais ana haki ya
kufungua shauri mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi, anayoamini yamekiuka masharti ya Katiba hii au sheria.
(5) Bunge litatunga sheria itakayoweka masharti kuhusu utekelezaji wa
masharti ya Ibara hii.
Katiba inayopendekeza imefuta Ibara ya 2 (3) (e) Kuweka utaratibu wa kuandikisha raia wa Jamhuri ya muungano wanaoishi nje kuweza kupiga kura katika uchaguzi au kura ya maoni

Rasimu iliyopendekezwa imeongeza fasili ya 5 Bunge litatunga sheria itakayoweka masharti kuhusu utekelezaji wa masharti ya ibara hii. Watanzania walio nje ya nchi wamenyimwa haki ya kupiga kura na kushiriki katika kura ya maoni.
Ibara ya 216 ya Katiba inayopendekezwa Katika Rasimu ya pili ya Katiba mgombea huru ilikuwepo kwenye sifa za mgombea Urais Ibara ya 79(1)(f) na Sifa za Mgombea Ubunge Ibara ya 125 (1) (c) Mgombea Huru
216.-(1) Bila kuathiri masharti ya Ibara ya 88 na Ibara ya 140, mtu atakuwa na haki ya kuwa mgombea huru katika uchaguzi unaosimamiwa na Tume Huru ya Uchaguzi.
(2) Bunge litatunga sheria itakayoweka masharti kwa mgombea huru kuhusu-

(a) idadi ya wapiga kura wanaohitajika kumdhamini kwa ngazi ya nafasi anayogombea;

(b) kipindi ambacho amekoma kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa kabla ya siku ya uchaguzi;

(c) kutojiunga na chama cha siasa katika kipindi ambacho atakuwa kiongozi baada ya kuchaguliwa;

d) utaratibu wa kuainisha vyanzo vya ndani na nje vya mapato ya kugharamia kampeni za uchaguzi;

(e) utaratibu wa kuainisha vigezo na sifa zitakazotumiwa kuwapata viongozi wa ngazi za juu kitaifa;

(f) kuweka wazi ilani ya uchaguzi inayoonesha mipango ya uendeshaji wa nchi;
(g) kuweka masharti yanayozuia sera zenye mrengo wa kuligawa Taifa; na

(h) masharti mengine kwa kadri itakavyoonekana inafaa.

Ibara hii ni mpya
Katika Katiba inayopendekezwa Mgombea huru imewekewa Ibara inayojitegemea tofauti na kwenye rasimu ya pili ya Katiba ambapo ilikuwepo katika Ibara ndogo za sifa ya mgombea urais na ubunge. Imeweka masharti magumu na inaweza ikatungiwa sheria ngumu na Bunge, ni haki inayoweza kushindwa kutekelezeka, inamnyima haki ya mtu kuwa mwanachama wa chama cha siasa.
Ni sawa na mtu kukung’oa meno kwa ahadi kuwa atakupikia mtoli wa kutosha. Kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba mgomea huru iolikuwa ni moja wapo ya vigezo vya mtu mwenye sifa kugombea.
Mgombea huru amewekewa masharti magumu sana. Hii inaweza kutafsiriwa kama ni geresha tu.
Mgombea huru ni haki isiyotekelezeka. Amewekewa pingamizi kuhusu kukihama chama. Ni haki anayopewa mtu mkono wa kushoto na kupokonywa mkono wa kulia.
Ibara ya 190 ya Rasimu ya pili na Ibara ya 217 ya Katiba inayopendekezwa Kuundwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi

190.-(1) Kutakuwa na Tume Huru ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano itakayoitwa “Tume Huru ya Uchaguzi”. (2) Tume Huru ya Uchaguzi itakuwa na Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wengine saba watakaoteuliwa na Rais baada ya kupendekezwa na Kamati ya Uteuzi.
(3) Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi watashika madaraka mara baada ya kuthibitishwa na Bunge.
(4) Uteuzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi utafanywa kwa misingi kwamba, endapo Mwenyekiti atateuliwa kutoka upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano, basi Makamu Mwenyekiti atateuliwa kutoka upande wa pili wa Jamhuri ya Muungano. (5) Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi watakuwa na sifa zifuatazo: (a) awe ni raia wa kuzaliwa na angalau mmoja kati ya wazazi wake ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano; (b) awe ni mtu aliyewahi kushika nafasi ya madaraka ya Jaji wa Mahakama ya Juu, Mahakama ya Rufani au Mahakama Kuu na ameshika nafasi ya madaraka hayo kwa kipindi kisichopungua miaka mitano; (c) awe ni mwaminifu, mwadilifu na mwenye mwenendo usiotiliwa shaka na jamii; (d) awe ni mtu ambaye, hajawahi kushika nafasi ya madaraka katika chama cha siasa; na (e) awe ni mtu ambaye hajawahi kutiwa hatiani kwa kosa lolote la jinai linalohusiana na uaminifu. (6) Mjumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi atakuwa na sifa zifuatazo: (a) awe ni raia wa kuzaliwa na angalau mmoja kati ya wazazi wake ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano;

(b) awe ni mtu mwaminifu, mwadilifu, na mwenye mwenendo usiotiliwa shaka na jamii; (c) awe ni mtu ambaye hajawahi kushika nafasi ya madaraka yoyote katika chama cha siasa; (d) awe na shahada ya chuo cha elimu ya juu kinachotambuliwa kwa mujibu wa sheria za nchi; na (e) awe ni mtu ambaye hajawahi kutiwa hatiani kwa kosa lolote la jinai linalohusu kukosa uaminifu. (7) Kwa madhumuni ya Ibara hii, watu wafuatao hawatakuwa na sifa ya kuwa Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi: (a) Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Mbunge wa Bunge la Tanganyika, Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi au Diwani katika Serikali ya Tanganyika au Zanzibar; au (b) mtu ambaye ni mtumishi wa umma. (8) Uteuzi wa Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi utazingatia uwakilishi wa kila upande wa Jamhuri ya Muungano.
217(1) Kutakuwa na Tume Huru ya U chaguzi ya Jamhuri ya
Muungano itakayoitwa “Tume Huru ya Uchaguzi”.
(2) Tume Huru ya Uchaguzi itakuwa na Mwenyekiti, Makamu
Mwenyekiti na wajumbe wengine saba watakaoteuliwa na Rais baada ya
kupendekezwa na Kamati ya Uteuzi.
(3) Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wa Tume Huru ya
Uchaguzi watashika madaraka mara baada ya kuapishwa na Rais.
(4) Uteuzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya
Uchaguzi utafanywa kwa misingi kwamba, endapo Mwenyekiti atateuliwa kutoka
upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano, basi Makamu Mwenyekiti atateuliwa
kutoka upande wa pili wa Jamhuri ya Muungano.
(5) Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi
watakuwa na sifa zifuatazo:
(a) awe ni raia wa kuzaliwa, na angalau mmoja kati ya wazazi wake ni
raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano;
(b) awe ni mtu aliyewahi kushika nafasi ya madaraka ya Jaji wa
Mahakama ya Juu, Mahakama ya Rufani au Mahakama Kuu na
ameshika nafasi ya madaraka hayo kwa kipindi kisichopungua miaka
mitano;
(c) awe ni mwaminifu, mwadilifu na mwenye mwenendo usiotiliwa
shaka na jamii;
(d) awe ni mtu ambaye hajawahi kushika nafasi ya madaraka ya juu
katika chama cha siasa; na
(e) awe ni mtu ambaye hajawahi kutiwa hatiani kwa kosa lolote la jinai.
(6) Mjumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi atakuwa na sifa zifuatazo:
(a) awe ni raia wa kuzaliwa na angalau mmoja kati ya wazazi wake ni
raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano;
(b) awe ni mtu mwaminifu, mwadilifu, na mwenye mwenendo usiotiliwa
shaka na jamii;
(c) awe ni mtu ambaye hajawahi kushika nafasi ya madaraka ya juu
katika chama cha siasa;
(d) awe na shahada ya chuo cha elimu ya juu kinachotambuliwa kwa
mujibu wa sheria; na
(e) awe ni mtu ambaye hajawahi kutiwa hatiani kwa kosa lolote la jinai.
(7) Kwa madhumuni ya Ibara hii, watu wafuatao hawatakuwa na sifa ya
kuwa Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi:
(a) Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Mjumbe wa Baraza

la Wawakilishi au Diwani; au
(b) mtu ambaye ni mtumishi wa umma.
(8) Uteuzi wa Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi utazingatia Ibara ndogo ya tatu ya Katiba inayopendekezwa ambayo inasema Mwenyekiti, Makamu mwenyekiti na wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi watashika madaraka mara baada ya kuapishwa na rais.
Madaraka ya bunge kuithibitisha Uteuzi wa Mwenyekiti, Makamu mwenyekiti na wajumbe wa Tume huru ya uchaguzi yameondolewa. Kifungu hicho kimepunguza madaraka ya wananchi na kuongeza madaraka ya Raisi.
Hapa kinachoonekana ni jina Tume Huru ya Uchaguzi na si mengineyo. Hii ni kwa sababu:
– Haiwezi kuwa Tume Huru wakati watendaji kazi wake wakuu ni watu wanaoteuliwa na rais, hata pasipokuidhinishwa na Bunge.
– Haiwezi kuwa tume huru wakati pesa zake inategemea serikali moja kwa moja.
– Haiwezi kuwa Huru wakati watendaji wake wanawajibika kwa rais wa nchi
Ibara hii imeendelea kumfanya rais awe ni zaidi ya Mungu mtu kwani kila kitu ni yeye na habanwi katka maamuzi yake.
Ibara a 191 ya Rasimu a pili a 218 ya Katiba inayopendekezwa Kamati ya Uteuzi.
191.-(1) Kutakuwa na Kamati ya Uteuzi wa Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi itakayokuwa na wajumbe wafuatao: (a) Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ambaye atakuwa ni Mwenyekiti; (b) Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ambaye atakuwa Makamu Mwenyekiti; (c) Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar; (d) Spika wa Bunge la Tanganyika; (e) Jaji Mkuu wa Tanganyika; (f) Jaji Mkuu wa Zanzibar; na (g) Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji. (2) Mkurugenzi wa Tume Huru ya Uchaguzi atakuwa Katibu wa Kamati ya Uteuzi. (3) Kamati ya Uteuzi itakuwa na jukumu la kupokea na kuchambua majina ya watu walioomba na waliopendekezwa kuwa wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi kwa mujibu wa utaratibu utakaoainishwa na sheria za nchi. (4) Kwa kuzingatia masharti ya ibara ndogo ya (3), Kamati ya Uteuzi mara baada ya kuchambua majina ya watu walioomba na waliopendekezwa kuwa wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi,itapendekeza kwa Rais majina ya watu wanaofaa kuteuliwa kuwa wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi. (5) Rais atateua Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi kutoka miongoni mwa majina yaliyowasilishwa na Kamati ya Uteuzi na atawasilisha majina hayo Bungeni kwa ajili ya kuthibitishwa na Bunge. (6) Kwa madhumuni ya Ibara hii, asasi za kiraia na zisizo za kiserikali zinaweza kupendekeza majina ya watu wanaoweza kuteuliwa kuwa Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi.
(7) Bunge litatunga Sheria ambayo pamoja na mambo mengine
itaweka masharti kuhusu kiapo cha Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti
na Wajumbe wengine wa Tume Huru ya Uchaguzi. 218.-(1) Kutakuwa na Kamati ya Uteuzi wa Mwenyekiti, Makamu
Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi itakayokuwa na Wajumbe
wafuatao:
(a) Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ambaye atakuwa ni Mwenyekiti;
(b) Jaji Mkuu wa Zanzibar ambaye atakuwa Makamu Mwenyekiti;
(c) Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano;
(d) Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar;
(e) Jaji Kiongozi; na
(f) Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
(2) Mkurugenzi wa Tume Huru ya Uchaguzi atakuwa Katibu wa Kamati
ya Uteuzi.
(3) Kamati ya Uteuzi itakuwa na jukumu la kupokea na kuchambua majina
ya watu walioomba kuwa Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi kwa mujibu wa
utaratibu utakaoainishwa na sheria.
(4) Kwa kuzingatia masharti ya ibara ndogo ya (3), Kamati ya Uteuzi mara
baada ya kuchambua majina ya watu walioomba kuwa Wajumbe wa Tume Huru
ya Uchaguzi, itapendekeza kwa Rais majina ya watu wanaofaa kuteuliwa kuwa
wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi.
(5) Rais atateua Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume
Huru ya Uchaguzi kutoka miongoni mwa majina yaliyowasilishwa na Kamati ya
Uteuzi.
(6) Bunge litatunga sheria ambayo pamoja na mambo mengine itaweka
masharti kuhusu kiapo cha Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe
wengine wa Tume Huru ya Uchaguzi.
-Jaji Mkuu wa Zanzibar kuwa makamu mwenyekiti badala ya spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano
-Spika wa bunge la Tanganyika
-Jaji Mkuu wa Tanganyika
– Mwenyekiti na makamu mwenyekiti wa wajumbe wa Tume huru ya uchaguzi kuthibitishwa na bunge imeondolewa katika katiba inayopendekezwa.
– Asasi za Kiraia na zisizo za Kiserikali zinaweza kupendekeza majina ya watu wanaoweza kuteuliwa kuwa mwenyekiti, makamu mwenyekiti na wajumbe wa tume huru ya uchaguzi pia imeondolewa katika katiba inayopendekezwa.
Asasi za kiraia zimenyimwa madaraka kushiriki katika kupendekeza majina ya mwenyekiti a makamu mwenyekiti a wajumbe wa tume.

Rais ameongezewa madaraka na bunge kupunguziwa madaraka.
Wametoa neon Maadili. Ifahamike kuwa mmomonyoko wa maadili katika jamii yetu, serikalini n.k umeshuka sana na hicho ndicho kilichokuwa kilioac ha watu wengi. Hivyo kuondoa misingi ya maadili ni kutokuwatendea haki Watanzania
Ibara ya 192 ya Rasimu ya pili na Ibara ya 219 ya Katiba inayopendekezwa Ukomo wa kushika nafasi ya madaraka yaTume Huru ya Uchaguzi.
192.-(1) Mjumbe wa Tume atashika nafasi ya madaraka kwa
kipindi cha miaka mitano na anaweza kuteuliwa tena kwa kipindi kingine kimoja cha miaka mitano.
(2) Mtu atakoma kuwa mjumbe wa Tume endapo litatokea tukio lolote kati ya matukio yafuatayo: (a) kujiuzulu; (b) kutokuwa na uwezo wa kutekeleza majukumu yake kwa sababu ya maradhi; (c) kuondolewa kwa makosa ya kukiuka Kanuni za Maadili ya Uongozi wa Umma; (d) kutiwa hatiani kwa kosa ambalo adhabu yake ni kifungo gerezani kwa muda unaozidi siku saba; (e) kupoteza sifa ya kuteuliwa kuwa mjumbe; au (f) kufariki dunia.
(3) Kwa madhumuni ya utekelezaji bora wa majukumu ya Tume,
kutakuwa na kanuni za maadili kama zitakavyoainishwa na sheria za
nchi.
(4) Mjumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi ambaye atakiuka
masharti ya kanuni za maadili atapoteza sifa za kuendelea kuwa mjumbe.
(5) Endapo suala la kumuondoa Mjumbe wa Tume Huru ya
Uchaguzi kwa kukiuka kanuni za maadili litajitokeza, Rais atateua
Kamati itakayoundwa na:
(a) Jaji wa Mahakama ya Rufani ambaye atakuwa Mwenyekiti;
(b) Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu;
(c) Mjumbe wa Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji; na
(d) Mawakili, mmoja kutoka Tanganyika na mmoja kutoka
Zanzibar watakaopendekezwa na Chama cha Wanasheria
Tanganyika na Chama cha Wanasheria Zanzibar,
na Kamati hiyo itafanya uchunguzi wa suala hilo na kisha kutoa mapendekezo kwa Rais.
(6) Endapo, baada ya uchunguzi, Kamati itapendekeza kuwa
mjumbe huyo aondolewe madarakani, Rais atamuondoa mjumbe huyo
madarakani na endapo Kamati itapendekeza kuwa mjumbe huyo
asiondolewe, suala la kumuondoa mjumbe huyo litakoma.
(7) Kamati itaweka utaratibu wa kufanya uchunguzi.
219 (1)Tume Huru ya Uchaguzi itakuwa na wajibu wa:
(a) kusimamia na kuendesha shughuli zote za uchaguzi wa Rais na
Wabunge katika Jamhuri ya Muungano;
(b) kusimamia na kuendesha kura ya maoni;
(c) kusimamia na kuratibu uandikishaji wa wapiga kura katika Jamhuri
ya Muungano;
(d) kugawa na kutangaza majimbo ya uchaguzi wa Wabunge wa Bunge
la Jamhuri ya Muungano; na
(e) kutangaza matokeo ya uchaguzi wa Rais na Wabunge, au matokeo ya
kura ya maoni.
(2) Tume Huru ya Uchaguzi itakuwa na wajibu wa kutoa elimu ya mpiga
kura wakati wa uchaguzi au kura ya maoni na kuratibu utoaji wa elimu ya uraia
kuhusu uchaguzi, au kura ya maoni na kusimamia asasi za kiraia, taasisi, jumuiya
au makundi ya watu yatakayotoa elimu hiyo.
(3) Tume Huru ya Uchaguzi pia ina wajibu wa kuhakikisha kuwepo kwa:
(a) uhuru wa wananchi katika kutumia haki ya uchaguzi na kuchaguliwa
kupitia vyama vya siasa au mgombea huru;
(b) uzingatiaji wa misingi ya upigaji kura wa mtu mmoja kura moja; na
(c) uchaguzi huru na wa haki.
(4) Tume Huru ya Uchaguzi inaweza kutekeleza shughuli zake bila kujali
kwamba kuna nafasi ya madaraka ya mjumbe iliyo wazi miongoni mwa wajumbe
au kwamba Mjumbe yeyote hayupo, lakini kila uamuzi wa Tume Huru ya
Uchaguzi ni lazima uungwe mkono na wajumbe walio wengi kati ya idadi ya
Wajumbe wote wa Tume Huru ya Uchaguzi.
(5) Katika kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba
hii, Tume Huru ya Uchaguzi haitalazimika kufuata amri, maagizo au maoni ya
mtu yeyote, mamlaka yoyote ya Serikali, chama cha siasa, taasisi au asasi yoyote.
(6) Katika utekelezaji wa madaraka yake kwa mujibu wa Katiba hii, Tume
Huru ya Uchaguzi itashauriana mara kwa mara na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar.
(7) Itakuwa ni marufuku kwa watu wanaohusika na uchaguzi kujiunga na
chama chochote cha siasa, isipokuwa tu kwamba kila mmoja wao atakuwa na haki
79
ya kupiga kura katika uchaguzi au kura ya maoni.
(8) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (7), watu wanaohusika na uchaguzi
au kura ya maoni ni:
(a) Mwenyekiti wa Tume;
(b) Makamu Mwenyekiti wa Tume;
(c) Wajumbe wote wa Tume;
(d) Mkurugenzi wa Uchaguzi pamoja na watumishi wote wa Tume; na
(e) wasimamizi wote wa uchaguzi.
Ibara ndogo ya 4 ya rasimu ya pili imeondolewa ambayo inasema, Mjumbe wa tume huru ya uchaguzi ambaye atakikua masharti ya kanuni za maadili atapoteza sifa za kuendelea kuwa mjumbe. Kuifuta ibara ndogo hiyo kumetoa mwanya kwa wajumbe kukiuka kanuni.
Ibara ya 193 ya rasimu ya pili na Ibara ya 220 ya Katiba iliyopendekezwa Wajibu wa Tume Huru ya Uchaguzi.
193.-(1) Tume Huru ya Uchaguzi itakuwa na wajibu wa:
(a) kusimamia na kuendesha shughuli zote za uchaguzi wa
Wabunge na Rais katika Jamhuri ya Muungano;
(b) kusimamia na kuendesha kura ya maoni;
(c) kusimamia na kuratibu uandikishaji wa wapiga kura katika
Jamhuri ya Muungano; na
(d) kugawa na kutangaza majimbo ya uchaguzi wa Wabunge wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano.
(2) Tume Huru ya Uchaguzi itakuwa pia na wajibu wa kutoa
elimu ya mpiga kura wakati wa uchaguzi au kura ya maoni na kuratibu
utoaji wa elimu ya uraia kuhusu uchaguzi na kusimamia asasi za kiraia,
taasisi, jumuiya au makundi ya watu yatakaotoa elimu hiyo.
-(3) Tume Huru ya Uchaguzi pia ina wajibu wa kuhakikisha
kuwepo kwa:
(a) uhuru wa wananchi katika kutumia haki ya uchaguzi na
kuchaguliwa kupitia vyama vya siasa au mgombea huru;
(b) uwakilishi unaozingatia jinsi;
(c) uwakilishi wa watu wenye ulemavu au mahitaji maalum
katika jamii;
(d) uzingatiaji wa misingi ya upigaji kura wa mtu mmoja kura
moja kwa kuzingatia uwakilishi wenye usawa; na
(e) uchaguzi huru na wa haki.
(4) Tume Huru ya Uchaguzi inaweza kutekeleza shughuli zake
bila kujali kwamba kuna nafasi ya madaraka ya mjumbe iliyo wazi
miongoni mwa wajumbe au kwamba Mjumbe yeyote hayupo, lakini kila
uamuzi wa Tume Huru ya Uchaguzi ni lazima uungwe mkono na
wajumbe walio wengi kati ya idadi ya Wajumbe wote wa Tume Huru ya
Uchaguzi.
(5) Katika kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya
Katiba hii, Tume Huru ya Uchaguzi haitalazimika kufuata amri, maagizo
au maoni ya mtu yeyote, mamlaka yoyote ya Serikali, chama cha siasa,
taasisi au asasi yoyote.
(6) Katika utekelezaji wa madaraka yake kwa mujibu wa Katiba
hii, Tume Huru ya Uchaguzi itashauriana mara kwa mara na Tume ya
Uchaguzi ya Tanganyika na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar.
(7) Itakuwa ni marufuku kwa watu wanaohusika na uchaguzi
kujiunga na chama chochote cha siasa, isipokuwa tu kwamba kila mmoja
wao atakuwa na haki ya kupiga kura katika uchaguzi au kura ya maoni.
(8) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (7), watu wanaohusika na
uchaguzi au kura ya maoni ni –
(a) Mwenyekiti wa Tume;
(b) Makamu Mwenyekiti wa Tume;
(c) Wajumbe wote wa Tume;
(d) Mkurugenzi wa Uchaguzi pamoja na watumishi wote wa
Tume; na
(e) wasimamizi wote wa uchaguzi.
220.-(1) Tume Huru ya Uchaguzi itakuwa na wajibu wa:
(a) kusimamia na kuendesha shughuli zote za uchaguzi wa Rais na
Wabunge katika Jamhuri ya Muungano;
(b) kusimamia na kuendesha kura ya maoni;
(c) kusimamia na kuratibu uandikishaji wa wapiga kura katika Jamhuri
ya Muungano;
(d) kugawa na kutangaza majimbo ya uchaguzi wa Wabunge wa Bunge
la Jamhuri ya Muungano; na
(e) kutangaza matokeo ya uchaguzi wa Rais na Wabunge, au matokeo ya
kura ya maoni.
(2) Tume Huru ya Uchaguzi itakuwa na wajibu wa kutoa elimu ya mpiga
kura wakati wa uchaguzi au kura ya maoni na kuratibu utoaji wa elimu ya uraia
kuhusu uchaguzi, au kura ya maoni na kusimamia asasi za kiraia, taasisi, jumuiya
au makundi ya watu yatakayotoa elimu hiyo.
(3) Tume Huru ya Uchaguzi pia ina wajibu wa kuhakikisha kuwepo kwa:
(a) uhuru wa wananchi katika kutumia haki ya uchaguzi na kuchaguliwa
kupitia vyama vya siasa au mgombea huru;
(b) uzingatiaji wa misingi ya upigaji kura wa mtu mmoja kura moja; na
(c) uchaguzi huru na wa haki.
(4) Tume Huru ya Uchaguzi inaweza kutekeleza shughuli zake bila kujali
kwamba kuna nafasi ya madaraka ya mjumbe iliyo wazi miongoni mwa wajumbe
au kwamba Mjumbe yeyote hayupo, lakini kila uamuzi wa Tume Huru ya
Uchaguzi ni lazima uungwe mkono na wajumbe walio wengi kati ya idadi ya
Wajumbe wote wa Tume Huru ya Uchaguzi.
(5) Katika kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba
hii, Tume Huru ya Uchaguzi haitalazimika kufuata amri, maagizo au maoni ya
mtu yeyote, mamlaka yoyote ya Serikali, chama cha siasa, taasisi au asasi yoyote.
(6) Katika kugawa majimbo ya uchaguzi kwa mujibu wa Ibara hii, Tume Huru ya Uchaguzi itazingatia:

(a) idadi ya watu katika eneo husika;

(b) upatikanaji wa njia za mawasiliano katika eneo linalokusudiwa;

(c) mipaka ya kiutawala; na

(d) maeneo ya kijiografia katika eneo husika.

(7) Masharti mengine kuhusu mgawanyo wa Jamhuri ya Muungano katika majimbo wa uchaguzi yatakuwa kama yatakavyofafanuliwa katika sheria itakayotungwa na Bunge.

(8) Katika utekelezaji wa madaraka yake kwa mujibu wa Katiba hii, Tume
Huru ya Uchaguzi itashauriana mara kwa mara na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar.
(9) Itakuwa ni marufuku kwa watu wanaohusika na uchaguzi kujiunga na
chama chochote cha siasa, isipokuwa tu kwamba kila mmoja wao atakuwa na haki
79
ya kupiga kura katika uchaguzi au kura ya maoni.
(10) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (7), watu wanaohusika na uchaguzi
au kura ya maoni ni:
(a) Mwenyekiti wa Tume;
(b) Makamu Mwenyekiti wa Tume;
(c) Wajumbe wote wa Tume;
(d) Mkurugenzi wa Uchaguzi pamoja na watumishi wote wa Tume; na
(e) wasimamizi wote wa uchaguzi.
Katiba inayopendekezwa imeongeza imeongeza ibara ndogo ya 1 (e) Tume huru ya uchaguzi itakuwa na wajibu wa kutangaza matokeo ya uraisi na ubunge au matokeo ya kura za maoni

Katiba inayopendekezwa imeondoa ibara ndogo ya 3(b) uwakilishi unaozingatia jinsi; na
(c) uwakilishi wa watu wenye ulemavu au mahitaji maalum katika jamii;

Nafasi za uwakilishi wa watu wenye ulemavu au mahitaji maalum katika jamii na uwakilishi unaozingatia jinsi zimeminywa na Katiba inayopendekezwa

Uwakili wa jinsi umeondolewa, na hihi ni kutaka kubana haki na usawa.

Uwakilishi wa watu wenye ulemavu umebanwa, Kama ni Tume huru ya taifa ya Uchaguzi kwanini isiendelee kusimamia uchaguzi mpaka ngazi ya wilaya na mikoa?
Ibara ya 194 ya rasimu ya pili na 221 ya Katiba inayopendekezwa Malalamiko kuhusu uchaguzi. 194.-(1) Tume Huru ya Uchaguzi itasimamia na kutatua mapema
iwezekanavyo malalamiko yanayohusu kuteuliwa kwa mgombea katika
uchaguzi.
(2) Kesi za malalamiko kuhusu uchaguzi wa Wabunge
zitafunguliwa Mahakama Kuu mapema iwezekanavyo baada ya Tume
Huru ya Uchaguzi kutangaza matokeo na kwa vyovyote vile si zaidi ya
muda ulioainishwa katika sheria za nchi.
(b) Mkurugenzi wa Uchaguzi
221 .-(1) Tume Huru ya Uchaguzi itasimamia na kutatua mapema
iwezekanavyo malalamiko yanayohusu kuteuliwa kwa mgombea katika uchaguzi.
(2) Kesi za malalamiko kuhusu uchaguzi wa Wabunge zitafunguliwa
Mahakama Kuu mapema iwezekanavyo baada ya Tume Huru ya Uchaguzi
kutangaza matokeo na kwa vyovyote vile si zaidi ya muda ulioainishwa katika
sheria za nchi.
Haijabadilika Haijabadilika
Ibara ya 195 ya rasimu ya pili na 222 ya Katiba inayopendekezwa Uteuzi wa Mkurugenzi wa Uchaguzi.
195.-(1) Kutakuwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi atakayeteuliwa na Rais baada ya kupendekezwa na Tume ya Utumishi wa Umma na kuthibitishwa na Bunge.
– 76 -(2) Mkurugenzi wa Uchaguzi atakuwa na sifa zifuatazo:
(a) awe ni raia wa kuzaliwa na angalau mmoja kati ya wazazi
wake ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano;
(b) awe ni mtu mwaminifu, mwadilifu, na mwenye mwenendo
usiotiliwa shaka na jamii;
(c) awe ni mtu ambaye hajawahi kushika nafasi ya madaraka
yoyote katika chama cha kisiasa;
(d) awe na shahada ya chuo cha elimu ya juu kinachotambuliwa
kwa mujibu wa sheria za nchi; na
(e) awe ni mtu ambaye hajawahi kutiwa hatiani kwa kosa lolote
la jinai linalohusu kukosa uaminifu.

222.-(1) Kutakuwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi atakayeteuliwa na Rais
(2) Mkurugenzi wa Uchaguzi atakuwa na sifa zifuatazo:
(a) awe ni raia wa kuzaliwa na angalau mmoja kati ya wazazi wake ni
raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano;
(b) awe ni mtu mwaminifu, mwadilifu, na mwenye mwenendo
usiotiliwa shaka na jamii;
(c) awe ni mtu ambaye hajawahi kushika nafasi ya madaraka ya juu
katika chama cha siasa;
(d) awe na shahada ya chuo cha elimu ya juu kinachotambuliwa kwa
mujibu wa sheria; na
(e) awe ni mtu ambaye hajawahi kutiwa hatiani kwa kosa lolote la jinai. Katiba inayopendekezwa imeondoa kuthibitishwa na bunge kwa mkurugenzi wa uchaguzi
Sifa za mkurugenzi wa uchaguzi zimebadilika kwa kuondoa awe ni mtu ambaye hajawahi kutiwa hatiani kwa kosa lolote la jinai linalohusu kukosa uaminifu Madaraka ya Rais yameongezwa na kupunguza madaraka ya bunge.

Hii inaweza kupelekea mtu asiye mwaminifu kupewa madaraka hayo.

Ibara ya 196 ya Rasimu ya pili na ibara ya 223 ya rasimu iliyopedekezwa Majukumu ya Mkurugenzi wa Uchaguzi.
196.-(1) Mkurugenzi wa Uchaguzi atakuwa ndiye msimamizi na mtekelezaji mkuu wa majukumu ya kila siku ya Tume Huru ya Uchaguzi kuhusiana na masuala ya uchaguzi, uandikishaji wa wapiga kura na uendeshaji wa kura ya maoni.
(2) Mkurugenzi wa Uchaguzi atatekeleza majukumu yake kwakufuata utaratibu ulioainishwa na sheria za nchi kuhusu masuala ya uchaguzi na kura ya maoni.
(3) Mkurugenzi wa Uchaguzi atatekeleza majukumu yake kwa kusaidiwa na watendaji ambao ni watumishi wa umma kwa kadri ya idadi inayohitajika.
(4) Katika kutekeleza majukumu yake, Mkurugenzi wa Uchaguzi atawajibika kwa Tume Huru ya Uchaguzi.
.223-(1) Mkurugenzi wa Uchaguzi atakuwa ndiye msimamizi na
mtekelezaji mkuu wa majukumu ya kila siku ya Tume Huru ya Uchaguzi
kuhusiana na masuala ya uchaguzi, uandikishaji wa wapiga kura na uendeshaji wa
kura ya maoni.
(2) Mkurugenzi wa Uchaguzi atatekeleza majukumu yake kwa kufuata
utaratibu utakaoainishwa na sheria kuhusu masuala ya uchaguzi na kura ya maoni.
(3) Mkurugenzi wa Uchaguzi atatekeleza majukumu yake kwa kusaidiwa
na watendaji ambao ni watumishi wa umma kwa kadri itakavyohitajika.
(4) Katika kutekeleza majukumu yake, Mkurugenzi wa Uchaguzi
atawajibika kwa Tume Huru ya Uchaguzi. Haijabadilika Haijabadilika
Ibara ya 197 ya rasimu ya pili na ibara ya 224 a Katiba inayopedekezwa Usajili wa vyama vya siasa.
197.-(1) Chama cha siasa kinaweza kufanya shughuli za siasa endapo kitasajiliwa kwa mujibu wa sheria za nchi.
(2) Haitakuwa halali kwa chama chochote cha siasa kusajiliwa ambacho kutokana na Katiba au sera yake –
(a) kinakusudia kukuza au kupigania maslahi ya –
(i) imani au kundi lolote la dini;
(ii) kundi lolote la kikabila, pahala watu watokeapo, rangi au
jinsi;
(iii) eneo fulani tu katika sehemu yoyote ya Jamhuri ya
Muungano;
(b) kinapigania kuvunjwa kwa Jamhuri ya Muungano;
(c) kinakubali au kupigania matumizi ya nguvu au mapambano
kama njia za kufikia malengo yake ya kisiasa;
(d) kinapigania au kinakusudia kuendesha shughuli zake za
kisiasa katika sehemu moja tu ya Jamhuri ya Muungano; au
(e) hakiruhusu uongozi wake kuchaguliwa kwa vipindi na kwa
njia za kidemokrasia.
– 77 -(3) Bila ya kuathiri sheria za nchi zinazohusika ni marufuku kwa
mtu yeyote kulazimishwa kujiunga na chama chochote au kwa chama
cha siasa kukataliwa kusajiliwa kwa sababu tu ya itikadi au falsafa.
(4) Bunge linaweza kutunga sheria inayoweka masharti
yatakayohakikisha kuwa vyama vya siasa vinazingatia mipaka na vigezo
vilivyowekwa na masharti ya ibara ndogo ya (2) kuhusu uhuru na haki ya
watu kushirikiana na kujumuika.
(5) Mambo yote yanayohusu uandikishaji na uendeshaji wa
vyama vya siasa nchini yatasimamiwa kwa mujibu wa masharti ya
Katiba hii.
(b) Msajili wa Vyama vya Siasa
224.-(1) Chama cha siasa kinaweza kufanya shughuli za siasa endapo
kitasajiliwa kwa mujibu wa sheria.
(2) Haitakuwa halali kwa chama chochote cha siasa kusajiliwa ambacho
kutokana na katiba au sera yake:
(a) kinakusudia kukuza au kupigania maslahi ya:
(i) imani au kundi lolote la dini;
(ii) kundi lolote la kikabila, mahali watu watokeapo, rangi au jinsi;
(iii) eneo fulani tu katika sehemu yoyote ya Jamhuri ya Muungano;
(b) kinapigania kuvunjwa kwa Jamhuri ya Muungano;
(c) kinakubali au kupigania matumizi ya nguvu au mapambano kama
njia za kufikia malengo yake ya kisiasa;
(d) kinapigania au kinakusudia kuendesha shughuli zake za kisiasa
katika sehemu moja tu ya Jamhuri ya Muungano; au
(e) hakiruhusu uongozi wake kuchaguliwa kwa kuzingatia jinsi, watu
wenye ulemavu na uwakilishi wa pande zote mbili za Muungano
kwa njia za kidemokrasia.
(3) Bila kuathiri sheria zinazohusika ni marufuku kwa mtu yeyote
kulazimishwa kujiunga na chama chochote au kwa chama cha siasa kukataliwa
kusajiliwa kwa sababu tu ya itikadi au falsafa.
(4) Bunge linaweza kutunga sheria kuhusu mipaka na vigezo
vilivyowekwa na masharti ya ibara ndogo ya (2) kuhusu uhuru na haki ya watu
kushirikiana na kujumuika.
(5) Mambo yote yanayohusu uandikishaji na uendeshaji wa vyama vya
siasa nchini yatasimamiwa kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.
Rasimiliyopendekezwa fasili 2(e) imebadilishwa na kusomeka; “hakiruhusu uongozi wake kuchaguliwa kwa kuzingatia jinsi, watu
wenye ulemavu na uwakilishi wa pande zote mbili za Muungano
kwa njia za kidemokrasia”. Na pia imeondoa maneno “kuchaguliwa kwa vipindi na kwa njia za kidemokrasia.”

Demokrasia ya kupokezana uongozi imeminywa kwa kuondoa “kuchaguliwa kwa vipindi na kwa njia za kidemokrasia.”

Ibara ya 198 ya rasimu ya pili ya katiba na 225 ya Katiba iliyopendekezwa Uteuzi wa Msajili wa Vyama vya Siasa. 198.-(1) Kutakuwa na Msajili wa Vyama vya Siasa
atakayeteuliwa na Rais baada ya kupendekezwa na Tume ya Utumishi
wa Umma na kuthibitishwa na Bunge.
(2) Msajili wa Vyama vya Siasa atakuwa na sifa zifuatazo:
(a) awe ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano;
(b) awe ni mtu mwaminifu, mwadilifu na mwenye mwenendo
usiotiliwa shaka na jamii;
(c) awe ni mtu ambaye hajawahi kushika nafasi ya madaraka
yoyote katika chama cha siasa; na
(d) awe na shahada ya chuo cha elimu ya juu kinachotambuliwa kwa mujibu wa sheria za nchi.
225.-(1) Kutakuwa na Msajili wa Vyama vya Siasa atakayeteuliwa na
Rais.
(2) Msajili wa Vyama vya Siasa atakuwa na sifa zifuatazo:
(a) awe ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano;
(b) awe ni mwaminifu, mwadilifu na mwenye mwenendo usiotiliwa shaka
na jamii;
(c) awe ni mtu ambaye hajawahi kushika nafasi ya madaraka ya juu katika
chama cha siasa; na
(d) awe na shahada ya chuo cha elimu ya juu kinachotambuliwa kwa
mujibu wa sheria. Kuthibitishwa na Bunge imeondolewa Imepunguza madaraka ya Umma ya kuthibitisha viongozi wakuu wa kitaifa.
Hapa tunaona Bunge nalo linapokonywa madaraka yake.
Ibara ya 226 ya Katiba inayopendekezwa Haikuwepo Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa 226.-(1) Kutakuwa na Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa atakayeteuliwa
na Rais.
(2) Mtu atateuliwa kuwa Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa endapo ana
sifa zilizotajwa katika Ibara ya 225(2).
(3) Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa atakuwa ndiye msaidizi mkuu wa
Msajili wa Vyama vya Siasa katika kutekeleza majukumu yake.
Katiba inayopendekezwa imeongeza Ibara ya 226 ambayo ni nafasi ya Naibu Msajili wa vyama vya siasa. Kuongeza nafasi hii ya Naibu Msajili wa vyama vya siasa ni kuiongezea serikali gharama.

Ibara ya 199 ya rasimu ya pili ya katiba na ibara ya 227 ya Katiba inayopendekezwa Wajibu wa Msajili wa Vyama vya Siasa.

199.-(1) Msajili wa Vyama vya Siasa atakuwa na wajibu wa:
(a) kusimamia na kuratibu uandikishaji na shughuli za vyama vya siasa kwa mujibu wa masharti ya Katiba na sheria za nchi;
(b) kutayarisha na kuchapisha taarifa za kila mwaka kuhusu ripoti za ukaguzi wa fedha kwa kila chama cha siasa; na
(c) kusimamia fedha za vyama vya siasa.
(2) Msajili wa Vyama vya Siasa atatekeleza majukumu yake kwa kufuata utaratibu ulioainishwa na sheria za nchi.
Wajibu wa Msajili na naibu Msajili wa vyama vya siasa.

227.-(1) Msajili na Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa watakuwa na
wajibu wa:
(a) kusimamia na kuratibu uandikishaji na shughuli za vyama vya siasa
kwa mujibu wa masharti ya Katiba na sheria;
(b) kutayarisha na kuchapisha taarifa za kila mwaka kuhusu ripoti za
ukaguzi wa fedha kwa kila chama cha siasa; na
(c) kusimamia fedha za vyama vya siasa.
(2) Msajili na Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa watatekeleza majukumu
yao kwa mujibu wa Katiba hii na kwa kufuata utaratibu utakaoainishwa na sheria itakayotungwa na Bunge. Katiba iliyopendekezwa imeongeza Msajili na Naibu Msajili wa vya vyama vya siasa kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa katiba hii na kwa kufuata utaratibu utakaoainishwa a sheria itakayotugwa na Bunge. Wajibu wao kama wasajili wa vyama vya siasa ni chanya, hakuna tofauti katika wajibu waliopewa kikatiba katika rasimu ya Katiba na Katiba inayopendekezwa.

SURA YA 15 NA 16
SURA YA 15 &16 (RASIMU YA PILI SURA YA 13 &14)
Ibara 2nd Draft Katiba Inayopendekezwa Tofauti Maoni

Tume ya Maadili
ya Uongozi na Uwajibikaji 200.-(1) Kutakuwa na Tume ambayo itaitwa “Tume ya Maadili ya
Uongozi na uwajibikaji” itakayokuwa na Mwenyekiti na Makamu
Mwenyekiti na wajumbe wengine wasiozidi saba.
(2) Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji watateuliwa na Rais baada ya kupendekezwa na na Kamati Maalum ya Uteuzi.
(3) Uteuzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya utafanywa kwa kuzingatia msingi kwamba endapo Mwenyekiti atateuliwa kutoka upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano, basi Makamu Mwenyekiti atateuliwa kutoka upande wa pili wa Jamhuri ya Muungano.
(4) Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti watashika madaraka baada
ya kuthibitishwa na Bunge.
(5) Sifa za Mwenyekiti wa Tume zitakuwa kama ifuatavyo:
(a) awe ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano
(b) mtu mwenye shahada ya chuo cha elimu ya juu kinachotambulika
kwa mujibu wa sheria;
(c) mtu mwenye uzoefu katika utumishi wa umma kwa kipindi
kisichopungua miaka kumi na tano;
(d) mtu mwenye heshima, weledi, uaminifu, uadilifu na asiye na tabia au
mwenendo wenye kutiliwa shaka na jamii; na
(e) awe ni mtu ambaye hajawahi kutiwa hatiani kwa kosa lolote la
jinai.
(6) Sifa za Makamu Mwenyekiti zitakuwa kama zilivyoainishwa katika ibara ndogo ya (5). 228.-(1) Kutakuwa na Tume ambayo itaitwa “Tume ya Maadili ya
Viongozi wa Umma” itakayokuwa na Mwenyekiti na Makamu
Mwenyekiti na wajumbe wengine wasiozidi saba.
(2) Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya
Viongozi wa Umma watateuliwa na Rais kutoka miongoni mwa majina
yatakayopendekezwa na Kamati ya Uteuzi.
(3) Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti watashika madaraka baada ya kuapishwa na Rais.
(4) Sifa za Mwenyekiti wa Tume zitakuwa kama ifuatavyo:
(a) awe ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano ambaye angalau
mmoja kati ya wazazi wake ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya
Muungano;
(b) mtu mwenye shahada ya chuo cha elimu ya juu kinachotambulika
kwa mujibu wa sheria;
(c) mtu mwenye uzoefu katika utumishi wa umma kwa kipindi
kisichopungua miaka kumi na tano;
(d) mtu mwenye heshima, weledi, uaminifu, uadilifu na asiye na tabia au
mwenendo wenye kutiliwa shaka na jamii; na
(e) awe ni mtu ambaye hajawahi kutiwa hatiani kwa kosa lolote la
jinai.
(5) Sifa za Makamu Mwenyekiti zitakuwa kama zilivyoainishwa katika ibara ndogo ya (4). 1. Jina la Tume limebadilishwa kutoka kuwa “ Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji na kuwa “Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma”

2. Neno uwajibikaji limeondolewa

3. Jina la Chombo cha Uteuzi wa Mwenyekiti na Makamu wake limeONDOLEWA neno “Maalum”

4. Uteuzi hautazingatia pande za muungano

5. Mwenyekiti na Makamu wake hawatathibitishwa na Bunge bali wataapishwa na Rais

6. Mwenyekiti si lazima wazazi wake wote wawe Raia wa Tanzania, Neno limeongezwa “ambaye angalau mmoja kati ya wazazi wake ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya
Muungano”;
 Kuondoa neno uwajibikaji ni kuondoa dhana kuu ya ibara hii, pia kukwepa uwajibikaji wa serikali na viongozi wa umma kwa wananchi
 Kuondolewa sharti la uthibitisho wa uteuzi wa tume hii Bungeni ni kuondoa madaraka ya wananchi kuwawajibisha viongozi wao kupitia chombo cha uwakilishi (bunge)
 Kutokuwepo usawa wa uteuzi kati ya pande mbili za muungano kwa suala hili ni kutojali uwakilishi wa pende za Muungano

Uteuzi na sifa za Mjumbe
201.-(1) Wajumbe wa Tume ya Maadili ya Uongozi na uwajibikaji
watateuliwa na Rais baada ya kupendekezwa na Kamati Maalum ya Uteuzi.
(2) Sifa za wajumbe wa Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji zitakuwa kama ifuatavyo:
(a) awe ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano;
(b) mtu mwenye shahada ya chuo cha elimu ya juu
kinachotambulika kwa mujibu wa sheria za nchi;
(c) mtu mwenye uzoefu kwenye uongozi kwa kipindi kisichopungua
miaka kumi;
(d) mtu mwenye heshima, weledi, uaminifu, uadilifu na asiye na tabia
au mwenendo wenye kutiliwa shaka na jamii. 229.-(1) Mjumbe wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma
atateuliwa na Rais baada ya kupendekezwa na Kamati ya Uteuzi.
(2) Sifa za Mjumbe wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma
zitakuwa kama ifuatavyo:
(a) awe ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano;
(b) mtu mwenye shahada ya chuo cha elimu ya juu
kinachotambulika kwa mujibu wa sheria;
(c) mtu mwenye uzoefu kwenye uongozi kwa kipindi kisichopungua
miaka kumi;
(d) mtu mwenye heshima, weledi, uaminifu, uadilifu na asiye na tabia
au mwenendo wenye kutiliwa shaka na jamii; na
(e) awe ni mtu ambaye hajawahi kutiwa hatiani kwa kosa lolote la jinai. 1. Sharti limeongezwa kwamba asiwe na historia ya makosa la jinai ONGEZEKO LA KIFUNGU HIKI
Kamati Maalum ya Uteuzi 202. Kutakuwa na Kamati ya Uteuzi ambayo itakuwa na Wajumbe wafuatao:
(a) Jaji Mkuu wa Mahakama ya Jamhuri ya Muungano;
(b) Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano
(c) Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya Zanzibar;
(d) Spika wa Bunge la Tanganyika
(e) Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar na
(f) Mwanasheria Mkuu wa Serikali 230. Kutakuwa na Kamati ya Uteuzi ambayo itakuwa na Wajumbe wafuatao:
(a) Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano;
(b) Jaji Mkuu wa Zanzibar;
(c) Jaji Kiongozi;
(d) Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano; na
(e) Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Nafasi za wajumbe zilizoongezwa na kuunguzwa ni:
(a) Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano (imeondolewa)
(b) Jaji Kiongozi (imeongezwa)
(c) Spika wa Bunge la Tanganyika (imeondolewa)

Majukumu ya
Tume 203. Ibara hii ni ndefu (tafadhali rejea rasimu halisi) 231.-(1) Majukumu ya Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma
yatakuwa ni kufuatilia na kuchunguza tabia na mwenendo wa viongozi wa umma
kwa madhumuni ya kusimamia na kuhakikisha kuwa maadili na miiko ya
uongozi wa umma inazingatiwa, inalindwa na kuheshimiwa katika utumishi wa
Serikali, Bunge, Mahakama, taasisi na idara nyingine zote za umma.
(2) Bila kuathiri masharti ya jumla ya ibara ndogo ya (1), majukumu
mahsusi ya Tume yatakuwa ni:
(a) kusimamia maadili katika utumishi wa umma;
(b) kuchunguza tabia na mwenendo wa kiongozi wa umma na kuchukua
hatua pale inapostahili; na
(c) kusimamia sheria kuhusu maadili ya viongozi wa umma.
(3) Bunge litatunga sheria kwa ajili ya utekelezaji wa masharti ya Ibara
hii. Masharti yaliyokua kwenye ibara hii mengi yameondolewa na kuongezwa ibara ndogo ya 231 (3) ambayo inatoa sharti ya kutungwa kwa Sheria ya utekelezaji wa Masharti ya ibara hii Masuala muhimu juu ya uwajibikaji yameondolewa kwa kisingizio cha kutungwa kwa sheria ya utekelezaji wa masharti ya ibara hii, mabadiliko haya yataathiri ‘nia’ ya wananchi katika kuwawajibisha viongozi
Muda wa Mjumbe
wa Tume kushika
madaraka 204.-(1) Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wengine wote
kila mmoja atashika madaraka yake kwa kipindi cha miaka mitatu au kipindi
kingine cha chini ya miaka mitatu kama itakavyoainishwa katika barua ya uteuzi,
ikizingatiwa kwamba uteuzi wa Wajumbe wa Tume utafanywa kwa namna
ambayo Wajumbe wa Tume hawataanza au kumaliza muda wao kwa wakati
mmoja.
(2) Bila kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (1), Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti au Mjumbe wa Tume anaweza kuteuliwa tena kwa kipindi kingine
kimoja tu cha miaka mitatu.
(3) Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume wakati
watakapokuwa madarakani hawataruhusiwa kuteuliwa, kuchaguliwa au kushika
nafasi ya madaraka nyingine yoyote.
232.-(1) Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wengine wote
kila mmoja atashika madaraka yake kwa kipindi cha miaka mitatu au kipindi
kingine cha chini ya miaka mitatu kama itakavyoainishwa katika barua ya uteuzi,
ikizingatiwa kwamba uteuzi wa Wajumbe wa Tume utafanywa kwa namna
ambayo Wajumbe wa Tume hawataanza au kumaliza muda wao kwa wakati
mmoja.
(2) Bila kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (1), Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti au Mjumbe wa Tume anaweza kuteuliwa tena kwa kipindi kingine
kimoja tu cha miaka mitatu.
(3) Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume wakati
watakapokuwa madarakani hawataruhusiwa kuteuliwa, kuchaguliwa au kushika
nafasi nyingine yoyote ya madaraka. Hakuna mabadiliko yeyote
Ibara ya 205:

Kuondolewa Madarakani kwa Mjumbe wa Tume Kifungu hiki kimeondolewa na kuhamishiwa kwenye ibara nyingine kama ibara ndogo inayohusu Uhuru wa Tume 232 (2), Bunge litatunga sheria itakayoweka masharti kuhusu:
muda wa kukaa madarakani na kuondolewa madarakani kwa mjumbe
Ibara hii imeondolewa masharti yake na kufanywa kuwa ibara ndogo katika ibara nyingine ya 232 (2), lakini pia uzito wake umeondolewa kikatiba kwa kuweka masharti ya kutunga sheria inayotamka masharti ya kifungu hiki. Makali ya ibara hii yamepunguzwa kwa kuondolewa masharti yake na kufanywa kuwa ibara ndogo katika ibara nyingine ya 227 (2), lakini pia uzito wake umeondolewa kikatiba kwa kuweka masharti ya kutunga sheria inayotamka masharti ya kifungu hiki, nia ya kifungu hiki haitaweza kujitokeza vema katika sheria ambayo hutungwa na Bunge.
Kuondolewa kwa ibara hii kunapunguza uhuru wa mjumbe wa tume hasa katika masharti ya kuondolewa katika nafasi yake ambapo awali Rasimu ya pili ilitamka wazi masharti ya kumwondoa mjumbe wa tume hii madarakani, ili asiweze kuondolewa kwa hila
Uhuru wa Tume 206.-(1) Tume itakuwa huru na kwa mantiki hiyo, haitaingiliwa na mtu au
mamlaka yoyote katika utekelezaji wa majukumu yake.
(2) Bunge litatunga sheria itakayoweka masharti kuhusu:
(a) utaratibu wa utekelezaji wa majukumu ya Tume;
(b) utayarishaji na utoaji wa taarifa za Tume;
(c) utaratibu wa utoaji wa mapendekezo na maamuzi ya Tume;
(d) watumishi wa Tume; na
(e) masuala mengine muhimu yanayoihusu Tume. 233.-(1) Tume itakuwa huru na kwa mantiki hiyo, haitaingiliwa na mtu au
mamlaka yoyote katika utekelezaji wa majukumu yake.
(2) Bunge litatunga sheria itakayoweka masharti kuhusu:
(a) utaratibu wa utekelezaji wa majukumu ya Tume;
(b) utayarishaji na utoaji wa taarifa za Tume;
(c) utaratibu wa utoaji wa mapendekezo na maamuzi ya Tume;
(d) muda wa kukaa madarakani na kuondolewa madarakani kwa mjumbe
wa Tume;
(e) watumishi wa Tume; na
(f) masuala mengine muhimu yanayoihusu Tume. Kifungu kidogo kimeongezwa ambacho kitatungiwa sheria ambacho ni:

233 (2),(d) muda wa kukaa madarakani na kuondolewa madarakani kwa mjumbe
wa Tume;

207. Uwezeshaji wa nyenzo na Rasilimali 207. Serikali itahakikisha kuwa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma
inapatiwa fedha, nyenzo na rasilimali watu ya kutosha kadri hali itakavyoruhusu ili kutekeleza kazi na wajibu wake kwa ufanisi. 234. Serikali itahakikisha kuwa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma
inapatiwa fedha, nyenzo na rasilimali watu ili kutekeleza kazi na wajibu wake
kwa ufanisi. Maneno yafuatayo yameondolewa: “ya kutosha kadri hali itakavyoruhusu” Maneno yaliyoondolewa yalikua yanaleta utata katika kipimo cha utoshelezi wa rasilimali, hivyo kifungu kilikuwa na utata (ambiguous) hapo awali.
SEHEMU YA PILI

Ibara ya 208 Tume ya Haki za Binadamu 208 (3) Ibara hii imeondolewa ambayo inaweka masharti ya uteuzi wa Mwenyekiti na Makamu mwenyekiti kuzingatia pande za Muungano yaani Zanzibar na Tanzania Bara 235.-(1) Kutakuwa na Tume itakayoitwa “Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora” itakayokuwa na Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Makamishna wasiozidi saba.
(2) Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora watateuliwa na Rais kutoka miongoni mwa majina yaliyopendekezwa na Kamati ya Uteuzi.
(3) Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti watashika madaraka baada ya kuapishwa na Rais.
1. Jina la Tume limebadilishwa kwa kuongezewa neno “na Utawala Bora”

2. Ibara hii imeondolewa ambayo inaweka masharti ya uteuzi kuzingatia pande mbili za Muungano Kifungu hakizingatii uteuzi kwa usawa wa pande mbili za Muungano
208 (4) Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti watashika madaraka baada ya kuthibitishwa na Bunge. 235 (3) Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti watashika madaraka baada ya
kuapishwa na Rais. Madaraka ya Bunge kuthibitisha uteuzi wa nafasi hizi yameondolewa na kupewa Rais kuapisha Ibara hii inalimbikiza madaraka kwa Rais, pia inamomonyoa mamlaka ya wananchi (bunge)
Sifa za Uteuzi
Ibara ya 208 (5), (6)
208(5), (6) Sifa za Mwenyekiti na Makamishna 236.-(1) Sifa za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za
Binadamu na Utawala Bora zitakuwa kama ifuatavyo:
(a) awe ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano;
(b) mtu mwenye shahada ya sheria kutoka chuo cha elimu ya juu
kinachotambuliwa na sheria;
(c) mtu mwenye kuheshimu haki za binadamu;
(d) mtu mwenye uzoefu wa utumishi wa umma, upeo mkubwa katika mambo ya haki za binadamu, utawala au mambo ya jamii kwa kipindi kisichopungua miaka kumi; na
(e) mtu mwenye heshima, weledi, uaminifu, uadilifu na asiye na tabia au
mwenendo wenye kutiliwa shaka na jamii.

(2) Sifa za Kamishna wa Tume zitakuwa kama ifuatavyo:
(a) awe ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano na angalau mmoja
kati ya wazazi wake ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano;
(b) mtu mwenye shahada ya chuo cha elimu ya juu kinachotambuliwa na
Awali ibara hii ilikua sehemu ya Ibara, kwa sasa masharti ya Sifa za Mwenyekiti na Makamishna zimetungiwa ibara inayojitegemea.
Kamati ya Uteuzi 209.-(1) Kutakuwa na Kamati ya Uteuzi wa Mwenyekiti, Makamu
Mwenyekiti na Makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu itakayokuwa na wajumbe wafuatao:
(a) Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ambaye atakuwa ni Mwenyekiti;
(b) Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano;
(c) Jaji Mkuu wa Zanzibar
(d) Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar; na
(e) Jaji mkuu wa Tanganyika

….Masharti yanaendelea……. 237.-(1) Kutakuwa na Kamati ya Uteuzi wa Mwenyekiti, Makamu
Mwenyekiti na Makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora
itakayokuwa na wajumbe wafuatao:
(a) Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ambaye atakuwa ni Mwenyekiti;
(b) Jaji Mkuu wa Zanzibar ambaye atakuwa ni Makamu Mwenyekiti;
(c) Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano;
(d) Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar; na
(e) Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye atakuwa ni Katibu.
(2) Kamati ya Uteuzi itakuwa na jukumu la kupokea na kuchambua
majina ya watu walioomba kuwa Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na
Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, kwa mujibu wa
utaratibu utakaoainishwa na sheria.
(3) Kutakuwa na Sekretarieti ya Tume itakayoongozwa na Katibu
Mtendaji atakayeteuliwa na Rais kutokana na orodha ya majina ya watu watatu
waliopendekezwa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora. Sehemu kubwa ya masharti ya ibara hii yameondolewa ikiwemo; kuthibitishwa kwa Mwenyekiti na Makamu wake kupitia Bunge Uzito wa masharti ya ibara hii umeondolewa hasa dhana ya uwajibikaji kwa kuondoa sharti la uthibitisho wa nafasi hizi kwa njia ya Bunge ambalo ndiyo wananchi

Kamati ya uteuzi 209 (6) Asasi za kiraia kuwa na uwezo wa kupendekeza majina ya watu wanaoweza kuteuliwa kushika nafasi ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti nad Makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu Ibara ndogo ya 209 (6) imeondolewa Kuondolewa kwa ibara hii ni kuzinyima haki asasi za kiraia na zisizo za kiserikali uwakilishi katika Tume hii, hivyo kuwanyima nafasi za kutetea haki za wananchi likiwa ndilo jukumu lao mahsusi
Kazi na majukumu ya Tume 210 (1), (a) Limeongezeka neno ‘nchi’ 238.-(1) Kazi na majukumu ya Tume yatakuwa kama ifuatavyo:
(b) kuhamasisha, kulinda na kufuatilia utekelezaji wa usawa wa jinsia na ulinganifu kwa ujumla katika maendeleo ya Taifa; Ibara ya 238(1) (b) imeongezwa kuhusu Usawa wa kijinsia umeongezwa Kifungu hiki kinachochea usawa wa kijinsia
210(2) Masharti ya ibara hii yanayoipa Tume Mamlaka maalum yameondolewa 238 (3) Ibara imeongezeka inayoweka vikwazo/ kifungu nyimivu inaathiri uhuru wa tume katika kuchunguza masuala mbalimbali kwa kusomeka:

Kwa madhumuni ya kutekeleza majukumu yake, Tume haitachunguza
mambo yafuatayo:
(a) jambo lolote ambalo liko mbele ya mahakama au chombo kingine cha
kimahakama;
(b) jambo lolote linalohusu uhusiano au ushirikiano kati ya Serikali na
Serikali ya nchi yoyote ya nje au shirika la kimataifa;
(c) jambo linalohusu madaraka ya Rais kutoa msamaha; au
(d) jambo jingine lolote lililotajwa na sheria yoyote.
 Masharti ya ibara 210 yaliyoondolewa yaliyokuwa yanaipa Tume Mamlaka maalum yameondolewa

 Ibara 238 (3) imeongezeka inayoweka vikwazo/ kifungu nyimivu inaathiri uhuru wa tume katika kuchunguza masuala mbalimbali Kuwekwa kwa kifungu nyimivu kwa tume kunaondoa dhana ya uwajibikaji kwa serikali na kupunguza wigo wa tume kutekeleza majukumu yake
Muda wa kukaa madarakani kwa kamishna wa Tume 211(3) Ibara hii inakataza wateuliwa wa nafasi hizo kutoteuliwa au kuchaguliwa au kushika nafasi ya madaraka nyingine 239 (3) Mtu yeyote akiteuliwa kuwa Kamishna wa Tume atalazimika kuacha
mara moja madaraka katika chama chochote cha siasa au madaraka ya aina nyingine yoyote yatakayotajwa kwa ajili hiyo na sheria itakayotungwa na Bunge. Katiba Inayopendekezwainaweka masharti kwa mteuliwa kutokushika nafasi hii atalazimika kuacha nafasi nyingine aliyonayo katika chama cha siasa Katiba Inayopendekezwainatamka kwa uwazi na usahihi zaidi kwa wateuliwa kuachia nafasi/ vyeo/ madaraka yao mengine katika vyama vya siasa
Ibara ya 212
Kuondolewa Madarakani kwa Kamishna wa Tume 212 (1)
Kuondolewa Madarakani kwa Kamishna wa Tume 240.-(1) Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti au Kamishna wa Tume
anaweza kuondolewa madarakani kwa:
(a) kutokuwa na uwezo wa utekeleza majukumu yake kwa sababu ya
maradhi;
(b) kukiuka kanuni za maadili ya viongozi wa umma;
(c) kukiuka Miiko ya Uongozi wa Umma;
(d) kukosa weledi;
(e) utovu wa nidhamu; au
(f) kutiwa hatiani kwa makosa ya jinai yanayohusiana na kukosa maadili au kukosa uaminifu. Kwenye Katiba Inayopendekezwaimeongezeka ibara ndogo ambayo inatoa masharti ya kuondolewa madarakani kwa mwenyekiti, Makamu au Kamishna kwa kuw na historia ya makosa ya jinai:

240 (1),(f) kutiwa hatiani kwa makosa ya jinai yanayohusiana na kukosa maadili
au kukosa uaminifu. Imeboreshwa ili kuzingatia historia ya makosa ya jinai ya mteuliwa
Uhuru wa tume Ibara ya 213 Ibara ya 241 Hakuna Mabadiliko yeyote
Uwezeshaji wa
nyenzo na
rasilimali 214. Serikali itahakikisha kuwa Tume ya Haki za Binadamu inapatiwa fedha, nyenzo na rasilimali watu ya kutosha kadri hali itakavyoruhusu ili kutekeleza kazi na wajibu
wake kwa ufanisi. 242. Serikali itahakikisha kuwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala
Bora inapatiwa fedha, nyenzo na rasilimali watu ili kutekeleza kazi na wajibu
wake kwa ufanisi. Maneno yamepunguzwa ambayo ni; “ya kutosha kadri hali itakavyoruhusu” Maneno yaliyopunguzwa yanaathiri uwezeshaji wa Tume kwa hali ya kutosheleza mahitaji yake ya rasilimali, serikali inaweza kutumia kifungi hiki kukwepa wajibu wake kwa Tume

SEHEMU YA TATU: MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI
Uteuzi wa
Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali 215.-(1) Kutakuwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
ambaye atateuliwa na Rais na kuthibitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
(2) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali atashika nafasi ya
madaraka yake baada ya kuapishwa na Rais.

243.-(1) Kutakuwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ambaye atateuliwa na Rais.
(2) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali atateuliwa kutoka katika orodha ya majina matatu ya watumishi wa umma yaliyopendekezwa na
Tume ya Utumishi wa Umma.
(3) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali atashika nafasi ya
madaraka yake baada ya kuapishwa na Rais. Nguvu ya Bunge kuthibitisha uteuzi wa Mkaguzi Mkuu imeondolewa Kuondolewa kwa nguvu ya Bunge Kuthibitisha uteuzi wa Mkaguzi Mkuu inaondoa dhana ya uwajibikaji kwa wananchi, pia inalimbikiza madaraka makubwa kwa Rais kama ilivyo katiba ya sasa ya mwaka 1977.
Sifa za Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali Ibara ya 216 Ibara ya 244 Hakuna mabadiliko
Kazi na
majukumu ya
Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu
wa Hesabu za
Serikali Ibara ya 217 Ibara ya 245  245(1) (a) Limebadilishwa neno; “atatosheka” na kuwa “ataridhika”

 245 (1),(c), (i), vimeongezwa vyombo/ taasisi za kufanyiwa ukaguzi ikiwamo; Hesabu za vyama vya Siasa na hesabu za Serikali za mitaa Kuongezwa kwa vyombo vya kufanyiwa ukaguzi ni jambo zuri, japo rasimu ya pili haikuorodhesha Serikali za Mitaa kwa sababu suala hili halikuwa sehemu ya masuala ya Muungano
Muda wa Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu
wa Hesabu za
Serikali kushika madaraka Ibara ya 218 Ibara ya 246 Hakuna mabadiliko yeyote
Kuondolewa
madarakani kwa
Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali Ibara ya 219 Ibara ya 247  Imeongezwa sharti ya kumuondoa madarakani katika ibara ndogo ya 247(1),(f) kutiwa hatiani kwa makosa ya jinai yanayohusu kukosa maadili au
uaminifu.

 Yameondolewa meneno; nchi washirka na kuwekwa ”Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano
au Mahakama Kuu ya Zanzibar” Nyongeza hii ni sahihi kuzingatia historia ya jinai au matendo ya jinai ya Mthibiti mkuu
Uwezeshaji wa
nyenzo na
rasilimali 220. Serikali itaweka utaratibu utakaowezesha Ofisi ya Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kupatiwa fedha, nyenzo na rasilimali
watu ya kutosha ili kulinda uhuru wake katika
kutekeleza kazi na majukumu yake kwa ufanisi. 248. Serikali itaweka utaratibu utakaowezesha Ofisi ya Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kupatiwa fedha, nyenzo na rasilimali
watu kulingana na uwezo wa kibajeti wa Serikali ili kulinda uhuru wake katika
kutekeleza kazi na majukumu yake kwa ufanisi. Ibara ya 242 yamebadilishwa na kuongezwa maneno: “kulingana na uwezo wa kibajeti wa Serikali” Maneno yaliyopunguzwa yanaathiri uwezeshaji wa Taasisi hii kwa hali ya kutosheleza mahitaji yake ya rasilimali, serikali inaweza kutumia kifungi hiki kukwepa wajibu wake wa kibajeti.
SEHEMU YA NNE
CHOMBO CHA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA
Uthibiti wa rushwa Ibara hii ni mpya 249.-(1) Kwa madhumuni ya kudhibiti rushwa, kutakuwa na chombo ambacho kitakuwa na jukumu la kuzuia na kupambana na rushwa.
(2) Bunge litatunga sheria itakayoweka masharti kuhusu muundo, majukumu na mamlaka ya chombo kilichorejewa katika ibara ndogo ya (1).  Ibara hii ni mpya haikuwepo katika rasimu.

 Ibara hii haidadafui kwa kina namna Chombo hiki kitakavyoanzishwa na kuendeshwa ikiwemo uteuzi wa viongozi wake.

 Ibara inaweka sharti la kutungwa sheria itakayofafanua maudhui ya ibara hii

 Ibara hii haielezei endapo suala hili litagusa pande zote za Muungano au vinginevyo
 Kutokuwepo kwa ufafanuzi huu kwenye katiba itaondoa dhana ya umuhimu wa chombo cha kupamabana na rushwa ikiwa ni tatizo kubwa na ndani ya Jamii.
 Ibara hii lazima ieleze endapo chombo hiki/ suala hili linagusa pande zote za Muungano
 Kama taasisi hii haitaendeshwa kwa uwazi na usawa itakuwa tatizo na has kuhusu mgogpro wa siku nyingi za muungano.

SURA YA KUMI NA SITA
MASHARTI KUHUSU FEDHA ZA JAMHURI YA MUUNGANO
(a) Mfuko Mkuu wa Hazina na Fedha za Jamhuri ya Muungano
Misingi ya
matumizi ya fedha
za umma Ibara hii haimo kwenye Rasimu ya pili
250. Misingi ifuatayo itaongoza matumizi ya fedha za umma katika
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania:
(a) fedha za umma zitatumika kwa uwazi, umakini na kwa uwajibikaji
pamoja na kuzingatia ushiriki wa wananchi kupitia wawakilishi wao;
(b) mfumo wa fedha za umma utalenga kuwepo kwa:
(i) utozwaji kodi usio wa upendeleo au ubaguzi;
(ii) bajeti ya Serikali inayoweka vipaumbele kwa makundi na
maeneo yaliyo nyuma kimaendeleo;
(c) matumizi ya rasilimali na mikopo ya Taifa yatazingatia ustawi
linganifu kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo; na
(d) taarifa za usimamizi wa fedha za umma zitatolewa katika lugha
inayoeleweka kwa wananchi.  Ibara hii inaweka masharti ya misingi inayoongoza matumizi ya fedha za umma
 Neno uwazi limejitokeza tofauti na ibara nyinginezo ikiwemo kwenye tunU za taifa, lakini uwazi huu hauna nguvu Ibara hii ni nzuri kwani inaanisha misingi ya matumizi ya fedha za umma
Akaunti ya Fedha
ya Pamoja Ibara hii haimo kwenye Rasimu ya pili
251. Serikali ya Jamhuri ya Muungano itatunza akaunti maalum
itakayoitwa “Akaunti ya Fedha ya Pamoja” na ambayo itakuwa ni sehemu ya
Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano, ambamo
kutawekwa fedha yote itakayochangwa na Serikali mbili kwa kiasi
kitakachoamuliwa na Tume ya Pamoja ya Fedha kwa mujibu wa sheria
itakayotungwa na Bunge, kwa madhumuni ya shughuli za Jamhuri ya Muungano
kwa Mambo ya Muungano.  Ibara hii imenakiliwa kama ilivyo kwenye Katiba ya 1977,

 Ibara hii inaanzishwa kwa sababu ya kuepuka mfumo wa Serikali tatu kwa nia ya kuboresha mfumo wa serikali mbili, ikiwa ni majibu ya kero ya Zanzibar katika Muungano wa serikali mbili Ibara hii sio mpya kwani imo kwenye katiba ya sasa lakini haijawahi kutekelezwa kwa mujibu wa katiba, hivyo hakuna uhakika endapo itatekelezwa (pia ibara hii inaashiria mabadiliko ya vifungu vya katiba ya 1977 na si upya wa katiba)
Tume ya Pamoja
ya Fedha Ibara hii haimo kwenye Rasimu ya pili
252.-(1) Kutakuwa na Tume ya Pamoja ya Fedha yenye Wajumbe
wasiozidi saba watakaoteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa
kushauriana na Rais wa Zanzibar ambapo wajumbe watatu watatoka Zanzibar na
wajumbe wanne watatoka Tanzania Bara.
(2) Majukumu ya Tume ya Pamoja ya Fedha yatakuwa ni:
(a) kuchambua mapato na matumizi yanayotokana na, au yanayohusu
utekelezaji wa mambo ya Muungano na kutoa mapendekezo kwa
Serikali zote mbili kuhusu mchango na mgawo wa kila mojawapo ya
Serikali hizo;
(b) kuchunguza kwa wakati wote mfumo wa shughuli za fedha wa
Jamhuri ya Muungano na pia uhusiano katika mambo ya kifedha kati
ya Serikali hizo mbili; na
(c) kutekeleza majukumu mengine ambayo Rais ataipatia Tume au kama
Rais atakavyoagiza, na kwa mujibu wa sheria itakayotungwa na
Bunge.
(3) Kwa madhumuni ya Ibara hii, Bunge litatunga sheria itakayoainisha
na kufafanua:
(a) masharti na taratibu za utekelezaji wa majukumu;
(b) masharti kuhusu wajumbe wa Tume;
(c) muundo na majukumu ya Sekretarieti;
(d) taratibu za uwasilishaji wa taarifa za Akaunti ya Pamoja ya Fedha na
taarifa nyingine za Tume kuhusu utekelezaji wa majukumu kwa
mujibu wa Katiba hii; na
(e) mambo mengine yote yanayohusu Tume ya Pamoja ya Fedha.  Ibara hii inalingana na masharti ya katiba ya mwaka 1977 pia.

 Ibara hii inaanzishwa kwa sababu yakukidhi mfumo wa serikali mbili, ikiwa ni majibu ya kero ya Zanzibar katika Muungano wa serikali mbili Mabadiko haya hayaakisi kutungwa kwa katiba mpya bali mabadiko ya vifungu vya katiba ya mwaka 1977
Mfuko Mkuu wa
Hazina Ibara ya 221 253. Kutakuwa na Mfuko Mkuu wa Hazina wa Serikali ya Jamhuri ya
Muungano utakaoitwa “Mfuko Mkuu wa Hazina” ambamo fedha zote
zitakazopatikana kwa njia mbalimbali zitawekwa, isipokuwa:
(a) fedha ambazo zimetajwa katika sheria kuwa zitumike kwa
shughuli maalum au ziwekwe katika mfuko mwingine kwa ajili ya
matumizi maalum; au
(b) fedha ambazo kwa mujibu wa sheria, taasisi za Serikali zimeruhusiwa
kukusanya na kubaki nazo kwa ajili ya kugharamia
uendeshaji wa taasisi hizo. Ibara hizi zinafanana hakuna mabadiliko
Masharti ya
kutoa fedha za
matumizi katika
Mfuko Mkuu wa
Hazina Ibara ya 222 254.-(1) Fedha zinaweza kutolewa kutoka katika Mfuko Mkuu wa
Hazina kwa ajili ya matumizi, kwa kuzingatia masharti yafuatayo:
(a) fedha hizo ziwe kwa ajili ya matumizi ambayo yameidhinishwa kuwa
yatokane na fedha zilizomo katika Mfuko Mkuu wa Hazina na
idhini hiyo iwe imetolewa kwa mujibu wa Katiba hii au sheria; na
(b) fedha hizo ziwe kwa ajili ya matumizi ambayo yameidhinishwa na
sheria inayohusu matumizi ya fedha ya Serikali itakayotungwa
mahsusi na Bunge au sheria nyingine yoyote iliyotungwa na
Bunge.
(2) Kwa kuzingatia masharti ya ibara ndogo ya (1), fedha zilizomo
katika Mfuko Mkuu wa Hazina zitatolewa kutoka Mfuko huo kwa ajili ya
matumizi kwa kuzingatia masharti kuwa matumizi hayo yawe yameidhinishwa na
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
(3) Fedha zilizomo katika mfuko maalum wowote wa Serikali,
isipokuwa Mfuko Mkuu wa Hazina, hazitatolewa kutoka mfuko huo kwa ajili
ya matumizi isipokuwa kwa mujibu wa sheria inayoidhinisha matumizi
hayo. Ibara hii haijabadilishwa
Utaratibu wa
kuidhinisha
matumizi ya fedha
zilizomo katika
Mfuko Mkuu wa
Hazina Ibara ya 223 255.-(2) Makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali ya Jamhuri ya
Muungano yaliyotayarishwa kwa mujibu wa ibara ndogo ya (1), yatawasilishwa
kwanza kwenye Kamati husika ya Bunge kwa ajili ya kufanyiwa tathimini na
uchambuzi.
(3) Kamati ya Bunge iliyopelekewa makadirio ya mapato na matumizi ya
Serikali kwa mujibu wa ibara ndogo ya (2), yaweza kukaribisha na kupokea
maoni na ushauri kutoka kwa wadau mbalimbali kuhusu makadirio hayo, na baada ya kukamilisha tathmini na uchambuzi wa mapato na matumizi ya Serikali
ya Jamhuri ya Muungano, Kamati itaandaa taarifa yake kuhusu makadirio ya
Serikali na kisha kuiwasilisha Bungeni. Baadhi ya ibara ndogo zimeongezwa kwa minajiri ya:
 Makadirio ya Mapato na matumizi yaanzie kwenye Kamati ya Bunge badala ya Bunge lote kwa ujumla, pia uataratibu wa kamati kuitisha vikao vya mashauriano na wadau

Maboresho ya Ibara hii ni mazuri katika kuhakikisha wananchi
Utaratibu wa
kuidhinisha
matumizi ya fedha kabla ya sheria
inayohusu
matumizi ya fedha
ya Serikali kuanza
kutumika Ibara ya 224 256.-(1) Iwapo mwaka wa fedha wa Serikali umeanza na sheria
inayohusu matumizi ya fedha ya Serikali inayohusika na mwaka huo
haijaanza kutumika, Rais anaweza kuidhinisha fedha zitolewe kutoka Mfuko
Mkuu wa Hazina kwa ajili ya kugharamia shughuli za lazima za Serikali, na
fedha hizo zitatumiwa ndani ya miezi minne tangu mwanzo wa mwaka wa fedha
wa Serikali au hadi sheria inayohusu matumizi ya fedha ya Serikali
itakapoanza kutumika, kutegemea ni lipi kati ya mambo hayo litatangulia
kutokea.
(2) Bunge litatunga sheria kwa ajili ya kuweka masharti ya
kuidhinisha matumizi ya fedha kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina kwa
kufuata utaratibu ulioelezwa katika ibara ndogo ya (1). Hakuna mabadiliko yeyote
Mfuko wa
Matumizi ya
Dharura Ibara ya 225 257.-(1) Kutakuwa na Mfuko wa Matumizi ya Dharura ambao
matumizi yake yatawekewa masharti katika sheria.
(2) Sheria iliyotajwa katika ibara ndogo ya (1) itaruhusu Rais au
Waziri mwenye dhamana ya masuala ya fedha, pale anaporidhika kuwa kuna:
(a) jambo la haraka na la dharura na ambalo halikutazamiwa
kutokea na ambalo halikupangiwa fedha, kuazima fedha kutoka Mfuko wa Matumizi ya Dharura kwa ajili ya kugharamia jambo hilo;
au

(b) jambo la haraka na la dharura kama ilivyoelezwa katika aya ya (a) ya
ibara ndogo ya (2), kutumia fedha zilizotengwa mahsusi kwa ajili ya
kugharamia shughuli fulani kulipia gharama za jambo hilo.
(3) Iwapo fedha zimeazimwa kutoka Mfuko wa Matumizi ya
Dharura au fedha zilizotengwa mahsusi kwa ajili ya shughuli fulani
zimetumiwa kugharamia jambo la haraka na la dharura, basi kutawasilishwa
kwenye Bunge makadirio ya matumizi ya nyongeza, na baada ya Bunge
kuyakubali makadirio hayo muswada wa sheria unaohusu matumizi ya
fedha za Serikali utakaowasilishwa kwenye Bunge kwa ajili ya kuidhinisha
matumizi hayo utahakikisha kwamba fedha zozote zilizoazimwa kwenye
Mfuko wa Matumizi ya Dharura zitarudishwa kwenye Mfuko huo kutoka
katika fedha za matumizi yatakayoidhinishwa na muswada huo. Hakuna mabadiliko
Mishahara ya
baadhi ya
watumishi
kudhaminiwa na
Mfuko Mkuu wa
Hazina Ibara ya 226 Ibara ya 258 Hakuna mabadiliko yeyote
(b) Deni la Taifa na Mikopo ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano
Deni la Taifa Ibara ya 227, 259.-(1) Deni la Taifa litadhaminiwa na Mfuko Mkuu wa Hazina.
(2) Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa Ibara hii, deni la Taifa
litajumuisha deni la Serikali ya Jamhuri ya Muungano pamoja na deni lolote
litakalodhaminiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano. Hakuna mabadiliko
Mamlaka ya
Serikali ya
Jamhuri ya
Muungano
kukopa Ibara ya 228 Ibara ya 260 Hakuna mabadiliko
Mamlaka ya Serikali za nchi washirika kukopa

Ibara ya 229 261.-(1) Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itakuwa na mamlaka ya
kukopa fedha ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano kwa ajili ya kugharamia
shughuli zilizo chini ya mamlaka yake.
(2) Endapo mkopo utahitaji dhamana, Serikali ya Jamhuri ya Muungano,
baada ya kushauriana na kukubaliana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,
yaweza kutoa dhamana kwa mkopo unaoombwa.
(3) Bila kuathiri masharti ya Ibara ya 73, Bunge litatunga sheria
itakayoweka utaratibu wa Serikali ya  Ibara hii imebadilishwa kutokana na mfumo wa Serikali mbili kupendekezwa tofauti na rasimu ya pili iliyopendekeza mfumo wa serikali tatu
 Maneno nchi washirika yameondolewa na kubakizwa Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar;
(Mamlaka ya Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar kukopa)badala ya Mamlaka ya Serikali za nchi washirika
Mamlaka ya kutoza kodi kwa Muungano na Tanzania Bara yote kukasimishwa kwa Serikali ya Muungano ni mkanganyiko mkubwa wa ukusanyaji wa Mapato kwani hakuna mstari unaoonekana wazi (clear demarcation) KAMA ILIVYO KWA KATIBA YA 1977
Masharti ya
kutoza kodi 230. Hakuna kodi ya aina yoyote itakayotozwa na mamlaka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano isipokiwa kwa mujibu wa Sheria za nchi
262.-(1) Mamlaka ya kutoza kodi kwa mambo yote ya Muungano na kwa mambo yasiyo ya Muungano yanayoihusu Tanzania Bara yatakuwa chini ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
(2) Mamlaka ya kutoza kodi kwa mambo yote yasiyo ya Muungano
yanayoihusu Zanzibar yatakuwa chini ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
(3) Hakuna kodi ya aina yoyote itakayotozwa katika Jamhuri ya
Muungano isipokuwa kwa mujibu wa sheria.  Neno Masharti limebadilishwa kuwa mamlaka
 Mamlaka ya Utozaji wa kodi kwa kuzingatia mambo ya Muungano yamewekwa kwa Serikali ya Muungano
 Mamlaka ya kutoza kodi kwa mambo yasiyo ya Muungano kwa Tanzania Bara yamewekwa kwa Serikali ya Muungano na Zanzibar kwa mambo yasiyo ya Muungano yanayoihusu Zanzibar
Vyanzo vya mapato vya serikali ya Jamhuri ya Muungano Ibara ya 231, Ibara hii imefutwa Ibara hii imefutwa kutokana na Muundo wa Serikali kubadilishwa kutoka serikali tatu kuwa serikali mbili
Ununuzi wa umma Ibara ya 232 263.-(1) Katika kufanya ununuzi wa umma, Serikali na taasisi zote za
umma zitatakiwa kutumia mfumo na utaratibu utakaozingatia haki, uwazi,
maslahi ya umma, uwajibikaji, ushindani na thamani halisi ya fedha.
(2) Bunge litatunga sheria itakayoainisha mfumo wa manunuzi kwa Serikali na taasisi zake ambao utazingatia misingi ifuatayo:
(a) makundi ambayo yatapewa kipaumbele katika utoaji wa mikataba;
(b) kuwapa fursa maalum watu au makundi yalioathiriwa na ushindani
usio wa haki;
(c) adhabu kwa mkandarasi ambaye amefanya kazi chini ya kiwango na
kukiuka taratibu za kitaaluma, mkataba husika au sheria; na
(d) adhabu kwa mtu aliyekwepa kulipa kodi au aliyehukumiwa kwa  Imeondolewa ibara ndogo ya 232(2); ambayo iliweka sharti kwamba katika manunuzi ya umma serikali itatakiwa kuweka mfumo utakaozingatia ununuzi wa bidhaa zinazozalishwa au huduma zinazotolewa nchini Mabadiliko haya yataathiri uchumi wa nchi kwa kutozingatia kipaumbele cha ununuzi wa bidhaa na huduma za ndani
Benki kuu ya Jamhuri ya Muungano Ibara ya 233 264.-(1) Kutakuwa na Benki Kuu ya Jamhuri ya Muungano itakayoitwa
“Benki Kuu ya Tanzania”.
(2) Benki Kuu ya Tanzania itakuwa na majukumu yafuatayo:
(a) kutoa sarafu;
(b) kudhibiti na kusimamia mzunguko wa sarafu;
(c) kuandaa na kusimamia sera na mipango inayohusiana na sarafu;
(d) kudhibiti na kusimamia masuala ya fedha za kigeni;
(e) kusimamia benki za biashara na taasisi zote za fedha ndani ya Jamhuri
ya Muungano; na
(f) kutunza akaunti ya fedha za Serikali.
(3) Katika utekelezaji wa majukumu yake, Benki Kuu ya Tanzania
itakuwa huru na haitaingiliwa ama kwa kupewa maelekezo au kudhibitiwa na
mtu au mamlaka yoyote.
(4) Bunge litatunga sheria itakayoweka masharti kuhusu muundo,
mamlaka, shughuli na utendaji wa Benki Kuu ya Tanzania. Ibara ndogo ya 264-.(2),(e) imeongezwa kwa kubadilisha neon nchi washirika na kuwa; kusimamia benki za biashara na taasisi zote za fedha ndani ya Jamhuri ya Muungano; Mabadiliko haya ni kwa kuzingatia mapendekezo ya muundo wa Serikali mbili badala ya Serikali tatu kama ilivyokuwa kwenye rasimu ya katiba

Benki kuu kwa mibu wa ib ara hii ni kero nyingine kwa wananchi. Benki kuu haitaingiliwa na mamlaka yoyote au haitangiliwa na mtu yoyote ama kupewa maelekezo na mamalaka yeyote. Hii itawafanya watawala kuiona benk kuu kama diyo sehemu yao ya kuchota na kuhifadhi hela.
Tumeshudia uchotwaji wa pesa nyingi sana kwenye benk kuu. Hivyo hali ya kutokuwaingilia awe mtu binafsi au mamlaka ya nje ni kilio kiubwa sana
Benki za Serikali za nchi washirika Ibara ya 234 Ibara hii imefutwa Ibara hii imefutwa kwenye Katiba Inayopendekezwakwa sababu ya mapendekeze ya muundo wa Serikali mbili tofauti na rasimu ya katiba ambapo imependekezwa muundo wa serikali tatu

Sura ya 19 ya Katiba Inayopendekezwana Sura ya 17 ya Rasimu ya Pili ya Katiba
IBARA RASIMU YA PILI
YA KATIBA KATIBA PENDEKEZI TOFAUTI MAONI
SEHEMU YA KWANZA: MASHARTI YATOKANAYO
257 & 282
Matumizi ya baadhi ya masharti ya Katiba Sura ya 2
257.-(1)Masharti Yatokanayo na Masharti ya Mpito yaliyoanishwa katika Surah ii ya Katiba yataanza kutumika tarehe ambayo Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 2014 itakapoanza kutumika.
(2)Kwa kuondoa shaka, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 itakuwa imefutwa na, isipokuwa kwa masuala yaliyoanishwa katika Sehemu ya Pili ya Sura hii, haitakuwa na nguvu ya sheria kuanzia tarehe ya kuanza kutumika kwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 2014 282.-(1) Masharti Yatokanayo na Masharti ya Mpito yaliyoainishwa
katika Sura hii ya Katiba yataanza kutumika tarehe ambayo Katiba ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 2014 itakapoanza kutumika.
(2) Kwa kuondoa shaka, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
ya Mwaka 1977 itakuwa imefutwa na, isipokuwa kwa masuala yaliyoainishwa
katika Sehemu ya Pili ya Sura hii, haitakuwa na nguvu ya sheria kuanzia tarehe
ya kuanza kutumika kwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya
Mwaka 2014. Hakuna Sioni tatizo kwenye ibara hii. Ni muhimu sababu inaonyesha uhalali wa sheria zilizotungwa kabla katiba mpya haijaanza kutumika.
SEHEMU YA PILI: MASHARTI YA KIKATIBA NA SHERIA ZA NCHI
258 & 283
Kuendelea kutumika kwa masharti ya Katiba

258.-(1) Masharti Yatokanayo na Masharti ya Mpito katika Sura hii ya
Katiba na yale yaliyowekwa katika Mabadiliko ya “Sheria Maalum” ambayo
bado yanaendelea kutumika katika Katiba zilizoainishwa katika Ibara hii,
yataendelea kutumika.
(2) Kwa madhumuni ya Ibara hii, “Sheria Maalum” maana yake ni “the Republic of Tanganyika (Consequential, Transitional and Temporary Provisions) Act, 1962, the Interim Constitution (Consequential, Transition and Temporary Provisions) Act, 1965, the Constitution (Consequential, Transitional and Temporary Provisions) Act, 1977, the Constitution (Consequential, Transitional and Temporary Provisions) Act, 1984 na “the Constitution (Consequential, Transitional and Temporary Provisions) Act, 1992”. 283.-(1) Masharti Yatokanayo na Masharti ya Mpito katika Sura hii ya
Katiba na yale yaliyowekwa katika Mabadiliko ya “Sheria Maalum” ambayo
bado yanaendelea kutumika katika Katiba zilizoainishwa katika Ibara hii,
yataendelea kutumika.
(2) Kwa madhumuni ya Ibara hii, “Sheria Maalum” maana yake ni:
“ (a) the Republic of Tanganyika (Consequential, Transitional and
Temporary Provisions) Act, 1962;
(b) the Interim Constitution (Consequential, Transition and
Temporary Provisions) Act, 1965;
(c) the Constitution (Consequential, Transitional and Temporary
Provisions) Act, 1977;
(d) the Constitution (Consequential, Transitional and Temporary
Provisions) Act, 1984; na
(e) the Constitution (Consequential, Transitional and Temporary
Provisions) Act, 1992”. Hakuna Ibara hii pia haina tatizo.
259 & 284

Kuendelea kutumika kwa sheria za nchi 259.-(1) Masharti ya sheria zilizoainishwa katika ibara ndogo ya (2) na ambazo zinatumika kabla ya tarehe ya kuanza kutumika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 2014 zitaendelea kutumika kwa namna ambayo imeelekezwa katika ibara hii.
(2) Sheria za nchi ambazo:
(a) zimetungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano kablya ya kuanza kutumika kwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 2014 zitaendelea kutumika kwa madhumuni ya masuala yaliyoelekezwa katika sheria hizo; na
(b) zimetungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano ambazo zinatumika Tanzania Bara zitaendelea kutumika Tanganyika kwa madhumuni ya masuala yaliyoelekezwa katika sheria hizo.
(3) Kwa madhumuni ya masharti ya ibara ndogo ya (2) wakati na baada ya Muda wa Mpito:
(a) sheria zote zilizotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano ambazo zinatumika Tanzania Bara na Zanzibar na kwa kuzingatia marekebisho yatakayohitajika, zitakuwa sheria za nchi ambazo zitatumika katika Jamhuri ya Muungano kwa Mambo ya Muungano;
(b) kwa kuzingatia mgawanyo wa Mambo ya Muungano na mambo yasiyo ya Muungano yaliyoelekezwa kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 2014, sheria zote zilizotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano ambazo zinatumika Tanzania Bara na Zanzibar, kwa kuzingatia marekebisho yatakayohitajika, zitatumika Tanganyika na Zanzibar kwa mambo yasiyo ya Muungano hadi Tanganyika au Zanzibar itakapotunga sheria kuhusu mambo hayo; na
(c) sheria zote zilizotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano ambazo zinatumika Tanzania Bara na kwa kuzingatia marekebisho yatakayohitajika, zitakuwa sheria za nchi ambazo zitatumika Tanganyika.
(4) Bila kujali masharti ya ibara ndogo ya (3), Bunge la Jamhuri ya Muungano linaweza kutunga sheria yoyote kuhusu mambo ya Muungano na mambo yote yasiyo ya Muungano yanayohusu Tanganyika hadi Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania litakapoundwa kwa mujibu wa masharti ya Katiba ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 2014. 284.-(1) Masharti ya sheria zilizoainishwa katika ibara ndogo ya (2) na
ambazo zimekuwa zinatumika kabla ya tarehe ya kuanza kutumika Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 2014, zitaendelea kutumika kwa
namna ambayo imeelekezwa katika Ibara hii.
(2) Sheria za nchi ambazo:
(a) zimetungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano kabla ya kuanza
kutumika kwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya
Mwaka 2014 zitaendelea kutumika kwa madhumuni ya masuala
yaliyoelekezwa katika sheria hizo; na
(b) zimetungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano ambazo zinatumika
Tanzania Bara zitaendelea kutumika Tanzania Bara kwa madhumuni
ya masuala yaliyoelekezwa katika sheria hizo.
(3) Kwa madhumuni ya masharti ya ibara ndogo ya (2), wakati na baada
ya Muda wa Mpito:
(a) sheria zote zilizotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano ambazo
zinatumika Tanzania Bara na Zanzibar na kwa kuzingatia
marekebisho yatakayohitajika, zitakuwa sheria za nchi ambazo
zitatumika katika Jamhuri ya Muungano kwa Mambo ya Muungano;
(b) kwa kuzingatia mgawanyo wa Mambo ya Muungano na mambo
yasiyo ya Muungano yaliyoelekezwa kwenye Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ya Mwaka 2014, sheria zote zilizotungwa
na Bunge la Jamhuri ya Muungano ambazo zinatumika Tanzania
Bara na Zanzibar, kwa kuzingatia marekebisho yatakayohitajika,
zitatumika Tanzania Bara au Zanzibar kwa Mambo yasiyo ya
Muungano hadi hapo Tanzania Bara au Zanzibar itakapotunga sheria
kuhusu mambo hayo; na
(c) sheria zote zilizotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano ambazo
zinatumika Tanzania Bara na kwa kuzingatia marekebisho
yatakayohitajika, zitakuwa sheria ambazo zitatumika Tanzania Bara. 1.Kuongezwa kwa neno “ zimekuwa” katika ibara ndogo ya 1 ya Ibara ya 284 ya Katiba Pendekezi
2. Kuondolewa neno “Tanganyika” na kubadilishwa na neno “Tanzania Bara” katika ibara ndogo za 2 na 3 za ibara ya 284 ya Katiba Pendekezi
3. Kuondolewa wa kwa ibara ndogo ya 4 Mabadiliko haya yamefanywa kupinga dhana ya serikali tatu.
SEHEMU YA TATU: UTUMISHI WA UMMA
260 & 285
Kuendelea kuwepo kwa Rais madarakani 260. Mtu aliyekuwa anashika nafasi ya madaraka ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano kabla ya kuanza kutumika kwa Katiba hii, ataendelea kushika nafasi
ya madaraka ya Rais kwa masharti ya Katiba hii hadi mtu mwingine
atakapochaguliwa badala yake katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kushika nafasi ya
madaraka ya Rais kwa mujibu wa Katiba hii. 285. Mtu aliyekuwa anashika nafasi ya madaraka ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano kabla ya kuanza kutumika kwa Katiba hii, ataendelea kushika nafasi
ya madaraka ya Rais kwa masharti ya Katiba hii hadi mtu mwingine
atakapochaguliwa badala yake katika Uchaguzi Mkuu wa kushika nafasi ya
madaraka ya Rais kwa mujibu wa Katiba hii. 1. Kuondolewa kwa maneno “mwka 2015” Hakuna maoni kwa kweli.
261 & 286
Kuendelea kuwepo kwa Makamu wa Rais madarakani 261.- Mtu aliyekuwa anashika nafasi ya madaraka ya Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano kabla ya kuanza kutumika kwa Katiba hii, ataendelea
kushika nafasi ya madaraka ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa
masharti ya Katiba hii hadi Rais wa Jamhuri ya Muungano
atakapochaguliwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. 286. Mtu aliyekuwa anashika nafasi ya madaraka ya Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano kabla ya kuanza kutumika kwa Katiba hii, ataendelea
kushika nafasi ya madaraka ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa
masharti ya Katiba hii hadi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
atakapochaguliwa badala yake katika Uchaguzi Mkuu. 1. Kuondolewa kwa maneno “…hadi Rais wa Jamhuri ya Muungano atakapochaguliwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015” na badala yake “….hadi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano atakapochaguliwa badala yake katika Uchaguzi Mkuu.” Haileti tatizo sana, kwani Rais na makamu wanachaguliwa wakati mmoja.
262 & 287 262.- .-(1) Mtu anayeshika nafasi ya Waziri Mkuu ataendelea kuwa katika
nafasi ya madaraka ya Waziri Mkuu hadi Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 utakapofanyika na
Rais wa Jamhuri ya Muungano ameshika madaraka.
(2) Mtu anayeshika nafasi ya madaraka ya Waziri au Naibu Waziri
ataendelea kushika nafasi hiyo ya madaraka hadi Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015
utakapofanyika na nafasi hiyo ya madaraka itakoma saa ishirini na nne kabla ya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuapishwa kushika nafasi ya
madaraka ya Rais.
287.-(1) Mtu anayeshika nafasi ya Waziri Mkuu ataendelea kuwa katika
nafasi ya madaraka ya Waziri Mkuu hadi Uchaguzi Mkuu utakapofanyika, na
Rais wa Jamhuri ya Muungano ameshika madaraka.
(2) Mtu anayeshika nafasi ya madaraka ya Waziri au Naibu Waziri
ataendelea kushika nafasi hiyo ya madaraka hadi Uchaguzi Mkuu
utakapofanyika na nafasi hiyo ya madaraka itakoma saa ishirini na nne kabla ya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuapishwa kushika nafasi ya madaraka ya Rais.
(3) Masharti ya ibara ndogo ya (1) na (2), hayatatafsiriwa kwamba
yanaondoa au kufifisha madaraka aliyonayo Rais kwa mujibu wa Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 au sheria za nchi kufuta
nafasi ya madaraka ya kumvua madaraka au kumwachisha kazi mtu anayeshika
au kukaimu nafasi ya madaraka au kumwachisha kazi mtu anayeshika au
kukaimu nafasi ya madaraka ya Waziri Mkuu, Waziri au Naibu Waziri
kujiuzulu. 1.Kuondolewa kwa maneno “mwaka 2015” katika ibara ndogo za 1 na 2 za ibara ya 280 ya Katiba Pendekezi
2.Kuongezwa kwa ibara ndogo ya 3 Mabadilko yaliyofanywa ni madogo sana na hayajaharibu mantiki.
263 & 288
Kuendelea kwa utumishi wa umma 263.- (1)Kila mtu aliyeshika au kukaimu nafasi ya madaraka ya utumishi
wa umma katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Bunge la Jamhuri ya
Muungano au Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano kabla ya tarehe ya kuanza
kutumika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 2014,
ataendelea na atatambuliwa kuwa amechaguliwa, kuteuliwa au kuajiriwa kushika
au kukaimu nafasi ya madaraka ya utumishi wa umma katika Serikali ya Jamhuri
ya Muungano, Bunge la Jamhuri ya Muungano au Mahakama ya Jamhuri ya
Muungano na kwamba masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Mwaka
2014 au sheria za nchi kuhusiana na kuchaguliwa, uteuzi, ajira na kula kiapo au
yamini yamezingatiwa na kutekelezwa.
(2) Kila mtu ambaye kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano waTanzania ya Mwaka 1977 au sheria za nchi, atahitajika kuondoka katika nafasi
ya madaraka baada ya muda maalum kupita au atakapotimiza umri wa kustaafu,
ataacha kushika nafasi ya madaraka katika utumishi wa umma baada ya kufika
mwisho wa muda huo maalum au atakapofika umri wa kustaafu.
(3) Masharti ya ibara ndogo ya (1) na (2), hayatatafsiriwa kwamba
yanaondoa au kufifisha madaraka aliyonayo mtu au
mamlaka imepewa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya
Mwaka 1977 au sheria za nchi kufuta nafasi ya madaraka na kumvua madaraka
au kumwachisha kazi mtu anayeshika au kukaimu nafasi ya madaraka au
kumtaka mtumishi wa umma kujiuzulu.
(4) Kwa madhumuni ya malipo ya kiinua mgongo au malipo mengine ya
uzeeni, muda wa utumishi wa mtumishi wa umma anayehusika na masharti ya
Ibara hii, utahesabika kuwa ni pamoja na muda wa utumishi aliokuwa nao kabla
ya kuanza kutumika kwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya
Mwaka 2014.
(5) Isipokuwa kama itaelekezwa vinginevyo, masharti ya kazi ya
mtumishi wa umma ambaye masharti ya Ibara hii yanamhusu hayatakuwa duni
au hafifu ukiliganisha na masharti ya kazi aliyokuwa nayo kabla ya kuanza
kutumika kwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 2014 au
sheria za nchi zitakazotungwa kwa ajili hiyo. 288.-(1)Kila mtu aliyeshika au kukaimu nafasi ya madaraka ya utumishi
wa umma katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Bunge la Jamhuri ya
Muungano au Mahakama ya Jamhuri ya Muungano kabla ya tarehe ya kuanza
kutumika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 2014,
ataendelea na atatambuliwa kuwa amechaguliwa, kuteuliwa au kuajiriwa kushika
au kukaimu nafasi ya madaraka ya utumishi wa umma katika Serikali ya Jamhuri
ya Muungano, Bunge la Jamhuri ya Muungano au Mahakama ya Jamhuri ya
Muungano na kwamba masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Mwaka
2014 au sheria za nchi kuhusiana na kuchaguliwa, uteuzi, ajira na kula kiapo au yamini yamezingatiwa na kutekelezwa.
(2) Kila mtu ambaye kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano waTanzania ya Mwaka 1977 au sheria za nchi, atahitajika kuondoka katika nafasi
ya madaraka baada ya muda maalum kupita au atakapotimiza umri wa kustaafu,
ataacha kushika nafasi ya madaraka katika utumishi wa umma baada ya kufika
mwisho wa muda huo maalum au atakapofika umri wa kustaafu.
(3) Masharti ya ibara ndogo ya (1) na (2), hayatatafsiriwa kwamba
yanaondoa au kufifisha madaraka aliyonayo mtu au yaliyowekwa kwa
mamlaka kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya
Mwaka 1977 au sheria za nchi kufuta nafasi ya madaraka na kumvua madaraka
au kumwachisha kazi mtu anayeshika au kukaimu nafasi ya madaraka au
kumtaka mtumishi wa umma kujiuzulu.
(4) Kwa madhumuni ya malipo ya kiinua mgongo au malipo mengine ya
uzeeni, muda wa utumishi wa mtumishi wa umma anayehusika na masharti ya
Ibara hii, utahesabika kuwa ni pamoja na muda wa utumishi aliokuwa nao kabla
ya kuanza kutumika kwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya
Mwaka 2014.
(5) Isipokuwa kama itaelekezwa vinginevyo, masharti ya kazi ya
mtumishi wa umma ambaye masharti ya Ibara hii yanamhusu hayatakuwa duni
au hafifu ukiliganisha na masharti ya kazi aliyokuwa nayo kabla ya kuanza
kutumika kwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 2014 au
sheria za nchi zitakazotungwa kwa ajili hiyo. 1.Kuondolewa kwa maneno “ Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano” na badala yake “ Mahakama ya Jamhuri ya Muungano” katika ibara ndogo ya 1 ya ibara ya 281 ya Katiba Pendekezi
2. Kubadilishwa kwa maneno “..mamlaka imepewa” na “yaliyowekwa kwa mamlaka” katika ibara ndogo ya 3 ya ibara ya 281 ya Katiba Inayopendekezwa
SEHEMU YA NNE: BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO
264 & 289
Kuendelea kwa Ubunge na Uongozi wa Bunge
264.-(1) Kwa kuzingatia masharti ya ibara ndogo ya (2) na sheria za nchi
kuhusu masuala ya uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano
na uchaguzi wa Spika, Naibu Spika na Viongozi wa Kamati za Bunge, Spika,
Naibu Spika, Viongozi wa Kamati za Bunge na Wabunge wataendelea kuwa
Spika, Naibu Spika, Viongozi wa Kamati za Bunge na Wabunge, hadi Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.
(2) Masharti ya Ibara ndogo ya (1) hayatatafsiriwa kwamba yanazuia
kuondolewa kwa Spika, Naibu Spika, Viongozi wa Kamati za Bunge au
Mbunge, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Mwaka 1977,
Sheria ya Uchaguzi ya Taifa na Kanuni za Kudumu za Bunge. 289.-(1) Kwa kuzingatia masharti ya ibara ndogo ya (2) na sheria za nchi
kuhusu masuala ya uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano
na uchaguzi wa Spika, Naibu Spika na Viongozi wa Kamati za Bunge, Spika,
Naibu Spika, Viongozi wa Kamati za Bunge na Wabunge wataendelea na nyadhifa hizo hadi tarehe ya mwisho wa Maisha ya Bunge kwa mujibu wa Katiba hii.
(2) Masharti ya Ibara ndogo ya (1) hayatatafsiriwa kwamba yanazuia
kuondolewa kwa Spika, Naibu Spika, Viongozi wa Kamati za Bunge au
Mbunge, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Mwaka 1977,
Sheria ya Uchaguzi ya Taifa na Kanuni za Kudumu za Bunge. 1. Kubadilishwa kwa maneno “..hadi Uchaguzi Mkuu mwaka 2015” na kuwekwa maneno “hadi Bunge litakapovunjwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Mwaka 2014” katika ibara ndogo ya 1 ya ibara ya 282 ya Katiba Pendekezi
2. Kuondolewa kwa maneno “..watendelea kuwa Spika, Naibu Spika, Viongozi wa Kamati za Bunge na Wabunge, hadi Bunge litakapovunjwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Mwaka 2014” na kuwekwa maneno “…wataendelea na nyadhifa hizo hadi tarehe ya mwisho wa Maisha ya Bunge kwa mujibu wa Katiba hii.”
265 & 290
Kuvunjwa kwa Bunge 265. .-(1) Endapo, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ya Mwaka 1977 au sheria za nchi, jambo au suala lolote linahitaji
kufanyika au linaweza kufanyika, jambo au suala hilo linaweza kufanyika
kutokana au kufuatia kuvunjwa kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
(2) Ikiwa umuhimu wa kuliitisha Bunge utatokea kabla ya kutangazwa
kwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu ambao utafanyika baada ya kuvunjwa Bunge
la Jamhuri ya Muungano.
(a) kwa madhumuni ya kuliitisha Bunge, Spika, Naibu Spika na
Wabunge waliochaguliwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Mwaka 1977, sheria za nchi na Kanuni za Bunge
wanaweza kuitwa na watakuwa Spika, Naibu Spika na Wabunge
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano litakaloitishwa.
(b) kwa madhumuni ya uteuzi katika nafasi ya madaraka wakati Bunge
limevunjwa, uteuzi unaweza kufanywa wa mtu ambaye alikuwa
Mbunge kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ya Mwaka 1977 na Sheria za nchi zinazohusika. 290.-(1) Endapo, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ya Mwaka 1977 au sheria za nchi, jambo au suala lolote linahitaji
kufanyika au linaweza kufanyika, jambo au suala hilo linaweza kufanyika
kutokana au kufuatia kuvunjwa kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
(2) Ikiwa umuhimu wa kuliitisha Bunge utatokea kabla ya kutangazwa
kwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu ambao utafanyika baada ya kuvunjwa Bunge
la Jamhuri ya Muungano.
(a) kwa madhumuni ya kuliitisha Bunge, Spika, Naibu Spika na
Wabunge waliochaguliwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Mwaka 1977, sheria za nchi na Kanuni za Bunge
wanaweza kuitwa na watakuwa Spika, Naibu Spika na Wabunge
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano litakaloitishwa; na
(b) kwa madhumuni ya uteuzi katika nafasi ya madaraka wakati Bunge
limevunjwa, uteuzi unaweza kufanywa wa mtu ambaye alikuwa
Mbunge kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ya Mwaka 1977 na Sheria za nchi zinazohusika. Hakuna
SEHEMU YA TANO: MAHAKAMA YA JAMHURI YA MUUNGANO
266 & 291
Kuendelea kwa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu
Sura ya 2 266 .-(1) Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano na Mahakama
Kuu zitaendelea na zitakuwa na mamlaka ya kusikiliza mashauri na kutoa
uamuzi au amri kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ya Mwaka 1977 na sheria za nchi.
(2) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (1), Majaji wa Mahakama ya
Rufani na Majaji wa Mahakama Kuu watakuwa na madaraka ya kusikiliza
mashauri, kutoa hukumu au amri kutokana na mashauri yaliyofunguliwa au
yatakayofunguliwa katika Mahakama ya Rufani au Mahakama Kuu. 291.-(1) Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano na Mahakama
Kuu zitaendelea na zitakuwa na mamlaka ya kusikiliza mashauri na kutoa
uamuzi au amri kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ya Mwaka 1977 na sheria za nchi.
(2) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (1), Majaji wa Mahakama ya
Rufani na Majaji wa Mahakama Kuu watakuwa na madaraka ya kusikiliza
mashauri, kutoa hukumu au amri kutokana na mashauri yaliyofunguliwa au yatakayofunguliwa katika Mahakama ya Rufani au Mahakama Kuu. Hakuna
267 & 292
Kuendelea kwa mashauri yaliyopo mahakamani 267.-(1) Shauri lolote ambalo halijakamilika au limekamilika katika
Mahakama ya Rufani au Mahakama Kuu litaendelea kusikilizwa hadi
kukamilika; na hukumu, hati ya kukazia hukumu na amri iliyotolewa au
itakayotolewa katika shauri hilo inaweza kutolewa na kutekelezwa na
Mahakama ya Rufani au Mahakama Kuu
(2) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (1), kila hukumu, hati ya kukazia
hukumu na amri iliyotolewa na Mahakama ya Rufani au Mahakama Kuu
ambayo haijatekelezwa kikamilifu kabla ya kufutwa kwa Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 inaweza kutekelezwa kikamilifu baada
ya kuanza kutumika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka
2014.
(3) Uamuzi wowote wa Mahakama ya Rufani uliotolewa kuhusu shauri
lolote lililofunguliwa kabla ya kuanzishwa kwa Mahakama ya Juu kwa mujibu
wa masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Mwaka 2014, hautakatiwa
rufaa katika Mahakama ya Juu. 292.-(1) Shauri lolote ambalo halijakamilika au limekamilika katika
Mahakama ya Rufani au Mahakama Kuu litaendelea kusikilizwa hadi
kukamilika; na hukumu, hati ya kukazia hukumu na amri iliyotolewa au
itakayotolewa katika shauri hilo inaweza kutolewa na kutekelezwa na
Mahakama ya Rufani au Mahakama Kuu
(2) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (1), kila hukumu, hati ya kukazia
hukumu na amri iliyotolewa na Mahakama ya Rufani au Mahakama Kuu
ambayo haijatekelezwa kikamilifu kabla ya kufutwa kwa Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 inaweza kutekelezwa kikamilifu baada
ya kuanza kutumika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka
2014.
(3) Uamuzi wowote wa Mahakama ya Rufani uliotolewa kuhusu shauri
lolote lililofunguliwa kabla ya kuanzishwa kwa Mahakama ya Juu kwa mujibu wa masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Mwaka 2014, hautakatiwa rufaa katika Mahakama ya Juu. Hakuna Ni sawa ikiwa ni katika kutekeleza majukumu yaliyoainishwa.
SEHEMU YA SITA: MASHARTI YA MPITO
268 & 293
Muda wa Mpito 268. Muda wa Mpito utakuwa muda wote kuanzia tarehe ya kuanza
kutumika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 2014 hadi tarehe 31 Disemba, 2018. 293. Muda wa Mpito utakuwa muda wote kuanzia tarehe ya kuanza
kutumika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 2014 hadi kupita miaka minne baada ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Mwaka 2014 kuanza kutumika. 1.Kubadilishwa kwa maneno “..hadi tarehe 31 Disemba, 2018” na “..hadi kupita miaka mine baada ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Mwaka 2014 kuanzana kutumika” Hakuna mabadilko ya maana.
269 & 294
Utekelezaji wa masharti ya Katiba Mpya
269.-(1) Mambo yafuatayo yatafanyika na kukamilika katika Muda wa
Mpito:
(a) kutungwa kwa Katiba ya Tanganyika;
(b) kurekebisha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 ili kuwiana na masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 2014;
(c) mgawanyo wa rasilimali baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali za Nchi Washirika;
(d) kutunga na kurekebisha sharia mbalimbali za Nchi Washirika ili kuwiana na masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 2014;
(e) mgawanyo wa watumishi wa umma baina ya Serikali za Muungano na Serikali za Nchi Washirika;
(g) kuundwa kwa Tume na taasisi za kikatiba zilizoainishwa kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 2014 na kwa kuzingatia masharti ya Katiba hiyo;
(h) kufanya uteuzi katika nafasi za madarak kwa utaratibu ulioanishwa kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 2014;
(i) kufanya maandalizi na kuendesha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kwa kuzingatia masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 2014;
(j) kufanya maandalizi na mambo yote muhimu kwa ajili ya utekelezaji bora wa masharti ya kikatiba yaliyomo kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 2014
(2) Maoni ya wananchi yaliyokusanywa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba yaliyotumika kuandaa Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 2014 yanaweza kutumika katika kuandika Rasimu ya Katiba ya Tangayika 294.-(1) Mambo yafuatayo yatafanyika na kukamilika katika Muda wa
Mpito:
(a) kurekebisha Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984 ili kuwiana na
masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka
2014;
(b) kutunga na kurekebisha sheria mbalimbali za Jamhuri ya
Muungano, sheria ambazo si za Muungano zinazohusu Tanzania Bara
na sheria za Zanzibar ili kuwiana na masharti ya Katiba ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 2014;
(c) kuanzishwa kwa Mahakama ya Juu;
(d) kuundwa kwa Tume na Taasisi nyingine za kikatiba zilizoainishwa
kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka
2014 na kwa kuzingatia masharti ya Katiba hii;
(e) kufanya uteuzi katika nafasi za madaraka kwa utaratibu ulioainishwa
kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka
2014; na
(f) kufanya maandalizi na mambo yote muhimu kwa ajili ya utekelezaji
bora wa masharti ya kikatiba yaliyomo kwenye Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ya Mwaka 2014. 1.Kuondolewa na kwa ibara ndogo 1(a) kuhusu kutungwa Katiba ya Tanganyika; (c) kuhusu mgawanyo wa rasilimali baina ya serikali za nchi washirika; (e) kuhusu mgawanyo wa watumishi wa umma baina ya nchi washirika; (f) kuhusu mgawanayo wa madeni baina ya serikali za nchi washirika; na (i) kuhusu maandalizi ya uchaguzi wa 2015 toka kwenye ibara ya 269 ya Rasimu ya Pili ya Katiba
2. Kubadilishwa kwa maneno “kutunga na kurekebisha sheria mbalimbali za Nchi Washirika ili kuwiana na masharti….” na badala yake kuwekwa maneno “kutunga na kurekebisha sheria mbalimbali za Jamhuri ya
Muungano, sheria ambazo si za Muungano zinazohusu Tanzania Bara
na sheria za Zanzibar…” katika ibara ndogo ya 1(b) ya Katiba Pendekezi
3. Kuondolewa kwa ibara ndogo ya 2 ya Rasimu ya Pili ya Katiba kinachohusu maoni ya wananchi yaliyokusanywa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba kutunga Katiba ya Tanganyika Kikubwa hapa ni kupinga uwepo au dhana ya serikali tatu. Kitu ambacho kimsingi ni kinyume na msingi wa rasimu ya pili ya katiba
270 & 295
Kamati ya kusimamia muda wa mpito/Kamati ya Utekelezaji wa Katiba 270.- (1) Kwa madhumuni ya utekelezaji wa masuala yanayohitaji kufanyiwa
kazi na kukamilishwa katika Muda wa Mpito, Rais atateua Kamati ya
Utekelezaji wa Katiba katika Muda wa Mpito.
(2) Kamati ya Utekelezaji wa Katiba itakuwa na:
(a) Mwenyekiti; na
(b) Wajumbe wengine wanane.
(3) Sekretarieti ya Kamati ya Utekelezaji itaongozwa na Katibu na itakuwa na watumishi wa idadi inayotosha katika utekelezaji wa kazi ya kamati kwa ufanisi.
(4) Uteuzi wa Mwenyekiti, Wajumbe na watumishi wa sekretarieti utazingatia uwakilishi wa kila upande wa Jamhuri ya Muungano. 295. (1)Kwa madhumuni ya utekelezaji wa masuala yanayohitaji kufanyiwa
kazi na kukamilishwa katika Muda wa Mpito, Rais kupitia Hati ya Uteuzi atateua Kamati ya
Utekelezaji wa Katiba katika muda wa Mpito.
((2) Majukumu ya Kamati ya Utekelezaji wa Katiba yatakuwa kama yatakavyoainishwa katika Hati ya Uteuzi. 1.Kuondolewa kwa ibara ndogo za 3 na 4 inayozungumzia Kamati ya Utekelezaji wa Katiba
271 & 296
Kufutwa kwa Masharti Yatokanayo na Masharti ya Mpito 271. Baada ya kumalizika kwa Muda wa Mpito, masharti ya Sura ya
Kumi na Saba yatakoma na hayatakuwa na nguvu ya kisheria. 296. Baada ya kumalizika kwa Muda wa Mpito, masharti ya Sura ya
Kumi na tisa yatakoma na hayatakuwa na nguvu ya kisheria. Hakuna Kama uratibu wa sheria husika utakuwa wa wazi na haki basi hapatakuwa na tatizo.
NYONGEZA RASIMU YA PILI YA KATIBA KATIBA PENDEKEZI TOFAUTI MAONI
Mambo ya Muungano
1. Katiba na mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
2. Ulinzi na usalama wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
3. Uraia na Uhamiaji.
4. Sarafu na Benki.
5. Mambo ya Nje.
6. Usajili wa Vyama vya Siasa
7. Ushuru wa Bidhaa na mapato yasiyo ya kodi yatokanayo na Mambo ya Muungano.
Nyongeza ya Kwanza [Mambo ya Muungano]
1. Katiba na Mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
2. Mambo ya nje.
3. Ulinzi na usalama wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
4. Polisi.
5. Mamlaka juu ya mambo yanayohusika na hali ya hatari.
6. Uraia na uhamiaji.
7. Utumishi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
8. Kodi ya Mapato inayolipwa na watu binafsi na Mashirika, ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa nchini Tanzania na zinazosimamiwa na Idara ya Forodha.
9. Mawasiliano.
10. Sarafu na Benki Kuu.
11. Elimu ya Juu.
12. Baraza la Taifa la Mitihani.
13. Usalama na usafiri wa anga.
14. Utabiri wa hali ya hewa.
15. Mahakama ya Juu na Mahakama ya Rufani.
16. Usajili wa vyama vya siasa.
Nyongeza ya Pili [ Sheria ambazo mabadiliko yake yanahitaji kuungwa mkono na theluthi mbili ya Wabunge toka Tanzania Bara na theluthi mbili ya Wabunge toka Zanzibar]
1. Muswada wa sheria wa kubadili masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano yanayohusu Mambo ya Muungano.
2. Kuongeza au kupunguza jambo lolote la Muungano.
Nyongeza ya Tatu [Mambo ambayo mabadiliko yake yanahitaji kuungwa mkono kwa zaidi ya nusu ya kura halali zilizopigwa na wananchi wa Tanzania Bara, na zaidi ya nusu ya kura halali zilizopigwa na wananchi wa Tanzania Zanzibar katika kura ya maoni]
1. Muundo wa Jamhuri ya Muungano.
2. Kuwepo kwa Jamhuri ya Muungano.
3. Kubadilisha masharti ya ibara ya 134(1)(c) ya Katiba hii. 1. Kuongezeka kwa idadi ya nyongeza toka 1 kwenye Rasimu ya Pili hadi 3 kwenye Katiba Pendekezi
2. Kuongezeka kwa mambo ya muungano toka 7 kwenye Rasimu ya Pili hadi 16 kwenye Katiba Pendekezi Tunarudi kulekule kwenye mambo mengi ya muungano, kitu ambacho kimekuwa ni chanzo cha migogoro kati ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Hitimisho
Katiba hii inayopendekezwa kwa uchambuzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu imerudi nyuma badala ya kusonga mbele. Kuondoa kinga kwenye masuala muhimu na nyeti kama Haki za Binadamu, kuondoa Tanzania kubanwa na mikataba ya Kimataifa iliyoridhia, kuongeza madaraka kwa Rais, kuongeza idadi ya wabunge, kuondoa teuzi za viongozi mbalimbali kuthibitishwa na Bunge kumeifanya Katiba hii inayopendekezwa iwe kama ni mabadiliko tu ya Katiba iliyopo ya mwaka 1977. Yaani kwa kifupi hakuna jipya kabisa.
Pia suala la wananchi kutokuwa na mamlaka ya kuwahoji wabunge wao, kuondoa masuala ya uwajibikaji, miiko ya viongozi, kupunguza tunu muhimu, kuondoa vifungu vya utekelezaji wa Haki muhimu kama Haki za Wanawake ni kurudi nyuma madaraja kadhaa kuhusu uwajibikaji.
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu hakiungi kabisa mkono Katiba hii inayopendekezwa kwani imeandikwa kwa maslahi ya kundi dogo la viongozi na wanasiasa huku ikiwaacha wananchi wakiamini kuwa wamekumbukwa kwa vile kuna Haki za Makundi.